BEYOND PAIN
SEHEMU YA 20
MTUNZI😛ATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Mke wangu Emmy na Chris walikuwa na mahusiano ya kimapenzi na kwa mujibu wa mawasiliano niliyoyanasa Chris alidai mtoto Baraka ni wake.Awali sikuliamini suala hilo nikafanya uchunguzi na kugundua kwamba ni kweli Chris na Emmy ni wapenzi.Ili kujiridhsha zaidi ikanilazimu kutumia kipimo cha DNA ili kuhakiki kama Baraka ni mwanangu na kipimo kikaonyesha kwamba Baraka si mwanangu .Nilipotoka katika vipimo nilimkuta mwanzangu tayari amekwisha hama nyumbani.Nilimtaarifu baba mkwe na kwa msaada wake tukafanikiwa kwenda hadi kwa huyo Chris ambako ndiko Emmy alikwua amehamia na kumkabidhi mwanae ili amlee.Hivi majuzi nikiwa Zanzibar nilipigiwa simu na Chris ambaye alikuwa akiishi na Emmy kwa wakati huo akaniambia kwamba yeye na Emmy wametengana baada ya kugundua kwamba Emmy amekuwa akimdanganya na yule mtoto Baraka si wa kwake pia.Baada ya kuachana na Chris,Emmy hakuwa na sehemu nyingine ya kwenda ikamlazimu kurudi katika nyumba yangu..? Ghafla nikakatizwa na sauti ya juu ya Emmy
ENDELEA??????..
?Wewe mwanaume ukome kusema ile ni nyumba yako.Pale ni kwangu.Tumejenga wote na nina uhuru wa kuingia pale muda wowote ninaotaka.Mbona unakwepa kusema ulikuwa Zanzibar na Malaya wako? Sema ukweli watu wote wakusikie..? akasema Emmy kwa sauti kali
?Emmy naomba uwe na adabu mbele ya wazee wako.Naomba ukae kimya hadi utakaporuhusiwa kuongea? baba mkwe akasema kwa ukali
?baba mnamsikiliza sana huyu muongo mkubw???..?akasema Emmy lakini akazuiwa ghafla na baba yake aliyeinuka kwa hasira
?kelele !! nitakunasa vibao sasa hivi ..? Baba mkwe akawa mkali na kuinuka kutaka kumfuata Emmy pale chini alipouwa amekaa lakini akazuiwa na wazee wenzake.
?Hapa ni nyumbani kwangu na ni mimi ndiye mwenye amri nani aongee ndani ya nyumba hii.Kama ni huo ufidhuli wako ni huko huko mtaani na si hapa.Wayne endelea? akasema baba mkwe nikakohoa kidogo na kuendelea.
?Baada ya kusikia kwamba Emmy amerudi nyumbani kwangu ikanilazimu kurejea Arusha mara moja kwa sababu nilitaka kufahamu ni kitu gani kilichomrudisha kwangu baada ya mambo yote aliyonifanyia.Nikiwa nimeongozana na rafiki yangu niliyekuwa naye Zanzibar Emmy alinitukana sana na kunitolea vitisho nikaamua kuondoka.Kabla sijaufungua mlango akanipiga na chupa kichwani nikapoteza fahamu .Namshukuru sana rafiki yangu huyo niliyekuwa naye kwani ni yeye ndiye aliyekimbia na kuwaita majirani ambao walinikimbiza hospitalini na Emmy akakamatwa akapelekwa polisi.Baada ya kutibiwa nikatoka hospitali .Kwa kumuonyesha kwamba mimi si mtu mkatili kama alivyo yeye imenilazimu kwenda polisi na kufuta kesi iliyokuwa ikimkabili.Baada ya hapo nikaona niwaite wazee wangu ili niwaeleze kwa ufasaha nini kinachoendelea kati yangu na Emmy? Nikanyamaza na kumeza mate.Mara mzee mmoja akaniuliza swali
?Huyu rafiki yako unayesema kwamba ulikuwa naye Zanzibar ni nani? Kwa sababu tumemsikia mwenzako hapa akimlalamikia?
