hili swali lako limenigusa mno.. ukifikiria kwa umakini utajua kwanini wazungu walileta dini ya kikristo.. dini ya kikristo inafundisha kuwa na huruma, kuwa wanyenyekevu, kuwa watu wa kutokuhoji vitu.. wakati wa ukoloni mababu zetu walikua watata sana yaani hawatii mamlaka ya mkoloni, ndo maana wakoloni wakaintroduce huu ukristo kwa waafrika ili wawe na roho ya huruma, wawe wanyenyekevu, yaani kwa kizungu unaweza kusema walitujenga tuwe SUBMISSIVE.
Kwa maana hiyo basi chochote mwafrika alichokua anatendewa na mzungu, mafundisho ya biblia kutoka kwa wamisionari yaliwaelekeza kuwa watu wa kukubali yanayotokea, NDO ULE MSTARI WA BIBLIA UNAOSEMA AKUPIGAE SHAVU LA KUSHOTO, MGEUZIE PIA NA LA KULIA. Kwamba mwisho wa dunia huyo mkoloni ataenda kuchomwa moto.
Kwa maana hiyo basi, neno la Biblia lilikua faraja sana kwa watumwa kwa kuwa neno liliwaambia, hao wakoloni wanaowatesa wana hukumu yao ambayo ni moto wa jehanam.. UNAONA MZUNGU ALIVYO MJANJA?
Sasa tujiulize swali moja, wote tunajua kwamba mzungu ni mbaguzi, anatuita waafrika masokwe, hapohapo anatuletea biblia tuisome tumwabudu Yesu mwisho wa siku twende tukaishi mbinguni.. hvi hawa jamaa kama huku duniani wanatubagua hivi na kutudhihaki, TUNAAMINI KABISA WAMETULETEA YESU ILI TUOKOKE MWISHO WA SIKU TUKAISHI NAO MBINGUNI??? YANI MZUNGU AMBAE MBAGUZI AISHI NA MWAFRIKA YAAN SOKWE, AISHI NAE MBINGUNI?
TAFAKARI.