Maskini UDSM!

Duh hiyo anglais yako umenichekesha sana --- sasa kuku akishazaa kifaranga si kinaenda kwake yaani mwaka kesho kinakuwa jogoo kinaweza kuja kumpanda mamake
 
ni kweli UDMS pameoza kila upande! suala la vyoo chuo kikuu halina mjadala, vyoo vinanuka si vya wanafunzi wala vya wafanyakazi, sasa faidi uwe na ofisi karibu na choo, hapakaliki, kwaweli ni aibu mara nyingine huwa nawaza jamani hata majumbani mwetu maji yakikosekana tunatafuta njia ya kutatua tatizo vipi sehemu kama UDSM, idara zinazojitahidi saaaana basi utakuta wakiona harufu na makaratasi yamejaa wanafunga vyoo!! jamani hao wanafunzi na wafanyakazi waende wapi, na je hilo ndio suluhisho!!

na pia haya makampuni ya usafi nadhani hayana hata wakaguzi, wanachojitahidi ni kumwagilia majani nje lakini ukiingia madarasani na vyooni hapatamanishi!!!

kielimu ndio kabisa anayosema SHY ni sahihi pana idara nyingi tu ukiingia komputa room ni stoo ya kuweka komputa zilizokufa kuna siku alikuwa anatembezwa mgeni "watoa misaada" akawa anatambulishwa kwamba hapa ni komputa room tuna komputa za kutosha kama unavyoona kwa kweli nilitamani kucheka maana hicho chumba wakati huo kilikuwa na komputa tatu tu nzima na wanafunzi wanangojeana!!

ok hii ndio hali ya chuo chetu inasikitisha, je nini kifanyike?? ingawa wapo watakaochukia kuwa tunasema hatuna mawazo ya nini kifanyike ila tu kusema ni mojawapo ya mchango wahusika walijue pengine hawafahamu au hawajaona umuhimu huo!!!hivyo inawez kusaidia kuwapa changamoto!!!
 
icho chuo ni moja ya vyuo ninavyovichukia kuliko vyuo vyote duniani. nimesoma hapo, nimesota vibaya mno. nilikuwa na akili nyingi, nilijitahidi kiasi kikubwa lakini muda mwingi nilikuwa naishia frustrations. nashukuru Mungu nilimaliza salama. nilitaka kusoma mastaz hapo, lakini moyoni sina hamu, naona kama naenda jehanam. kwanza kabisa, ni kuhusu wanavyojifanya kubana maksi wakati mtu unapiga msuli na una akili za kumwaga. ndio maana first class kama ya wanasheria kule huwa hamna, ni kuanzia second. sasa kama hamna, ina maana maprof hawana uwezo wa kumfundisha mtu akapata hiyo first class. nili piga msuli niipate first lakini walinibania.

Yaani kushindwa kwako kupata first class ndio uchukie chuo kwa ujumla wake. Na tuliokuwa tukitimuliwa kila siku tufanyaje?

I LOVE UDSM.....I have learned a lot through the all the challenges i have faced there......solidarity forever.....

omarilyas
 
Ukiliangalia swala hili kwa mapana ni dhahiri, Tanzania haina dira. Nadhani nguvu imehamishiwa Dodoma university hivyo UDSM imesahaulika. Kuanhaja ya kuangalia mikakati ya kuanjisha vyuo Vs uwezo wakumaintain vilivyopo.
 
Inasikitisha kuwa chuo kikuu kinaoza. Lakini hiyo isitushitue sana kwani nchi nzima ndivyo inavyofanywa. Hakuna mpangilio wowote wa kuangalia na kupanga miundombinu iliyopo, na ile ambayo inabidi iwepo kwa miaka ijayo. Panapowezekana tunasubiri donors wasaidie! Hivi donors wana credit crunch kwetu viongozi wameshaanza kulia kuwa misaada isipunguzwe! Uchumi tunao, tunaukalia - is still very true statement: SADLY!!
 
Kipi kigeni hapo, kwani hamjui MUKANDARA ni SWAHIBA wa KAKA MKUBWA,heri yangu mimi niliyemaliza KAdegree kangu wakati bado tupo wa 13 AFRICA.Halihalisi inajulika coz baada ya MUKANDARA kuwa MAKAMU MKUU wa UDSM,kila kitu kimebadilika,na matatizo yamekuwa kibao.POLE SANA TENA SANA.

Noma sana,ubinafsi na umimi .Anyway may be tutafika
 
Ili nchi yetu iendelee vizuri kumanage rasilimali zilizopo elimu ni kitu muhimu sana kwa wananchi wake. Naogopa kama tutafika sehemu tukaanza kusomesha ili kutimiza wajibu bila kuangalia watu tunaowasomesha watakuwa na contribution gani kwa nchi...kama UDSM imefikia sehemu kufanya mambo bora liende basi wakujionea huruma ni wenyewe mana itakuwa ngumu kukabiliana na changamoto zinazokuja kila kukicha kutokana na mabadiliko mbalimbali duniani.
Nafikiri tufike mahala sasa tuwe jasiri na kujua kwamba mustakabali wa nchi yetu ni wetu sote na sio wa viongozi wachache. Kwahiyo kila mtu kadri anavyoweza, including viongozi waliopo chuoni na madarakani sasa tukafanya kazi kuboresha zaidi nchi. Hakuna balaa kubwa kama leo tukiamua kukata tamaa..tutachemsha
 
Chuo kikuu kimekuwa hivyo muda mrefu sana tangu ilipoanza transformation program ya kuongeza number ya wanafunzi. Hapo mambo ndipo yalipoharibika. Sasa hivi pale hakuna reference kwani hata zilizopo niza kizamani hakuna vitabu vipya mambo mengi yamebadirika japo ofcourse principles ni zilezile.

Maintenance huwa inafanyika mara moja moja sana. Hivyo sishangai ukisema kuwa corridal zinavuja. Pale mlimani kama kweli wanataka chuo kirudi kwanye hadhi yake ya enzi zile then basi walete Lectures wapya maana hawa waliopo wengi wazee, facilities ziboreshwe ikiwepo madarasa yawe ya kisasa zaidi, mabweni yawe mabweni kweli siyo kama ilivyo sasa na vitabu viwe vinapatikana kwa wingi maana wanaoenda pale for reference ni wengi si wanachuo tu mpaka watu wa nje ya chuo.

MABADILIKO YANATAKIWA HASA ITAKAPOINGIA DAMU MPYA NA IWEZESHWE HAPO MAMBO YATAENDA VIZURI.
 
Uchunguzi unaonyesha kuwa haya yote yanasabishwa kwa kiasi kikubwa na ukweli kwamba uongoji wa chuo upo kwa ajili tu ya kuhakikisha wanafunzi hawagomi basi hawana lolote lamaana huko ofisini kwao hakua anayejali na miaka kadhaa ijayo udsm itakuwa ni magofu tu na mitaani kutakua na wasomi/wataalamu feki kibao.

Tatizo halipo UDSM peke yake na si la mwaka huu. Si tatizo la vyuo tu mashule ya msingi na sekondari vivyo hivyo!!!.

Mwanafunzi mmoja wa kidato cha II miaka ya 2003 kabla ya shule za kata(yebo yebo) aliniambia shuleni kwao (ya serikali huko MZA) hakukuwa na mwal wa hesabu wala physics kwa miaka 2!!! Watoto wale walishindanishwa sawia na wenzao waliokuwa na walimu wote mwishoni mwa Kozi yaho(FIV) kwenye mitihani ya NECTA.

Ukisema tatizo ni uongozi huko ni kuangalia tatizo juujuu,na kama ni hivyo basi viongozi wote wa vyuo na mashule Tz ni waovu!!! Tatizo si uongozi;ni zaidi ya hapo.

Wanafunzi hao wa MZA na wengine wanaopenya kufikia vyuo wanatambua mapungufu yao wakijilinganisha na wenzao waliopata walimu na mitaala sawia,hivyo kuiba mitihani,kudesa nk.

Taifa, Necta na baadhi yetu hatukawii kuwalaumu kwa vitendo hivyo tukisahau kuwa Taifa,wanasiasa na Necta wamechangia hali hiyo kwa kutahini wanafunzi wasokuwa na walimu sawia wala kukamilisha mitaala sawia. Necta inalijua hilo lkn haiangaiki nalo walau hata kuweka sharti la ukamilifu wa syllabus kabla ya kutahiniwa!!!. Kwa nini wasiibe mitihani au kudesa wakati wameandaliwa hivyo.

Idadi ya wanafunzi vyuoni,mashuleni inapangwa na wanasiasa na si taasisi husika na inapangwa pasipo kuzingatia idadi ya walimu,madarasa,maabara na miundombinu ya vyuo na mashule

Na wao wamebakia kusema bora liende. Ni pale akina Mnali watakaponyanyua mikono ndipo tutaanza kutafuta chanzo cha tatizo. Mungu apishe mbali...

Natamani safari hii iwe zamu ya wakuu wa vyuo na mashule badala ya Mnali.
Wasiwapige wanasiasa bali wawaite,waandamane na kukataa mashinikizo ya kipuuzi.

Fanya utafiti wa kina zaidi, Tukishakubaliana watz wote kwamba tatizo ni hili na kudhamilia kwa pamoja tutaliondoa vinginevyo tumekwisha.
 
Ukiliangalia swala hili kwa mapana ni dhahiri, Tanzania haina dira. Nadhani nguvu imehamishiwa Dodoma university hivyo UDSM imesahaulika. Kuanhaja ya kuangalia mikakati ya kuanjisha vyuo Vs uwezo wakumaintain vilivyopo.

Hebu tusaidiane kulielewa tatizo na nani alaumiwe.
Kubwa ktk meseji ya kwanza ilikuwa ni yale tunayosema mwisho wa yote, ELIMU DUNI.

Hapo wanaingia TCU. Karibuni wameviondoa vyuo visivyotambulika. Sawa kabisa. UDSM haikuhitaji kutambulika upya kwa sababu zilizo wazi lakini je, TCU haifuatilii kuona kama hiyo list yake ya mwanzo bado inahitaji Vyuo kama hivyo? Yaani inakuwa kama nembo ya TBS mtaani?

Tambua ubora, yes! baadaye fuatilia muelekeo.

Prof. Mayunga Nkunya Exec. Director wa TCU ni mwajiliwa wa UDSM, kwa hili anasemaje? Au bado hakijashuka kufikia levo ya SUA, UDOM,Tumaini, nk.
 
Watanzania wezangu inabidi tubadirike.

Ningeomba kuuliza fedha za stationary wanafunzi wa udsm wanapata kiasi gani na wanazifanyia nini?
Na kwanini ulilie kununuwa kitabu wakati una access na INTERNET?

Maajabu kabisa haya COMPUTER zipo ila zimeharibika maajabu kweli sasa hiyo course ya computer na IT hapo udsm wanafanya nini? waifute basi.

Mwalimu sijui tutor ama profesa mimi naona hana haja ya kuwaambia wanafunzi wa kitengo chake kuandika mtihani badala yake nadhani kila mwanafunzi amkabidhi komputa moja kama project ndani ya term computer iwe nzima na aandike DOCUMENTATION jinsi archtecture ya comp hiyo na jinsi alivyoitengeneza Akifanya hivyo kapita mtihani. Hapo hakuna cha wireless teh teh teh
 
Sasa kama hawa wataalamu tunawapika hapo UDSM wananusa marashi ya kinyesi, watakapokuwa wanaongoza wizara wataona umuhimu wa kuwa na vyoo safi kweli??? Waafrika ndivyo tulivyo ,by Nyani Ngabu.
 
Sasa kama hawa wataalamu tunawapika hapo UDSM wananusa marashi ya kinyesi, watakapokuwa wanaongoza wizara wataona umuhimu wa kuwa na vyoo safi kweli??? Waafrika ndivyo tulivyo ,by Nyani Ngabu.

Oh yeah Miafrika Ndivyo Tulivyo and so far, apart from rhetoric, no one has been able to disprove me. If we can't even run our learning institution(s) what else can we run?
 
Ni chuo kizuri kwa mtizamo wangu sema tu wabongo ni watu wa kuponda vyakwetu.
Ni chuo kilichozalisha wataalamu wengi wa taifa hili.
Hata JK kapita pale,Museveni nae vile vile
 
Ni chuo kizuri kwa mtizamo wangu sema tu wabongo ni watu wa kuponda vyakwetu.
Ni chuo kilichozalisha wataalamu wengi wa taifa hili.
Hata JK kapita pale,Museveni nae vile vile
Ndugu yangu,hebu acha kufuga maradhi hivi kweli;katika ulimwengu huu wa sasa tukianza ku-rank ubora wa vyuo vikuu duniani hivi hii UDSM unafikiri inaweza kuwa ya ngapi?Au ndiyo unababaika kwa hao wanasiasa waliopitia hapo!?Hata hivyo lazima ujiulize wana mafanikio kiasi gani katika kuzitumikia nchi zao;ni watu wangapi hadi hivi sasa ukipita mtaani wana-appreciate mchango wao katika nchi?
Nadhani unaweza ukawa unashindwa kutofautisha kati ya nadharia na vitendo au siasa na taaluma katika utendaji kazi.
Take care.
 
Bado UD ndo chuo bora zaidi Tz na pia ni 18th kwa ubora Afrika!

Tuna mambo ya kurekebisha..we need more investment ktk hii sekta!

Taabu ni Hii Quantity Versus Quality? Kipi kianze?

Ukifikiria kwanza numbers yaani wingi wa wanafunzi kwanza..yaani na kila mtz apate opportunity elimu ya juu..then we compromise quality of output!

More investment is needed..je is it a priority kwa wazazi na serikali???

Kwa nini Taifa Stars iliposhinda Burkinafaso chapu chapu zaidi ya 300m zilipatikana?

Jamii tu ya Tz hatuko makini ktk prioritization..sii tu serikali ya kulaumu!
 
Tatizo ni kuchanganya siasa na sayansi,kisha siasa ikatawala jamani tunajiua wenyewe halafu tunatafuta wenye shahada feki.bora feki ya enzi hizo kuliko ya sasa kwani hata chuo mtu hajui kiliko yeye ni kuskani na kuediti na hatimae anatoka na cheti saaaaaaaafi.
 
Back
Top Bottom