Maskini akipata makalio hulia mbwata!!!!!!!!!!!

Maskini akipata makalio hulia mbwata!!!!!!!!!!!

nsee a muro

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2012
Posts
241
Reaction score
124
Weee ulie tu ucheke una mbavuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!!!

Leo nataka nije na mchambo kwako wewe bi dada, shosti la mujini uliyekuja upofu wa kijijini tukakufunza viunga vya mjini.

Tunajua kabisa wewe unatoka na BOSS!! Tumekuchunia manake hapa mjini ya nini kumbania mtu riziki yake.
Tuliotangulia mjini twajua kabisa ya kwamba riziki mafungu 7 ukikosa bara huwez kosa na pwani, na ukikosa wa kutoezea basi hutokosa wa kurumangia. Siye tukakupa mbinu zote za angani na majini, ili umweke sawa BOSS wala hatukuwa na hiyana ya kukuharibia pishi lako, lakini mwenzetu wewe umetutoka kama mti uliopururwa majani.

Hatukuwa na nongwa ulipobebeshwa mimba na Boss. Tulikufariji ulipokata tamaa na kutulilia kwamba unahisi kitumbua kitangia mchanga. tulilia na wewe na kukusaidia hadi ulipojifungua kwa siza.

Sasa hivi tunakushangaa shostito unavyotupandishia vioo, umekuwa mringi, unanata unajiona wewe ndo wewe hapa mjini kumbe si loote si chochote wewe sawa na maji ya deki, hadhi yake kumwagwa uwani. Siku hizi umembadilisha hadi boss uwajibikaji wake, yaani kazini huji ingawa umemaliza martenity leave, kila siku Boss anaturundikia kazi zako kana kwamba salary tunagawana kisa wewe wenzio hata ruhusa hatupewi tunaambiwa kazi ni nyingi.

Kila siku unakisingizo mara ooh!!!!!!!!!!! leo mshono unauma, mara oooh! mshono haujapona vizuri,.................. mara ooh!................... mshono haujafunga wewe mtu mmoja mwali tumechoka.................mshono huo mshono gani nakuuuliza WA DERA AMA WA SOLO?????........................na hicho kibwana chako ndo usipime kinatutumikishaaaaaaaaaa kisa eti unalea unalea kwani wewe wa kwanza kulea????............... oooh! ...............umezaaa............ umezaa almasi wewe.

Mbaya zaid tabia yako ya kusema eti nkhune............ nkhune........... namilikiwa na wakubwa, mkubwa kitu gani kazaa tembo ama nyumba??? unatuona sisi sote mafala kisa kibwana chako hiki na sasa tunakupa kubwa labda wenine hatukutoka umatumbini,,,,,,,,,,,,,lazima mwaka huu ukalie mgongo badala ya ------. Tena uwe makini na kibwana chako tunakipeperusha ofisi lazima kaikimbie mwanga mkubwa wewe............safari hatupewi kisa wewe, pesa zetu za overtime unakula wewe sasa utajua kwanini samaki japo anapenda maji hakai kwenye maji ya moto. Umelikoroga bibie lazima utalinywa, na utaula wa chuya kwa uvivu wa kutwanga.

Habari ndiyo hiyo.
 
HAYA bidada naona kuandika kumekufanya upunguze hasira,poleni,ila kama hauridhiki si utafute kazi nyingine?
 
HAYA bidada naona kuandika kumekufanya upunguze hasira,poleni,ila kama hauridhiki si utafute kazi nyingine?
Kazi ngumu mjini hapa, na utahama ngapi ili upate isiyokuwa na makwazo???? ishu si kuhama ishu ni kukomaa hadi kieleweke.

nimetangaza kabisa hii vita hadi nishinde.
 
Wewe unapiga kelele na kulalamika chinichini, lakini unazidi kuumia, mwite mweleze live kuwa unatukwaza wenzio, hapo utakuwa umefanya la maana, kuliko kuja hapa JF unaongea weeeeee, lkn muhusika hafahamu. WEWE WAPIGA KELELE WENZIO YAKE YANAMWENDEA.@nsee a muro.
 
aah wapyyyyy!!!
watoto wa mjini huwa hatushindwi kitu, hapa ni mwanzo tu bado picha litaendelea.
labda nisiwe mmatumbi mimi. anajidai ana minyatoooooooo....................mtu mwenyewe kila nikimkagua simwoni palipozidi. sasa ngoma ndo kwanza bichi hadi likauke kesha nyweaaaaaaaaaa zamani............wakuja huyu ataniwezea wapi??
 
Yaani mpk hapo umeshashindwa , ndiyo maana umekuja kupigia kelele humu jamvini, ungekuwa kweli wewe ni mwanamke mahiri ungemwita na kumwambia live, kwa sababu unamwogopa ndiyo maana unabaki kuweyaweya.
Pia hayo mambo ya kutishiana kuwa wewe matumbi sijui nani yalishapitwa na wakati. kama kweli wewe ulikuwa mzuri boss angevutiwa na wewe, lakini kwa kuwa hukuwa na vigezo vya kumvutia ndiyo maana kamchukua huyo, Na kamwe siku zote wakuja ndiyo analeta maendeleo sehemu, wewe huoni wenye mji wa Dar walivyouza viwanja kwa wakuja na tukabadilisha mji? kuwa mjasiri wa kuweza kumfuata mtu na kumweleza kanayokukwaza, itakusaidia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom