Master Nabi anabaki kuwa mmoja tu, arudii makosa mara mbili, kawaonyesha Rivers leo

Mtanzanias

JF-Expert Member
Jul 30, 2021
1,747
3,723
Kocha Nasridine Nabi ni kocha wa viwango, ni kocha asiyetabirika, ni kocha master sana wa kuusoma mchezo na kumalizia kazi yake kwa uweledi mkubwa, Leo kaingia uwanja wa Uyo na back 3 akijua rivers watakuja kwa kasi sana kwenye goli la yanga kutafuta mabao hivyo akaweka viungo wa shoka, baada ya kucheza dk 45 za kwanza na kuusoma vizuri mchezo akabadili mbinu na kucheza 4;4;2 ili timu isogee mbele kushambulia kwa kasi na imemlipa kwa 100%

Ni mechi ya kwanza kwa Rivers kupoteza kwenye uwanja wake wa nyumbani tokea 2013, matokeo mabaya kwao huwa ni sare ya magoli na sio vinginevyo, Whydad kafa pale goli 2, Asec mimosas kafa pale goli 3, diable noirs kadroo goli 2 kwa 2, ivyo Sio timu ya kubeza ata kidogo, lakini wamekutana na kisiki cha mpingo Master Nabi pamoja na ubora wa kikosi cha wananchi, Mpaka hapo walipofikia Yanga sina cha kuwadai, wamefanya mambo muhimu kwa muda muafaka,

Wamewaheshimu wapinzani wakiwa ugenini na wamefanikiwa kwa 100%, Nawaona yanga wakiendelea kufanikiwa zaidi na zaidi,

Najua wale mashabiki na vijana wa Rage watakuja kukumbushia matokeo ya Simba na yanga kuwa kwanini akufanikiwa kushinda lakini nawajibu hapa hapa ya kwamba kipindi cha pili kilikuwaje? Aliweka mbinu zake na tatizo likawa kwenye wachezaji wenyewe kukosa nafasi,

Nabi bado ataendelea kuwa moja ya makocha bora na wasiotabirika kirahisi jambo linalowaumiza vichwa makocha wengi namna bora ya kukabiliana na yanga hii, Yanga kushinda mechi 3 za ugenini sio masikhara, inahitaji uwe vizuri kuanzia benchi lako la ufundi, wachezaji, viongozi na mshikamano wa wanachama na mashabiki wote kiujumla kwa maana mpira wa kiafrika unajulikana ni figisu juu ya figisu kwaiyo unapotoboa kupata matokeo unakuwa umefanya kazi ya ziada

Ongereni yanga, ongereni viongozi na tunawatakieni kila la kheri🙌🙌🙌
 
K-Vant Sometimes Sio Nzuri Hasa Kwa Vijana Wanaochipukia Na Wenye Miandiko Kama Hii...

Anywayz Haya Ni Mawazo Mawazo....

Comma

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 
fbbae943-eb4f-4795-a7e2-de7b5032a42e.jpg

Tumeumbwa kusahau
Samahani lkn
 
Zuwena fc wametepeta wanalia ovyo nawaona bado wako kijiweni wanajadili imekuwaje Yanga kutia mguu nusu fainali Shirikisho na wao kuumaliza mwendo kwa kukandwa week huko Morocco, ijumaa si mbali panapo uhai! Maana usiku wa deni hauchelewi kuisha!

sidhani kama Hakimi fc watakuja kwenye huu Uzi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom