Maswali magumu tume ya mchanga wa dhahabu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,563
729,449
-Nani mkweli kati ya tume ya rais na wahusika?
-Je ni mtambo gani ulitumika kugundua kiwango cha madini yaliyomo kwenye makontena?
- Je huo mtambo tunao ama ulikodishwa?
-Kama ulikodishwa ni kutoka wapi?
-Kampuni gani ilipewa hiyo tenda?
-Je yalufunguliwa ama yalihamishwa hapo bandarini ama ilitumika technology gani kugundua KIASI cha madini?
-Kifaa gani kilitumika kufanya sorting?
-Kulikuwa na mizani maalum ya kupimia madini yaliyopatikana?
-Je mchanga na madini mpaka sasa bado vimetenganishwa ama vimerudishiwa kama zamani?
-Zoezi lilisimamiwa na nani?
-Je tume husika ina uwezo wa kupambana kisheria ikashinda ili kuepuka kutia taifa hasara kwa kulipa fidia?

MWISHO! Je tunaibiwa kwenye sheria na mikataba ama kwenye mchanga au kwenye vyote viwili?

Nawasilisha
 
Mfano hai
HTB1EtDcFVXXXXXyXpXXq6xXFXXXS.jpg
Gold-Ore-Color-Sorting-Machine-Golden-Mine.jpg_220x220.jpg
Je tume ilifanya hivi?kwa gharama gani? Je tender ilitangazwa? Mlipaji alikuwa nani? Kalipwa bei gani?
 
Mkuu mbona maswali yako mepesi sana hata mimi pia naweza kukujibu.

Leo mshana jr kiukweli umeuliza vitu ambavyo hata havifikilishi na namashaka makubwa hukusikiliza siku ile wakati tume inasoma ripoti yake mbele ya raisi.

Pale walifanya uchunguzi kwa kuchukua sample za mchanga katika makontena machache na kwenda nayo maabala kupima.

Na kumbuka yale majibu ni makadilio kwa wastani.
 
-Nani mkweli kati ya tume ya rais na wahusika?
-Je ni mtambo gani ulitumika kugundua kiwango cha madini yaliyomo kwenye makontena?
- Je huo mtambo tunao ama ulikodishwa?
-Kama ulikodishwa ni kutoka wapi?
-Kampuni gani ilipewa hiyo tenda?
-Je yalufunguliwa ama yalihamishwa hapo bandarini ama ilitumika technology gani kugundua KIASI cha madini?
-Kifaa gani kilitumika kufanya sorting?
-Kulikuwa na mizani maalum ya kupimia madini yaliyopatikana?
-Je mchanga na madini mpaka sasa bado vimetenganishwa ama vimerudishiwa kama zamani?
-Zoezi lilisimamiwa na nani?
-Je tume husika ina uwezo wa kupambana kisheria ikashinda ili kuepuka kutia taifa hasara kwa kulipa fidia?
MWISHO! Je tunaibiwa kwenye sheria na mikataba ama kwenye mchanga au kwenye vyote viwili?
Nawakilisha
Ilitume ifanye KAZI YAKE inawezeshwa kila wanacho hisi wanahitaji Na huwa vinapatikana . Nahao waliokuwa kwenye hiyo tume ni maprofessor wanajua wanachokifanya.Hayo maswali yako yote yanakuwa yanapatika pale hadidu rejea. Ukibahatika kuipata ripoti yote Majibu yote utayaona
 
Mkuu mbona maswali yako mepesi sana hata mimi pia naweza kukujibu.

Leo mshana jr kiukweli umeuliza vitu ambavyo hata havifikilishi na namashaka makubwa hukusikiliza siku ile wakati tume inasoma ripoti yake mbele ya raisi.

Pale walifanya uchunguzi kwa kuchukua sample za mchanga katika makontena machache na kwenda nayo maabala kupima.

Na kumbuka yale majibu ni makadilio kwa wastani.
OK ni makadirio ya wastani kwa kila container? Asante kwa kujibu hili moja....jamaa wakiamua kwenda mahakamani watashinda asubuhi mapema asubuhi...tuendelee na maswali mengine
LEGE kumbuka mahakamani hakuna makadirio kuna FACTS
 
Ilitume ifanye KAZI YAKE inawezeshwa kila wanacho hisi wanahitaji Na huwa vinapatikana . Nahao waliokuwa kwenye hiyo tume ni maprofessor wanajua wanachokifanya.Hayo maswali yako yote yanakuwa yanapatika pale hadidu rejea. Ukibahatika kuipata ripoti yote Majibu yote utayaona
Asante kuondoa maswali kama haya invewekwa wazi...kuna maswali hayatajibika hapo trust me
 
Mkuu hao walifanya analytical analysis. Unachukua sample unaweka kwenye machine. Machine yenyewe inasema kila kila kilichomo kwenye hiyo sample imo kwa kiasi gani. Dhahabu, silver, copper. Shida pekee walioonesha ambae mtaalamu yoyote amefanya kwa ngazi ya uzalishaji ni kuamini kila kilichomo kwenye concentrate unaweza kukivuna. Hao maprofesa hawajawahi kufanya kazi ngazi ya plant. Kwa kifupi huwezi kutoa dhahabu yote kwa smelting. Au rare element . Utatumia gharama nyingi kuliko unachozalisha. Ndo maana material mengine yanakuwa uchafu(waste product). Mfano wazalishaji wa sukari kuna sukari zaidi ya asilimia 30 huwa inabaki kwenye molasses na 1% kwenye makapi. Hiyo sukari ukiihitaji utatumia gharama kubwa kuitoa kuliko bei yako. Ndo maana wanawauzia wafugaji au watengeneza spilit au viroba . Acacia wametumia % of commercial value.
 
