SEHEMU YA 17
MTUNZI 😛ATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
?tafadhali usilie Clara.Huu ni wakati wa
kufurahi na si wakati wa kudondosha
machozi? nikamwambia huku nikimfuta
machozi
?Wayne ninalia kutokana na furaha
niliyonayo.Nimekaa miaka mingi nikijihisi ni
mwenye furaha lakini sikuwahi hata mara
moja kuipata furaha kubwa kama niipatayo
sasa kwa kuwa nawe.Ni wewe ndiye uliyenipa
furaha hii kubwa maishani.? Akasema
Clara.na kuniangalia usoni.
?Darling twende tukaendelee na ratiba yetu ya
siku.Tuna kila sababu ya kufurahi? Tukatoka
na kuingia garini tukaelekea eneo la meserani
ambako kuna hifadhi ya nyoka.Mimi si mpenzi
kabisa wa nyoka na ni moja kati ya vitu
ninavyoviogopa sana katika hii dunia lakini
niliamua kwenda huko kwa sababu Clara
alipenda kwenda kutazama nyoka wa aina
mbali mbali wanaofugwa.Amekuwa akisikia
hifadhi hii ya nyoka na alipanga siku moja
aitembelee na sasa ameipata nafasi hiyo
hakutaka kuipoteza.
ENDELEA????????..
Meserani park moja kati ya sehemu nzuri
kutembelea iko kilometa 25 magharibi mwa
jiji la Arusha katika barabara ya kuelekea
hifadhi ya taifa ya Serengeti na bonde la
Ngorongoro.Hifadhi hii imejumuisha nyoka wa
kila aina wanaopatikana mashariki na kusini
mwa afrika.Ukiwa katika hifadhi hii ya
Meserani utapata pia kuwashuhudia mamba
wenye ukubwa wa zaidi ya meta tatu na vile
vile utafurahia safari za ngamia kuelekea
katika maboma ya wamasai na utabahatika
kujifunza utamaduni wa kimasai.
Saa kumi za jioni tulirejea jiijini
Arusha.Ilikuwa ni siku niliyofurahi
mno.Tulipanda ngamia na kwenda katika kijiji
cha wamasai ,tulikaa na kujifundisha mambo
mengi kuhusiana na utamaduni wa kimasai
pamoja na kununua badhi ya vitu walivyokuwa
wakiviuza.Kwa miaka yangu yote ya kuishi
Arusha sikuwahi hata mara moja kutembelea
vivutio mbalimbali vilivyopo hapa jijini.Nilijisi
kia furaha sana baada ya kugundua faida
ipatikanayo kutokana na utalii wa ndani.
?Clara bado naendelea kukushukuru kwa
sababu kupitia kwako nimejifunza mambo
mengi.Katika miaka yote hii niliyoishi hapa
Arusha sijawahi kutembelea hata kivutio
kimoja ha utalii.Nimehamasika sana kwa
ziara tuliyoifanya leo na kila nipatapo nafasi
nitakuwa nikifanya utalii wa ndani na
kuliongezea taifa mapato? Clara hakujibu kitu
alinitazama na kutabasamu
Clara hakutaka tena kukaa pale hotelini
.Hakutaka tena kuwa mbali nami.Akaniomba
kwa siku hizi chache ambazo atakuwepo hapa
Arusha azimalizie akiwa nyumbani
kwangu.Nilifurahi sana kwa uamuzi ule
Pale hotelini Clara hakuwa akidaiwa chochote
akapakia vitu vyake na tukaelekea nyumbani
kwangu.Furaha ikaingia tena ndani kwangu.
**********************
Siku mbili kabla ya safari ya kuelekea
Zanzibar kwa ajili ya mapumziko nilipokea
taarifa kwamba ninahitajka katika ofisi za
taasisi ya kupambana na kuzuia
rushwa.Walikuwa wakihitaji kunihoji .Tayari
Emmy alipeleka mashitaka kama alivyokuwa
ameahidi kama nisingetimiza matakwa
yake.Sikuwa tayari kutimiza matakwa ya
Emmy.Nilimweleza Clara kuhusiana na mwito
ule na akanipa moyo kwamba nisiwe na wasi
wasi hata chembe kwa sababu suala hilo liko
ndani ya uwezo wake na nihesabu kama
limekwisha.
