Maskini Wambura...

Katika kijiji cha Matare wilaya ya
Mugumu Serengeti, bwana
Wambura alikamatwa kwa kesi ya
kusingiziwa na kuhukumiwa kwenda
jela miaka mitatu.
Huku nyuma akiacha mke na
watoto wanne waliokuwa
wanasoma. Hukumu hiyo ilimtesa
sana kichwa chake, alitamani kila
mtu anayemhisi kuwa ana makosa
aingie katika moyo wake na
kuupata ukweli.
Alilia na umaskini wake, lambda
angepata wakili mzuri angeweza
kumtetea, kumkosa wakili
kukahalalisha kifungo hicho!!
Alikwenda gerezani huku akiumia
sana rohoni. Aliyaanza maisha
mapya kwa shida sana, akawa
mnyonge kila mara na mwili
ukapoteza afya kiujumla.
Huko gerezani alifanikiwa kupata
rafiki aliyekuwa na cheo ama
jukumu la uzikaji wa wafungwa
hasahasa ambao hawakuwa na
ndugu ama ambao ndugu zao huwa
hawajitokezi pale gerezani.
Mzikaji alijaribu sana kumtia nguvu
Wambura na kumwaminisha kuwa
hiyo ilikuwa hatua tu ya maisha
anapaswa kuizoea na siku moja
ukweli utajulikana tu! Bwana
Wambura maneno ya mzikaji
hayakumuingia kabisa.. alizidi
kunyong’onyea.
“Siwezi kuvumilia kukaa gerezani
miaka mitatu…..kama unajali kilio
changu nisaidie nitoroke kwa
namna yoyote ile ndugu yangu!!”
Wambura alimsihi mzikaji.
SIKU MOJA mzikaji akamwambia
Wambura kuwa msaada
umepatikana. Lakini yataka moyo!!
“Nipo tayari kwa lolote ilimradi tu
nitoke humu!!” alijibu kwa msisitizo
huku akimtegea sikio mzikaji.
“Msaada pekee wa kukutorosha
humu ndani ni kwa njia ya jeneza…
yaani mfungwa akifa mimi
nakuunganisha naye kwenye
jenerza…..” akashusha pumzi kisha
akaendelea “Wewe ukisikia kengere
ya msiba, njoo mara moja kwenye
chumba cha maiti, utakuta tayari
sanduku liko katikati ya chumba
linakuwa halijafungwa, funua
kifunioko ingia ndani yake ulale
pembeni ya maiti kwani sanduku
huwa kubwa la kutosha kila aina ya
maiti na hata miili miwili inaingia.
Kisha nitakuja na kulipigilia
misumari. Baada ya muda
tutalipakia kwenye gari na kutoka
kwenda nje ya gereza makaburini
nikiongozana na baadhi ya
wafungwa na maaskari magereza.
Tutakuzika huko lakini baada ya
dakika 20 hadi 30 nitarudi
kukufukua. Hautaweza kushindwa
kupumua kwa dakika hizo, utatoka
ukiwa huru.”
JAPOKUWA wazo lilikuwa zuri lakini
lilimtisha sana Wambura. Hata
hivyo akaona afadhali afanye hivyo
kuliko kukaa gerezani miaka mitatu
bila kosa.
Siku moja akasikia kengere ya
msiba. Akafanya kama
alivyoelekezwa na mzikaji. Akaenda
na kuingia chumba cha maiti. Kweli
akalikuta sanduku, akiwa na hofu
kuu akaingia na kulala pembeni ya
maiti iliyokuwepo. Mara akasikia
mtu ameingia na kulipigilia
msumari sanduku. Muda mfupi
baadaye sanduku likainuliwa na
kuwekwa kwenye gari.
Gari ikatoka nje ya gereza hadi
makaburini. Sanduku likashushwa
na kuwekwa kaburini na kuanza
kufukiwa.
Wambura alijitahidi sana kuvumilia
japo hofu ilizidi kutanda.
Alimtegemea sana mzikaji na
alianza kumuona mkombozi wa
maisha yake.
Kama alivyoambiwa, akasubiri
dakika kumi, ishirini.. zikapita
kimya!!
Dakika thelathini kimya. Joto nalo
likazidi kuongezeka.
“Nitavumilia hadi afike…”
alijisemea kisha akajiongezea kauli
ya ujasiri.
“Kama nilitakiwa kuishi gerezani
miaka mitatu kivipi dakika kadhaa
za hapa kaburini”
KWA kuwa alishakaa gerezani kwa
muda kiasi akatamani kujua
aliyekufa ni nani… ni kwewli
aliogopa kuitazama maiti lakini
aliona kama inatisha zaidi ikiwa
imefunikwa vile kuliko ikiwa wazi.
Akaifunua upande wa usoni… Kwa
kuwa kulikuwa na giza nene
alikodoa sana macho kuitazama.
LAHAULA!!! MACHO YAKAKUTANA
NA SURA YA MZIKAJI!!!
MZIKAJI ALIKUWA AMEKUFA NA
AMEZIKWA NA AHADI ZAKE ZA
UKOMBOZI!!
________________
FUNZO::
Usimtegemee sana mwanadamu
katika maisha yako, kwanza ni
dhambi!!
Pili mwanadamu anakumbana na
vikwazo kama unavyokumbana
navyo wewe hadi kumwendea yeye.
Hivyo kumpatia maisha yako ni
kuzidi kuyaweka hatarini zaidi!!
Umeonewa umesingiziwa
unanyanyaswa….. mwachie Mungu
afanye maamuzi…
_______________
Haya mzikaji aliyetegemea
atamfukua naye ni maiti…… tazama
mateso atakayoyapata hadi kufa
kwake…..
Bila shaka atatamani kurudi
gerezani kwa miaka mingine kumi
lakini haitawezekana tena!!!
 
ww uache kunakili stori za watu kisha unatuletea hapa,kwa yeyote aliewah kusafiri na gar za saibaba au hai express kuna vijarida mle huwa vinawekwa kwenye seat kwa nyuma ili abiria asome,unaruhusiwa kuondoka nacho au ukiache,hyo stor inapatkana kwenye hvyo vijarida,ww umenakili na hujamkredt mwandsh.
 
mmmh! Nakikumbuka sana kitabu cha kusadikika cha shaban robert, nikiongeza na hii bac napata majibu... Tusubiri hiyo tarehe sijui itakuwa blue pearl ubungo!!
 
Hata kama umekopi mahali bado ina funzo kwa wategemea wanadamu.
 
kunakili stor za watu sio vzr mkuu,hii stor inapatkana kwenye vijarida ambavyo huwa vinawekwa kwenye seat za magar ya saibaba au hai express ili abiria asome,anaruhusiwa kuvichukua au kuviacha,ww umenakili na kubadili majina,ni story za kingo,mkredt mmiliki mkuu,ukubali kua umenakili.
 
nashangaa anaye lala mika kuwa nimecopy!kuna kitu ambacho kinafanyika hapa duniani sio cha ku copy? tunacho jali ni mafundisho yanayo patikana,unaweza kushangaa 90%walikuwa hawajaisoma but now wameisoma na kupata mafundisho muhimu.
 
Yeriko, mimi nasubiria hiyo tarehe 4.1.2014, hapo ndipo nitakuelewa, najua siku si nyingi; panapo uzima tutafika na nitakuelewa.

Happy New Year!

Ni siku ya Kuliwa Kichwa cha Zitto,angekuwa JB angeweka straight bila kificho.
 
nimejikuta nimeduwaa kama wambura alivyoduwaa baada ya kugundua kazikwa na mzikaji
Usione uvivu kusoma. Kuna ujumbe mzito sana ndani yake...

Katika kijiji cha Matare wilaya ya
Mugumu Serengeti, bwana
Wambura alikamatwa kwa kesi ya
kusingiziwa na kuhukumiwa kwenda
jela miaka mitatu.

Huku nyuma akiacha mke na
watoto wanne waliokuwa
wanasoma. Hukumu hiyo ilimtesa
sana kichwa chake, alitamani kila
mtu anayemhisi kuwa ana makosa
aingie katika moyo wake na
kuupata ukweli.

