Masimulizi: Beyond Pain

Masimulizi: Beyond Pain

SEHEMU YA 19
MTUNZI😛ATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
?nashukuru sana Clara kwa uamuzi wako wa
kubaki nami.Hata mimi sikuwa tayari
kukupoteza kirahisi rahisi namna hii kwa
sababu ya mwanamke mwendawazimu kama
Emmy.Nakuahidi nitakuwa nawe siku zote na
sintakubali yule kichaa akuguse tena.Safari
hii nimedhamiria kumfundisha adabu.na kama
anahitaji kuufahamu ubaya wangu basi
ajaribu kunifuatilia tena.Iwapo atanifuata
fuata tena sintakuwa na huruma kwake hata
kidogo.? Nikasema na kumfanya Clara
atabasamu.
?Wayne muda unakwenda kwa kasi .Jiandae ili
tuweze kuondoka hapa hospitali kwa sababu
daktari amekwisha toa ruhusa? Clara akasema
huku taratibu akinishika mkono na
kunishusha kitandani.Akanisaidia kuvaa nguo
zangu halafu taratibu tukatoka pale hositali
na kuondoka.Sikutaka kwenda na Clara
nyumbani kwangu tena kwa kuepusha
mtafaruku mwingine.Niliichukia mno nyumba
ile licha ya kwamba ni nyumba yangu
mwenyewe.Badala yake tulikwenda kuchukua
chumba hotelini ili tupumzike kwa usiku
mmoja kabla ya kupanga nini kinaendelea.
ENDELEA?????????..
Ni usiku wa saa saba.Chumba kilikuwa na
mwanga mdogo uliotoka katika taa iliyokuwa
pembeni ya kitanda.Muziki laini wa ala
ulikuwa ukisika kwa mbali.Clara alikuwa
amekiegemeza kichwa chake karibu na kifua
changu huku mkono wake mmoja ukinichezea
kifuani.Sikuhisi tena maumivu ya
kichwa.Nilisikia raha ya ajabu mno.
?Wayne umefikiria kufanya nini ili kujiepusha
na kadhia zisizokwisha za Emmy? Clara
akauliza kwa sauti ndogo
Nikamtazama usoni mrembo yule mwenye
uzuri uliotukuka nikanyoosha mkono na
kuzishika nyewe zake ndefu
?Nimefikiria kuachana naye kisheria.Nina
maana kwamba nitampa talaka yake
mahakamani ili hata sheria isimtambue kama
mke wangu halali.?
?Unadhani atakubaliana nawe kuhusu suala la
talaka?
?Hayo ni mamuzi yangu na ni lazima
ayakubali.Hii ndiyo njia pekee ya kuweza
kuachana naye.Bila hivyo atanisumbua sana
kwa sababu kisheria bado anatambulika kama
mke wangu halali wa ndoa.?
Clara akaniangalia kwa makini usoni kisha
akasema
?Wayne pamoja na mambo yote aliyoyafanya
Emmy kuna kitu kimoja nataka kukuomba?
?Sema chochote Clara nitakupatia?
nikamwambia na kumfanya atabasamu
?Naomba kesho ukamtoe Emmy polisi na ufute
kesi inayomkabili?
Nilistushwa sana na ombi lile la Clara
ikanilazimu kuinuka na kukaa kitandani na
kumtazama kwa makini
?Unasema nini Clara !! Nikauliza
?Nasema hivi naomba kesho ukamtoe Emmy
polisi na ufute ile kesi .Usipofanya hivyo
anaweza akafungwa gerezani?
Nilishindwa nimjibu nini Clara ikanilazimu
kucheka kidogo
?Usicheke Wayne.Kweli ninaomba ukamtoe na
ufute ile kesi?
?Clara ninacheka kwa sababu hilo ni jambo
ambalo haliwezekani hata kidogo.Mimi
ninataka afungwe tena kifungo kirefu gerezani
kwa sababu ndiko mahala pekee anakostahili
kuwepo,Mwanamke baradhuli yule anastahili
kifungo gerezani.? Nikasema nikiwa na
uchungu mwingi nikikumbuka kila jambo
ambalo Emmy amenifanyia.
?Wayne nafahamu ni jinsi gani Emmy
alivyokuumiza moyo wako.Nimekuwa nawe
kwa kipindi hiki kifupi na nimeyashuhudia
mambo ya Emmy.Amenitukana na kuniumiza
sana lakini pamoja na hayo yote aliyoyafanya
bado moyo wangu unakuwa mzito sana
kuacha afungwe gerezani.Sielewi ni kwa nini
imenitokea hivi .Namuonea huruma sana
.Wayne sintakuomba kitu kingine chochote
zaidi ya hiki.Naomba umsaidie Emmy aweze
kutoka ?
Niliinama nikatafakari kwa muda.Nilimshang
aa sana Clara kwa uamuzi ule.Niliyatazama
macho yake wakati akiongea na nilihakikisha
kwamba alikuwa akimaanisha kile
alichokisema.Lengo langu lilikuwa ni
kuhakikisha kwamba Emmy anafungwa
gerezani na hivyo kuniachia uhuru wa
kujivinjari na malaika wangu Clara.Kitendo
cha kumfutia kesi Emmy kingemfanya
