Maswali 20 kwa Mungu

Maswali 20 kwa Mungu

lakini kumbuka ni maandiko hayohayo yalitumika kusaidia ku "abolish" slave trade in Afrika kama kweli ulisoma history utakua umenielewa.

Mkuu slave trade was abolished because slavery was uneconomical anymore following industrialization. Ownership of slaves became more expensive than owning machinery and less efficient so missionaries pretended that they helped end slave trade and colonialism but it was actually a business decision.

Akili ya kusoma, changanya na ya kufikiria mkuu.
 
JIBU NO 4 NA 5

4;Huku mbinguni hakuna KUOA /KUOLEWA URAFIKI/VIJIWE VYA STORI hivyo kaa ukijua maisha ya huko duniani ni tofauti kabisa na Mbinguni

5;maji yale baada ya gharika yalirudi yalipo toka kwani hayakuletwa kutoka katika sayari zingine namaanisha ya ardhini yalirudi "water table" yaliyo yeyuka yalirudi kuganda "snow , ice" vivyo hivyo kwa mawingu kikubwa zaidi Hydrogen na Oxygen zilitengana ili isiform water H2O. hivyo ndivyo maji yalirudi.

Kwa hiyo mkuu, unataka kusema kwamba maji yote yaliyopo kwenye mawingu leo hii yakishuka yanatosha kuifunika dunia nzima by more than 7000 metres (kilele cha mlima Everest, maana imeandikwa vilele vyote vilifunikwa)? Unajua ni mita ngapi za ujazo zinahitajika kufikia hapo? mkuu hata kama ukievaporate maji yote ya kwenye water tables zote (maziwa na bahari usiyaguse kwa sababu lazima yawe part ya mafuriko) bado maji hayatoshi kufanya dunia nzima ifurike kama ilivyoelezwa kwenye biblia.

Na hata kama ukiforce evaporation hivyo, bado maji uliyoyatoa kwenye water table yatarudi kwenye water table. kimantiki story ya gharika haiingii akilini mkuu, labda uniambie kwa namna nyingine.
 
Mkuu huku jf kuna watumishi wake, so I hope watatupa majibu.
Nilitaka nikujibu maswali yako lakini nashuhudiwa niache kwa sasa nisije nikainajisi nafsi yangu. Chamiton pole sana kwa wakati unaopitia.

Swali langu kwako "je udongo unaweza ukamwuliza mfinyanzi kwa nini unanifinyanga hivi na siyo vile?"
 
Najibu swali lako la 11:

Ni kwamba wakati MUNGU anaumba dunia aliwatuma malaika waende pande za kila ya dunia na kuleta udongo.

Kwahiyo watu weusi tumetokana na udongo mweusi
 
Nilitaka nikujibu maswali yako lakini nashuhudiwa niache kwa sasa nisije nikainajisi nafsi yangu.Chamiton pole sana kwa wakati unaopitia.Swali langu kwako "je udongo unaweza ukamwuliza mfinyanzi kwa nini unanifinyanga hivi na siyo vile?"
Acha kuuliza traditional questions, maswali toka karne ya kwanza yadi leo mnakaririsha??? kama huna majibu subiri wapo wanaojua....lol pole kwa wakati naopitia??? wakati gani huo???
 
najibu swali lako la 11:

Ni kwamba wakati MUNGU anaumba dunia aliwatuma malaika waende pande za kila ya dunia na kuleta udongo.

Kwahiyo watu weusi tumetokana na udongo mweusi
Mungu alitumia udongo wa aina moja tu kumfinyanga Adam so hakutengeneza watu wengi!!! watu wote wakatokana na Adam...je kwanini kuna rangi mbalimbali???
 
Acha kuuliza traditional questions, maswali toka karne ya kwanza yadi leo mnakaririsha??? kama huna majibu subiri wapo wanaojua....lol pole kwa wakati naopitia??? wakati gani huo???
Mkuu hata haya maswali unayouliza hapa yalishaulizwa wewe si wa kwanza ,kwani kwenye yale makosa 10 ya Mungu ni wewe au umechukua online aliainisha profesa mmoja?