?Huyu rafiki yangu anaitwa Clara.Ni mtanzania ambaye anaishi na kufanya kazi nchini afrika ya kusini.Nilikutana naye hapa hapa Arusha siku kadhaa zilizopita .Ni yeye ndiye aliyenisaidia katika kuyatenegeza upya maisha yangu yaliyokuwa yameharibika.Ni yeye ndiye alinifanya nijione kama mtu ninayeishi tena baada ya kukata tamaa na maisha haya kutokana na vituko vya Emmy.Huyo ndiye niliyekuwa naye Zanzibar na huyo ndiye aliyenipeleka hospitali baada ya Emmy kunipiga na chupa kichwani.? Nikasema na kuwafanya wazee wote mle sebuleni kutikisa vichwa vyao kukubaliana nami.Nikaendelea
?Wazee wangu mahala nilikofika mimi na mwenzanu ni pabaya kwa sababu tumefikia mahala pa kuhatarisha uhai wetu.Kwa hatua tuliyofikia naweza kukiri kwamba hakuna namna tunayoweza kufanya ili kuweza kutuweka tena pamoja.Hapa nina maana kwamba kuishi pamoja kati yangu na Emmy haiwezekani tena na kwa maana hiyo basi ninaomba kuchukua nafasi hii kuweka wazi kwamba nimefikia uamuzi wa kuachana na Emmy rasmi.? Nikanyamaza na kuyaacha maneno yale niliyoyaongea yaweze kuingia masikioni mwao kisha nikaendelea
? Nimeamua kuachana na Emmy.na kila mmoja aendelee kuishi maisha yake.Nimeona niwafahamishe kwanza wazee wangu ili muweze kufahamu na msishangae mtakapolisikia shauri hili mahakamani.Nitafuata taratibu zote za kisheria za kutoa talaka.Jambo jingine ambalo nataka kuliweka wazi kwenu ni kwamba hata kama sheria itatutaka tugawane mali zote sawa kwa sawa lakini mimi ninamuachia mwenzangu kila kitu tulichonacho.Ninamuachia nyumba zetu mbili,magari yetu mawili,maduka yetu ya nguo pamoja na duka kubwa la vipodozi.Mimi ninaondoka na nguo zangu tu.Sitaki kuwa na kitu chochote kitakachonikumbusha kuhusu Emmy.Nataka kuyaanza maisha mapya kabisa yenye amani ya moyo.Kwa hiyo wazee wangu nimeona niwataarifuni kwani tayari mwanasheria wangu amekwisha anza kulishughulikia kisheria suala la kuachana kwetu.Ni hayo tu niliyotaka kuwafahamisha.A
hsanteni sana? Nikasema na kukaa chini.Watu walikuwa wakijifuta majasho .Kila mmoja aliuona ugumu wa suala hili.Baba yake mkubwa Emmy akakohoa kidogo na kusema.