aendelee kuniandama kila kukicha na
kunifanya niishi maisha ya ndege.
?Unaniahidi nini Wayne? Clara akaniuliza tena
na kunistua toka mawazoni
?Ok ! kwa vile ni wewe umeomba basi
nitafanya hivyo.Tutakwenda sote kesho
kumtoa Emmy na kuifuta kesi.Baada ya hapo
nitawakusanya wazee na kuwataarifu rasmi
kuhusu azma yangu ya kuachana na Emmy
kisheria na kisha nitaanza kushughulikia
taratibu zote za kumuacha kisheria.Ila
napenda kukuonya kitu kimoja kwamba Emmy
ana roho ya kikatili sana,si mtu wa kuonea
huruma hata kidogo.?
?Ouh ! Wayne thank you so much my
love.Umenifanyia kitu kikubwa sana.Maandiko
yanatufundisha kwamba tuwe na moyo wa
kusamehe.Mimi nimemsamehe Emmy ? Clara
akasema huku akiiweka mikono yake yote
miwili kifuani Nilisikitika sana kwa Clara kuwa
mwepesi vile wa kumsamehe Emmy.hakuwa
akimfahamu Emmy kiundani.Emmy hakuhitaji
msamaha.Emmy alikuwa na roho ya kinyama
sana.
***********************
Saa tatu za asubuhi siku iliyofuata ilitukuta
tayari tumekwisha wasili katika kituo cha kati
cha polisi.Tulienda kushughuikia kufuta kesi
ya Emmy kama Clara alivyokuwa ameomba
Haikuwa kazi rahisi sana kufanya hivyo hasa
ukizingatia ukubwa wa kosa alilolifanya
Emmy ambalo lingeweza hata kusababisha
kifo.Tulihangaika sana na mpaka ilipotimu
saa saba za mchana ndipo tulipofanikiwa
zoezi letu la kuifuta kesi na kumtoa Emmy .
Hakutaka kuongea nasi badala yake
aliponiona nimesimama na Clara alituangalia
kwa chuki ,akasonya na kupiga hatua
kuondoka maeneo yale
?Clara nilikwambia huyu mwanamke ni
shetani.Ona dharau anazozionyesha.hata
shukrani hana.Hakukuwa na sababu yoyote ya
kumuonea huruma.Tulitakiwa tumuache
kwanza aende jela ili akajifunze adabu.?
Nikasema nikiwa na hasira
?Usijali Wayne.Asikuumize kichwa Pamoja na
dharau zote alizozionyesha lakini nashukuru
kwa kuwa moyo wangu una amani .Najisikia
furaha sana kwa Emmy kutoka.Nashukuru
sana kwa jambo hili.Usiumize kichwa kwa
suala hili.twende tukapumzike kabla
hujakutana na wazee jioni ya leo? Clara
akaniambia huku amenishika
mkono.Tukawaaga maafisa wa polisi
waliokuwa wametusaida kulifanikisha jambo
lile ambao kila mmoja alishangaa kwa namna
Emmy alivyoondoka kwa dharau pale
kituoni.Kisha maliza kuagana ,tukaingia garini
na kuondoka zetu kurudi hotelini kupumzika ..
saa kumi na moja za jioni tayari nilikwisha
jiandaa kuelekea katika kikao kinachofanyika
nyumbani kwa wazazi wa Emmy.Clara alikuwa
ameniomba kuongozana nami akiwa na wasi
wasi kwamba pengine Emmy anaweza
akanifanyia vurugu..Kutokana na mambo
aliyonifanyia Emmy sikuwa na hamu hata ya
kuiona nyumba yangu tena.Nyumba ambayo
kwa miaka mingi imekuwa ni sehemu ya
maisha yangu leo hii niliiona ya moto na
sikuwa radhi hata kutia mguu ndani
yake.Kabla sijaingia katika ndoa nilikuwa
nikisikia toka kwa watu mbali mbali au kupitia
nyimbo na simulizi mbali mbali kwamba kuna
nyakati ndoa hubadilika na kuwa
ndoano.Sikuelewa usemi huu ulimaanisha kitu
gani hadi yalipokuja kunikuta ndipo
nilipotambua maana ya usemi ule.Ndoa ni
tamu kama ukimpata mtu aliye sahihi lakini
ukimpata ambaye si sahihi ndoa huchacha na
hupoteza utamu wake wote na hutatamani
kuisikia tena maishani mwako..
?You look so nervous? akasema Clara wakati
akijifunga mkanda na kunistua toka
mawazoni.Nikageuza shingo na kumtazama ni
katabasamu
?Yah..I?m a bit nervous .Nimekwisha choka
kabisa na maisha haya ya vurugu kila
kukicha.Nataka kuishi maisha ya amani na
furaha .Najaribu kutafakari ni lini mambo
haya ya vurugu na chuki yatakwisha na
nikawa huru? Nikasema taratibu
?Usife moyo Wayne,mambo haya yatakwisha
tu.Mungu atakusaidia.? Akasema Clara huu
amenishika bega
?Yah ..nadhani kuanzia jioni ya leo nitakuwa
na uhuru na amani.? Nikasema na kuinama
chini.Clara akanitazama na kusema
?Wayne sidhani kama litakuwajambo la busara
