Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,474
- 29,186
Nimefurahi muswada wa kuwalipa wenza wa viongozi wa nchi. Ni uzalendo wa hali ya juu sana. Hii itachochea maendeleo makubwa ya nchi.
Pia Ndugu yangu na Kaka yangu Robert Heriel Mtibeli ameshauri Watoto wa viongozi wakuu wa nchi walipwe ili kuwatia moyo pia watoto wa hao wakubwa nao wawe wanalipwa mishahara .
Sasa ninaishauri pia serikali, isiishie tuu hapo iende mbali zaidi kuchochea maendeleo ya nchi yetu kwa kuwalipa Masuria, Concubines au Nyumba Ndogo za Hawa viongozi. (Sitaki kuwaita vimada)
Hawa nao ni watu muhimu sana katika maisha ya viongozi wetu. Viongozi wetu wanapokua wamekwazana na wenza wao nyumba kuu basi hawa huchukua jukumu la kuwaliwaza.
Yaan maisha ya viongozi wetu tunawaona hawana stress za nyumbani sababu ya uwepo wa Hawa vimada, nashauri nao pia walipwe mishahara. Wengi wao sababu ya kujihusisha na maisha ya hawa viongozi wakubwa unakuta wanashindwa hata kufanya shughuli zingine za kiuchumi kwao.
Hawa Masuria wakiwa na furaha itasababisha wawatunze vizuri viongozi wetu hivyo nchi itasonga mbele Kwa kasi kubwa. Sababu viongozi wetu watafanya kazi bila stress kwani nyumba kubwa kukiwa na tatizo basi masuria hawa husawazisha hali.
Tunaweza tukaona tunaongeza gharama lakini ni heri hivyo kuliko tusiwalipe halafu viongozi wetu washindwe kufanya kazi Kwa utulivu. Kuna maamuzi pengine tunayaona ya ajabu kumbe mtu usiku aligombana na mkewe.
Iwepo kamati ya siri ya kuwasajili Hawa sababu wengine (wengi wao) watakua wako Kwa siri hawajulikani kwenye nyumba kubwa. So isije ikaleta mtafaruku.
Yangu ni hayo tu.