Saa tatu za asubuhi katika siku niliyotakiwa
nifike pale ofisini ilinikuta nikiwa katika
chumba maalum kwa ajili ya mahojiano.Watu
tatu wakaingia pale wakiwa na mafaili yenya
nyaraka mbali mbali tukasalimiana na
mahojiano yakaanza.
Nilihojiwa mambo mengi sana kuhusiana na
fedha zile zilizokuwa benki.Niliwaeleza ukweli
kuhusiana na ugomvi wangu na Emmy na jinsi
gani Emmy anavyotaka kuhakakisha kwamba
ninaporomoka.Niliwaeleza vile vile kwamba si
kweli kwamba fedha zile zilitokana na ufisadi
nilioufanya wakati nikiwa mfanyakazi wa
halmashauri ya jiji la Arusha bali fedha zile
zimetokana na biashara tuliyokuwa tukiifanya
kwa ubia kati yangu mimi na Clara.Clara
akaitumia nafasi hiyo pia kulezea kwa upana
kuhusiana na biashara tunayoiendesha kwa
ubia .Aliwaonyesha vithibitisho mbalimbali
vilivyokuwa katika kompyuta yake ndogo
vilivyoonyesha kwamba nimekuwa nikipokea
mgao wa fedha toka katika kampuni ile.Kitu
kilichowaumiza kichwa ni kwamba ni wapi
basi Emmy alizitoa nyaraka zile alizokuwa
nazo? Nyaraka kuhusiana na fedha
iliyokuwepo benki nilikiri ni zangu na Emmy
alizichukua wakati nikiwa sipo nyumbani
lakini nyaraka mbalimbali ambazo alikuwa
nazo kuhusiana na ufujaji wa fedha za
halmashauri nilizikana na kuwaomba waende
wakapate taarifa sahihi kutoka halmashauri
nilikokuwa nikifanya kazi.Baada ya masaa
takribani sita ya mahojiano,tukaondoka na
kuwaacha wakiumiza vichwa vyao na
kumlaani Emmy kwa kuwasumbua pasi na
faida yoyote.Nilimshukuru sana Clara kwa
kuniokoa katika sakata lile.
?Pamoja na kulimaliza suala hili bado
nitabaki na msimamo ule ule kwamba fedha
zile ni za wananchi na itabidi tuzirudishe kwa
wananchi kwa kuzipeleka katika miradi ya
maendeleo? akanikumbusha Clara.
?Clara nalikumbuka hilo.Mara tutakaporejea
kutoka Zanzibar fedha zile zote tutazipeleka
katika miradi .Tutapanga na kuamua ni kitu
gani tunaweza tukaifanyia jamii kwa fedha
zile?
Nikamwambia Clara akatabasamu na
kunibusu.
***********************
Ni Siku ya tano sasa toka tumefika hapa
Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Serena
Inn.Baada ya misuko suko iliyotupata Arusha
tuliamua kuja huku mbali kwa ajili ya
mapumziko na kupanga maisha yetu.Ni mida
ya saa tisa za alasiri tukiwa katika ufukwe wa
Mangapwani unaomilikwa na hoteli hii ,simu
yangu ikaita.Niijilaumu sana kwa kutembea
na simu sehemu kama hii.Nikaitoa simu na
kuangalia mpigaji.Zilikuwa ni namba ngeni
kabisa.
?hallo ? nikaita
?hallo Wayne? Ikajibu sauti ya upande wa pili
ambayo nilihisi kama ninaifahamu.
?nani mwenzangu? Nikauliza
?Ni mimi Chris?
?Chris !! nikastuka mno.Sikuitegemea kama
Chris angeweza kunipigia simu hasa baada ya
kitendo alichonifanyia.
?Wayne najua hukutegema kama ningeweza
kukupigia simu tena.Nimelazimika kukupigia
kuongea na wewe mambo mawili makubwa?
