Maskini UDSM! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maskini UDSM!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Zwangedaba, Mar 2, 2009.

 1. Zwangedaba

  Zwangedaba Member

  #1
  Mar 2, 2009
  Joined: Feb 1, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Ndugu wanajamii hali ya chuko kikuu cha Dsm sehemu ya mlimani inatisha sana. Hii ni katka nyanja za elimu usafi mazingira na maadili.
  Unapoongelea suala la ELIMU hali mbaya kwani siku zijazo tutaanza kuwa na wataalamu feki mitaani. Hii inatokana na ukweli kuwa miundombinu iliyopo haikizi mahitaji ya muda/haiendani na wakati, na ile iliyopo ni michache ukilinganisha na watumiaji. Ufundishaji umekuwa wa shida, upatikanaji wa vifaa vya kujisomea kama vitabu library na kompyuta imekuwa shida sana.Hali inapelekea wanafunzi kutumia madaftari ya na madesa ya waliomaliza zamani (kama miaka ya 90) na kutokana na uchache wa vitu hivi imekuwa ni kawaida wanafunzu wanapokuwa kwenye mitihani wanaingia navyo kwa minajili ya kuangaliziana siku hizi wanaitaa wayalesi (wireless). Sasa hapo tutegemee wasomi/wataalamu gani??!
  HATA SEHEMU YA CHUO AFRICA IMESHUKA KWA SASA NI CHA 18 KUTOKA 13 NA NI CHA 3,496 DUNIANI KUTOKA 2500 NA.
  USAFI ni mbaya sana hasa sehemu za kutoa haja. Vyoo vinanuka usafi wa maeneo hayo haupewi kipaumbele lakini kuna makampuni yaliyoajiliwa kwa ajili ya usafi huo uangalizi ndo hakuna. Kama wewe ni mgeni maeneo yale utatamani ukimbie utapokuwa unakatiza katika korido za majengo ya chuo sababu ya harufu.
  MAJENGO nayo hayako kwenye hali nzuri kuna baadhi ya maeneo hasa kwenye korido mvua inapokuwa ikinyesha utafikiri chini ya mti, kuta zimechakaa, paa zinashuka, kuna vyumba huwa lazima viwe na AIR CONDITIONER lakini kwa sasa zina miaka kadhaa hazifanyi kazi n.k.
  MIUNDOMBINU kama baranara za ndani zimeboka hakuna lolota linafanywa, taa za kumulika barabara usiku haziwaki na hii ni hatari kwani inasababisha kuwapo vibaka, waporaji na wabakaji wa dada na mama zetu.
  Hiyo ni baadhi tu ya uozo kwa ufupi.
  Uchunguzi unaonyesha kuwa haya yote yanasabishwa kwa kiasi kikubwa na ukweli kwamba uongoji wa chuo upo kwa ajili tu ya kuhakikisha wanafunzi hawagomi basi hawana lolote lamaana huko ofisini kwao hakua anayejali na miaka kadhaa ijayo udsm itakuwa ni magofu tu na mitaani kutakua na wasomi/wataalamu feki kibao.
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Mar 2, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Mimi niko UDSM sasa hivi katika LAB ya computer kuna wanafunzi wengi hapa wa mambo ya uhasibu humu ndani kuna komputer karibu 50 lakini zinazofanya kazi ni chini ya 12 darasa hili wanafunzi huwa wanaingia kila siku kufundishwa humu sijui wanafundishwa nini huko vyumbani wanafunzi wengine wanalia njaa hawajala toka jana ukienda hill pakr ndio usiseme
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Mar 2, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Heheheheee....Miafrika Ndivyo Tulivyo....nani anabisha?
   
 4. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  icho chuo ni moja ya vyuo ninavyovichukia kuliko vyuo vyote duniani. nimesoma hapo, nimesota vibaya mno. nilikuwa na akili nyingi, nilijitahidi kiasi kikubwa lakini muda mwingi nilikuwa naishia frustrations. nashukuru Mungu nilimaliza salama. nilitaka kusoma mastaz hapo, lakini moyoni sina hamu, naona kama naenda jehanam. kwanza kabisa, ni kuhusu wanavyojifanya kubana maksi wakati mtu unapiga msuli na una akili za kumwaga. ndio maana first class kama ya wanasheria kule huwa hamna, ni kuanzia second. sasa kama hamna, ina maana maprof hawana uwezo wa kumfundisha mtu akapata hiyo first class. nili piga msuli niipate first lakini walinibania.
   
 5. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  suggestion zako opinion baada ya kugundua ndivyo tulivyo?
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Mar 2, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  jinsi ulivyo ni ndivyo ulivyo...sasa suggestion za nini wakati ni ndivyo ulivyo? wee vipi wewe? kila kitu kwenye hiyo phrase ni self explanatory, kipi ambacho hujakielewa ms. yo yo you can't play with my yo yo?

  huoni kila siku watu wanavyotoa ma-suggestions humu ndani? je, unaona mabadiliko yoyote? the answer is no. kila aina ya suggestions zimeshatolewa humu...ooh ifanyike hivi...aaah kifanyike vile....

  bottom line..ukiwa mfupi ni mfupi tu hata uvae magongo kuongeza urefu wako bado utakuwa mfupi tu! git it sucka?
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ngojeni Uchaguzi mtatiliwa kila kitu kipya na mambo yote kukalabatiwa ,halafu kura zenu mkaipigie CCM. hapo mmeanzishiwa tawi la CCM jiungeni kwa wingi tu ,ili mutumiwe kuuzibiti upinzani.
   
 8. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Hakuna kuchoka ukichoka ndio utazidi kuwa ulivyo......kwahiyo kama masuggestions yanatolewa na hakuna mabadiliko una njia gani mbadala?
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Mar 2, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Halafu nini cha kushangaza hapa? Hali nzima ya nchi na hakika karibu bara zima la Afrika kusini mwa jangwa la sahara ni mbofu na yakusikitisha.

  Kama mnadhani hapo UD kuna msoto hebu tembeleeni vijijini muone jinsi mazingira ya elimu ya msingi na sekondari yalivyo....heheheheheee...mnacheza nyie. UD ina afadhali maradufu.
   
 10. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nani alikwambia kwamba ulikuwa na akili nyingi...and wait, so sasa huna akili nyingi tena?

  Nani kakwambia ulibaniwa first class...? Na kama hilo ni kweli ulichukua hatua gani baada ya hapo ndugu? au unalalamika tu sasa mkuu?

  Anyway, mimi sikupingi wala sikuungi mkono madai yako.....coz sina base!

  Kwa mtoa mada kwa ujumla, sidhani kama madai yake yote ni kweli kwa 100% e.g barabara zimebomoka, mifumo ya maji taka mibovu, majengo yamecrack or kucollapse etc. though madai ya uhaba wa vifaa vya kufundishia na vyumba vya lectures /seminars hili ni kweli! Mengine ngoja tufuatilie kwa karibu kama hali imekuwa mbaya kiasi hicho tangia tumetoka hapo 5 years ago!
   
 11. m

  mtoni New Member

  #11
  Mar 2, 2009
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kipi kigeni hapo, kwani hamjui MUKANDARA ni SWAHIBA wa KAKA MKUBWA,heri yangu mimi niliyemaliza KAdegree kangu wakati bado tupo wa 13 AFRICA.Halihalisi inajulika coz baada ya MUKANDARA kuwa MAKAMU MKUU wa UDSM,kila kitu kimebadilika,na matatizo yamekuwa kibao.POLE SANA TENA SANA.
   
 12. JohnShaaban

  JohnShaaban JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2009
  Joined: Aug 23, 2007
  Messages: 465
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  ...duh, unatumia kipimo gani kujua ulikuwa unasoma na kustahili alama nzuri? Kusota sio kipimo cha kupata alama nzuri, unaweza kusota lakini usisome yenye manufaa kwa somo husika.
   
 13. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #13
  Mar 2, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Duh,hapo kuna tatizo la uongozi.kompyuta 12 tu?what a joke!
   
 14. Zwangedaba

  Zwangedaba Member

  #14
  Mar 2, 2009
  Joined: Feb 1, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Tatizo sio msoto wala hali ya mazingira vijijini ila ni ukweli kwamba haya matatizo mengi hayakuwapo ila yamekuja au yameongeza siku za karibumi yaani katika huu uongozi wa sasa. Matatizo ya UDSM yana solution na ni tofauti na Kijijini kwani hapa vitu vyote hivyo vina bajeti we unataka kusma hiyo inaenda wapi..... Fikiria ndo utende....
  na jamani tuache kujindanganya eti hali ni mbaya sijui vijijini sijui kusi ya sahara..... Hapo mnataka wakoloni warudi kuwatoa katika huu msoto au inabidi mpiganie mabadilko?
  We unasema eti sijui Africa nzima... una data gani hebu fika tu hapo Rwanda uone alafu linganisha na kwenu sijui Msoma wapi huko Kigoma sijui.....
   
 15. Madago

  Madago Senior Member

  #15
  Mar 2, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tatizo la UDSM ni kuwa kwa wanasiasa wetu chuo kile sio kipaumbele chao hata kidogo, na hata watu waliopita hapo wakiingia mtaani hatukiangalii. Hua najiuliza, pamoja na mambo mengine hiz alumni zinafanya nini kushinikiza maendeleo chanya ya hichi chuo. Kwa upande mwingine kuanzishwa kwa vyuo vingine kama Dodoma na kile cha Morogoro ambavyo vilichukua wahadhiri wengi tu wazuri, inaweza kuwa imechangia kushuka kwa kiwango chake.
  Kuna kipengele kimoja nakiunga mkono 100%, kuhusu vyoo. Lakini sio UD peke yake, ni kwenye public places zote TZ, si kwenye mabaa au makanisani, la choo tumeshindwa kabisa. Kuna kipindi niliona TZ imekua rated kwenye top ten ya nchi zenye worst public toilets duniani.
   
 16. Madago

  Madago Senior Member

  #16
  Mar 2, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tatizo la UDSM ni kuwa kwa wanasiasa wetu chuo kile sio kipaumbele chao hata kidogo, na hata watu waliopita hapo wakiingia mtaani hatukiangalii. Hua najiuliza, pamoja na mambo mengine hiz alumni zinafanya nini kushinikiza maendeleo chanya ya hichi chuo. Kwa upande mwingine kuanzishwa kwa vyuo vingine kama Dodoma na kile cha Morogoro ambavyo vilichukua wahadhiri wengi tu wazuri, inaweza kuwa imechangia kushuka kwa kiwango chake.
  Kuna kipengele kimoja nakiunga mkono 100%, kuhusu vyoo. Lakini sio UD peke yake, ni kwenye public places zote TZ, si kwenye mabaa au makanisani, la choo tumeshindwa kabisa. Kuna kipindi niliona TZ imekua rated kwenye top ten ya nchi zenye worst public toilets duniani.
   
 17. A

  AMETHYST Senior Member

  #17
  Mar 2, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna matatizo ya uongozi uliopo, na sijui kwanini Tanzania kila mtu aiwa kiongozi anakuwa mheshimiwa haguswi utadhani hakuna namna ya kudhibiti viongozi, hilo linapaswa kufanyiwa kazi kwa sheria za vyuo vya umma, lakini watanzania sisi ni waoga wa kumkosoa mtu live..na hilo imekuwa kama hulka na silika yetu watanzania kuoneana aibu..

  Kuhusu miundombinu, ni kutoona mbele tu ndo kunasumbua. Madarasa ya lecture ya arts pale, yalikuwa kwa ajili ya watu 25 - 30 enzi hizo, hawakutazamia kuna siku wangekuwa 500 ktk darasa hilo. Sasa sijui hapa tunafanyeje kwa sasa. Ila kibaya ktk hili ni siasa..waziri analazimisha kuwa wanafunzi waongezwe ili apate ujiko wa kuwa wakati wangu chuo kilidahili wanafunzi wengi bila kujali miundombinu..hapo ndipo pia unaona nguvu kubwa ya siasa inapotumika kuharibu hata maamuzi ya kisomi..na binafsi sina jawabu rahisi juu ya hili..maana ni kweli kuwa siasa ndizo zinatawala dunia na ni pale utashi wa wanasiasa utakapokuwa ni wa kujali maeneo yote ya maendeleo tutakapoondokana na matatizo yanayoweza kutibika kama haya wajumbe wanayaweka hapa ukumbini
   
 18. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Kwa nini msiwe mnalalamika pale mnapoitwa kukabidhiwa kadi za CCM !!
   
 19. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Kuna tofauti gani kati ya nafasi ya 13 na 15 katika ranking ya vyuo :confused: Hapa Marekani vifaa vyote vya shule nilijitegemea. Na kitabu kimoja ni kati ya dollar 70 mpaka 100. Niambie mwanafunzi anachukua masomo matano katika semester moja atatatumia kiasi gani ?

  Kwanini wanafunzi wa Tanzania hawalipi technology fee ?? Computers hazishuki kutoka mbiguni ??
   
 20. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Lawama tu kila siku!

  Ila kwa mazingira ya nje ya Chuo..mnasema uwongo!

  Hiki chuo mazingira ya nje yanapendeza sana ukilinganisha na sehemu zingine za Dar!

  sasa ndo Watz tunaambiwa hakuna cha bure..we invest ktk Elimu na tuache kutegemea serikali kwa kila kitu!

  sasa kama wanafunzi wanasema wao ni maskini..hawataki wazazi wachangie..je hapo nini cha kulalamika?

  Serikali ikupe mkopo, ilipia umeme, ilipie kufeka nyasi, ilipe waalimu, inunue computa, vifaa vya maabara n.k .nk

  It is high time Watz tupunguze kupenda vya bure..nasi tuwe tayari kuchangia!
   
Loading...