Masuala Matatu ya Kutafakari

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
1,240
Kongamano la Ubungo lilifanyika, na washiriki waliazimia kufanya maandamano siku za usoni. Wameunda Kamati ya Maandalizi. Ifuatayo ni mada ambayo niliwasilisha katika kongamano hilo:

KONGAMANO LA DEMOKRASIA NA MAENDELEO JIMBO LA UBUNGO

MASUALA MATATU YA KUTAFAKARI

Na John Mnyika

USULI

Leo Jumamosi 14 Juni 2008 tumekutana hapa katika Ukumbi wa Kilato kata ya Kimara wakazi mbalimbali wa Jimbo la Ubungo kujadili kuhusu demokrasia na maendeleo katika Kongamano la Kwanza liloandaliwa na CHADEMA Jimbo la Ubungo.

Nimetakiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano nitoe mada kuhusu ajenda za WanaUbungo. Kwa ujumla ajenda za wanaUbungo ni nyingi; kama ukiamua kutazama ajenda za Fursa, basi ziko nyingi tu katika Jimbo hili lililojaliwa kuwa na Idadi kubwa ya wakazi wa kada mbalimbali; Viwanda na Vitega uchumi vikubwa; Vyuo vya pekee nchini;vyombo vya habari nk. Ukiamua kutazama Changamato basi ajenda hizo ni nyingi zaidi: ukianzia na masuala ya maji, usafiri, barabara, wafanyabiashara ndogo ndogo, umeme, mipango miji, mfumo wa utawala, uwajibikaji, ardhi, makazi, biashara ikiwemo biashara ndogo ndogo; katika kila eneo kati ya hayo niliyoyataja kuna maswali na masuala yanayoibua mjadala mzito. Naamini utaratibu huu wa kuwa na Kongamano la Demokrasia na Maendeleo unapaswa kuwa wakudumu ili walau mara moja kila mwaka upatikane wasaa wa wakazi kukusanyika pamoja kujadili fursa na changamoto mbalimbali zinazokabili jimbo la Ubungo.

Kwa leo nimechagua kuyalenga masuala matatu tu ambayo yanahitaji tafakari ya haraka; tukiunganisha nguvu za pamoja kuyashughulikia masuala hayo, basi harakati za mabadiliko zitakuwa zimeanza. Mafanikio ya kuunganisha nguvu katika masuala haya matatu yatachochea harakati pana zaidi za mabadiliko zenye kuhusisha kuongeza elimu ya uraia na kuchochea uwajibikaji katika ngazi mbalimbali kuanzia kwenye mitaa, kwenye halmashauri na hatimaye taifa.

SUALA LA KWANZA: HATMA YA RICHMOND/DOWANS

“NI WAKATI WA KUCHUKUA HATUA”

UTANGULIZI:
Februari 6 mwaka 2008 Kamati Teule ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoundwa tarehe 13 Novemba, 2007 iliwasilisha taarifa yake bungeni. Kamati hiyo iliundwa kuchunguza mchakato wa Zabuni ya Uzalishaji umeme wa dharura ulioipa ushindi Richmond Development Company LLC ya Houston, Texas Marekani mwaka 2006.

Kutokana na uchunguzi wa kina ulioanishwa katika taarifa ya Kamati Teule, Bunge lilijulishwa kuwa mchakato wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura wa MW 100, uliopelekea Richmond Development Company LLC kuteuliwa na hivyo kusaini mkataba na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tarehe 23 Juni 2006 na baadaye kurithiwa na Dowans Holdings S.A tarehe 23 Desemba 2006, uligubikwa na vitendo vya ukiukwaji taratibu, kanuni na sheria za nchi na hivyo kujenga kiwingu cha mashaka ya upendeleo, ubadhirifu na rushwa ambavyo vimechangia kumuongezea mwananchi mzigo wa gharama za umeme.

Aidha, Kamati Teule ilithibitisha kuwa uteuzi wa Kampuni dhaifu kifedha, kiufundi na kiuzoefu na ambayo haina usajili Marekani wala Tanzania kama kampuni yenye ukomo wa hisa, yaani Richmond Development Company LLC, ulitokana na kubebwa na viongozi waandamizi wa Serikali.

Kamati hiyo ilibaini mapungufu makubwa na kamati ilitoa mapendezo mbalimbali na kutoa maelekezo kwa serikali kuhakikisha yanatekelezw; Baadaye Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliunda Kamati ya kusimamia utekelezaji huo.

Leo Juni 14, 2008 takribani miezi minne imepita toka Kamati iwasilishe taarifa yake Bungeni. Baadhi ya mapendekezo ya msingi yaliyomo kwenye kamati hayakuhitaji muda mrefu kiasi hiki kuweza kutekelezwa lakini mpaka hivi sasa serikali iko kimya kuhusu utekelezaji wake. Ni wakati wa kuyatafakari tena mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge na maazimio ya Bunge baada ya mapendekezo hayo.

WANANACHI TUTANGAZE WAZI KUWA HAKUNA MKATABA KATI YETU NA RICHMOND/DOWANS:

Kamati tuele iliweka bayana kuwa, Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC ulikuwa wa uzalishaji umeme wa dharura kipindi ambacho nchi ilikuwa katika hali ngumu ya ukame uliokausha mabwawa yote ya kuzalishia umeme. Kamati Teule iliitaka Serikali kutathmini upya uhalali wa kuwepo na kuendelea kuwepo na mkataba huo kutokana na udanganyifu bayana uliofanywa na Richmond Development Company LLC kuhusu uwezo wake kifedha, kiufundi, na uzoefu wake katika masuala ya uzalishaji umeme; usajili na uwepo wake kisheria kama kampuni halali yenye ukomo wa hisa nchini Marekani na Tanzania; uhusiano wake kisheria na Kampuni kubwa ya Kimataifa ya Pratt & Whitney na utambulisho wa Mzungu mmoja kwa jina la John Perun kama mwakilishi wa Pratt & Whitney, mambo ambayo Kampuni hiyo kubwa ya Kimataifa imeyakanusha vikali.

Kamati Teule ilishuhudia bei za mitambo hiyo jijini Houston, Texas Marekani kwa watengenezaji kiwandani ikiwemo kampuni ya Kawasaki Gas Turbines – Americas ambayo iko chini ikilinganishwa na bei zinazotolewa na mawakala hao, jambo ambalo lingeiwezesha Serikali kununua na kumiliki badala ya kukodi kwa muda mfupi na kwa gharama kubwa. Mathalan, MW 105 zingepatikana kwa kununua mitambo sita ya MW 17,5 kila mmoja kwa gharama ya shilingi bilioni 56.25 badala ya shilingi bilioni 108.7 tulizotandikwa na Richmond Development Company LLC mitambo hiyo ikibaki mali ya wakodishaji. Kamati Teule ilithibitisha kwamba kauli iliyokuwa inatolewa mara kwa mara na baadhi ya viongozi wote tuliowahoji kwamba kipindi hicho cha ukame haikuwa rahisi kupata mitambo hiyo na ilikuwa ikigombaniwa na nchi nyingi kauli hiyo ilikuwa sio ya ukweli na upotoshaji mkubwa.

Ilielezwa kuwa Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC na sasa Dowans Holdings S.A, kama ilivyo mikataba kati ya TANESCO na IPTL, SONGAS, AGGREKO na Alstom Power Rentals inatoa unafuu usiostahili kwa makampuni hayo ya umeme na kuiumiza TANESCO na hatimaye watumiaji na walipa kodi kimapato, k.m mikataba hiyo kuwa na vipengele vya kuibana TANESCO kuyalipia makampuni hayo kodi zinazohusika na uendeshaji (operations), matengenezo/marekebisho ya mara kwa mara ya mitambo (maintenance) gharama za bima, ada za mawakili na washauri elekezi (consultants) gharama za mafuta na gesi ya kuendeshea mitambo, gharama za ukodishaji mitambo (capacity charges) ambazo TANESCO hulipa kila mwezi si chini ya wastani wa shilingi bilioni 2 kwa kila kampuni, izalishe au isizalishe umeme. Kamati Teule ilitoa rai kwa Serikali kuwa mikataba yote hii ipitiwe upya mapema iwezekanavyo kama ambavyo mikataba ya madini inavyopitiwa upya sasa na Serikali. Bila kufanya hivyo, mzigo mkubwa wa gharama za umeme utawaelemea wananchi. Lakini mpaka sasa serikali imeendelea kuutambua mkataba huu kwa niaba ya watanzania, miezi minne baada ya pendekezo hili. Ni wakati wa wananchi kuungana pamoja kutamka wazi kwamba hatuutambui mkataba huo; kwa kuwa umeingiwa na wawakilishi wetu kwa hila la bila ridhaa yetu. Hivyo, ni vyema mitambo yao ikaondolewa katika Jimbo la Ubungo.

TUSHINIKIZE MALIPO YA MILIONI 152 KWA SIKU KWA DOWANS YASITISHWE MARA MOJA; FEDHA ZILIZOLIPWA MPAKA SASA ZIREJESHWE.

Kamati Tuele ilieleza bayana kuwa, Madhumuni ya Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC yalikuwa kuzalisha umeme wa dharura kwa kipindi cha miezi kumi na mbili (12) tu. Muda huo ungeweza kuongezwa baada ya kutathmini hali ya ongezeko la maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme nchini. Kabla ya muda wa tathmini hiyo haujafikiwa, wakati majadiliano yakiendelea GNT ikaongezea Richmond Development Company LLC muda wa kukodi mitambo hiyo kuwa miaka miwili (2). Kamati Teule haikuona vielelezo vyovyote vilivyojenga uhalali kwa GNT kuongeza muda huo. Uamuzi huo umeliongezea Taifa mzigo mkubwa wa gharama zisizokuwa za lazima. Mathalan, kwa upande wa capacity charges tu, TANESCO itailipa Dowans Holdings S.A jumla ya shilingi bilioni 54.8 kwa kipindi kilichongezwa cha mwaka mmoja. Aidha, GNT ilishindwa kutambua ulaghai wa Richmond Development Company LLC kuhusu mwakilishi wa Pratt & Whitney na hivyo kuamini karatasi ambayo ilikuwa haijathibitishwa na mawakili na diskette zenye picha za mitambo ya Pratt & Whitney, vielelezo ambavyo Kamati Teule iligundua na kuthibitisha kuwa vilikuwa vya kugushi. Vilevile, bila kujali kwamba TANESCO ingelezimika kuilipa Richmond Development Company LLC shilingi milioni 152 kwa siku kama gharama ya kuweka vifaa vyao nchini, GNT ikakubali kilegelege kuitoza Richmond Development Company LLC shilingi milioni 12 tu kwa siku kama fidia kwa ucheleweshaji wa kuanza kuzalisha umeme kulingana na tarehe iliyokubalika kwenye mkataba. Tunasikitika kwamba hata baada ya kuelezwa mambo yote hayo, serikali bado imeendelea kuilipa kampuni ya DOWANS kiasi cha fedha sawa na takribani milioni 152 kila siku. Hivyo tunataka serikali iache kutumia vibaya fedha zetu na isitishe malipo hayo mara moja na kudai fedha zilizolipwa mpaka sasa zirejeshwe.

MIKATABA IWEKWE WAZI KWA WANANCHI WA ENEO AMBALO MRADI/UWEKEZAJI UNAFANYIKA ILI KUJUA HAKI NA WAJIBU WAO:

Kamati tuele ilipendekeza wazi kuwa; Utaratibu tuliourithi kutoka kwa wakoloni na kuuzoea wa kuiona mikataba ya kibiashara kuwa ni siri hata kwa walipa kodi wenyewe na kuwa uwanja wa pekee wa watendaji, ambao Waziri wa Mipango Uchumi na Uwezeshaji Mhe. Dk Juma Ngasongwa (Mb) aliusifia bungeni tarehe 19 Aprili 2007 kuwa best practice wakati akijibu swali la Mhe. Masolwa C. Masolwa (Mb) Mbunge wa Bububu, umepitwa na wakati na unakiuka misingi ya demokrasia na uwajibikaji. Matokeo ya utaratibu huu ni kuwepo kwa mikataba mibovu inayoficha vipengele vinavyoibebesha Taifa mizigo mikubwa ya gharama zisizokuwa za lazima. Wakati umefika sasa wa wananchi wa eneo husika kudai kuonyeshwa mikataba ya kibiashara ya maeneo yao ili kujua haki na wajibu wao. Mathalani, kuna malalamiko ya wakazi wa Jimbo la Ubungo wanaoishi karibu na mitambo ya Richmond/Dowans kuhusu masuala ya joto, mionzi na kelele zinazotokana na mitambo hiyo. Wananchi hao wanalalamikia kuwa waliahidiwa kulipwa fidia na kuondolewa katika maeneo ya jirani na mitambo hiyo. Maswali ya kujiuliza; Je, tathmini kamili ya madhara katika mazingira(EIA) ilifanyika kikamilifu kabla ya mradi huo? Je, suala la wananchi kulipwa fidia lilikuwa sehemu ya mkataba? Kama mkataba huu ungekuwa wazi mapema ikiwemo kwa wananchi wa jimbo la Ubungo, ni wazi kuwa wananachi wangeelewa haki na wajibu wao katika mkataba husika.

SERIKALI IACHE KUIGOPA TAKUKURU, ICHUKUE HATUA YA KUBADILI UONGOZI WA TAASISI HIYO

Taarifa ya Kamati Teule ilidhihirisha wazi jinsi Taifa lilivyotumbukizwa kwenye hasara kubwa kutokana na mkataba huo wa Richmond Development Company LLC na Dowans Holdings S.A, kinyume na taarifa iliyotolewa na TAKUKURU (wakati huo TAKURU) kwamba Taifa halikupata hasara yoyote. Taarifa ya TAKUKURU ililenga kuficha ukweli (white wash) hivyo ikaishia kujikanganya kwa kukiri kuwepo kwa mapungufu lakini yasiyokuwa na athari. Taarifa hiyo imemong’onyoa kwa kiasi kiasi kikubwa hadhi na heshima ya chombo hiki muhimu cha kitaifa kilichopewa dhamana ya kupambana na rushwa na sio kuipamba ili kurejesha heshima ya umma katika taasisi hiyo. Kamati teule ilipendekeza mabadiliko ya haraka ya uongozi wa taasisi hiyo. Mpaka sasa mabadiliko hayo hayajafanyika, na Mkurugenzi wa TAKUKURU ameendelea kuwa Edward Hosea ambaye ametuhumiwa hadharani kwa kuigeuza TAKUKURU kuwa Taasisi ya kulinda na kutetea rushwa. Ni wakati wa wananchi kutaka serikali iache kuigopa TAKUKURU na kuchukua hatua za haraka za kubadili uongozi wa Taasisi hiyo.MWAKAPUGI, MRINDOKO NA WATENDAJI VINARA WACHUKULIWE HATUA HARAKA

Kamati Teule iliainisha katika taarifa yake vitendo vya ubabe, ujeuri na kiburi vilivyofanywa na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini alimradi kampuni waliyoitaka iteuliwe kiasi cha kupindisha hata maamuzi ya Baraza la Mawaziri bila wasiwasi wowote, kukaidi ushauri wa kitaalamu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma mara tatu mfululizo na kinyume na maagizo ya Baraza la Mawaziri lililotaka Sheria ya Ununuzi wa Umma izingatiwe, kukiuka sheria kwa makusudi kwa kuingilia mchakato wa zabuni wa taasisi nyingine ya ununuzi, kuvipuuza vyombo vya ndani vya maamuzi vya TANESCO (Bodi ya Wakurugenzi, Bodi ya Zabuni n.k), kuilazimisha Bodi na Menejimenti ya TANESCO kuridhia maamuzi yaliyofanywa na Wizara ya kuibeba Richmond Development Company LLC kinyume cha sheria na taratibu n.k. Wizara hiyo katika kuibeba Richmond Development Company LLC ilifikia hatua ya kupotosha kwa makusudi ushauri wa Wizara ya Fedha uliozuia malipo ya awali ya Dola za Kimarekani Milioni 10 katika Barua ya Dhamana ya Benki ya Richmond Development company LLC. Kamati Teule ilipendekeza kwamba Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo Mhe. Dk. Ibrahim Msabaha (Mb) na Katibu Mkuu Ndugu Arthur Mwakapugi wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza Taifa kwa makusudi kwenye mkataba na kampuni ya mfukoni ambao umesababisha hasara kubwa kwa nchi. Aidha Kamishna wa Nishati Ndugu Bashir Mrindoko naye ilipendekezwa achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu mpya wa Wizara kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC ambao ulijulikana dhahiri na Wizara toka mwaka 2004 kwenye mkataba wa Bomba la Mafuta. Ndugu Mrindoko ndiye aliyeiandikia barua kampuni hiyo kusitisha mkataba wake na Serikali mwezi mmoja tu kabla ya mchakato wa zabuni ya umeme wa dharura haujaanza. Wakati umefika wa wananchi kuitaka serikali kuwachukulia hatua za kinadhamu Mwakapugi, Mrindoko kama ilivyopendezwa na Kamati teule. Katika hali ya kawaida ya uwajibikaji, ilitarajiwa Rais Jakaya Kikwete, mara baada ya Waziri Mkuu Pinda kuunda Kamati ya kusimamia utekelezaji wa maazimio ya Bunge kutokana na Taarifa ya Kamati Teule; angewachukulia hatua wateule wake, hususani makatibu wakuu waliohusika na kashfa hii kwa kuwasimamisha kazi wakati wote ambapo kamati inatafakari hatua za kinadhamu zinazopaswa kuchukuliwa.

MAPENDEKEZO:

Ni wakati wa wananchi kuchukua hatua. Kwa kuwa makao makuu ya TANESCO yako jimbo la Ubungo; na kwa kuwa Kampuni ya Richmond ilikuwa Ubungo; Na kwa kuwa Kampuni ya Dowans iko Jimbo la Ubungo. Ni wakati wa wakazi wa Ubungo kwa niaba ya watanzania wengine, kujiunga pamoja chini ya ‘falsafa ya nguvu ya umma’; kuiwajibisha serikali kutekeleza mapendekezo ya Kamati Tuele ya Bunge mapema iwezekanavyo.SUALA LA PILI: HAKI ZA WAFANYAKAZI

“SHUTUMA ZA WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA NGUO URAFIKI”

UTANGULIZI

Kiwanda cha nguo cha Urafiki kiliingia ubia na kati ya Tanzania na China mwaka 1997. Wakati wachina wanaingia ubia katika kiwanda hicho, kiwanda hilikuwa kinafanya kazi kiwanda kizima kikiwa na vinu vitatu. Mashine zote zilikuwa zikifanya kazi na kwa ujumla wafanyakazi; kwa ujumla kiwanda kilikuwa kinafanya kazi shifti tatu kwa siku. Lakini mara baada ya ubia huo, pamejitokeza malalamiko mengi ya Wafanyakazi kwa zaidi ya miaka kumi ambayo mara nyingine yamesababisha migomo na kutoelewana.

SHUTUMA ZINAZOTOLEWA

Kupunguzwa kwa mashine za uzalishaji

Wafanyakazi wanatoa shutuma kwamba, walipoanza kazi wachina hawakuchukua muda mrefu wakafunga kinu namba mbili kwa kuua sehemu ya usokotaji na kubaki sehemu ya ufumaji pekee. Kinu hiki kilifungwa kwa madai kwamba mashine za kisasa zingeletwa, mpaka wakati wa kuandikwa kwa taarifa hii kinu hicho hakijaletwa. Zipo tuhuma kwamba kinu hiki kilichoondolewa kimeuzwa kama vyuma chakavu. Pamoja na kuathirika kwa uzalishaji, matokeo ya kufungwa kwa kinu hiki ni wafanyakazi kupunguzwa. Mara baada ya wafanyakazi wengine kupunguzwa, palitolewa ahadi na kiwanda kwamba mishahara na maslahi ya wafanyakazi waliobaki ingeboreshwa, ahadi ambayo mpaka leo haijatekelezwa. Wafanyakazi waliitisha migomo kuhusu suala hili, Waziri wa Viwanda na Biashara wa wakati huo, Juma Ngasongwa alifika katika kiwanda na kuzomewa na wafanyakazi. Kutokana na hali hiyo Waziri alitoa amri mfanyakazi huyo akakamatwa na hatimaye akafukuzwa kazi. Waziri Mkuu wa wakati huo, Fredrick Sumaye, naye alitembelea mara kadhaa katika kiwanda hicho lakini hakuweza kushughulikia kikamilifu shutuma zilizotolewa.Mishahara finyu na maslahi duni kwa Wafanyakazi

Wafanyakazi wanatoa shutuma kwamba toka kiwanda kiingie ubia mishahara na maslahi ya wafanyakazi havijaboreshwa kwa mujibu wa matarajio yaliyotolewa na wabia. Wafanyakazi wa Kiwanda hiki wamelalamika kwa zaidi ya miaka kumi kuhusu kunyonywa na kunyanyaswa, malalamiko yao yapo serikalini na baadhi yamefikishwa mahakamani. Hata hivyo serikali haijayapatia ufumbuzi malalamiko hayo na kesi zilizoko mahamani zinaendelea kuahirishwa na kuchukua muda mrefu. Baadhi ya mambo yanayolalamikiwa na wafanyakazi ni kuhusu ufinyu wa mishahara na uduni wa maslahi ni pamoja na:
• Kwa miaka kumi wamehangaika mahakamani kuhusu suala la kupunjwa kwa mishahara yao, wafanyakazi wanataka ufumbuzi wa kesi upatikane mapema.
• Kukatwa posho zao za likizo kwa miaka tisa bila kupewa fedha wala likizo; baada ya mihangaiko mengi iliamuliwe walipwe fedha hizo. Hata hivyo mwajiri amemua kuwalipa fedha hizo kwa kulazimisha wafanyakazi walipwe kama mavazi badala ya kupewa fedha taslimu. Baadhi ya wafanyakazi kwa unyonge wamechukua nguo, waliokataa hawajapewa fedha zao mpaka leo.
• Septemba 2007 Serikali kupitia kwa Waziri wa Kazi wa wakati huo, Mheshimiwa Chiligati ilitangaza kima cha chini ya mishahara ya sekta binafsi cha shilingi 150,000 toka 48,000 baada ya kupokea mapendekezo toka kwa bodi inayohusika. Baadhi ya bidhaa/huduma zikapanda bei baada ya tangazo hilo la kupanda kwa mishahara. Lakini ilipofika mwezi Oktoba siku chache kabla ya tarehe ya utekelezaji wa agizo hilo, Waziri alitangaza kuahirisha utekelezaji wa tangazo hilo hadi Januari 2008.
• Matokeo ya tangazo la serikali la kima cha chini kuwa shilingi laki unusu kwa upande mwingine ni baadhi ya waajiri kupunguza wafanyakazi licha ya tangazo la serikali kukataza kufanya hivyo. Kwa upande wa Kiwanda cha Urafiki wafanyakazi wanalalamika kuwa wenzao 725 walipunguzwa, wengi hao ni vijana waliokuwa wakifanya kazi kama vibarua wa muda mrefu(japo sheria ya kazi inakataza vibarua wa muda mrefu).
• Baadaye Waziri Chiligati akatangaza kwamba baada ya mazungumzo na Shirikisho la Wenye viwanda Tanzania(CTI) kwamba wameomba msamaha wa kulipa 80,000 badala ya 150,000 kama kima cha chini; na kubadilisha vigezo vya awali vilivyopendekezwa na bodi. Kauli hii ilikinzana na kauli ambayo Rais Kikwete aliitoa mwishoni mwa mwaka 2007 alipotembelea Kiwanda cha Mafuta Kurasini kwamba “ifikapo Januari 2008, walipeni wafanyakazi walau shilingi laki na hamsini kama kima cha chini”.
• Mnamo tarehe 24 Januari, 2008 Wafanyakazi wa Kiwanda cha Urafiki chini ya ulinzi mkali wa polisi walipewa barua ya mishahara mipya. Na ilipofika 25 Januari, 2008 Wafanyakazi walipewa mshahara mpya wa shilingi 80,000; wakati wafanyakazi wakiendelea na kazi kama kawaida-mwajiri akaenda kuripoti tena kituo cha Polisi urafiki kwamba wafanyakazi wanataka kuleta vujo kiwandani na matokeo yake viongozi wa wafanyakazi wakaitwa kuhojiwa na polisi.
• Mpaka tunaandika taarifa hii, bado kuna malalamiko na shutuma mbalimbali kuhusu ufinyu wa mishahara na uduni wa maslahi katika kiwanda cha nguo cha Urafiki. Kwa kuwa kiwanda hiki ni ubia kati ya serikali na mwekezaji, ni vyema suala hili likatafakariwa kwa kina ili kuepusha migogoro inayojirudiarudia.