Je udongo unaweza kumwuliza mfinyanzi kwa nini unanifinyanga hivi na siyo vile?Jibu hili swali mkuu, mimi nimnekuuluza moja tu wewe umeuliza 20 kabla sijakujibu yako 20 nahitaji jibu la swali langu mmoja.
 
Mkuu hata haya maswali unayouliza hapa yalishaulizwa wewe si wa kwanza ,kwani kwenye yale makosa 10 ya Mungu ni wewe au umechukua online aliainisha profesa mmoja?
Je udongo unaweza kumwuliza mfinyanzi kwa nini unanifinyanga hivi na siyo vile?Jibu hili swali mkuu,mimi nimnekuuluza moja tu wewe umeuliza 20 kabla sijakujibu yako 20 nahitaji jibu la swali langu mmoja.
Yale makosa 10 hamna copy hata moja...ni mambo niliyofikiri yakagoma kuingia akilini...BTW mimi kutoa kitu haimanishi kwamba nimekopi hata kama kuna mtu aliwahi kuuliza...mbona USA na URUSI wanatengeneza slaa kali je nani aliyekopi kwa mwenzake?

Its just a matter of distance, udongo hauwezi kumwuliza mfinyanzi kwa sababu udongo ni irrational non-living things. Unapo fanya comparison tumia vitu vinavyo fanana, binadamu na udongo tunatofauti kubwa sana.
 
Nimefocus zaidi kwenye SLAVERY. Biblia iliandikwa na watu wenye ufahamu wa hali ya juu.. na ilikua imeandikwa ili kutekeleza mikakati ya muda mrefu sana.. haya maisha yote tunayoishi watu walishapanga miaka na miaka kwamba itakuwa hivi.. na ndo maana kila kinachotokea sasa kimeandikwa kwenye biblia, watu wanasema ni mwisho wa dunia umefika, hapana, ni mipango ile ilishapangwa.. ndo maana hata maneno yanayohusu utumwa yameandikwa kwenye biblia.. walijua wanachokuja kukifanya baadae.. Ngumu kuelewa ila jitahidi tu hivyohivyo
Mh! maneno mazito haya
 
MASWALI MENGINE YA KUJIULIZA..
kabla ya wazungu kuja babu zetu walikua hawamjui Mungu? ina maana wote wapo motoni? na wachina wahindi waarabu na wajapan ambao hawamjui yesu wataenda motoni? sisi waafrika na wazungu ndo tutaenda mbinguni? yani mtu na mbaguzi wake wanaenda kuishi mbingu moja!!!??
Tusiwe wapumbavu kiasi hiki.
Dah! haya mambo haya!!!
 
Mh! maneno mazito haya
mzungu alichofanya ni sawasawa na mtu anaemuua mzazi wako angali wewe bado mdogo, halafu anakuchukua na kukulea kama mwanae, anakufundisha kusoma kuandika kuwinda na kusali kwa mungu anaemwamini yeye.

Mwisho wa siku unakuja kujua kwamba huyo unaemdhania ni baba sio mzee wako, mzee wako alishauliwa na huyohuyo aliekukuza mpaka umekua mtu mzima..

halafu mwisho wa siku badala ya kushtuka kwa kufanywa zumbukuku, unasema aah acha tu yapite huyu mzee kanilea na kunifundisha vitu vingi sana ninampenda..

unashindwa hata kuhoji kwanini huyo mzee alimuua babako? hivi we una akili kweli?
 
1.Mungu kama ulimwumba kila mtu kwa mfano wako, je wewe ni mwamaume au mwanamke?

2.Mtu akiugua, aende hospitalini kupewa tiba au akafanyiwe maombi? Na akifanya vyote, kipi kitasaidia zaidi?

3.Mungu wakati unamwumba mwanaume uliweka govi, hukujua ni najisi? mbona unasema likwatwe? huko siyo kuediti uumbaji wako?

4.Watakaoingia mbinguni, watafurahi vipi kama ndugu zao wawapendao watakuwa jehanamu?

5.Baada ya gharika ya Nuhu, maji ya mafuriko yalielekea wapi??? Kwa sababu kila mahali palijaa maji.

6.Kwanini ulichelewa kumwumba mwanamke ilihali ulimuumba mwanaume na uhitaji wa mwanamke? Nadhani hapo ndo chanzo cha kujichua.

7.Mungu kwanini uliumba bangi? ni ya kazi gani? Mbona watu wako wanaipinga sana?

8.Mungu kama wewe ni mpangaji wa maisha yetu, kwanini tukusumbue kwa sala?

9.Mbona watu wema wanapatwa na mabaya? Si uliahidi mema ya nchi kwa watenda mema?

10.Kama watu wote ni uzao wa Adam na Eva, mbona tunatofautiana sana...nini chanzo cha kuwepo kwa watu weupe na weusi?

11.Mungu mbona kwenye maandiko yako umechochea sana utumwa(slavery)? kwani tukiishi kwa usawa haikupendezi?

12.Mungu una urafiki na shetani? mbona mnakutana mara kwa mara na kupiga stori( Ayubu 1:6-12)

14.Kwanini ulimtese Ayubu kwa lengo la kuridhisha matakwa shetani?

15.Mungu mbona ulimpa Musa amri ya usiue lakini ukampa maagizo ya kuua...Mungu hadi leo pale middle east wanauana.

16.Mungu kwa kuwa ulisema tupumzike siku ya 7, mbona watu wanatembea umbali mrefu kutafuata majumba ya ibada na wengine wanatumia hiyo siku ya 7 kupata pesa kwa njia ya sadaka? kwanini tusibaki nyumbani tupumzike?

17.Baada ya Kaini kumua Abeli ulimuuliza Kaini ndugu yako yupo wapi, hivi ni kweli hukujua alipokua Abeli?

18.Mungu kama unalounganisha hakuna awezae kulitenganisha, mbona ndoa zinavunjika?

19.Mungu hivi Suleiman ndiye aliyekuwa na hekima kuliko wote? mbona alifanya mambo kuntu sana? Wanawake 1000 siyo mchezo...au polygamism ndio hekima yenyewe?

20.Mungu kwanini ulimpa Hitler roho mabaya kiasi kile? yaani alichokifanya humu duniani we acha tu.

Naamini kuna watumishi wa Mungu huku jf, kwahiyo ningepende wanisaidie majibu ya haya maswali...nimeuliza siyo ayajibu Mungu bali watu wenye uelewa na haya mambo...Kama mtu huna jibu kuwa mvumilivu maana wapo wenye ufahamu wa kutosha na siyo kulaani, kuhukumu na kuniona kana kwamba nimepotea...Muhimu zaidi jibu la uongo halitakiwi...pia kama jibu lina utata nitauliza.Karibuni kwa majadiliano yenye nia ya kueleweshana
1.MUNGU in mwanaume,amesema hivyo throughout the bible....ndo mana tukisali tunasema "baba yetu ulie mbinguni"
 
Mungu hayupo , God is yourself depending on how to use your power within your mind only (watu watakuona mchawi but not)
Yupo na amaishi,Manabii wa zamani baadhi wamemuona...wewe jipe matumaini ya mwendokasi alafu siku ukutane nae kule mbinguni,utaisoma namba siku hiyo.
 
Yupo na amaishi,Manabii wa zamani baadhi wamemuona...wewe jipe matumaini ya mwendokasi alafu siku ukutane nae kule mbinguni,utaisoma namba siku hiyo.
Ahah! unazani namuogopa Mungu wako? and soon hako kamungu Tutakachinja kafe! kabisa ! Atomic bomb zipo ! hapo hachomoki!
 
Pole sana hiyo jeuri ya kumuuliza Mungu maswali umeitoa wapi? Hiyo pumzi unayovuta ndiyo inakupa kibuli? Nakushauri ukatubu na kuomba msamaha.
 
Ahah! unazani namuogopa Mungu wako? and soon hako kamungu Tutakachinja kafe! kabisa ! Atomic bomb zipo ! hapo hachomoki!
Mkuu to be honest hii post imenitoa mbavu nje...Hahahaa kwamba kuna atomic bombs??? loh!!! atomic bombs plus poison weapons kwakweli ana kazi.
 
Back
Top Bottom