Mkuu mbona maswali yako mepesi sana hata mimi pia naweza kukujibu.

Leo mshana jr kiukweli umeuliza vitu ambavyo hata havifikilishi na namashaka makubwa hukusikiliza siku ile wakati tume inasoma ripoti yake mbele ya raisi.

Pale walifanya uchunguzi kwa kuchukua sample za mchanga katika makontena machache na kwenda nayo maabala kupima.

Na kumbuka yale majibu ni makadilio kwa wastani.

Bwana Lege umefanya nijiulize swali ala kijinga,

Hivi standards za machine/mitambo ya kupima kiwango cha madini kilichoko kwenye mchanga ambayo inatumika kuupima mchanga huu migodini kabla ya kupakiwa kwenye container na ile inayotumika kupima pale bandarini ukilinganisha na hizo machine/mitambo iliyopima kiwango cha madini maabara zote tatu zilizotumika ni standard moja?

Je ni nani anaefunga hiyo mitambo/machine za kupimia huo Mchanga kule mgodini pamoja na bandarini? Ni mwekezaji au Serikali?

Kama tulifunga sisi, anaedanganya ni mwekezaji au ni sisi wenyewe tumejidanganya?

Anyway, ngoja niache ujinga
 
Ndio maana nikasema tunaweza kushindwa kirahisi mno na tukaingia kwenye kulipa mabilioni mengine ya fidia
Kilichofanyika nakiunga mkono ila kimekuwa na loose ends nyingi sana
 
Mkuu mbona maswali yako mepesi sana hata mimi pia naweza kukujibu.

Leo mshana jr kiukweli umeuliza vitu ambavyo hata havifikilishi na namashaka makubwa hukusikiliza siku ile wakati tume inasoma ripoti yake mbele ya raisi.

Pale walifanya uchunguzi kwa kuchukua sample za mchanga katika makontena machache na kwenda nayo maabala kupima.

Na kumbuka yale majibu ni makadilio kwa wastani.

Mahabara iko wapi na ina uwezo gani
 
Bwana Lege umefanya nijiulize swali ala kijinga,

Hivi standards za machine/mitambo ya kupima kiwango cha madini kilichoko kwenye mchanga ambayo inatumika kuupima mchanga huu migodini kabla ya kupakiwa kwenye container na ile inayotumika kupima pale bandarini ukilinganisha na hizo machine/mitambo iliyopima kiwango cha madini maabara zote tatu zilizotumika ni standard moja?

Je ni nani anaefunga hiyo mitambo/machine za kupimia huo Mchanga kule mgodini pamoja na bandarini? Ni mwekezaji au Serikali?

Kama tulifunga sisi, anaedanganya ni mwekezaji au ni sisi wenyewe tumejidanganya?

Anyway, ngoja niache ujinga
Mkuu hiyo inafanya na serikali kupitia kwa wakala wao TMAA. Wenye mgodi hata wakipima wanawatumia SGS ambayo ni ya kimataifa. Ila serikali inachukua sample kujiridhisha. Ninaamini sample zote wameweka archive za kila kontena zikihitajika.
 
Nitakujibu maswali yako kwa ufupi ila yote kwa mapana.

Kwanza Tanzania ipo kwenye Minerals Belt kila madini yanayochimbwa hapa yanakua yameshikana na madini zaidi ya moja ila too bad kwetu sisi madini yenye thamani tunafikiri ni dhahabu pekee.

Kwanza kuhusu vifaa vya uchunguzi maabara zetu inawezekana kabisa kufanya hapo hizo kampuni za Madini wanapokua wanatest sample wanafanye kwenye maabara hapa hapa nchini na hasa wanatumia maabara ya SGS so haihiitaji mtambo mkubwa kama ulivyo uliza.

Kamati ilisema zoezi lilisimamiwa na vyombo vya ulinzi pia walichukua samples pekee hawakupima mchanga wote unapochukua sample ni kuchukua kiasi kidogo kuwakilisha namba kubwa sio rahisi kupima kiasi chote katika majaribio ni gharama na waste of resources..

Kuhusu tunaibiwa sheria/mikataba ama mchanga jibu litakuja kamati ya pili ikitoa majibu ila kwa ufupi na mtazamo inaweza kua vyote kwani sheria ya madini na kanuni zake maboresho ya 2009 inataka uchanjuzi ufanyike nchini .
 
Back
Top Bottom