?Wayne tumekusikia na kukuelewa. Mambo uliyotueleza ni makubwa na ninapenda kukupa pole sana kwa matatizo yote yaliyokupata ndani ya ndoa yenu.Hiyo ndiyo mikiki mikiki ya ndoa ambayo tunakutana nayo.Usituone sisi tumeishi na ndoa zetu hadi tumekuwa wazee namna hii,tumepitia mambo mengi sana lakini tulisimama imara na ndiyo maana mpaka leo hii bado tuko na mama zenu.Pamoja na yote yaliyotokea bado nina imani lazima iko fursa ya majadiliano kati yetu na nyie ili kujaribu kuzuia ndoa hii isianguke. Bado kuna uwanja mpana sana wa majadiliano na mambo haya yote yanaweza yakasawazishwa na mkaendelea kuishi kwa amani.Mnapitia katika kipindi kigumu cha majaribu na ambacho lazima msimame imara ili msije mkaanguka.Mimi napendekeza yafanyike maongezi.Sisi wazee tupo hapa na hakuna chochote kinachoweza kuharibika.Tuta
wasuluhisha na mtaendelea kuishi kwa amani katika ndoa yenu.Hakuna binadamu mkamilifu.Sisi sote tuna mapungufu yetu.Au mnasemaje wazee wenzangu? Akasema baba yake mkubwa na Emmy.Wazee wote mle ndani wakamuunga mkono isipokuwa baba mkwe yaani baba yake Emmy.Nilimshangaa sana mzee yule kwa mawazo kama yale hata baada ya kusikia vituko alivyokuwa akivifanya Emmy.Wakati wakiendelea na mjadala wa chini chini Emmy akasimama
?Wazee wangu naomba mnipe nafasi na na mimi niseme ya kwangu.Huyu mwanaume ni mlaghai na ni yeye ambaye amekuwa si mwaminifu.Mara nyingi tu nimemfuma na wanawake kibao .Sasa nasema hivi mimi sina maneno mengi ya kusema.kwa sababu yeye amekwisha sema kwamba amefikia mwisho mimi siwezi kumlazimisha na wala sitaki kuendelaa kuishi naye.Yeye aniache huru niishi maisha yangu na yeye akaendelee na maisha yake na wanawake zake.Sitaki usuluhishi wa namna yoyote ile na huyu mwanaume.Nakwam
bia hivi Wayne ukitaka usiende hata mahakamani na kupoteza wakati wako.Wewe ondoka zako na ukaishi na huyo Malaya wako.Mimi sintakufuatilia tena na ninaomba usinifuatilie katika maisha yangu.Sahau kama mimi na wewe tuliwahi kulala kitanda kimoja.Lakini nakuapia kwamba iko siku moja utakuja kunipigia magoti kunguru wewe? akasema kwa kiburi Emmy na kuondoka kwa kasi mle sebuleni akapanda gari lake na kuondoka.
?Jamani mmeona kiburi cha huyu mtoto? Mmeona mtoto alivyo shetani huyu? ? akasema baba mkwe.Babamkubwa wa Emmy akitikisa kichwa.na kusema
?Sikujua kama Emmy amebadilika na kuwa na kiburi namna hii.Emmy niliyemfahamu mimi si Emmy huyu niliyemuona dakika chache zilizopita.Nilifanya makosa makubwa sana kutaka kumtetea ili aweze kurudiana na mumewe.Kwa hatua aliyofikia tayari ameshindikana kabisa.?
Baba mkwe akasimama na kusema
?wayne wewe ni kijana wetu ,tunakupenda sana.Wewe ni kijana ambaye ninaweza kusema kwamba ni wa pekee kabisa.Kwa mambo aliyoyafanya Emmy ingekuwa ni mtu mwingine saa hizi tungekuwa tukiongea mambo mengine ,lakini wewe umevumilia mambo yote.Nimekuwa nawe toka mwanzo wa vituko vya huyu mtoto na ninafahamu ni uchungu kiasi gani aliokusababishia.Kwa hapa ilipofika mimi nakubaliana nawe kabisa Wayne kwamba imetosha.Achana na Emmy.Sisi kama wazi tunakupa baraka zote na tunakuombea kwa Mungu ili aweze kukupa furaha na mafanikio katika maisha yako mapya.Huyu mwana kulaanika atafundishwa na ulimwengu.Una baraka zote toka kwetu wazazi na endelea na taratibu zote za kisheria ili sheria isiendelee kumtambua kama mke wako. Kwa sababu kuna uwezekano mkubwa akaja kukusumbua sana siku za usoni.Mimi sina mengi ya kusema zaidi ya kukutakia baraka nyingi na Mungu akutangulie katika kila jambo unalolifanya.Hapa bado ni nyumbani kwako na siku zote unakaribishwa .Sisi bado ni wazee wako na siku zote ukipatwa na tatizo lolote lile usisite kututaarifu na tutakupatia kila aina ya msaada unaouhitaji? akasema baba mkwe.Ninampenda sana mzee huyu kwa sababu ni mzee mwelewa na siku zote amekuwa upande wangu.Niliwashu
kuru wazee wale ambao waliniasa mambo mengi sana .Ilipofika saa nne za usiku nikawaaga na kuondoka kurejea hotelini kuonana na barafu wa moyo wangu Clara nikiwa ni mwingi wa furaha nikiamini kwamba Emmy hatanisumbua tena maishani.Nikiwa njiani nikapokea ujumbe mfupi wa maandishi katika simu yangu
?Mapambano bado yanaendelea.Huu si mwisho wako.Your life will be a living hell? Nilihisi moja kwa moja ujumbe ule ulitoka kwa Emmy.Nikaupuuza na kuufuta katika simu yangu
?Its your turn to get pain Emmy?anza kujiandaa? Nikasema taratibu nikiwa na tabasamu usoni.
Nilifika hotelini na kumkuta Clara barafu wa moyo wangu akinisubiri kwa hamu kutaka kufahamu kilichojiri katika kikao kile.Alikuwa na wasi wasi mwingi.Aliponiona tu alinikumbatia kwa nguvu na kunipa mabusu kemkem.Sikuwahi kufanyiwa hivi na Emmy katika miaka yote niliyoishi naye.Nilizidi kumshukuru Mungu kwa zawadi hii ya kunipatia mwanamke ambaye anafahamu mapenzi.Anajua kupenda .Nilimkumbatia Clara kwa mahaba mazito ,nikafumba macho na kupumua kwa nguvu na kumshukuru Mungu kwa kuniletea malaika huyu ambaye amenifanya niifurahie dunia na kila kitu kilichomo ndani yake.Ndugu msomaji mapenzi ni matamu kama ukimpata mtu ambaye unampenda naye akakupenda na si mtu mwenye tabia kama za Emmy ambaye anaweza akakufanya ukaichukia dunia.
?Ouh My darling..I missed you soo much ? akasema Clara na kunibusu mdomoni.
Haraka haraka akachukua koti na kunivalisha kwani hali ya Arusha usiku huu ilikuwa ni ya kiubaridi baridi na malaika wangu hakutaka kuniona nikitetemeka kwa baridi.Baada ya kuhakikisha nimevaa koti akaleta kikombe cha kahawa
?Karibu kahawa mpenzi wangu? akasema Clara.Nlishindwa nijibu nini,nikabaki nikitabasamu.
?Nini..mbona unanishangaa hivyo? Akauliza Clara
?Ninakushangaa kwa sababu kila dakika nakuona kama mpya..nakuona kama unazidi kuwa mrembo..sichoki kukutazama ..kwa jinsi ninavyosikia raha nikiiona sura yako niko tayari kukesha nikikutazama usiku kucha?.? Kauli ile ikaamsha kicheko mle ndani.Clara akacheka kwa nguvu sana.
?Enhee hebu nipe habari za huko ulikotoka? akasema Clara
?Ulifanya jambo zuri sana kuamua kutokwenda katika kikao kile.Mwanamke yule sina hakika kama ana akili timamu.? Nikasema
?Nilikwisha lisoma hilo toka awali na ndiyo maana nikakuomba kwamba uende peke yako.Nimekwisha usoma ubongo wa Emmy ? akasema Clara huku akitabasamu.
?katika maisha yangu yote niliyoyaishi hapa duniani,nilifanya kosa moja kubwa sana na ambalo nitaendelea kujilaumu hadi siku ninaingia kaburini .Nilifanya kosa kubwa sana kumuoa Emmy..That?s the biggest mistake of my life? nikasema .Clara akanisogelea ,akanibusu na kusema
?Usiseme hivyo Wayne.Sisi wote tunafanya makosa katika maisha yetu lakini tunapogundua kwamba tulifanya makosa tunajitahidi sana kutoyarudia tena.Tafadhali nakuomba usahau yote yaliyotokea na endelee na maisha yako mapya.Siku zote makosa tuliyoyafanya nyuma yanatufana tuishi maisha bora zaidi huko tuendako ..kwa hiyo usijilaumu kwa kutokufanya chaguo sahihi..I think this time you have chosen the right one?? akasema Clara akiwa karibu yangu..
?Safari hii sikufanya chaguo mimi..bali baada ya kumlilia Mungu kutokana na shida na mateso niliyoyapata toka kwa Emmy.aliamua kunichagulia mtu yeye mwenyewe..kwa maana hiyo wewe ni chaguo langu toka kwa Mungu na siku zote huwa hakosei katika kila jambo analolitenda.Mungu ametukutanisha kwa sababu anazozifahamu yeye mwenyewe.Sikuot
a katika maisha yangu kama nitakuja kupata mapenzi na furaha kama niipatayo nikiwa nawe.Naona ni kama muujiza mkubwa sana ambao Mungu amenitendea.Thamani yako kwangu hailinganishwi na kitu chochote kile katika hii dunia.Hi ndiyo sababu niko tayari kwa lolote lile kwa ajili yako pekee.Nakupenda Clara.Nakupenda zaidi ya unavyofikiri..N
akupenda zaidi ya ninavyojipenda mwenyewe.nakupenda sasa na daima? Maneno yale yalimtoa machozi Clara.Ni kweli nilitamka maneno yale toka uvunguni kabisa mwa moyoni mwangu..Nilimpenda Clara kupita ninavyoweza kuelezea.
?Maneno yako yananifanya nijione ni mwanamke mwenye bahati kubwa sana kumpata mtu anayenipenda kupita nafsi yake mwenyewe.Katika maisha yangu nimekutana na watu mbali mbali ambao wamekuwa wakijaribu kupata bahati ya kuwa na nafasi ndani ya moyo wangu.Wengi wa hao ni watu matajiri wakubwa na wenye majina makubwa lakini wote hawa walinipenda mimi kwa sababu ya jina langu kubwa ,mafanikio yangu na wengine lengo lao ni kutaka kuweka historia ya kuwa na mtu kama mimi.Sikuwa tayari kutoa nafasi kwa mtu yeyote ambaye alionekana kuwa na chembe chembe za kuvutiwa nami kutokana na aidha uwezo wangu,jina langu au uzuri wangu.Nilikwisha umizwa hapo awali na safari hii sikutaka tena kufanya makosa.Nilihitaji mtu ambaye atanipenda mimi kama Clara na si kama mrembo au mwanamitindo au tajiri.Baada ya kukutana nawe Wayne nimegundua kwamba wewe unanipenda mimi kama mimi na si kwa sababu ya uzuri,jina au uwezo wangu.Moyo wangu umekuchagua wewe kati ya mabilioni ya wanaume wa dunia hii.Nakuahdi kwamba nitakupenda na kukuenzi hadi siku naingia kaburini.Siku zote utakuwa mwanaume wa pekee ambaye umeuteka moyo wangu kwa namna ya ajabu sana kiasi kwamba umenifanya niisahau dunia..Ninajiona ni kama ninaishi katika dunia yenye watu wawili .mimi na wewe tu.Nakupenda sana Wayne na nitazidi kukupenda hadi mwisho wa uhai wangu? Clara akasema na kunikumbatia,akanipiga busu zito na kukilaza kichwa chake mapajani mwangu.
?Tuachane kwanza na hayo?niambie nini kimeendela katika kikao? Akauliza Clara.
?Kikao kilikwenda vizuri.Wazee walihudhuria wengi..Nilianza kwa kuwapa historia nzima ya wapi nimetoka na Emmy,mambo gani amenifanyia .Niliwaeleza kila kitu bila kuwaficha vitendo vyote vichafu vya Emmy na kila mmoja alionekana kufumba macho kutokana na vitendo vya aibu alivyokuwa akivifanya mtoto wao.Mwisho nikawaeleza kwamba kutokana na hali ilivyo hivi sasa mimi na Emmy hatuwezi kupikwa chungu kimoja tena kwa maana hiyo nimeamua kuachana naye kisheria na tayari wanasheria wangu wamekwisha anza kulishughulikia suala hilo.Nikaweka wazi mbele ya wazazi kwamba ili kumfanya Emmy asiendelee kunifuata fuata katika maisha yangu ninamuachia kila kitu nilichonacho.Sihitaji kitu chochote kutoka katika mali nilizonazo.Vyote ninamuachia Emmy ili aweze kuyaendesha maisha yake kwa raha na amani bila kubughudhiwa na mtu yeyote yule.? Nikanyamaza na kumtazama Clara aliyekuwa kimya akinisikiliza.
?Emmy akasemaje uliposema hivyo?
?Ingawa hakusema wazi lakini nina imani moyoni mwake alifurahi sana kwani atakuwa huru sasa kufanya kila anachotaka kukifanya.Kitu cha kushangaza kwa mwanamke yule aliinuka na kuongea kwa kiburi sana na kuondoka zake kitendo ambacho kiliwaacha hoi baadhi ya wazee ambao hawajawahi kuvishuhudia vibweka vya Emmy wazi wazi.baada ya hapo kikao kikaendelea kati yangu mimi na wazee na wamenipa baraka zote za mimi kumtaliki mtoto wao na wote wako upande wangu?
?Stupid woman?sijawahi kuona mwanamke mwenye akili mbovu kama yule.Badala ya kushukuru ameachiwa kila kitu ili aweze kuyaendesha maisha yake lakini badala yake anaondoka kwa kiburi na tambo..? akasikitika Clara
?Nadhani sikufanya jambo baya kufanya maamuzi nliyoyafanya.Nilifanya vile ili kumuondoa kabisa katika maisha yangu na kuanza maisha mapya na kila kitu kipya.Maisha mapya,mpenzi mpya,nyumba mpya na kila kitu kipya,au unasemaje malaika wangu? Nikamuuliza Clara aliyekuwa amechanua tabasamu pana.
?Wayne naweza kusema kwamba wewe ni mwanaume wa kipekee sana na nina bahati kubwa sana kukutana nawe.Una roho ya kipekee ambayo wengi hawana.Umefanya jambo la busara sana kumuachia kila kitu.Nyumba magari,mali pesa ni vitu vinavyotafutwa kwa maana hiyo tutaunganisha nguvu na kwa juhudi zetu tutayaanza upya maisha yetu mapya.Kitu kikubwa cha kushukuru ni kwamba roho yako iko salama salimini.Mimi niko tayari kuishi nawe hata katika nyumba ya udongo kwa sababu pesa mali na kila kitu si vitu vinavyotengeneza penzi la kweli.Niko tyari kuwa nawe katika maisha yoyote yale kwa sababu ninakupenda na kukujali.Lakini naomba nikukumbushe kwamba bado makubaliano yetu yanasimama pale pale kwamba zile fedha tulizopanga kuzipeleka katika miradi ya kijamii bado zitafanya kazi ile ile iliyokusudiwa.?
?Usihofu kuhusu hilo Clara..makubaliano yetu hayajabadilika na kila kitu kitafanyika kama kilivyopangwa.Zile pesa zote ambazo sikuzipata katika njia zilizo halali zitarudi kwa wananchi kwa kupitia miradi ya maendeleo.? Kauli ile ikamfurahisha Clara akanivuta karibu yake na kunipa busu zito.Tuliongea mambo mengi sana siku hiyo kuhusiana na maisha yetu ya baadae hasa baada ya suala la kuachana na Emmy kisheria kukamilika.Tulipochoka kuongea tukaenda zetu kulala.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO?????