Masoud Kipanya Uhuru Umezidi Mipaka

Masoud Kipanya Uhuru Umezidi Mipaka

Una maadili ya kufikiri isivyotakiwa
Maadili, ni kuzidhibiti na kujizuia kufanya yasiyofaa...
Lazima kwanza uwe na hekima, busara na weledi wa kujua kipi kinafaa na kipi hakifai....
Bila hivyo utakuwa unaropoka tu..kuwa makini.
 
Ndio nilichosema Haswa. Hakuna tusi.
Unajua Wabongo wanapenda matusi ndiyo maana maneno yote ya kiswahili fasaha kwao ni matusi. Juzi nilikuta ugomvi mtaani eti jamaa kamwambia mwenzake 'kakanyagwa' kwa vile wote ni wahuni walianza kupigana kwa madai kuwa amemtusi. Yapo maneno mengi ambayo wameyaharibia maana ili kukidhi haja yao ya kutusi
 
Shida hapa kwa masoud ni kwamba ukifupisha utapata neno UKU. MA au ni ujumbe uliomo sijaelewa
 
Maadili, ni kuzidhibiti na kujizuia kufanya yasiyofaa...
Lazima kwanza uwe na hekima, busara na weledi wa kujua kipi kinafaa na kipi hakifai....
Bila hivyo utakuwa unaropoka tu..kuwa makini.
Maadili pia ni kuamini mwenzako analofanya, ni kwa nia njema. Sio kumlisha fikra zako na kuamini katika tafsiri zako tu.
 
Shida hapa kwa masoud ni kwamba ukifupisha utapata neno UKU. MA au ni ujumbe uliomo sijaelewa
Hayo ni matakwa yako kwani Abbreviations za maneno zinategemea na mtazamo wako . Mimi nimeona UKM au hicho nacho si kifupi? CHAMA CHA MAPINDUZI Kifupi chake ni CCM lakini pia wangesema CM, CHACHAMA au CHAMA kama wangependa
 
... lakini akipewa discipline kuna wapuuzi watasema demokrasia inavunjwa ... Hii nchi acha tupelekane kibabe walimchezea sana JK.
We ndiyo mpuuzi, yeye kaandika kwa uhuru. Usifupishe maneno hayo kwa jinsi akili yako inavyotaka. Mi kwangu ni UKM, UMOKMA, UKUM, UKUSM, UKUSMA, UMOSM, UMOSUM, UKUSUPMA, N.K. sasa we fikiria ki""K"" hivo hivo. Hata akili ndogo ya kindergarten huna. Kiwango cha usanii cha KP ni cha PHD.
 
View attachment 387395
Huyu ni mtu mbaya sana ata kama ni uhuru wa vyombo vya habari hii ni too much. Hiyo katuni alikua anamaanisha nini!! si ni matusi kabisa haya. Huwezi fanya uhuni kwenye gazeti kubwa kama mwananchi tena kwa kutaka kufupisha kitu ili liwe tusi na jina la Rais likiwemo hapo hapo.

Huyu mtu ni jipu ashauriwe kufanya kazi kwa weledi wataaluma yake aache kuleta uhuni wa kijiweni kwenye magazeti.
Hahahahaaaa.. Ukum.a. Ila nadhani ni mawazo yetu tu. Uvccm walisema wanaandamana kumpongeza Magufuli. Kwa sababu wao ni umoja ni kweli sasa ni Umoja wa KUmpongeza MAgufuli
 
Hahahahaaaa.. Ukum.a. Ila nadhani ni mawazo yetu tu. Uvccm walisema wanaandamana kumpongeza Magufuli. Kwa sababu wao ni umoja ni kweli sasa ni Umoja wa KUmpongeza MAgufuli
Wabongo kwa matusi mmejaaliwa. Hivi ukienda Ghana ule mji ambao uko mkoa wa AShanti si utasema WAGHANA wanatukana. Kule Japan kuna mji ambao kwa kiswahili na waswahili kama nyie mtasema tusi. hivi kiongozi akienda kutembelea ule mji wa Japan ambao uko kaskazini na magazeti yetu ya karipoti mngesema yametukana.? Acheni fikra mgando. Precision air walikuwa au wanae maana sijui habari zake kwa sasa RUBAN wao mmoja Mkenya jina lake siwezi hata kuliandika hapa maana kwa kiswahili linafanana na haja kubwa lakini kwao lina maana nyingine kabisa
 
Kwani Katuni ina shida gani hiyo? Mbona iko poa matusi lbd utukane ww, hebu fupisha tuone km ni matusi kweli
 
Wabongo kwa matusi mmejaaliwa. Hivi ukienda Ghana ule mji mkuu wake si utasema WAGHANA wanatukana. Kule Japan kuna mji ambao kwa kiswahili na waswahili kama nyie mtasema tusi. hivi kiongozi akienda kutembelea ule mji wa Japan ambao uko kaskazini na magazeti yetu ya karipoti mngesema yametukana.? Acheni fikra mgando. Precision air walikuwa au wanae maana sijui habari zake kwa sasa RUBAN wao mmoja Mkenya jina lake siwezi hata kuliandika hapa maana kwa kiswahili linafanana na haja kubwa lakini kwao lina maana nyingine kabisa
Mji mkuu wa Ghana ni Accra nadhani siyo tusi ila kwa Japan kuna KUMAMOTO UNIVERSITY. rejea kumamoto university - Google Search
 
Sorry Nilimaanisha Mji ule ambao uko Mkoa wa Ashanti KUMASI. Unajua tena zama za mwendokasi hata chai ilijkuwa haijapita
Tena sio university tu hilo jina ndilo linatumika kama Wilaya au kama wenyewe wanavyoita
KUMAMOTO Prefecture
 
View attachment 387395
Huyu ni mtu mbaya sana ata kama ni uhuru wa vyombo vya habari hii ni too much. Hiyo katuni alikua anamaanisha nini!! si ni matusi kabisa haya. Huwezi fanya uhuni kwenye gazeti kubwa kama mwananchi tena kwa kutaka kufupisha kitu ili liwe tusi na jina la Rais likiwemo hapo hapo.

Huyu mtu ni jipu ashauriwe kufanya kazi kwa weledi wataaluma yake aache kuleta uhuni wa kijiweni kwenye magazeti.

Ni kiswahili fasaha kabisa, wala si tusi. Blame your dirty mind
 
Back
Top Bottom