Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,904
13,660
Na; Mwandishi Wetu - DODOMA

BUNGE limepitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria za Hifadhi ya Jamii wa Mwaka 2024 wenye mambo kadhaa yanayolenga kuondoa changamoto zinazowakabili wanachama na utaratibu wa upatikanaji wa mafao.
IMG-20240829-WA0032.jpg

Marekebisho hayo yanagusa Sheria tatu ambazo ni Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, Sura ya 50, Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, Sura ya 371, na Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, Sura ya 263.

Akiwasilisha maelezo ya muswada huo bungeni Agosti 29, 2024, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema marekebisho hayo yanatokana na nia ya dhati ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutatua changamoto ikiwamo mkwamo wanaoupata watumishi wanapostaafu.

Pia, amesema muswada huo umelenga kutatua suala la wastaafu hao kukutana na kizingiti cha Waajiri kutowasilisha michango kwa wakati kwenda kwenye Mifuko na kuongeza makusanyo.

“Pia unalenga kuondoa changamoto ya uonevu wakati wa kuwapatia haki wafanyakazi wanaoumia makazini na anayepaswa kutoa taarifa anaposhindwa kutoa taarifa ndani ya muda; malipo yasiyo ya lazima na kulinda watumishi katika stahiki zao; kwa Waajiri kuwapa ulinzi wa taarifa, na kuwajengea mazingira wachangie na kuwapa nafuu katika malipo,”amesema.

Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq amesema kamati inakubaliana na marekebisho hayo yaliyopo kwenye muswada huo.

Ameshauri serikali iimarishe Mifumo ya TEHAMA ili wanachama wapate taarifa za michango yao kutoka kwa waajiri kila mwezi kwenye simu zao za kiganjani ili kuondoa tatizo la wanachama kutolipwa mafao kwa wakati kutokana na kutopelekwa kwa michango yao kwenye mifuko.
 
Kwani anyeyafanya hayo ni nani
 
Bunge limepitisha muswada wa marekebisho ya sheria za hifadhi ya jamii wa mwaka 2024 kuhusu utaratibu wa upatikanaji wa mafao kwa watumishi wa kada mbalimbali.

Marekebisho hayo ambayo yamegusa sura ya 50 ya Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, Sura ya 371 ya Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma na Sura ya 263 ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi yamepitishwa leo Agosti 29, 2024 Bungeni jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa mapema hii leo Bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete.

“Marekebisho haya yanatokana na nia ya dhati ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutatua changamoto za watumishi pindi wanapostaafu” amesema Kikwete.

Kabla ya maelezo hayo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Fatuma Toufiq amesema kamati inakubaliana na marekebisho hayo yaliyopo kwenye muswada huo.
 
nadhani kuna mabadiliko mengine yanatakiwa hasa katika FAO la kukosa ajira. Sheria inasema Aliyeachishwa kazi atalipwa theluthi moja ya mshahara aliokua analipwa kabla ya kuachishwa Kazi kwa miezi sita tu. Ni bora akaendelea kulipwa mpaka atakapopata Kazi, au salio la michango litakapokwisha
 
Kuna hili jambo Wabunge hawalioni na kulijadili: Kimahesabu hili ndilo lilipunguza mafao ya Wastaafu:
Katika formula: waliweka 1/580 badala ya 1/540; pia wakaweka 12.5 badala ya 15.5...
Tangia hapo kikokotoo kimekuwa kero!
 
Na; Mwandishi Wetu - DODOMA

BUNGE limepitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria za Hifadhi ya Jamii wa Mwaka 2024 wenye mambo kadhaa yanayolenga kuondoa changamoto zinazowakabili wanachama na utaratibu wa upatikanaji wa mafao.
View attachment 3082252
Marekebisho hayo yanagusa Sheria tatu ambazo ni Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, Sura ya 50, Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, Sura ya 371, na Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, Sura ya 263.

Akiwasilisha maelezo ya muswada huo bungeni Agosti 29, 2024, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema marekebisho hayo yanatokana na nia ya dhati ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutatua changamoto ikiwamo mkwamo wanaoupata watumishi wanapostaafu.

Pia, amesema muswada huo umelenga kutatua suala la wastaafu hao kukutana na kizingiti cha Waajiri kutowasilisha michango kwa wakati kwenda kwenye Mifuko na kuongeza makusanyo.

“Pia unalenga kuondoa changamoto ya uonevu wakati wa kuwapatia haki wafanyakazi wanaoumia makazini na anayepaswa kutoa taarifa anaposhindwa kutoa taarifa ndani ya muda; malipo yasiyo ya lazima na kulinda watumishi katika stahiki zao; kwa Waajiri kuwapa ulinzi wa taarifa, na kuwajengea mazingira wachangie na kuwapa nafuu katika malipo,”amesema.

Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq amesema kamati inakubaliana na marekebisho hayo yaliyopo kwenye muswada huo.

Ameshauri serikali iimarishe Mifumo ya TEHAMA ili wanachama wapate taarifa za michango yao kutoka kwa waajiri kila mwezi kwenye simu zao za kiganjani ili kuondoa tatizo la wanachama kutolipwa mafao kwa wakati kutokana na kutopelekwa kwa michango yao kwenye mifuko.
Huyo mwenyekiti wa kamati inamaana hana taarifa kua tayari kuna psssf na nssf kiganjani kutazama kichango yako? Niaibu kuishauri serikali jambo ambalo tayari limefanyika kwenye mifuko husika Inaonesha kutokua serious na kazi wanahoifanya hiyo kamati, wafanyakazi wanahitaji kusikia maboresho kwenye fao lakujitoa na asilimia ya kiinua mgongo kupanda na hii mifuko kuacha kufanya uwekezaji usiokua nantija kwenye miradi isiyolipa nakuhatarisha michango ya wanachama
 
Kuna hili jambo Wabunge hawalioni na kulijadili: Kimahesabu hili ndilo lilipunguza mafao ya Wastaafu:
Katika formula: waliweka 1/580 badala ya 1/540; pia wakaweka 12.5 badala ya 15.5...
Tangia hapo kikokotoo kimekuwa kero!
Hawawezi kuona kwakua wao hawahusiki na hili ila nisehemu yakula michango toka kwenye hii mifuko
 
Back
Top Bottom