Tuhuma za Ufisadi na/ama matumizi mabaya ya madaraka katika uuzaji na/ama ukodishaji wa nyumba za wafanyakazi:

Zipo tuhuma za ufisadi na/ama matumuzi mabaya ya madaraka katika uuzaji na/ama ukodishaji wa nyumba za wafanyakazi kama ifuatavyo:
• Uongozi wa Kitanzania ukiongozwa na Ndugu Nasoro Baraza ambae ni Naibu Meneja Mkuu na Msaidizi wake Ndugu Moses Swai unatuhumiwa kumshawishi Meneja Mkuu wa Kichina wa wakati huo Ndugu Yu Kai Ming wakaziuza nyumba za wafanyakazi. Kwanza waliwaondoa wafanyakazi kwenye nyumba hizo kwa madai nyumba hizo zinatakiwa zifanyiwe ukarabati na kwamba zingerejeshwa kwa wafanyakazi. Badala yake wafanyakazi wanatoa tuhuma nzito kwamba, nyumba hizo zilununuliwa na viongozi wenyewe na/ama familia zao kwa bei ya chini sana. Ikumbukwe kwamba awali ya yote nyumba hizo zilizopo maeneo ya Manzese zilinunuliwa kwa faida ya wafanyakazi (bonus) ili ziwasaidie wafanyakazi walio wengi. Kwa kuwa kampuni hii ni ubia kati ya serikali na mwekezaji, ni vyema ikawekwa wazi kwa umma, nyumba hizo ziliuzwa kwa kina nani na kwa bei gani.
• Kiwanda cha Urafiki kina nyumba zingine za ghorofa(urafiki flats); baadhi ya nyumba hizo kwa sasa zimefanyiwa marekebisho makubwa- hususani Block F. Lakini wafanyakazi wanalalamika kuhamishwa katika jengo hilo baada ya kukarabatiwa na sasa jengo hilo limekodishwa kwa wafanyabiashara badala ya kuwa makazi ya wafanyakazi. Ikumbukwe kwamba majengo haya yalijengwa kwa ajili ya wafanyakazi. Ikumbukwe kwamba ubia kati ya serikali na mwekezaji katika kiwanda cha Urafiki si wa biashara ya kukodisha majengo ila ni wa uzalishaji wa nguo. Lakini pia wafanyakazi wanatoa tuhuma za ziada kwamba fedha zinazotokana na kodi za majengo haya toka kwa wafanyabiashara nyingi zinaishia mikononi mwa mafisadi; hazipo wazi na kwa ukamilifu katika mahesabu ya kampuni.

MAPENDEKEZO:

Kutokana na shutuma hizo, yafuatayo yanapendekezwa:
1) Uchunguzi Huru ufanyike kuhusu shutuma hizo zinazotolewa na wafanyakazi ili kuepusha migogoro na migomo ambayo itaendelea kutokea katika kiwanda hicho.
2) Mkataba wa ubia baina ya China na Tanzania uwekwe wazi kwa wafanyakazi na wadau muhimu ili wafanyakazi waweze kuweza kujua haki zao na wadau waweze kulinda maslahi ya nchi katika ubia huo.
3) Haki za wafanyakazi wa Kiwanda cha Nguo cha Urafiki zilindwe ikiwemo kuhakikisha kuwa mishahara na maslahi yanaboreshwa.SUALA LA TATU: UFISADI-ARDHI

TUHUMA ZA UFISADI KATIKA ULIPAJI WA FIDIA KWA WAKAZI LUGURUNI

UTANGULIZI

Hivi karibuni Serikali pia iliridhia mpango wa kujenga miji midogo yenye hadhi pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam ili kupunguza idadi ya watu wanaokwenda kufuata huduma katikati ya jiji. Moja ya mji huo wa mfano ni Mradi wa Luguruni, uliopo kiasi cha kilometa 25 kutoka Dar es Salaam kuelekea Kibaha, mkoani Pwani. Eneo la Luguruni ipo ndani ya Kata ya Kibamba, Manispaa ya Kinondoni; tathmini ya kwanza ilifanyika Juni mwaka 2007.

Uamuzi huu ni wa kupongezwa na kuungwa mkono na kila mpenda demokrasia na maendeleo katika Jimbo la Ubungo na Tanzania kwa ujumla. Hata hivyo tangu serikali kuanza kuzilipa fidia familia 259 zinazohusika katika eneo hilo la mradi lenye ukubwa wa hekta 54, kumekuwepo na malalamiko mengi yaliyowahusisha watendaji wa serikali ya mtaa na kata ya Kibamba , manispaa ya Kinondoni na wizara ya Ardhi nyumba na makazi waliokuwa wasimamizi wa mradi huo. Tuhuma kadhaa za rushwa, uonevu, upendeleo na kutokuwajibika kwa viongozi hao ndiyo chanzo cha migogoro inayojirudia rudia katika eneo hilo.

TISHIO LA WANANCHI KUHAMISHWA KIMABAVU (FORCED EVICTION)

Disemba 2007 wananchi wa Jimbo la Ubungo Kata ya Kibamba eneo la Luguruni walipata tishio la kuhamishwa kimabavu. Wakazi hao waliungana na wapenda demokrasia na maendeleo kupinga kitendo cha kutaka kuwahamisha Kimabavu kutoka katika ardhi na makazi yao ambavyo wamevimiliki kihalali kwa mujibu wa sheria za nchi ya Tanzania kwa kushirikisha ngazi zote za Serikali ya Muungano wa Tanzania zikiwemo Serikali za Vijiji, Mitaa, Kata, Manispaa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi. Uamuzi wa kuwahamisha wananchi Kimabavu ni ukiukwaji mkubwa wa Sheria za Ardhi pamoja na Haki za Makazi kama zilivyoainishwa katika Sheria ya Kimataifa ya Haki za Binadamu, ambayo Tanzania imeridhia.

Kwa ujumla, vitendo vya watumishi wa Wizara Ardhi na Makazi, Halmashauri ya Jiji na Manispaa ya Kinondoni waliokabidhiwa jukumu la kutekeleza mradi huu vilipelekea utekelezaji wa mradi huu kuchukua sura ya kuhamisha watu kimabavu kutokana na kukiuka kabisa mwongozo wa uhamishaji watu kama ulivyoainishwa katika Sheria ya Kimataifa ya Haki za Binadamu na Haki za Makazi; mikataba ambayo Tanzania imeridhia.

Wakati huo, wakazi husika waliungana na wapenda haki wengine kudai yafuatayo:
• Wizara isitishe notisi ya siku 30 iliyotolewa kwa waathrika kuwa wamehama.
• Wizara husika isitishe vitendo vya kuvunja mkataba kati yake na wananchi wa Luguruni na Kibamba Hospitali uliofikiwa mwezi Febrauari 2007 kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ngazi ya wilaya eneo la Luguruni na Kibamba Hospitali kwa kutumia ardhi ya wananchi waliopo.
• Wizara husika ifanyie uchunguzi wa kina malalamiko ya ukiukwaji taratibu zilizomo ndani ya Sheria ya Ardhi na Sheria ya Kimataifa ya Haki za Binadamu na Haki za Makazi.
• Wizara husika isitishe zoezi zima la utekelezaji wa mradi huu hadi hapo tathmini itakayo washirikisha waathrika kuhusu kuepukika au kutoepukika kwa uhamishwaji watu katika utekelezaji wa mradi huu.
• Endapo baada ya tathmini shirikishi, baadhi ya kaya zingelazimika kuhamishwa, mpango kabambe ambao utakaokuwa shirikishi ulipaswa kuandaliwa kuhusu hatma ya kaya zitakazolazimika kuhamishwa. Mpango huo uandae kwa uwazi raslimali za kutosha kuwalipa fidia itakazowezesha kaya husika kurejea katika kiwango cha maisha walioyokuwa nayo kabla ya kuhamishwa.
• Wizara husika isimamie majadiliano ya pamoja kati ya watekelezaji wa mradi na waathrika kutathmini endapo zipo mbinu zinzoweza kutumika kuepuka watu wasihamishwe kutoka katika ardhi na makazi yao k.m waathrika wakaelekezwa kuwekeza katika miradi mchanganyiko na makazi kama inavyofanyika eneo la Kariakoo.

Uamuzi huu wa serikali wa kuwahamisha wananchi kimabavu ulisitishwa baada ya kuwepo kwa ishara zote za wananchi kupinga azma hiyo kwa nguvu ya umma.

TUHUMA ZA VITENDO VYA UFISADI NA/AMA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA NA/AMA UKIUKWAJI WA SHERIA KATIKA ULIPAJI WA FIDIA

Mwishoni mwa Disemba 2007, Madai ya kuwepo malipo ya fidia hewa na watu kuzidishiwa malipo yalianza kutolewa miongoni mwa wakazi na hatimaye yakafanyika mazungumzo kati ya mwakilishi wa waathrika wa mradi husika na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, yaliyofanyika siku ya Ijumaa tarehe 21 Desemba 2007 yakihusu madai hayo.

Kwa mujibu wa majibu ya Kaimu Katibu Mkuu kwa wawakilishi wa waathirika baada ya kikao cha uchunguzi kuitishwa, Kaimu Katibu Mkuu alinukuliwa akisema kuwa wizara itasimamisha malipo kwa majina yaliyowasilishwa wizarani yakidaiwa kuwa ni malipo hewa. Pia Kaimu Katibu Mkuu alinukuliwa akisema kuwa imeamuliwa kuwa uhakiki wa malipo ya fidia katika mradi huu utafanyika mara moja.

Kutokana na uamuzi huo wa wizara, matendo yafuatayo yalifuatia yaliyolenga kukwamisha azma ya wizara kuokoa fedha za serikali, kuwatambua na kuwanasa wote waliolipwa fidia isvyo halali. Vitendo hivyo ni pamoja na:-

• Waliohusika kulipwa malipo hewa kuonekana kushughulika kutafuta ardhi na majengo ya kuonyesha wakati wa zoezi la uhakiki. Hii ikashiria ya kuwa tayari wafanya uhakiki (wale wale waliohusika) wamearifiwa kufanya hivyo ili kuficha uovu.
• Uongozi na watendaji wa mradi kuonekana mara kwa mara eneo la mradi wakati wa sikukuu za krismasi na mwaka mpya wakizunguka zunguka na wanaodaiwa kulipwa malipo hewa na wanaodaiwa kuzidishiwa malipo isivyo halali.
• Meneja wa mradi kuwapigia simu na kuwatishia Ndg Selestine Michael na Mama Edgar walionekana wakitoa malalamiko yao katika kituo cha ITV kuwa watabomolewa pasipo kulipwa fidia yoyote. Vitisho hivi vilikuwa na azma ya kuzima ari ya wananchi kutoa taarifa zaidi za vitendi viovu.