?Chris tafadhali naomba usiniharibie siku.Kwa
sasa niko Zanzibar mapumzikoni na mpenzi
wangu mpya.Sitaki unisumbue Chris?
Nikasema kwa ukali
?Wayne tafadhali naomba unipe dakika mbili
tu za kuongea na wewe na baada ya hapo
sintakusumbua tena.? Chris akasema
?Unataka kuniambia kitu gani Cris? Nikauliza
kwa ukali
Clara aliyekuwa amebaki nyuma yangu
akanikaribia na kuniuliza
?Darling mbona unaongea kwa ukali namna
hiyo.nani huyo aliyekupigia simu ?
?Ni mume wa Emmy? nikamjibu Clara ambaye
akasogea pembeni na kunipa nafasi niongee
na Chris.
?Wayne kwanza kabisa nachukua nafasi hii
kukuomba msamaha japokuwa nafahamu
kwamba si rahisi kunisamehe kwa mambo
niliyokufanyia.Nimekuwa sina amani maishani
mwangu.jambo hili limenikondesha
mno.Japokuwa ni ngumu kwako kunisamehe
lakini naomba nikiri kwamba nilikukosea sana
na ninaomba unisamehe.?
?Chris mimi sina tatizo na wewe hata kidogo.
Nimekwisha kusamehe muda mrefu sana na
nikaendelea na maisha yangu.Nilikupa Emmy
kwa kuamini kwamba ndiye mwanamke pekee
anayekufaa maishani.Mimi kwa sasa niko na
mpenzi ambaye ndiye niliyeandikiwa na
Mungu.Ninayafurahia maisha yangu tofauti
na nilipokuwa na huyo mke wako? Nikasema
huku nikitabasamu
?nashukuru sana Wayne kama umekwisha
nisasemehe.Jambo la pili ninalotaka
kukueleza ni kwamba mimi na Emmy
tumeachana.Niligundua kwamba mtoto yule
ambaye alisema ni wa kwangu hakuwa mtoto
wangu.Kutokana na matendo yake nilipata
shauku ya kwenda kupima DNA na majibu
yakaonyesha kwamba Baraka si mwanangu
kama alivyodai.Sikuweza kuvumilia nikaamua
kumfukuza kwangu na kwa sasa amesema
kwamba anarudi kwako kwani bado ni mkeo
halali.Hivi tunavyongea tayari amerejea
nyumbani kwako anadai ni nyumbani kwake
na wewe ni mume wake halali wa
ndoa.Nimeona nikufahamishe kuhusu jambo
hilo ili ujue nini kinaendelea huku na uchukue
tahadhali.Mwanamke yule ni baradhuli na
hafai katika jamii..kwa heri wayne? Chris
akakata simu
?bastard !! nikasema kwa hasira.Nilihisi
kijasho chembamba kikinitoka
Clara aliniangalia jinsi nilivyobadilika ghafla
akahisi mambo hayakuwa sawa akanisogelea
na kunishika bega.
?Wayne huyo mume wa Emmy amekuambia
nini cha kukuudhi namna hiyo? Akauliza
Clara.Nilikuwa nikihema kwa nguvu kwa
hasira
?Clara ninajuta kwa nini nilimfahamu
Emmy.Nashindwa kuelewa ni mwanamke wa
aina gani yule?
?Nini kimetokea tena? Kwa nini anaendelea
kukufuata fuata wakati kila mmoja ana
maisha yake kwa sasa? Clara akauliza
?Chris amenipigia simu na kuniambia kwamba
yeye na Emmy wametengana .Amegundua
kwamba yule mtoto Baraka ambaye Emmy
alisema ni wake kumbe si wake.Jambo hilo
limemfanya amtimue Emmy na hivi
tunavyoongea amerudi nyumbani kwangu
akidai bado ni nyumbani kwake.Nashindwa
kuelewa nitamfanya nini huyu mwanamke ili
aachane na mimi.Nimechoka sasa na matukio
ya Emmy?
Clara akaniangalia kwa makini usoni na kisha
akasema
? Suala hili limekuwa gumu sana kwa
sasa.Ukiangalia kisheria Emmy bado ni mkeo
wa ndoa.Kwa mujibu wa ndoa za kikristu ni
kwamba mkisha funga ndoa kanisani hakuna
kitu kinachoweza kuwatenganisha zaidi ya
kifo.kwa maana hiyo wewe bado ni mume
halali wa ndoa wa Emmy.Kwa Emmy kurudi
katika nyumba yenu ni halali yake kwa sababu
bado ni mke wako.? Clara akasema taratibu
lakini nilijua ndani ya moyo wake alikuwa
ameumia sana.Nilijaribu kutafakari kwa kina
ni kwa nini Emmy amekuwa akinifanyia vituko
vya namna hii.Kwa nini hataki kuniona nikiwa
na furaha katika maisha yangu? Niliuma
meno kwa hasira na kusema
?Clara pamoja na yote uliyoniambia lakini ni
ukweli ulio wazi kwamba ndoa kati yangu na
Emmy ipo katika makaratasi tu.Lakini katika
uhalisia hakuna ndoa baina yetu.Hata Mungu
mwenyewe analiona hilo na hata hao viongozi
wa dini nikiwaelezea watakubaliana nami
kwamba Emmy hafai kuwa mke.Nimekwisha
mtoa Emmy moyoni mwangu na sintarudi
nyuma tena.Simtaki Emmy maishani
mwangu.Sitaki kabisa kumuona mbele ya
macho yangu.? Nikasema kwa ukali
?punguza hasira Wayne.Suala hili linatakiwa
kushughulikiwa taratibu na kwa umakini
mkubwa ili kupata suluhisho la kudumu la
mgogoro huu usiokwisha.Mimi nina wazo
moja? Clara akasema
?Wazo gani hilo Clara?
?Ninakushauri kwamba uwaite wazee wa
pande zote mbili ili muweze kukaa na
kutafuta suluhu kwa sababu kuivunja ndoa
yenu ni jambo ambalo haliwezekani.Ki
nachotakiwa kufanyika hapa ni kuitafuta
suluhu ya kudumu ili muweze kuishi kwa
amani tena.?
?Una maanisha nini Clara? Nikauliza
?Nina maana suluhisho hapa ni wewe
kurudiana na Emmy .Inavyoonekana ni
kwamba Emmy bado anakupenda na kwa
maana hiyo hata mfanye nini katu hamuwezi
kutengana?
?Tafadhali usiseme hivyo Clara?
Nikasema.Nilikuwa nimestushwa sana na
kauli ile ya Clara
?Wayne suala hili mbona liko wazi kwamba
wewe na Emmy kamwe hamuwezi
kutengana.Mnachotakiwa kukifanya kwa sasa
ni kutafuta suluhu ili muweze kuishi kwa
amani katika ndoa yenu.?
?Clara naomba tafadhali usiseme hayo
maneno.yananiumiza sana moyo
wangu.Macho yangu kwa sasa nimeyaelekeza
kwako tu.Ninachokihitaji ni kuwa nawe
maishani.?
Clara akanishika mikono miwili,akanitazama
usoni na kusema taratibu
?Wayne Nakupenda sana .Toka moyoni
mwangu nakiri kwamba nakupenda zaidi ya
unavyoweza kufikiri.Nakupenda zaidi ya
ninavyojipenda mwenyewe.Sijawahi kupenda
kama nilivyotokea kukupenda.Wewe ni kila kitu
kwangu.Wewe ni mwanaume wa pekee kabisa
ambaye hujawahi kutokea maishani
mwangu.Kila nikiwa nawe najihisi kama niko
juu mawinguni.nasikia furaha ya ajabu kila
ninapokuwa nawe.Nilipokuona kwa mara ya
kwanza niliweka ahadi kwamba nitafanya kila
niwezalo kwa ajili ya kulipigania penzi
lako.Nilikuwa tayari kwenda hadi mwisho wa
dunia kwa sababu yako.Niliweka ahadi ile
kutokana na jinsi ninavyokupenda
Wayne.Kutokana na hali halisi ilivyo
ninasikitika kusema kwamba Wayne mimi na
wewe hatuwezi katu kuwa pamoja tena.Katu
hatutaweza kuwa na furaha katika maisha
yetu.Wewe ni mume halali wa Emmy.hata
kama ndoa yenu iko katika mgogoro mzito
kwa sasa lakini ukweli utabaki pale pale
kwamba wewe ni mume wa mtu.Nimekuwa
nikilifikiria sana jambo hili na limeniumiza
sana moyo.Mwanzoni nilijipa moyo
nikitegemea labda mambo haya yanaweza
yakatulia na hivyo tukapata nafasi ya
kufurahia maisha tukiwa sisi wawili bila
bughudha ya aina yoyote ile lakini kadiri siku
zinavyozidi kwenda ndivyo karaha na vituko
toka kwa mkeo vinazidi.Kusema ukweli
nimekuwa nikiumizwa sana na mambo
anayoyafanya mkeo lakini nimekuwa
nikivumilia kutokana na upendo wangu
kwako.Kwa muda huu mfupi tulioonana kila
siku limekuwa likiibuka jambo jipya toka kwa
Emmy ambaye hataki kukuona
ukipumzika.Hataki kukuona ukifurahi.Wayne
naomba nikuambie ukweli kwamba
nimevumilia na sasa nimechoka.Ninaona
itakuwa vyema kwetu sisi kuusitisha huu
uhusiano wetu ili usiendelee kuumia
zaidi.Iwapo nitaendelea kuwa nawe Emmy
hatatuacha hata kidogo.Ataendelea
kutuandama usiku na mchana.Kwa maana
hiyo ni bora kama nitajiweka pembeni na
kukuacha uendelee na Emmy?
Clara akasema kwa uchungu huku machozi
yakimtoka.Alikuwa ameumizwa mno na
mambo aliyokuwa akiyafanya Emmy.Alikilaza
kichwa chake kifuani kwangu na kukilowesha
kifua changu kwa machozi.Nilisikia uchungu
mwingi kwa machozi aliyoyamwaga malaika
wangu ,nikapandwa na zisizomithilika.Laiti
kama Emmy angekuwa karibu yangu wakati
ule ningeweza kumfanyia kitu kibaya
sana.Sikujua ni kwa nini niendelee kuteseka
kwa mambo anayonifanyia Emmy.Sijui
nimemkosea nini Emmy kiasi cha kuwa na
chuki nami ya namna hii.Niliumia sana kwa
aumuzi ule wa Clara.Baada ya kuachana na
Emmy nilitegema kwamba Clara ndiye furaha
ya maisha yangu.Nilimuona ni kama malaika
aliyeshushwa kwa ajili ya kuja kunirudishia
furaha ya maisha iliyokwisha potea.Kwa muda
huu mfupi niliokuwa na Clara nimekuwa ni
mtu mwenye furaha kubwa maishani na
nilikuwa na mipango mingi ya siku za usoni
nikiwa na Clara. Kwa upande mwingine
sikulaumu sana uamuzi huu aliouchukua Clara
kwa sababu ni kweli alikuwa amechoshwa na
karaha zinazoendelea. Toka siku ya kwanza
tuliyoanza mapenzi yetu imekuwa ni matukio
moja baada ya jingine.Clara hakuwa ametaka
kujiingiza katika mambo ya mahusiano kwa
sababu ya kuogopa mambo kama haya
yanayotokea sasa.Aliufuingua moyo wake
baada ya kuamini kwamba mimi ni
mwanaume wa pekee ambaye ninaweza
kumpa furaha ya maisha lakini kumbe alikuwa
akielekea mahala ambako alikuwa
akipakimbia miaka hii yote aliyokuwa akiishi
peke yake.Alikuwa akiyakimbia matatizo na
karaha zilizomo ndani ya mahusiano lakini
badala yake amejikuta akitumbukia katika
shimo lililojaa kila aina ya matatizo.
?Wayne nakupenda sana na sitaki kuachana
nawe lakini sintaweza kuendelea nawe kwa
sababu ya ukweli ulio wazi kwamba Emmy
anakuhitaji .Emmy ana kila sababu ya
kunifanyia vituko kwa sababu wewe ni mume
wake halali wa ndoa.Siwezi kuendelea
kupambana na Emmy kila kukicha
.Ninamuachia mume wake na kujiweka
pembeni.Nimeamua kuyarudia maisha yangu
niliyokuwa ninaishi yaani maisha ya kuwa
peke yangu.Sitegemei kama nitaingia katika
mahusiano tena kwa sababu baada ya miaka
mingi ya kuwa nje ya mahusiano nimeufungua
moyo wangu na kujaribu kupenda tena lakini
kilichotokea ni kitu kile kile nilichokuwa na
kikwepa kwa miaka mingi yaani mumivu ya
moyo.Ninaumia sana Wayne..Moyo wangu
umeumia sana na sijui kama kidonda hiki
kitaweza kupona.Nitateseka kwa maisha
yangu yote kwa sababu mtu niliyetokea
kumpenda naye akanipenda hataweza kuwa
nami.Inaniuma sana ?.? Clara alizidi
kumwaga machozi.Nikamuonea huruma
.Alikuwa amemumia moyo.Alikuwa akiteseka
kupita kiasi.Nilimlaani Emmy kwa laana zote
za dunia hii.kwa machungu na hasira
nilizokuwa nazo sikuwa tayari kumuona tena
Emmy katika maisha yangu.Nilimchukia
kupita kiasi.Nilimtazama Clara alivyokuwa
akilia na kuteseka kwa maumivu ya moyo
nikasikia uchungu sana.Huku machozi
yakinilenga nikamwambia
?Clara nafahamu ni uchungu kiasi gani ulio
nao kwa uamuzi huu mgumu uliouchukua.Naf
ahamu vile vile mateso na maumivu makali
unayoyasikia moyoni kwa mambo yote
ambayo yametokea katika kipindi hiki kifupi
tulichokuwa pamoja.Mateso na maumivu haya
hata mim ninayasikia kwa sababu sipendi
kukuona ukitoa machozi au ukiumia moyo
wako.Ninapokuona katika hali hii ninapatwa
na uchungu mwingi kwa sababu lengo langu
ni kukuona ukiwa ni mwenye furaha na
matumaini siku zote.Hata hivyo Clara uamuzi
huu umeuchukua haraka sana.Nadhani bado
nina nafasi ya kuweza kuyaweka sawa mambo
haya ili mimi na wewe tuweze kuishi kwa
amani katika maisha yetu.Naomba tafadhali
unipe nafasi nyingine ili niweze kuyamaliza
mambo haya na sisi tuweze kuishi kwa amani
bila bughudha ya aina yoyote ile.Nitafanya
lolote linalowezekana kufanyika ili mimi na
wewe tuweze kuwa pamoja.? Nikamwambia
Clara ambaye akainua kichwa na kunitazama
?Wayne nakuamini kwamba unaweza ukafanya
unavyoweza na sisi tukaishi kwa
furaha.Ndiyo ! tutaishi kwa furaha lakini
hatutakuwa na amani katika maisha
yetu.Hatutaweza kufunga ndoa kwa sababu
kisheria wewe bado ni mume wa mtu.Pamoja
na hayo Emmy hataweza kukuacha uishi kwa
furaha.Ataendelea kukuandama mpaka
mwisho wa uhai wake.Jambo la msingi
ninaloliona hapa ni sisi kuusitisha huu
uhusiano wetu ili Emmy aweze kuwa na
amani.Ninahisi vituko vyote hivi
anavyovifanya ni kwa sababu anakupenda.?
Clara akasema .
Nilijaribu kuendelea kumshawishi abadili
maamuzi yake lakini ilikuwa ngumu
sana.Msimamo wake haukutetereka.Kwa mara
nyingne tena nilikuwa nimeumizwa na
Emmy.Nilisikia maumivu makali sana tofauti
na hata pale mwanzo Emmy aliponiacha na
kwenda kwa Chris.kwa sababu yake nilikuwa
nimemkosa mwanamke niliyempenda zaidi
maishani mwangu.Nilikuwa nimeikosa furaha
ya maisha yangu.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO???????..