Alilia na umaskini wake, lambda
angepata wakili mzuri angeweza
kumtetea, kumkosa wakili
kukahalalisha kifungo hicho!!
Alikwenda gerezani huku akiumia
sana rohoni. Aliyaanza maisha
mapya kwa shida sana, akawa
mnyonge kila mara na mwili
ukapoteza afya kiujumla.

Huko gerezani alifanikiwa kupata
rafiki aliyekuwa na cheo ama
jukumu la uzikaji wa wafungwa
hasahasa ambao hawakuwa na
ndugu ama ambao ndugu zao huwa
hawajitokezi pale gerezani.

Mzikaji alijaribu sana kumtia nguvu
Wambura na kumwaminisha kuwa
hiyo ilikuwa hatua tu ya maisha
anapaswa kuizoea na siku moja
ukweli utajulikana tu! Bwana
Wambura maneno ya mzikaji
hayakumuingia kabisa.. alizidi
kunyong’onyea.

“Siwezi kuvumilia kukaa gerezani
miaka mitatu…..kama unajali kilio
changu nisaidie nitoroke kwa
namna yoyote ile ndugu yangu!!”
Wambura alimsihi mzikaji.

SIKU MOJA mzikaji akamwambia
Wambura kuwa msaada
umepatikana. Lakini yataka moyo!!
“Nipo tayari kwa lolote ilimradi tu
nitoke humu!!” alijibu kwa msisitizo
huku akimtegea sikio mzikaji.

“Msaada pekee wa kukutorosha
humu ndani ni kwa njia ya jeneza…
yaani mfungwa akifa mimi
nakuunganisha naye kwenye
jenerza…..” akashusha pumzi kisha
akaendelea “Wewe ukisikia kengere
ya msiba, njoo mara moja kwenye
chumba cha maiti, utakuta tayari
sanduku liko katikati ya chumba
linakuwa halijafungwa, funua
kifunioko ingia ndani yake ulale
pembeni ya maiti kwani sanduku
huwa kubwa la kutosha kila aina ya
maiti na hata miili miwili inaingia.

Kisha nitakuja na kulipigilia
misumari. Baada ya muda
tutalipakia kwenye gari na kutoka
kwenda nje ya gereza makaburini
nikiongozana na baadhi ya
wafungwa na maaskari magereza.

Tutakuzika huko lakini baada ya
dakika 20 hadi 30 nitarudi
kukufukua. Hautaweza kushindwa
kupumua kwa dakika hizo, utatoka
ukiwa huru.”
JAPOKUWA wazo lilikuwa zuri lakini
lilimtisha sana Wambura.

Hata hivyo akaona afadhali afanye hivyo kuliko kukaa gerezani miaka mitatu bila kosa.
Siku moja akasikia kengere ya
msiba. Akafanya kama
alivyoelekezwa na mzikaji.

Akaenda
na kuingia chumba cha maiti. Kweli
akalikuta sanduku, akiwa na hofu
kuu akaingia na kulala pembeni ya
maiti iliyokuwepo. Mara akasikia
mtu ameingia na kulipigilia
msumari sanduku. Muda mfupi
baadaye sanduku likainuliwa na
kuwekwa kwenye gari.

Gari ikatoka nje ya gereza hadi
makaburini. Sanduku likashushwa
na kuwekwa kaburini na kuanza
kufukiwa.
Wambura alijitahidi sana kuvumilia
japo hofu ilizidi kutanda.
Alimtegemea sana mzikaji na
alianza kumuona mkombozi wa
maisha yake.

Kama alivyoambiwa, akasubiri
dakika kumi, ishirini.. zikapita
kimya!!
Dakika thelathini kimya. Joto nalo
likazidi kuongezeka.
“Nitavumilia hadi afike…”
alijisemea kisha akajiongezea kauli
ya ujasiri.

“Kama nilitakiwa kuishi gerezani
miaka mitatu kivipi dakika kadhaa
za hapa kaburini”
KWA kuwa alishakaa gerezani kwa
muda kiasi akatamani kujua
aliyekufa ni nani… ni kwewli
aliogopa kuitazama maiti lakini
aliona kama inatisha zaidi ikiwa
imefunikwa vile kuliko ikiwa wazi.

Akaifunua upande wa usoni… Kwa
kuwa kulikuwa na giza nene
alikodoa sana macho kuitazama.
LAHAULA!!! MACHO YAKAKUTANA
NA SURA YA MZIKAJI!!!
MZIKAJI ALIKUWA AMEKUFA NA
AMEZIKWA NA AHADI ZAKE ZA
UKOMBOZI!!
________________
FUNZO::
Usimtegemee sana mwanadamu
katika maisha yako, kwanza ni
dhambi!!
Pili mwanadamu anakumbana na
vikwazo kama unavyokumbana
navyo wewe hadi kumwendea yeye.
 
Kistaarab km umechukua stor ya mtu unamtaja au unatambua haki yake kwenye hyo kaz ili kuonyesha sio yako,ukikaa kimia inaonekana km ni yako wakati umenakili kaz yake,ulaya n kosa kisheria.
nashangaa anaye lala mika kuwa nimecopy!kuna kitu ambacho kinafanyika hapa duniani sio cha ku copy? tunacho jali ni mafundisho yanayo patikana,unaweza kushangaa 90%walikuwa hawajaisoma but now wameisoma na kupata mafundisho muhimu.
 
mimi niliwahi kwenda zanzibar safari ya kwenda na kurudi siku hiyohiyo nikawa wakati nataka kurudi nauli ilikuwa imepungua kwani nilitumia muda mwingi kumtafuta mtu niliekwenda kumuona hadi narudi bandarini hela ni kama imeisha na sikumpata na sikuwa na hela ya kulala kule istoshe kesho yake kulikuwa na chance ya kupigwa test chuo. mbaya zaidi kumbe boat za jioni huwa ni kama dili usafiri wa jioni ulikuwa shida sana na boat iliyokuwepo ni moja na imejaa. nikatafuta means ya kuondoka kule, basi sikwenda kwa wakata ticket au wasimamizi wa kuingia mule ila niliwafuata wazee wa kazi 'opportunities seekers' mara makuli, au madalali wale jamaa ambao unakuta wapowapo tu wanachofanya hakieleweki popote pale penye mikusanyiko. nikawaeleza hali yangu, basi jamaa wakaniweka sehemu wakaenda huyko baada ya muda wakarudi. mchongo ulifanywa kule ndani kabisa na abilia hawajaruhusiwa kuanza kuingia. mchogno ulipokamilika nikapelekwa moja kwamoja kama mkaguzi nikaingizwa ndani na nilikuwa nimepiga pamba kali sana na sikuwa na mzigo wowote, basi nikapita check point zao tena kabla hata abilia hawajaanza kuingia, nikaingia hadi ndani kule ndani jamaa walikuwa bado wanapanga vitu hapa na plae nakufanya usafi. tulipofika kule jamaa kwanza akanificha chooni wakaguzi rasmi walipoanza kuingia, then akanipeleka kwenye engine chini kabisa kuna mfuniko unafunuliwa halafu mnashuka chini kwa ngazi yaani kwa maana nyingine unakuwa below sea level. kufika kule akataka anifungie halafu yeye apande juu ili aje anifungule baadaye lakini kule chini giza sana kelele ya mashine na hewa hakuna. nilipoona anapanda na mimi nikagoma akaniambia ntahaharibu kazi yake nikakataa kwani nilihisi yule jamaa atashuka hatasafiri. nikagoma tukatoka wote kule kwenye mashine kwani nilimwambia kama ni hivyo tukae wote kagoma. nilipotokana kurudi huku juu wanakokaa abilia nikaamua liwalo liwe niajitokeza nikaaenda kukaa kaunta ya vinywaji na kujidai kujiamini na kukaa katika hali ambayo ni very intimidating na kumuulizaluliza jamaa wa kaunta maswali maswali yaani hata wale wakaguzi hawakuniuliza chochote wakidhani ndo wamiliki wenyewe wa boat, mara abilia wakapanda safari
 
Hahaaaa nimefurahi kuona umejibu pigo.

Lakini Mzikaji huyu tarehe 4 ndio jibu.
 
Back
Top Bottom