Kwa mujibu wa vitendo vilivyofuatia uamuzi huo wa serikali, kuna kila sababu ya kuamini kuwa vitendo vya rushwa, malipo ya fidia hewa na baadhi watu kuzidishiwa malipo isivyo halali vilifanyika kwa ufahamu na baraka za uongozi wa mradi huu (Meneja), na ndio maana baada ya wizara kuagiza uhakiki ufanyike vitendo vya kupoteza ushahidi na kujaribu kuwanyamazisha watoa habari vilifanyika.

Sababu hizo zinakuwa na uzito zaidi kwa kuwa meneja huyu aliwaruhusu maafisa ardhi na maafisa wa kutathmini mali (Valuers) walio chini yake kuwatumia madalali wa viwanja na nyumba katika kutambua maeneo na kuthibitisha wamiliki halali badala ya kutumia Ofisi ya serikali za Mitaa. Kutumika kwa madalali badala ya ofisi ya serikali ya kulifanyika kwa nia ya kufanikisha malipo hewa kwa kuwa dalali aliyetumika anatambua mashamba na viwanja ambavyo wamiliki aidha wamefariki, kuwa nje ya nchi au kukaa muda mrefu pasipo kuhudumiwa.

Maafisa ardhi na maafisa wa kutathmini thamani ya mali waliokuwa chini ya meneja huyu walimtumia sana dalali wa viwanja aitwaye Ndugu Norbert Mtewele (Mbenna) kinyume na sheria za ardhi. Dalali huyu ni mjumbe wa shina la CCM eneo la Kibamba hospitali lakini aliweza kutumika na watekelezaji wa mradi huu hadi maeneo ya Luguruni, Msakuzi na Kibamba CCM na katika Mitaa ya Kwembe na Kiruvia kutambua maeneo na kuthibitisha uhalali wa wamiliki badala ta ofisi za serikali ya Mitaa husika.

Kama ujira wa dalali huyu, maafisa ardhi na maafisa wa kutathmini thamani ya mali wa mradi huu walimpatia dalali Morbert Mtewele malipo ya fidia katika jengo lililopo katika barabara ya zamani ya Morogoro, wafanyabiashara wengine zaidi ya 30 katika eneo hilo hilo walinyimwa fidia hiyo kwa kuwa barabarani. Aidha inadaiwa kuwa dalali huyu alipatiwa fidia inayozidi thamani ya jengo husika kwa zaidi ya mara 10. Vile vile inadaiwa kuwa watekelezaji wa mradi huu walitumia majina ya wadogo wawili wa dalali huyu kujipatia fidia isiyostahili kwa kutumia viwanja na majengo wasiyo kuwa wamiliki halali. Inakadiriwa kuwa kisai cha zaidi ya shilingi million 40 za serikali zinazotosha kujenga madarasa 5 (tano) zimepotea kwa watu hawa watatu tu. Haiwezekani mtendaji aruhusu/afanikishe/afanye malipo hewa halafu ajihakiki mwenyewe. Kwa mujibu wa uchunguzi wa kamati ya wananchi orodha ya watu waliohusika kulipwa malipo hewa na watu kulipwa zaidi kuliko wanavyostahili ni ndefu na itahusisha kiwango kikubwa sana cha fedha za serikali kupotea. Upo ushahidi unaoonyesha ya kuwa wapo watu ambao hawakuwa wakazi wa Kibamba kabisa ambao wamelipwa fidia na kutokomea na fedha za serikali isivyo halali. Na hii itathibitika tu pale uhakiki kamili utakapo fanyika na kuwabainisha wazi wazi wahusika.

MAJINA YALISHATOLEWA, SERIKALI INASUBIRI NINI KUCHUKUA HATUA?

Januari 17 mwaka 2008 palifanyika Mkutano kati ya Wakazi wa Luguruni na Waziri wa Ardhi na Makazi wa wakati huo, Mheshimiwa John Magufuli. Katika mkutano huo wa wazi Waziri Magufuli alitangaza hadharani katika viwanja vya Kibamba kuwa fedha zilizotengwa na serikali kwa fidia ni shilingi bilioni 3(Shilingi Milioni elfu tatu). Kwa hakika hizo ni pesa nyingi kutolewa na serikali, kama tu kila anayestahili angepatiwa gawio lake kwa haki. Mheshimiwa Magufuli aliendelea alitangaza kuwa hadi tarehe ile ya 17 Januari, 2008, watu 189 tayari walikuwa wamechukua fidia zao; uchunguzi unaonyesha wananchi hao walichukua fidia baadhi kwa kuridhika na wengi kwa kutokujua kama fedha walizopewa ni halali yao.

Baada ya kusomewa orodha ya majina ya watu wanaotuhumiwa kuwa wameshiriki kula rushwa au wamepinda sheria katika upimaji na ukadiriaji wa viwanja hivi, Waziri alikiri kuwa hata yeye ameridhika kuwa mpango mzima wa tathmini na ugawaji wa pesa za fidia ulikuwa “una kaharufu kasikotia shaka ka rushwa.” Na kutangaza kwamba kuwa anakabidhi makabrasha na harufu zote za rushwa kwa polisi (OCD), TAKUKURU, na watendaji wa Wizara ya ardhi ili wote watakaopatikana washughulikiwe kikamilifu; wahusika walikabidhiwa nyaraka hizo pale pale.

Leo, 14 Juni 2007 Takribani miezi mitano toka Serikali ilivyokabidhiwa Tuhuma hizi za Ufisadi; bado hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa kuhusiana na tuhuma zilozotolewa.

MAPENDEKEZO:

USHAHIDI HADHARANI, WANANCHI TUCHUKUE HATUA!

Kutokana na ukimya wa serikali katika kushughulikia suala hili na kuibuka kwa tuhuma nyingine za ziada; ni vyema suala hili sasa likarudishwa kwa umma. Kutokana na hali hiyo basi:
• Tunatoa hadharani sehemu ya ushahidi kuhusu tuhuma za ufisadi katika ulipaji wa fidia ikiwemo baadhi ya majina ya wahusika (Tazama kiambatanisho kuhusu uchambuzi wa fomu za malipo).
• Tunatoa hadharani maswali ambayo wananchi na wawakilishi wao wanapaswa kujiuliza na kuiuliza serikali kuhusu suala hili (Rejea kiambatanisho cha maswali).
• Tunarudia kusisitiza kuwa zoezi la uhakiki na ulipaji fidia halipaswa kuhusisha watendaji wale wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi na/ama upindishaji wa sheria. Na matokeo yake fedha za serikali hazitaweza kuokolewa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi, Halmashauri ya Jiji na Manispaa ya Kinondoni hazitaweza kuwabaini watendaji wanojihusiha na vitendo vya rushwa na kukiuka taratibu za utendaji kazi katika masuala ya uboreshaji makazi yasiyopimwa.
• Kutochokuliwa hatua za kinadhamu na/ama za kisheria watendaji hawa wabovu kutapelekea vitendo vya aina hii kuendelea kushamiri katika masuala yanayohusu uboreshaji makazi yasiyopimwa na fedha nyingi sana za serikali kuendelea kupotea.
• Pia uwepo wa tuhuma za ufisadi katika masuala ya ardhi na makazi kunaendeleza kufedheheshwa kwa serikali mbele ya wananchi, ambao wanatazamia kupata huduma safi kutoka kwa watumishi wa serikali badala ya kuombwa rushwa, kupunjwa malipo ya fidia kutokana na kuwepo vitendo vya malipo hewa na baadhi ya watu kuzidishiwa malipo isivyo halali. Wakati umefika wa wananchi kuchukua hatua ya kuishinikiza serikali kuleta mabadiliko.
 
Asante Mkuu Mnyika, nimeikopi naenda kuisomea nyumbani pakiwa pametulia tuli !!,
anyway, huu utaratibu utakuwa mzuri sana na naamini mtatakiwa mwende na nje ya ubungo kwa kuwa matatizo yapo sehem nyingi sana tanzania, si ubungo peke yake,
 
Yale matatizo ya kawaida ya maji, miundombinu nakadhalika mmetuachia wenyewe?
 
Kongamano la Ubungo lilifanyika, na washiriki waliazimia kufanya maandamano siku za usoni. Wameunda Kamati ya Maandalizi. Ifuatayo ni mada ambayo niliwasilisha katika kongamano hilo:

KONGAMANO LA DEMOKRASIA NA MAENDELEO JIMBO LA UBUNGO

MASUALA MATATU YA KUTAFAKARI

Na John Mnyika

USULI

Leo Jumamosi 14 Juni 2008 tumekutana hapa katika Ukumbi wa Kilato kata ya Kimara wakazi mbalimbali wa Jimbo la Ubungo kujadili kuhusu demokrasia na maendeleo katika Kongamano la Kwanza liloandaliwa na CHADEMA Jimbo la Ubungo.

Nimetakiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano nitoe mada kuhusu ajenda za WanaUbungo. Kwa ujumla ajenda za wanaUbungo ni nyingi; kama ukiamua kutazama ajenda za Fursa, basi ziko nyingi tu katika Jimbo hili lililojaliwa kuwa na Idadi kubwa ya wakazi wa kada mbalimbali; Viwanda na Vitega uchumi vikubwa; Vyuo vya pekee nchini;vyombo vya habari nk. Ukiamua kutazama Changamato basi ajenda hizo ni nyingi zaidi: ukianzia na masuala ya maji, usafiri, barabara, wafanyabiashara ndogo ndogo, umeme, mipango miji, mfumo wa utawala, uwajibikaji, ardhi, makazi, biashara ikiwemo biashara ndogo ndogo; katika kila eneo kati ya hayo niliyoyataja kuna maswali na masuala yanayoibua mjadala mzito. Naamini utaratibu huu wa kuwa na Kongamano la Demokrasia na Maendeleo unapaswa kuwa wakudumu ili walau mara moja kila mwaka upatikane wasaa wa wakazi kukusanyika pamoja kujadili fursa na changamoto mbalimbali zinazokabili jimbo la Ubungo.

Kwa leo nimechagua kuyalenga masuala matatu tu ambayo yanahitaji tafakari ya haraka; tukiunganisha nguvu za pamoja kuyashughulikia masuala hayo, basi harakati za mabadiliko zitakuwa zimeanza. Mafanikio ya kuunganisha nguvu katika masuala haya matatu yatachochea harakati pana zaidi za mabadiliko zenye kuhusisha kuongeza elimu ya uraia na kuchochea uwajibikaji katika ngazi mbalimbali kuanzia kwenye mitaa, kwenye halmashauri na hatimaye taifa.

. Wakati umefika wa wananchi kuchukua hatua ya kuishinikiza serikali kuleta mabadiliko.

Si niliwaambia! Wachochezi hawa. Ameacha mambo ya miundo mbinu, barabara nk karukia masuala ya Richmond, Urafiki na Kibamba! Wameachochea wananchi mpaka wanataka kuandamana. Sasa serikali ifuatilie hayo maandamano. Maana juzi kwenye kongamano lao waliazimia kuandamana kwenda Dowans, Urafiki na TANESCO ambavyo vyote ofisi zake zipo jimbo la Ubungo.

PM
 
Hivi wewe Mnyika shule utaenda lini?

Niliwahi kuwadokeza hapa miezi kadhaa nyuma kuwa tayari huyu mtoto alishawaandikia viongozi wake barua kuwa anaachana na uongozi na kwenda kusoma. Habari kutoka ndani zinasema ametaja kabisa tarehe ya kuondoka kwake. Bado naifuatilia hiyo barua yake ambayo inesemekana watu wa karibu na Chacha Wangwe wamempelekea Rostam Aziz. Kwani si mnakumbuka lile bandiko langu hapa kwamba Zitto na Mnyika kumsusia Mbowe CHADEMA?

PM
 
WATANZANIA wote wana wajibu wa kuyajua,kuyafafanua na kuyasema matatizo yanayotukabili.tuwaze kwa pamoja jinsi ya kuyatatua...keep it up ndugu yangu Mnyika.
 
Hivi wewe Mnyika shule utaenda lini?

Masatu Hayakuhusu.!!!

Kwani Mnyika kurudi shule ndo itatatua matatizo yanayoikabili jamii ya Ubungo ama ni moyo wake wa Kimapinduzi na Utanzania wake?

Kaka Mnyika tunashukuru kwa Changamoto hii na tupo pamoja katika mapambano.

Mpaka kieleweke!
 
Hivi wewe Mnyika shule utaenda lini?

While this may be feigned as a genuine or even benevolent concern , I sense it is a direct and deliberate distraction by those who cannot and maybe do not have a rebuttal for the issues presented.

Make no mistake about my commitment to the value of education, I am fully committed.However, much too often certification in the so called formal education is mistaken for "education".One of the best U.S Presidents, Harry S. Truman, never had a college degree.President Truman rose through the ranks from a local judge in Independence Missouri, to a Senator, to the Vice Presidency and eventually to be president.Although he could not finish night school (law), his life experience, ranging from farming ,fighting in WW1, small business ventures to public service gave him a perspective that many a giant like the patrician East Coast baron Roosevelt - posh, born with a golden spoon in his mouth, Ivy League educated, the works- lacked.

I am not certain about Mr. Mnyika's "formal education" achievements and goals .I know the education he is receiving from the political process -indeed many a time giving- is of a more practical nature than a dry, theoretical, Political Science degree from a University.

Should Mr. Mnyika choose to further immerse himself in public service, his party manifesto and commitment to the issues, personal record and competence in dealing with the issues - rather than his formal education- shall prove to be more of a deciding factor on whether he will get my endorsement or not.

We are witnessing a debacle in leadership, not because we do not have enough Ivy League educated bureaucrats -Look at Chenge (Harvard) Lowassa (Bath) Prof. Malima (Princeton) Prof. Mbilinyi (Cornell, Stanford) the list is endless- They all failed not because they do not have fancy formal education, but they failed to change a dilapidated system from within.

We need more practical education, bright people - I know Mr. Mnyika to be one-, innovative ideas and downsized egos.

Can you for a moment address the issues presented and not distract?

A bright person will show, degree or no degree, Ivy League or no Ivy League.

Go ahead with your bad self Mnyika.
 
Kongamano la Ubungo lilifanyika, na washiriki waliazimia kufanya maandamano siku za usoni. Wameunda Kamati ya Maandalizi. Ifuatayo ni mada ambayo niliwasilisha katika kongamano hilo:

KONGAMANO LA DEMOKRASIA NA MAENDELEO JIMBO LA UBUNGO

MASUALA MATATU YA KUTAFAKARI

Na John Mnyika

USULI

Leo Jumamosi 14 Juni 2008 tumekutana hapa katika Ukumbi wa Kilato kata ya Kimara wakazi mbalimbali wa Jimbo la Ubungo kujadili kuhusu demokrasia na maendeleo katika Kongamano la Kwanza liloandaliwa na CHADEMA Jimbo la Ubungo.

Nimetakiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano nitoe mada kuhusu ajenda za WanaUbungo. Kwa ujumla ajenda za wanaUbungo ni nyingi; kama ukiamua kutazama ajenda za Fursa, basi ziko nyingi tu katika Jimbo hili lililojaliwa kuwa na Idadi kubwa ya wakazi wa kada mbalimbali; Viwanda na Vitega uchumi vikubwa; Vyuo vya pekee nchini;vyombo vya habari nk. Ukiamua kutazama Changamato basi ajenda hizo ni nyingi zaidi: ukianzia na masuala ya maji, usafiri, barabara, wafanyabiashara ndogo ndogo, umeme, mipango miji, mfumo wa utawala, uwajibikaji, ardhi, makazi, biashara ikiwemo biashara ndogo ndogo; katika kila eneo kati ya hayo niliyoyataja kuna maswali na masuala yanayoibua mjadala mzito. Naamini utaratibu huu wa kuwa na Kongamano la Demokrasia na Maendeleo unapaswa kuwa wakudumu ili walau mara moja kila mwaka upatikane wasaa wa wakazi kukusanyika pamoja kujadili fursa na changamoto mbalimbali zinazokabili jimbo la Ubungo.

Kwa leo nimechagua kuyalenga masuala matatu tu ambayo yanahitaji tafakari ya haraka; tukiunganisha nguvu za pamoja kuyashughulikia masuala hayo, basi harakati za mabadiliko zitakuwa zimeanza. Mafanikio ya kuunganisha nguvu katika masuala haya matatu yatachochea harakati pana zaidi za mabadiliko zenye kuhusisha kuongeza elimu ya uraia na kuchochea uwajibikaji katika ngazi mbalimbali kuanzia kwenye mitaa, kwenye halmashauri na hatimaye taifa.

SUALA LA KWANZA: HATMA YA RICHMOND/DOWANS

“NI WAKATI WA KUCHUKUA HATUA”

UTANGULIZI:
Februari 6 mwaka 2008 Kamati Teule ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoundwa tarehe 13 Novemba, 2007 iliwasilisha taarifa yake bungeni. Kamati hiyo iliundwa kuchunguza mchakato wa Zabuni ya Uzalishaji umeme wa dharura ulioipa ushindi Richmond Development Company LLC ya Houston, Texas Marekani mwaka 2006.

Kutokana na uchunguzi wa kina ulioanishwa katika taarifa ya Kamati Teule, Bunge lilijulishwa kuwa mchakato wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura wa MW 100, uliopelekea Richmond Development Company LLC kuteuliwa na hivyo kusaini mkataba na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tarehe 23 Juni 2006 na baadaye kurithiwa na Dowans Holdings S.A tarehe 23 Desemba 2006, uligubikwa na vitendo vya ukiukwaji taratibu, kanuni na sheria za nchi na hivyo kujenga kiwingu cha mashaka ya upendeleo, ubadhirifu na rushwa ambavyo vimechangia kumuongezea mwananchi mzigo wa gharama za umeme.

Aidha, Kamati Teule ilithibitisha kuwa uteuzi wa Kampuni dhaifu kifedha, kiufundi na kiuzoefu na ambayo haina usajili Marekani wala Tanzania kama kampuni yenye ukomo wa hisa, yaani Richmond Development Company LLC, ulitokana na kubebwa na viongozi waandamizi wa Serikali.

Kamati hiyo ilibaini mapungufu makubwa na kamati ilitoa mapendezo mbalimbali na kutoa maelekezo kwa serikali kuhakikisha yanatekelezw; Baadaye Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliunda Kamati ya kusimamia utekelezaji huo.

Leo Juni 14, 2008 takribani miezi minne imepita toka Kamati iwasilishe taarifa yake Bungeni. Baadhi ya mapendekezo ya msingi yaliyomo kwenye kamati hayakuhitaji muda mrefu kiasi hiki kuweza kutekelezwa lakini mpaka hivi sasa serikali iko kimya kuhusu utekelezaji wake. Ni wakati wa kuyatafakari tena mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge na maazimio ya Bunge baada ya mapendekezo hayo.

WANANACHI TUTANGAZE WAZI KUWA HAKUNA MKATABA KATI YETU NA RICHMOND/DOWANS:

Kamati tuele iliweka bayana kuwa, Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC ulikuwa wa uzalishaji umeme wa dharura kipindi ambacho nchi ilikuwa katika hali ngumu ya ukame uliokausha mabwawa yote ya kuzalishia umeme. Kamati Teule iliitaka Serikali kutathmini upya uhalali wa kuwepo na kuendelea kuwepo na mkataba huo kutokana na udanganyifu bayana uliofanywa na Richmond Development Company LLC kuhusu uwezo wake kifedha, kiufundi, na uzoefu wake katika masuala ya uzalishaji umeme; usajili na uwepo wake kisheria kama kampuni halali yenye ukomo wa hisa nchini Marekani na Tanzania; uhusiano wake kisheria na Kampuni kubwa ya Kimataifa ya Pratt & Whitney na utambulisho wa Mzungu mmoja kwa jina la John Perun kama mwakilishi wa Pratt & Whitney, mambo ambayo Kampuni hiyo kubwa ya Kimataifa imeyakanusha vikali.

Kamati Teule ilishuhudia bei za mitambo hiyo jijini Houston, Texas Marekani kwa watengenezaji kiwandani ikiwemo kampuni ya Kawasaki Gas Turbines – Americas ambayo iko chini ikilinganishwa na bei zinazotolewa na mawakala hao, jambo ambalo lingeiwezesha Serikali kununua na kumiliki badala ya kukodi kwa muda mfupi na kwa gharama kubwa. Mathalan, MW 105 zingepatikana kwa kununua mitambo sita ya MW 17,5 kila mmoja kwa gharama ya shilingi bilioni 56.25 badala ya shilingi bilioni 108.7 tulizotandikwa na Richmond Development Company LLC mitambo hiyo ikibaki mali ya wakodishaji. Kamati Teule ilithibitisha kwamba kauli iliyokuwa inatolewa mara kwa mara na baadhi ya viongozi wote tuliowahoji kwamba kipindi hicho cha ukame haikuwa rahisi kupata mitambo hiyo na ilikuwa ikigombaniwa na nchi nyingi kauli hiyo ilikuwa sio ya ukweli na upotoshaji mkubwa.

Ilielezwa kuwa Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC na sasa Dowans Holdings S.A, kama ilivyo mikataba kati ya TANESCO na IPTL, SONGAS, AGGREKO na Alstom Power Rentals inatoa unafuu usiostahili kwa makampuni hayo ya umeme na kuiumiza TANESCO na hatimaye watumiaji na walipa kodi kimapato, k.m mikataba hiyo kuwa na vipengele vya kuibana TANESCO kuyalipia makampuni hayo kodi zinazohusika na uendeshaji (operations), matengenezo/marekebisho ya mara kwa mara ya mitambo (maintenance) gharama za bima, ada za mawakili na washauri elekezi (consultants) gharama za mafuta na gesi ya kuendeshea mitambo, gharama za ukodishaji mitambo (capacity charges) ambazo TANESCO hulipa kila mwezi si chini ya wastani wa shilingi bilioni 2 kwa kila kampuni, izalishe au isizalishe umeme. Kamati Teule ilitoa rai kwa Serikali kuwa mikataba yote hii ipitiwe upya mapema iwezekanavyo kama ambavyo mikataba ya madini inavyopitiwa upya sasa na Serikali. Bila kufanya hivyo, mzigo mkubwa wa gharama za umeme utawaelemea wananchi. Lakini mpaka sasa serikali imeendelea kuutambua mkataba huu kwa niaba ya watanzania, miezi minne baada ya pendekezo hili. Ni wakati wa wananchi kuungana pamoja kutamka wazi kwamba hatuutambui mkataba huo; kwa kuwa umeingiwa na wawakilishi wetu kwa hila la bila ridhaa yetu. Hivyo, ni vyema mitambo yao ikaondolewa katika Jimbo la Ubungo.

TUSHINIKIZE MALIPO YA MILIONI 152 KWA SIKU KWA DOWANS YASITISHWE MARA MOJA; FEDHA ZILIZOLIPWA MPAKA SASA ZIREJESHWE.

Kamati Tuele ilieleza bayana kuwa, Madhumuni ya Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC yalikuwa kuzalisha umeme wa dharura kwa kipindi cha miezi kumi na mbili (12) tu. Muda huo ungeweza kuongezwa baada ya kutathmini hali ya ongezeko la maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme nchini. Kabla ya muda wa tathmini hiyo haujafikiwa, wakati majadiliano yakiendelea GNT ikaongezea Richmond Development Company LLC muda wa kukodi mitambo hiyo kuwa miaka miwili (2). Kamati Teule haikuona vielelezo vyovyote vilivyojenga uhalali kwa GNT kuongeza muda huo. Uamuzi huo umeliongezea Taifa mzigo mkubwa wa gharama zisizokuwa za lazima. Mathalan, kwa upande wa capacity charges tu, TANESCO itailipa Dowans Holdings S.A jumla ya shilingi bilioni 54.8 kwa kipindi kilichongezwa cha mwaka mmoja. Aidha, GNT ilishindwa kutambua ulaghai wa Richmond Development Company LLC kuhusu mwakilishi wa Pratt & Whitney na hivyo kuamini karatasi ambayo ilikuwa haijathibitishwa na mawakili na diskette zenye picha za mitambo ya Pratt & Whitney, vielelezo ambavyo Kamati Teule iligundua na kuthibitisha kuwa vilikuwa vya kugushi. Vilevile, bila kujali kwamba TANESCO ingelezimika kuilipa Richmond Development Company LLC shilingi milioni 152 kwa siku kama gharama ya kuweka vifaa vyao nchini, GNT ikakubali kilegelege kuitoza Richmond Development Company LLC shilingi milioni 12 tu kwa siku kama fidia kwa ucheleweshaji wa kuanza kuzalisha umeme kulingana na tarehe iliyokubalika kwenye mkataba. Tunasikitika kwamba hata baada ya kuelezwa mambo yote hayo, serikali bado imeendelea kuilipa kampuni ya DOWANS kiasi cha fedha sawa na takribani milioni 152 kila siku. Hivyo tunataka serikali iache kutumia vibaya fedha zetu na isitishe malipo hayo mara moja na kudai fedha zilizolipwa mpaka sasa zirejeshwe.

MIKATABA IWEKWE WAZI KWA WANANCHI WA ENEO AMBALO MRADI/UWEKEZAJI UNAFANYIKA ILI KUJUA HAKI NA WAJIBU WAO:

Kamati tuele ilipendekeza wazi kuwa; Utaratibu tuliourithi kutoka kwa wakoloni na kuuzoea wa kuiona mikataba ya kibiashara kuwa ni siri hata kwa walipa kodi wenyewe na kuwa uwanja wa pekee wa watendaji, ambao Waziri wa Mipango Uchumi na Uwezeshaji Mhe. Dk Juma Ngasongwa (Mb) aliusifia bungeni tarehe 19 Aprili 2007 kuwa best practice wakati akijibu swali la Mhe. Masolwa C. Masolwa (Mb) Mbunge wa Bububu, umepitwa na wakati na unakiuka misingi ya demokrasia na uwajibikaji. Matokeo ya utaratibu huu ni kuwepo kwa mikataba mibovu inayoficha vipengele vinavyoibebesha Taifa mizigo mikubwa ya gharama zisizokuwa za lazima. Wakati umefika sasa wa wananchi wa eneo husika kudai kuonyeshwa mikataba ya kibiashara ya maeneo yao ili kujua haki na wajibu wao. Mathalani, kuna malalamiko ya wakazi wa Jimbo la Ubungo wanaoishi karibu na mitambo ya Richmond/Dowans kuhusu masuala ya joto, mionzi na kelele zinazotokana na mitambo hiyo. Wananchi hao wanalalamikia kuwa waliahidiwa kulipwa fidia na kuondolewa katika maeneo ya jirani na mitambo hiyo. Maswali ya kujiuliza; Je, tathmini kamili ya madhara katika mazingira(EIA) ilifanyika kikamilifu kabla ya mradi huo? Je, suala la wananchi kulipwa fidia lilikuwa sehemu ya mkataba? Kama mkataba huu ungekuwa wazi mapema ikiwemo kwa wananchi wa jimbo la Ubungo, ni wazi kuwa wananachi wangeelewa haki na wajibu wao katika mkataba husika.

SERIKALI IACHE KUIGOPA TAKUKURU, ICHUKUE HATUA YA KUBADILI UONGOZI WA TAASISI HIYO

Taarifa ya Kamati Teule ilidhihirisha wazi jinsi Taifa lilivyotumbukizwa kwenye hasara kubwa kutokana na mkataba huo wa Richmond Development Company LLC na Dowans Holdings S.A, kinyume na taarifa iliyotolewa na TAKUKURU (wakati huo TAKURU) kwamba Taifa halikupata hasara yoyote. Taarifa ya TAKUKURU ililenga kuficha ukweli (white wash) hivyo ikaishia kujikanganya kwa kukiri kuwepo kwa mapungufu lakini yasiyokuwa na athari. Taarifa hiyo imemong’onyoa kwa kiasi kiasi kikubwa hadhi na heshima ya chombo hiki muhimu cha kitaifa kilichopewa dhamana ya kupambana na rushwa na sio kuipamba ili kurejesha heshima ya umma katika taasisi hiyo. Kamati teule ilipendekeza mabadiliko ya haraka ya uongozi wa taasisi hiyo. Mpaka sasa mabadiliko hayo hayajafanyika, na Mkurugenzi wa TAKUKURU ameendelea kuwa Edward Hosea ambaye ametuhumiwa hadharani kwa kuigeuza TAKUKURU kuwa Taasisi ya kulinda na kutetea rushwa. Ni wakati wa wananchi kutaka serikali iache kuigopa TAKUKURU na kuchukua hatua za haraka za kubadili uongozi wa Taasisi hiyo.MWAKAPUGI, MRINDOKO NA WATENDAJI VINARA WACHUKULIWE HATUA HARAKA

Kamati Teule iliainisha katika taarifa yake vitendo vya ubabe, ujeuri na kiburi vilivyofanywa na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini alimradi kampuni waliyoitaka iteuliwe kiasi cha kupindisha hata maamuzi ya Baraza la Mawaziri bila wasiwasi wowote, kukaidi ushauri wa kitaalamu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma mara tatu mfululizo na kinyume na maagizo ya Baraza la Mawaziri lililotaka Sheria ya Ununuzi wa Umma izingatiwe, kukiuka sheria kwa makusudi kwa kuingilia mchakato wa zabuni wa taasisi nyingine ya ununuzi, kuvipuuza vyombo vya ndani vya maamuzi vya TANESCO (Bodi ya Wakurugenzi, Bodi ya Zabuni n.k), kuilazimisha Bodi na Menejimenti ya TANESCO kuridhia maamuzi yaliyofanywa na Wizara ya kuibeba Richmond Development Company LLC kinyume cha sheria na taratibu n.k. Wizara hiyo katika kuibeba Richmond Development Company LLC ilifikia hatua ya kupotosha kwa makusudi ushauri wa Wizara ya Fedha uliozuia malipo ya awali ya Dola za Kimarekani Milioni 10 katika Barua ya Dhamana ya Benki ya Richmond Development company LLC. Kamati Teule ilipendekeza kwamba Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo Mhe. Dk. Ibrahim Msabaha (Mb) na Katibu Mkuu Ndugu Arthur Mwakapugi wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza Taifa kwa makusudi kwenye mkataba na kampuni ya mfukoni ambao umesababisha hasara kubwa kwa nchi. Aidha Kamishna wa Nishati Ndugu Bashir Mrindoko naye ilipendekezwa achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu mpya wa Wizara kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC ambao ulijulikana dhahiri na Wizara toka mwaka 2004 kwenye mkataba wa Bomba la Mafuta. Ndugu Mrindoko ndiye aliyeiandikia barua kampuni hiyo kusitisha mkataba wake na Serikali mwezi mmoja tu kabla ya mchakato wa zabuni ya umeme wa dharura haujaanza. Wakati umefika wa wananchi kuitaka serikali kuwachukulia hatua za kinadhamu Mwakapugi, Mrindoko kama ilivyopendezwa na Kamati teule. Katika hali ya kawaida ya uwajibikaji, ilitarajiwa Rais Jakaya Kikwete, mara baada ya Waziri Mkuu Pinda kuunda Kamati ya kusimamia utekelezaji wa maazimio ya Bunge kutokana na Taarifa ya Kamati Teule; angewachukulia hatua wateule wake, hususani makatibu wakuu waliohusika na kashfa hii kwa kuwasimamisha kazi wakati wote ambapo kamati inatafakari hatua za kinadhamu zinazopaswa kuchukuliwa.

MAPENDEKEZO:

Ni wakati wa wananchi kuchukua hatua. Kwa kuwa makao makuu ya TANESCO yako jimbo la Ubungo; na kwa kuwa Kampuni ya Richmond ilikuwa Ubungo; Na kwa kuwa Kampuni ya Dowans iko Jimbo la Ubungo. Ni wakati wa wakazi wa Ubungo kwa niaba ya watanzania wengine, kujiunga pamoja chini ya ‘falsafa ya nguvu ya umma’; kuiwajibisha serikali kutekeleza mapendekezo ya Kamati Tuele ya Bunge mapema iwezekanavyo.SUALA LA PILI: HAKI ZA WAFANYAKAZI

“SHUTUMA ZA WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA NGUO URAFIKI”

UTANGULIZI

Kiwanda cha nguo cha Urafiki kiliingia ubia na kati ya Tanzania na China mwaka 1997. Wakati wachina wanaingia ubia katika kiwanda hicho, kiwanda hilikuwa kinafanya kazi kiwanda kizima kikiwa na vinu vitatu. Mashine zote zilikuwa zikifanya kazi na kwa ujumla wafanyakazi; kwa ujumla kiwanda kilikuwa kinafanya kazi shifti tatu kwa siku. Lakini mara baada ya ubia huo, pamejitokeza malalamiko mengi ya Wafanyakazi kwa zaidi ya miaka kumi ambayo mara nyingine yamesababisha migomo na kutoelewana.

SHUTUMA ZINAZOTOLEWA

Kupunguzwa kwa mashine za uzalishaji

Wafanyakazi wanatoa shutuma kwamba, walipoanza kazi wachina hawakuchukua muda mrefu wakafunga kinu namba mbili kwa kuua sehemu ya usokotaji na kubaki sehemu ya ufumaji pekee. Kinu hiki kilifungwa kwa madai kwamba mashine za kisasa zingeletwa, mpaka wakati wa kuandikwa kwa taarifa hii kinu hicho hakijaletwa. Zipo tuhuma kwamba kinu hiki kilichoondolewa kimeuzwa kama vyuma chakavu. Pamoja na kuathirika kwa uzalishaji, matokeo ya kufungwa kwa kinu hiki ni wafanyakazi kupunguzwa. Mara baada ya wafanyakazi wengine kupunguzwa, palitolewa ahadi na kiwanda kwamba mishahara na maslahi ya wafanyakazi waliobaki ingeboreshwa, ahadi ambayo mpaka leo haijatekelezwa. Wafanyakazi waliitisha migomo kuhusu suala hili, Waziri wa Viwanda na Biashara wa wakati huo, Juma Ngasongwa alifika katika kiwanda na kuzomewa na wafanyakazi. Kutokana na hali hiyo Waziri alitoa amri mfanyakazi huyo akakamatwa na hatimaye akafukuzwa kazi. Waziri Mkuu wa wakati huo, Fredrick Sumaye, naye alitembelea mara kadhaa katika kiwanda hicho lakini hakuweza kushughulikia kikamilifu shutuma zilizotolewa.Mishahara finyu na maslahi duni kwa Wafanyakazi

Wafanyakazi wanatoa shutuma kwamba toka kiwanda kiingie ubia mishahara na maslahi ya wafanyakazi havijaboreshwa kwa mujibu wa matarajio yaliyotolewa na wabia. Wafanyakazi wa Kiwanda hiki wamelalamika kwa zaidi ya miaka kumi kuhusu kunyonywa na kunyanyaswa, malalamiko yao yapo serikalini na baadhi yamefikishwa mahakamani. Hata hivyo serikali haijayapatia ufumbuzi malalamiko hayo na kesi zilizoko mahamani zinaendelea kuahirishwa na kuchukua muda mrefu. Baadhi ya mambo yanayolalamikiwa na wafanyakazi ni kuhusu ufinyu wa mishahara na uduni wa maslahi ni pamoja na:
• Kwa miaka kumi wamehangaika mahakamani kuhusu suala la kupunjwa kwa mishahara yao, wafanyakazi wanataka ufumbuzi wa kesi upatikane mapema.
• Kukatwa posho zao za likizo kwa miaka tisa bila kupewa fedha wala likizo; baada ya mihangaiko mengi iliamuliwe walipwe fedha hizo. Hata hivyo mwajiri amemua kuwalipa fedha hizo kwa kulazimisha wafanyakazi walipwe kama mavazi badala ya kupewa fedha taslimu. Baadhi ya wafanyakazi kwa unyonge wamechukua nguo, waliokataa hawajapewa fedha zao mpaka leo.
• Septemba 2007 Serikali kupitia kwa Waziri wa Kazi wa wakati huo, Mheshimiwa Chiligati ilitangaza kima cha chini ya mishahara ya sekta binafsi cha shilingi 150,000 toka 48,000 baada ya kupokea mapendekezo toka kwa bodi inayohusika. Baadhi ya bidhaa/huduma zikapanda bei baada ya tangazo hilo la kupanda kwa mishahara. Lakini ilipofika mwezi Oktoba siku chache kabla ya tarehe ya utekelezaji wa agizo hilo, Waziri alitangaza kuahirisha utekelezaji wa tangazo hilo hadi Januari 2008.
• Matokeo ya tangazo la serikali la kima cha chini kuwa shilingi laki unusu kwa upande mwingine ni baadhi ya waajiri kupunguza wafanyakazi licha ya tangazo la serikali kukataza kufanya hivyo. Kwa upande wa Kiwanda cha Urafiki wafanyakazi wanalalamika kuwa wenzao 725 walipunguzwa, wengi hao ni vijana waliokuwa wakifanya kazi kama vibarua wa muda mrefu(japo sheria ya kazi inakataza vibarua wa muda mrefu).
• Baadaye Waziri Chiligati akatangaza kwamba baada ya mazungumzo na Shirikisho la Wenye viwanda Tanzania(CTI) kwamba wameomba msamaha wa kulipa 80,000 badala ya 150,000 kama kima cha chini; na kubadilisha vigezo vya awali vilivyopendekezwa na bodi. Kauli hii ilikinzana na kauli ambayo Rais Kikwete aliitoa mwishoni mwa mwaka 2007 alipotembelea Kiwanda cha Mafuta Kurasini kwamba “ifikapo Januari 2008, walipeni wafanyakazi walau shilingi laki na hamsini kama kima cha chini”.
• Mnamo tarehe 24 Januari, 2008 Wafanyakazi wa Kiwanda cha Urafiki chini ya ulinzi mkali wa polisi walipewa barua ya mishahara mipya. Na ilipofika 25 Januari, 2008 Wafanyakazi walipewa mshahara mpya wa shilingi 80,000; wakati wafanyakazi wakiendelea na kazi kama kawaida-mwajiri akaenda kuripoti tena kituo cha Polisi urafiki kwamba wafanyakazi wanataka kuleta vujo kiwandani na matokeo yake viongozi wa wafanyakazi wakaitwa kuhojiwa na polisi.
• Mpaka tunaandika taarifa hii, bado kuna malalamiko na shutuma mbalimbali kuhusu ufinyu wa mishahara na uduni wa maslahi katika kiwanda cha nguo cha Urafiki. Kwa kuwa kiwanda hiki ni ubia kati ya serikali na mwekezaji, ni vyema suala hili likatafakariwa kwa kina ili kuepusha migogoro inayojirudiarudia.

Tuhuma za Ufisadi na/ama matumizi mabaya ya madaraka katika uuzaji na/ama ukodishaji wa nyumba za wafanyakazi:

Zipo tuhuma za ufisadi na/ama matumuzi mabaya ya madaraka katika uuzaji na/ama ukodishaji wa nyumba za wafanyakazi kama ifuatavyo:
• Uongozi wa Kitanzania ukiongozwa na Ndugu Nasoro Baraza ambae ni Naibu Meneja Mkuu na Msaidizi wake Ndugu Moses Swai unatuhumiwa kumshawishi Meneja Mkuu wa Kichina wa wakati huo Ndugu Yu Kai Ming wakaziuza nyumba za wafanyakazi. Kwanza waliwaondoa wafanyakazi kwenye nyumba hizo kwa madai nyumba hizo zinatakiwa zifanyiwe ukarabati na kwamba zingerejeshwa kwa wafanyakazi. Badala yake wafanyakazi wanatoa tuhuma nzito kwamba, nyumba hizo zilununuliwa na viongozi wenyewe na/ama familia zao kwa bei ya chini sana. Ikumbukwe kwamba awali ya yote nyumba hizo zilizopo maeneo ya Manzese zilinunuliwa kwa faida ya wafanyakazi (bonus) ili ziwasaidie wafanyakazi walio wengi. Kwa kuwa kampuni hii ni ubia kati ya serikali na mwekezaji, ni vyema ikawekwa wazi kwa umma, nyumba hizo ziliuzwa kwa kina nani na kwa bei gani.
• Kiwanda cha Urafiki kina nyumba zingine za ghorofa(urafiki flats); baadhi ya nyumba hizo kwa sasa zimefanyiwa marekebisho makubwa- hususani Block F. Lakini wafanyakazi wanalalamika kuhamishwa katika jengo hilo baada ya kukarabatiwa na sasa jengo hilo limekodishwa kwa wafanyabiashara badala ya kuwa makazi ya wafanyakazi. Ikumbukwe kwamba majengo haya yalijengwa kwa ajili ya wafanyakazi. Ikumbukwe kwamba ubia kati ya serikali na mwekezaji katika kiwanda cha Urafiki si wa biashara ya kukodisha majengo ila ni wa uzalishaji wa nguo. Lakini pia wafanyakazi wanatoa tuhuma za ziada kwamba fedha zinazotokana na kodi za majengo haya toka kwa wafanyabiashara nyingi zinaishia mikononi mwa mafisadi; hazipo wazi na kwa ukamilifu katika mahesabu ya kampuni.

MAPENDEKEZO:

Kutokana na shutuma hizo, yafuatayo yanapendekezwa:
1) Uchunguzi Huru ufanyike kuhusu shutuma hizo zinazotolewa na wafanyakazi ili kuepusha migogoro na migomo ambayo itaendelea kutokea katika kiwanda hicho.
2) Mkataba wa ubia baina ya China na Tanzania uwekwe wazi kwa wafanyakazi na wadau muhimu ili wafanyakazi waweze kuweza kujua haki zao na wadau waweze kulinda maslahi ya nchi katika ubia huo.
3) Haki za wafanyakazi wa Kiwanda cha Nguo cha Urafiki zilindwe ikiwemo kuhakikisha kuwa mishahara na maslahi yanaboreshwa.SUALA LA TATU: UFISADI-ARDHI

TUHUMA ZA UFISADI KATIKA ULIPAJI WA FIDIA KWA WAKAZI LUGURUNI

UTANGULIZI

Hivi karibuni Serikali pia iliridhia mpango wa kujenga miji midogo yenye hadhi pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam ili kupunguza idadi ya watu wanaokwenda kufuata huduma katikati ya jiji. Moja ya mji huo wa mfano ni Mradi wa Luguruni, uliopo kiasi cha kilometa 25 kutoka Dar es Salaam kuelekea Kibaha, mkoani Pwani. Eneo la Luguruni ipo ndani ya Kata ya Kibamba, Manispaa ya Kinondoni; tathmini ya kwanza ilifanyika Juni mwaka 2007.

Uamuzi huu ni wa kupongezwa na kuungwa mkono na kila mpenda demokrasia na maendeleo katika Jimbo la Ubungo na Tanzania kwa ujumla. Hata hivyo tangu serikali kuanza kuzilipa fidia familia 259 zinazohusika katika eneo hilo la mradi lenye ukubwa wa hekta 54, kumekuwepo na malalamiko mengi yaliyowahusisha watendaji wa serikali ya mtaa na kata ya Kibamba , manispaa ya Kinondoni na wizara ya Ardhi nyumba na makazi waliokuwa wasimamizi wa mradi huo. Tuhuma kadhaa za rushwa, uonevu, upendeleo na kutokuwajibika kwa viongozi hao ndiyo chanzo cha migogoro inayojirudia rudia katika eneo hilo.

TISHIO LA WANANCHI KUHAMISHWA KIMABAVU (FORCED EVICTION)

Disemba 2007 wananchi wa Jimbo la Ubungo Kata ya Kibamba eneo la Luguruni walipata tishio la kuhamishwa kimabavu. Wakazi hao waliungana na wapenda demokrasia na maendeleo kupinga kitendo cha kutaka kuwahamisha Kimabavu kutoka katika ardhi na makazi yao ambavyo wamevimiliki kihalali kwa mujibu wa sheria za nchi ya Tanzania kwa kushirikisha ngazi zote za Serikali ya Muungano wa Tanzania zikiwemo Serikali za Vijiji, Mitaa, Kata, Manispaa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi. Uamuzi wa kuwahamisha wananchi Kimabavu ni ukiukwaji mkubwa wa Sheria za Ardhi pamoja na Haki za Makazi kama zilivyoainishwa katika Sheria ya Kimataifa ya Haki za Binadamu, ambayo Tanzania imeridhia.

Kwa ujumla, vitendo vya watumishi wa Wizara Ardhi na Makazi, Halmashauri ya Jiji na Manispaa ya Kinondoni waliokabidhiwa jukumu la kutekeleza mradi huu vilipelekea utekelezaji wa mradi huu kuchukua sura ya kuhamisha watu kimabavu kutokana na kukiuka kabisa mwongozo wa uhamishaji watu kama ulivyoainishwa katika Sheria ya Kimataifa ya Haki za Binadamu na Haki za Makazi; mikataba ambayo Tanzania imeridhia.

Wakati huo, wakazi husika waliungana na wapenda haki wengine kudai yafuatayo:
• Wizara isitishe notisi ya siku 30 iliyotolewa kwa waathrika kuwa wamehama.
• Wizara husika isitishe vitendo vya kuvunja mkataba kati yake na wananchi wa Luguruni na Kibamba Hospitali uliofikiwa mwezi Febrauari 2007 kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ngazi ya wilaya eneo la Luguruni na Kibamba Hospitali kwa kutumia ardhi ya wananchi waliopo.
• Wizara husika ifanyie uchunguzi wa kina malalamiko ya ukiukwaji taratibu zilizomo ndani ya Sheria ya Ardhi na Sheria ya Kimataifa ya Haki za Binadamu na Haki za Makazi.
• Wizara husika isitishe zoezi zima la utekelezaji wa mradi huu hadi hapo tathmini itakayo washirikisha waathrika kuhusu kuepukika au kutoepukika kwa uhamishwaji watu katika utekelezaji wa mradi huu.
• Endapo baada ya tathmini shirikishi, baadhi ya kaya zingelazimika kuhamishwa, mpango kabambe ambao utakaokuwa shirikishi ulipaswa kuandaliwa kuhusu hatma ya kaya zitakazolazimika kuhamishwa. Mpango huo uandae kwa uwazi raslimali za kutosha kuwalipa fidia itakazowezesha kaya husika kurejea katika kiwango cha maisha walioyokuwa nayo kabla ya kuhamishwa.
• Wizara husika isimamie majadiliano ya pamoja kati ya watekelezaji wa mradi na waathrika kutathmini endapo zipo mbinu zinzoweza kutumika kuepuka watu wasihamishwe kutoka katika ardhi na makazi yao k.m waathrika wakaelekezwa kuwekeza katika miradi mchanganyiko na makazi kama inavyofanyika eneo la Kariakoo.

Uamuzi huu wa serikali wa kuwahamisha wananchi kimabavu ulisitishwa baada ya kuwepo kwa ishara zote za wananchi kupinga azma hiyo kwa nguvu ya umma.

TUHUMA ZA VITENDO VYA UFISADI NA/AMA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA NA/AMA UKIUKWAJI WA SHERIA KATIKA ULIPAJI WA FIDIA

Mwishoni mwa Disemba 2007, Madai ya kuwepo malipo ya fidia hewa na watu kuzidishiwa malipo yalianza kutolewa miongoni mwa wakazi na hatimaye yakafanyika mazungumzo kati ya mwakilishi wa waathrika wa mradi husika na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, yaliyofanyika siku ya Ijumaa tarehe 21 Desemba 2007 yakihusu madai hayo.

Kwa mujibu wa majibu ya Kaimu Katibu Mkuu kwa wawakilishi wa waathirika baada ya kikao cha uchunguzi kuitishwa, Kaimu Katibu Mkuu alinukuliwa akisema kuwa wizara itasimamisha malipo kwa majina yaliyowasilishwa wizarani yakidaiwa kuwa ni malipo hewa. Pia Kaimu Katibu Mkuu alinukuliwa akisema kuwa imeamuliwa kuwa uhakiki wa malipo ya fidia katika mradi huu utafanyika mara moja.

Kutokana na uamuzi huo wa wizara, matendo yafuatayo yalifuatia yaliyolenga kukwamisha azma ya wizara kuokoa fedha za serikali, kuwatambua na kuwanasa wote waliolipwa fidia isvyo halali. Vitendo hivyo ni pamoja na:-

• Waliohusika kulipwa malipo hewa kuonekana kushughulika kutafuta ardhi na majengo ya kuonyesha wakati wa zoezi la uhakiki. Hii ikashiria ya kuwa tayari wafanya uhakiki (wale wale waliohusika) wamearifiwa kufanya hivyo ili kuficha uovu.
• Uongozi na watendaji wa mradi kuonekana mara kwa mara eneo la mradi wakati wa sikukuu za krismasi na mwaka mpya wakizunguka zunguka na wanaodaiwa kulipwa malipo hewa na wanaodaiwa kuzidishiwa malipo isivyo halali.
• Meneja wa mradi kuwapigia simu na kuwatishia Ndg Selestine Michael na Mama Edgar walionekana wakitoa malalamiko yao katika kituo cha ITV kuwa watabomolewa pasipo kulipwa fidia yoyote. Vitisho hivi vilikuwa na azma ya kuzima ari ya wananchi kutoa taarifa zaidi za vitendi viovu.

Kwa mujibu wa vitendo vilivyofuatia uamuzi huo wa serikali, kuna kila sababu ya kuamini kuwa vitendo vya rushwa, malipo ya fidia hewa na baadhi watu kuzidishiwa malipo isivyo halali vilifanyika kwa ufahamu na baraka za uongozi wa mradi huu (Meneja), na ndio maana baada ya wizara kuagiza uhakiki ufanyike vitendo vya kupoteza ushahidi na kujaribu kuwanyamazisha watoa habari vilifanyika.

Sababu hizo zinakuwa na uzito zaidi kwa kuwa meneja huyu aliwaruhusu maafisa ardhi na maafisa wa kutathmini mali (Valuers) walio chini yake kuwatumia madalali wa viwanja na nyumba katika kutambua maeneo na kuthibitisha wamiliki halali badala ya kutumia Ofisi ya serikali za Mitaa. Kutumika kwa madalali badala ya ofisi ya serikali ya kulifanyika kwa nia ya kufanikisha malipo hewa kwa kuwa dalali aliyetumika anatambua mashamba na viwanja ambavyo wamiliki aidha wamefariki, kuwa nje ya nchi au kukaa muda mrefu pasipo kuhudumiwa.

Maafisa ardhi na maafisa wa kutathmini thamani ya mali waliokuwa chini ya meneja huyu walimtumia sana dalali wa viwanja aitwaye Ndugu Norbert Mtewele (Mbenna) kinyume na sheria za ardhi. Dalali huyu ni mjumbe wa shina la CCM eneo la Kibamba hospitali lakini aliweza kutumika na watekelezaji wa mradi huu hadi maeneo ya Luguruni, Msakuzi na Kibamba CCM na katika Mitaa ya Kwembe na Kiruvia kutambua maeneo na kuthibitisha uhalali wa wamiliki badala ta ofisi za serikali ya Mitaa husika.

Kama ujira wa dalali huyu, maafisa ardhi na maafisa wa kutathmini thamani ya mali wa mradi huu walimpatia dalali Morbert Mtewele malipo ya fidia katika jengo lililopo katika barabara ya zamani ya Morogoro, wafanyabiashara wengine zaidi ya 30 katika eneo hilo hilo walinyimwa fidia hiyo kwa kuwa barabarani. Aidha inadaiwa kuwa dalali huyu alipatiwa fidia inayozidi thamani ya jengo husika kwa zaidi ya mara 10. Vile vile inadaiwa kuwa watekelezaji wa mradi huu walitumia majina ya wadogo wawili wa dalali huyu kujipatia fidia isiyostahili kwa kutumia viwanja na majengo wasiyo kuwa wamiliki halali. Inakadiriwa kuwa kisai cha zaidi ya shilingi million 40 za serikali zinazotosha kujenga madarasa 5 (tano) zimepotea kwa watu hawa watatu tu. Haiwezekani mtendaji aruhusu/afanikishe/afanye malipo hewa halafu ajihakiki mwenyewe. Kwa mujibu wa uchunguzi wa kamati ya wananchi orodha ya watu waliohusika kulipwa malipo hewa na watu kulipwa zaidi kuliko wanavyostahili ni ndefu na itahusisha kiwango kikubwa sana cha fedha za serikali kupotea. Upo ushahidi unaoonyesha ya kuwa wapo watu ambao hawakuwa wakazi wa Kibamba kabisa ambao wamelipwa fidia na kutokomea na fedha za serikali isivyo halali. Na hii itathibitika tu pale uhakiki kamili utakapo fanyika na kuwabainisha wazi wazi wahusika.

MAJINA YALISHATOLEWA, SERIKALI INASUBIRI NINI KUCHUKUA HATUA?

Januari 17 mwaka 2008 palifanyika Mkutano kati ya Wakazi wa Luguruni na Waziri wa Ardhi na Makazi wa wakati huo, Mheshimiwa John Magufuli. Katika mkutano huo wa wazi Waziri Magufuli alitangaza hadharani katika viwanja vya Kibamba kuwa fedha zilizotengwa na serikali kwa fidia ni shilingi bilioni 3(Shilingi Milioni elfu tatu). Kwa hakika hizo ni pesa nyingi kutolewa na serikali, kama tu kila anayestahili angepatiwa gawio lake kwa haki. Mheshimiwa Magufuli aliendelea alitangaza kuwa hadi tarehe ile ya 17 Januari, 2008, watu 189 tayari walikuwa wamechukua fidia zao; uchunguzi unaonyesha wananchi hao walichukua fidia baadhi kwa kuridhika na wengi kwa kutokujua kama fedha walizopewa ni halali yao.

Baada ya kusomewa orodha ya majina ya watu wanaotuhumiwa kuwa wameshiriki kula rushwa au wamepinda sheria katika upimaji na ukadiriaji wa viwanja hivi, Waziri alikiri kuwa hata yeye ameridhika kuwa mpango mzima wa tathmini na ugawaji wa pesa za fidia ulikuwa “una kaharufu kasikotia shaka ka rushwa.” Na kutangaza kwamba kuwa anakabidhi makabrasha na harufu zote za rushwa kwa polisi (OCD), TAKUKURU, na watendaji wa Wizara ya ardhi ili wote watakaopatikana washughulikiwe kikamilifu; wahusika walikabidhiwa nyaraka hizo pale pale.

Leo, 14 Juni 2007 Takribani miezi mitano toka Serikali ilivyokabidhiwa Tuhuma hizi za Ufisadi; bado hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa kuhusiana na tuhuma zilozotolewa.

MAPENDEKEZO:

USHAHIDI HADHARANI, WANANCHI TUCHUKUE HATUA!

Kutokana na ukimya wa serikali katika kushughulikia suala hili na kuibuka kwa tuhuma nyingine za ziada; ni vyema suala hili sasa likarudishwa kwa umma. Kutokana na hali hiyo basi:
• Tunatoa hadharani sehemu ya ushahidi kuhusu tuhuma za ufisadi katika ulipaji wa fidia ikiwemo baadhi ya majina ya wahusika (Tazama kiambatanisho kuhusu uchambuzi wa fomu za malipo).
• Tunatoa hadharani maswali ambayo wananchi na wawakilishi wao wanapaswa kujiuliza na kuiuliza serikali kuhusu suala hili (Rejea kiambatanisho cha maswali).
• Tunarudia kusisitiza kuwa zoezi la uhakiki na ulipaji fidia halipaswa kuhusisha watendaji wale wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi na/ama upindishaji wa sheria. Na matokeo yake fedha za serikali hazitaweza kuokolewa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi, Halmashauri ya Jiji na Manispaa ya Kinondoni hazitaweza kuwabaini watendaji wanojihusiha na vitendo vya rushwa na kukiuka taratibu za utendaji kazi katika masuala ya uboreshaji makazi yasiyopimwa.
• Kutochokuliwa hatua za kinadhamu na/ama za kisheria watendaji hawa wabovu kutapelekea vitendo vya aina hii kuendelea kushamiri katika masuala yanayohusu uboreshaji makazi yasiyopimwa na fedha nyingi sana za serikali kuendelea kupotea.
• Pia uwepo wa tuhuma za ufisadi katika masuala ya ardhi na makazi kunaendeleza kufedheheshwa kwa serikali mbele ya wananchi, ambao wanatazamia kupata huduma safi kutoka kwa watumishi wa serikali badala ya kuombwa rushwa, kupunjwa malipo ya fidia kutokana na kuwepo vitendo vya malipo hewa na baadhi ya watu kuzidishiwa malipo isivyo halali. Wakati umefika wa wananchi kuchukua hatua ya kuishinikiza serikali kuleta mabadiliko.

Habari nilizozipata toka kwa waandishi wenzangu ni kwamba baada ya uchochezi mwingi uliofanyika serikali imeamua kufanya uthamini upya. Na sasa uthamini utafanyika huku kukiwa na polisi wa kulinda usalama. Na mwananchi atayekataa ataondolewa bila fidia yoyote. Waziri Chiligati tayari ameshatoa maelekezo yote.

PM
 
Mnyika shule lini ?? wewe kila siku ubungo, ubungo.... tumekusika ! Na sidhani kama kuna jipya utakaloleta kuhusiana na ubungo !
 
Kada unafanya kazi nzuri sana humu hasa unapotumia jina la masaka. Kila huyu dogo anapotoa hoja zake huwa unakuja wakati muafaka kugeuza hoja kwa kuanzisha suala lingine. Keep it up. Huyu mtoto ni mchochezi tu. Ona sasa wananchi wa Luguruni Kibamba wanavyoshinikizwa kusaini fomu za kukubali kulipwa fidia. Serikali haitaki hata kuwaambia itawalipa bei gani kwa kiwanja. Mambo yote kimya kimya.

PM
 
Ni wakati wa kuisogelea ile mitambo pale. Labda wahusika watachukuliwa hatua mapema zaidi na fedha zitarudishwa kwa watanzania

JJ
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom