Why Kigamboni? Nikiangalia Resources zinazokwenda hapo sipati justification.
La swali la msingi, tunataka kufanya Land Reclamation Tanzania? Kwa nini?
Na kama hatuhitaji, kwa nini mlienda kujifunza?
Kuna case moja ya TZ na mikaratusi Australia nayo ilikuwa hivi hivi
Lakini mh. Kwanini mumeshindwa kuboresha huu mji tulionao sasa hivi na munaanza kutafuta mpya wakati bado hamjachelewa? Tunahitaji tuone mabadiliko hapa tulipo sasa, Hizi sheria ndogondogo za miji zinafanya kazi?
Mtu kuweka maeneo ya mjini vibanda, parking ziko ndani ya barabara ukipita maeneo yote ya mjini sehemu za kupita watu na magari zimepakiwa gari na barabara inakua finyu. Majumba mjini yamekua kama magovu je hakuna sheria ya kuwaagiza wamiliki kuyarekebisha kila kipindi inapofika?
Suala la msingi ni Waziri anakusudia kupata nini kutokana na hiki alichokiandika?
Yeye ndiye msimamizi wa ardhi yote ya Tanzania. Kama sheria hazifuatwi, hakuna nidhamu, kuna matani na mchezo ndio maana miji yetu iko chaotic, anataka sisi tufanyaje wakati yeye mwenye madaraka makubwa zaidi kwenye suala hilo ukiacha rais ameshindwa kuonyesha lolote?
Kwa nini anataka kutubebesha lawama Watanzania na anaacha kuchukua yeye lawama ya kushindwa kufanya kazi zake kwa ufanisi stahiki?
Majibu ya matatizo mengi ya Tanzania yamo humu humu nchini. Ujenzi holela unaendelea mbele ya viongozi wetu waliozeoa kukaa ndani ya mashangingi wakifurahia viyoyozi. Hakuna michoro, sijui safari ya kujifunza nje au hata mbiu za uwekeji zitakazo tatua ujenzi holela kama walio kwenye ngazi za kusimamia sheria wataendelea kuwa bubu.
Kinadharia, sipingi hoja ya mama Tibajiuka, ila najiuliza tatizo ni mipango miji? Kwa upande mwingine mama Tibajiuka anaweza kuondoka kwenye hii wizara ya ardhi bila legacy ya kueleweka. So far sijaona mchango/mageuzi wa maana japo amekuwa anaongea mambo makubwa! amepatwa na nini?
Mkuu naona umesahau kuwa vichwa vya nchi vinakutana hapa JF? mama amekuja kupata mawazo toka kwa Great Thinkers halafu tena unauliza swali kama hilo hapo kwa red!
Mama Anna Tibaijuka,
Nakushauri kuwa Serikali ijitowe katika huu mradi na iwawachie "real estate developers" wa Kimataifa, wenye uzoefu wa hizi kazi.
Serikali yetu haina uzoefu wa hizi kazi na historia inatuonesha Serikali imeshindwa ku-manage mradi wowote wa maana wa kibiashara. Hata NHC inawashinda ni uozo mtupu, ilhali majumba yalikuwa ya kudhulumiwa watu.
Ikiwa Serikali imeshindwa kuendesha viwanda vya umma, leo itaweza kuendesha project ya "magnitude" ya jiji? Jiulize.
Tusipoteze wakati, tuwawachie wenye utaalaam, na uzoefu wafanye haya mambo, wazo ni zuri, watendaji hatuna, tuna wizi tu Tanzania.
Leo ni zaidi ya miaka 6 tunasikia hii lelemama ikiimbwa tu, hebu ondoeni ukiritimba muwape wenye uwezo, kama hamjui pa kuwapata mnaweza wasiliana na mimi kwa PM.
Hii habari ya mji wa Kigamboni mbona maneno mengi vitendo sifuri? Yaani mpaka sasa ndio tupo kwenye hatua ya kuahidiwa kusaidiwa na watu wa Singapore! Je, ni aina gani ya msaada tunayotaka? What was our plan kabla wasingapore hawajaahidi kutusaidia? What are the timelines of implementation?
Hili nalo ni la msingi, anataka kupata nini kwa sred hii. Na kitu kidogo kama jengo limemsumbua kusimamia utekelezaji, vipi kuhusu mpango/project kubwa kama hii yenye wadau wengi zaidi?
Lakini mie bado najiuliza, kwa nini walienda kujifunza hii reclamation?
kilimo kwanza imefia wapi?WanaJF
Nilikuwa mmojawapo wa viongozi tulioandamana na Mhe Rais katika ziara yake ya majuzi nchini Singapore. Ninawaletea sehemu ya Master Plan ya mji wao mpya unaojengwa kutokana na kuokoa ardhi baharini (reclamation). Unaona kila kipande cha ardhi mpya kimeshapangiwa matumizi yake na kuwekewa malengo ya majengo yanayotakiwa.
Kupanga ni kuchagua. Kunahitaji nidhamu na hakuna mchezo wala utani. Huwezi kuwa na mji uliopangwa kama unapenda na kuendekeza uholela na vurugu (chaos). Kinachotakiwa ni kushirikisha wadau wote kupanga malengo na viwango baada ya kupata maoni ya wataalam. Wanaoarithirika na kulazimisha kuhama kupisha maendelezo mapya wanalipw fidia stahiki na endelevu.
Anayedai vinginevyo si msema kweli. WaSingapore wamehaidi kutusaidia katika ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni. Ninakaribisha maoni yenu hasa nyie mlio nje na mnaishi katika miji iliyopangwa? Je uholela unavumiliwa au kuendekezwa? Tupe habari.
View attachment 97055
Mama Tibaijuka
na hii ndio plani ya miji ya Tanzania, sasa mama kwa nini angalau usiunde vikosi jamii kwenye kila kata kama mfano inavyoanzishwa vikundi vya polisi jamii vitavyohakikisha kuwa kila kiwanja kina access the barabara na kuweka kipimo cha chini cha kiwanja. hamuwezi kukaa mnajivunia miji ya wenzenu huku yakwetu inazidi kuhabirika