Maskini UDSM!

Ndugu wanajamii hali ya chuko kikuu cha Dsm sehemu ya mlimani inatisha sana. Hii ni katka nyanja za elimu usafi mazingira na maadili.
Unapoongelea suala la ELIMU hali mbaya kwani siku zijazo tutaanza kuwa na wataalamu feki mitaani. Hii inatokana na ukweli kuwa miundombinu iliyopo haikizi mahitaji ya muda/haiendani na wakati, na ile iliyopo ni michache ukilinganisha na watumiaji. Ufundishaji umekuwa wa shida, upatikanaji wa vifaa vya kujisomea kama vitabu library na kompyuta imekuwa shida sana.Hali inapelekea wanafunzi kutumia madaftari ya na madesa ya waliomaliza zamani (kama miaka ya 90) na kutokana na uchache wa vitu hivi imekuwa ni kawaida wanafunzu wanapokuwa kwenye mitihani wanaingia navyo kwa minajili ya kuangaliziana siku hizi wanaitaa wayalesi (wireless). Sasa hapo tutegemee wasomi/wataalamu gani??!
HATA SEHEMU YA CHUO AFRICA IMESHUKA KWA SASA NI CHA 18 KUTOKA 13 NA NI CHA 3,496 DUNIANI KUTOKA 2500 NA.
USAFI ni mbaya sana hasa sehemu za kutoa haja. Vyoo vinanuka usafi wa maeneo hayo haupewi kipaumbele lakini kuna makampuni yaliyoajiliwa kwa ajili ya usafi huo uangalizi ndo hakuna. Kama wewe ni mgeni maeneo yale utatamani ukimbie utapokuwa unakatiza katika korido za majengo ya chuo sababu ya harufu.
MAJENGO nayo hayako kwenye hali nzuri kuna baadhi ya maeneo hasa kwenye korido mvua inapokuwa ikinyesha utafikiri chini ya mti, kuta zimechakaa, paa zinashuka, kuna vyumba huwa lazima viwe na AIR CONDITIONER lakini kwa sasa zina miaka kadhaa hazifanyi kazi n.k.
MIUNDOMBINU kama baranara za ndani zimeboka hakuna lolota linafanywa, taa za kumulika barabara usiku haziwaki na hii ni hatari kwani inasababisha kuwapo vibaka, waporaji na wabakaji wa dada na mama zetu.
Hiyo ni baadhi tu ya uozo kwa ufupi.
Uchunguzi unaonyesha kuwa haya yote yanasabishwa kwa kiasi kikubwa na ukweli kwamba uongoji wa chuo upo kwa ajili tu ya kuhakikisha wanafunzi hawagomi basi hawana lolote lamaana huko ofisini kwao hakua anayejali na miaka kadhaa ijayo udsm itakuwa ni magofu tu na mitaani kutakua na wasomi/wataalamu feki kibao.

Ungesoma mara yapili nakufanya Editing mkuu, upepaniki?
 
Back
Top Bottom