mimi kwenda pamoja nawe.Yule mwanamke
anaweza akanitolea maneno machafu na
nikashindwa kuvumilia halafu tukaanzisha
zogo mbele ya wazee.Sitaki jambo hilo
litokee.Mimi naona ni bora kama nitabaki
hapa hapa hotelini ? akasema Clara.Nikafikiri
na kuona maneno yake yana busara kwa
sababu Emmy ni mwanamke mwenye tabia
chafu sana na hasiti kumtukana mtu yeyote
hata mbele ya wazazi wake.Nisingeweza
kuvumilia kuona Clara akitukanwa na Emmy
na hivyo nikaona ni bora abaki.
?Sawa Clara.Hilo ni jambo la msingi
sana.Ngoja niende mimi peke yangu
nitahakikisha kila kitu kinakwisha leo mbele
ya wazee.Mwanamke yule ni nusu kichaa na
kama ulivyosema anaweza akakukutukana
mbele za wazee kitu ambacho siwezi
kukivumilia .? Nikasema na kumvutia Clara
kwangu nikambusu
?Nakutakia kila la heri mpenzi wangu.Mambo
yote yatakwenda sawa.Usiwe na hofu hata
kidogo? akasema Clara akiwa amekiegemeza
kichwa chake kifuani kwangu
?Thank you so much my angel.I love
you?Nikasema na kumbusu tena
?I love you too Wayne.Drive safe? akasema
Clara nikashuka na kumfungulia mlango
akashuka akanibusu tena na kisha akaanza
kutembea kuelekea hitelini.Nilisimama kwa
muda huku nikitabasamu nikimuangalia
malaika huyu akitembea kwa madaha ule
mwendo wanaopenda kutembea wanamitindo
wengi.
?Ee Mungu nakushukuru kwa kuniletea
mrembo huyu .Kwa kuwa naye ninajihisi kama
ninaishi tena.Baada ya Emmy kunitenda
nilijiona kama mfu.I felt dead but now I feel
life.? Nikaomba kimoyomoyo kisha nikaingia
garini.
?Ninampenda Clara toka moyoni.Kwa mara ya
kwanza ninahisi kupenda toka moyoni.Hata
Emmy sikuwahi kumpenda kama
ninavyompenda Clara.? Nikawaza nikiwa
garini kuelekea nyumbani kwa wazazi wa
Emmy katika kikao.
?Leo ni mwisho wangu na Emmy.Nataka
akome kabisa kunifuatilia na aniache niishi
maisha yangu kwa amani na Clara.Najuta
sana kufahamiana na Emmy.Nimepoteza
muda mwingi nikitegemea nina mtu maishani
kumbe nilikuwa naishi na shetani
ndani.Mwanamke yule hafai kabisa kuwekwa
ndani kama mke, na kwa vituko alivyonifanyia
hakuna mwanaume yeyote duniani ambaye
anaweza akamvumilia.Kweli nimeamini si kila
mwanamke anafaa kuwa mke.Namsikitikia
sana Baraka.Mtoto yule mpaka sasa hivi hajui
aelekee wapi,hamfahamu baba yake ni
nani.Toka amezaliwa alijua kwamba mimi ni
baba yake mzazi.baadae amekuja kuambiwa
kwamba baba yake ni Chris na sasa
anaambiwa tena kwamba Chris si baba
yake.Mtoto huyu lazima ameathirika
kisaikolojia na maisha yake lazima
yatayumba sana.Damn you Emmy ! ?
Nilishikwa na hasira za ghafla baada ya
kufikiria kuhusu mateso na machungu
aliyonayo mtoto Baraka.
************************
Niliwasili nyumbani kwa wazazi wa Emmy
nikapokelewa na baba yake Emmy .Mara
Baraka akaja akikimbia na kunikumbatia.Ak
anisalmu.Nilishindwa kuyazuia machozi
kunidondoka baada ya kumuona
Baraka.Nilimpenda sana mtoto huyu ,niliamini
yeye ndiye maisha yangu .Hata baada ya
kugundua kwamba si mwanangu Baraka
ameendela kuwa sehemu ya moyo
wangu.Namuwaza kila dakika ya maisha
yangu tatizo ni kwamba mama yake amekuwa
hataki kabisa Baraka akaribiane
nami.Nilimshika Baraka na kukumbuka mbali
sana jinsi nilivyokuwa nikiishi naye kama
mwanangu.
Baada ya maongezi mafupi na baba mkwe
pale nje akanikaribisha sebuleni ambako
kulikuwa na watu ambao kwa hesabu ya
haraka haraka hawakupungua thethili.Wengi
walikuwa ni wazee wa heshima.Niliwasalimu
wote kwa pamoja na kisha nikaelekezwa
mahala pa kukaa nikapatiwa kinywaji.Dakika
kama nane hivi toka nimewasili pale ndani
Emmy akaingia .Alikuwa amevaa miwani
mikubwa kuyafunika macho yake
,akawasalimu watu wote mle ndani na kisha
akatoka nje ambako alikuwa na maongezi
kidogo na baba yake Mama yake Emmy
hakuonekan akujishughulisha na suala lolote
kuhusiana na Emmy,yeye alikuwa amekaa
pamoja na akina mama wengine wakiongea
na kucheka pale sebuleni .
Emmy na baba yake wakaingia tena sebuleni
na Emmy akaenda kukaa pembeni ya zuria
walilokuwa wamekalia akina mama.Baba yake
akanong?onezana jambo na mzee mmoja
mwenye mvi nyingi na kisha akakohoa kidogo
na kusema
?Ndugu zanguni napenda kuchukua nafasi hii
kuwakaribisheni sana katika kikao hiki cha
dharura.Wengi mmepata taarifa kwa
kuchelewa na ninashukuru sana kwa kuweza
kufika.Ni mzee Mmasi pekee ambaye bado
hajafika mpaka mida hii lakini nina imani
atakuwa njiani kwani alinihakikishia kwamba
lazima atafika.Ndugu zangu najua mtakuwa
mkijiuliza sana kuhusu dhumuni la kuitana
hapa mida hii.Kwa ufupi tu ninaweza kusema
kwamba watoto wetu hawa wawili Wayne na
Emmy wana matatizo katika ndoa yao
Nadhani nyote mmekwisha yasikia sina haja
ya kuyarudia tena hapa.Mgogoro huu
umekuwa ukichukua sura mpya kila
kukicha.Leo linazuka hili ,kesho linazuka lile
ilimradi kila siku kumekuwa na matukio .Ndoa
ya watoto wetu naweza kusema kwamba
imepapigwa na dhoruba kali na sijui kama
inaweza ikahimili dhoruba hilo.Nasikitika
sana kwa sababu ni mapema sana kwa wao
kuingia katika matatizo makubwa ya namna
hii.Kutokana na hali kuendelea kuwa mbaya
kila kukicha kijana Wayne aliniomba niitishe
kikao cha wazee akadai kwamba kuna jambo
anataka kutueleza.Yeye wazazi wake wako
mbali kwa maana hiyo sisi tuliopo hapa
tunasimama kama wazazi wake na wazazi wa
Emmy.Naombeni tumsikilize kijana wetu kwa
analotka kutueleza.Karibu sana Wayne.?
Akasema baba mkwe na kunikaribisha.N
ikasimama na kuwasalimu tena wazee wale
kwa mara ya pili.
?Wazee wangu napenda kutoa shukrani zangu
za dhati sana kwa kuahirisha shughuli zenu
mbalimbali na kufika hapa kunisikiliza mimi
kijana wenu.Kama baba mkwe alivyowadokeza
ni kweli kwamba ndoa kati yangu na
mwenzangu Emmy Imepigwa na dhoruba kali
sana na ninaweza kusema kwamba
imeshindwa kuhimili dhoruba hilo na sasa
inaelekea kuzama baharini ? Nikanyamaza na
kuwatazama wazee wale waliokuwa kimya
kabisa wakinisikiliza.Emmy alikuwa ameinama
akichezea simu yake.Sikumjali nikaendelea.
?Nina hakika nyote mtakuwa mnafahamu au
mmesikia mambo yaliyoipata ndoa yetu.Kwa
kweli ni mambo ya aibu na nisingependa
kuendelea kuyaongelea hapa kwa sababu
yanafahamika kwa kila mtu.Labda kwa
kuweka kumbu kumbu sawa na kwa faida ya
wale ambao hawakuwa wakifahamu
kilichotokea ni kwamba baada ya miaka
kadhaa ya ndoa yetu niligundua kwamba
mwenzangu hakuwa mwaminifu katika ndoa
yetu.Niligundua kwamba mtoto ambaye siku
zote nilikuwa nikiamini na kumpenda kama
mwanangu si mtoto wangu.Nililigundua hilo
baada ya kunasa mawasiliano kati ya Emmy
na rafiki yangu wa karibu sana aitwaye Chris
nafikiri wengi mnamfahamui kwa sababu
ndiye aliyeisimamia harusi yetu.Mke wangu
Emmy na Chris walikuwa na mahusiano ya
kimapenzi na kwa mujibu wa mawasiliano
niliyoyanasa Chris alidai mtoto Baraka ni
wake.Awali sikuliamini suala hilo nikafanya
uchunguzi na kugundua kwamba ni kweli
Chris na Emmy ni wapenzi.Ili kujiridhsha zaidi
ikanilazimu kutumia kipimo cha DNA ili
kuhakiki kama Baraka ni mwanangu na kipimo
kikaonyesha kwamba Baraka si mwanangu
.Nilipotoka katika vipimo nilimkuta
mwanzangu tayari amekwisha hama
nyumbani.Nilimtaarifu baba mkwe na kwa
msaada wake tukafanikiwa kwenda hadi kwa
huyo Chris ambako ndiko Emmy alikwua
amehamia na kumkabidhi mwanae ili
amlee.Hivi majuzi nikiwa Zanzibar nilipigiwa
simu na Chris ambaye alikuwa akiishi na
Emmy kwa wakati huo akaniambia kwamba
yeye na Emmy wametengana baada ya
kugundua kwamba Emmy amekuwa
akimdanganya na yule mtoto Baraka si wa
kwake pia.Baada ya kuachana na Chris,Emmy
hakuwa na sehemu nyingine ya kwenda
ikamlazimu kurudi katika nyumba yangu..?
Ghafla nikakatizwa na sauti ya juu ya Emmy
TUKUTANE SEHEMU IJAYO???????
 
Dah mkuu Peterchoka kwa heshima sana naomba ongezea simulizi ata tatu zaid mkuu sanaa
 
Simulizi Nzuri sana haichoshi kusoma kwa kuwa ni ngumu kujua kitakachoendelea....
 
Good job Peter. ...

Hiyo story kuna mtu imemtokea mwanzo mpaka hapo kwenye DNA.

Huko mbele ndio imepishana
 
Kama unataka hiyo simulizi tembelea website ya masimulizi, utaweza kuisoma yote mpaka mwisho. Ipo katika mfumo wa pdf
 
Kama unataka hiyo simulizi tembelea website ya masimulizi, utaweza kuisoma yote mpaka mwisho. Ipo katika mfumo wa pdf
Ungeweka hiyo site hapa mkuu ungekuwa umesaidia!
 
peterchoka, ukuendelea hivi tutakuchoka kama jina lako, aaarggh tangi majuzi twangoja hadithi halafu kimyaaa....
 
Last edited by a moderator:
Kama unataka hiyo simulizi tembelea website ya masimulizi, utaweza kuisoma yote mpaka mwisho. Ipo katika mfumo wa pdf

Asante sana mkuu nimeipata sasa nitaisoma vizuri mwanzo mwisho .....maana nisha dwnld kwenye simu yangu.😊
 
Back
Top Bottom