Masimulizi: Beyond Pain

Lumbi9

JF-Expert Member
Oct 12, 2014
8,564
11,799
BEYOND PAIN
SEHEMU YA 1
MTUNZI : PATRICK .CK
Ni saa kumi jioni nikiwa maeneo ya
Kimandolu nikielekea Usa river katika baa
iliyotulia ya Roterdam garden mahala
panapofanyika vikao vya harusi
yangu.Wanakamati ya maandalizi walichagua
mahala hapa kutokana na utulivu wake kwani
kuna bustani nzuri na hata huduma zake ni
nzuri sana.Nikiwa maeneo haya ya Kimandolu
gari ikienda taratibu kutokana na magari
mengi kukaa pembeni ya bara bara kwa muda
mrefu kwa kupisha misafara ya viongozi wa
jumuia ya Afrika mashariki waliokuwa na
kikao chao hapa Arusha.Siku zote
kunapokuwa na mikutano ya namna hii jijini
Arusha huwa kunakuwa na adha kubwa kwa
watumiaji wa bara bara hii ya Moshi - Arusha
kwa sababu ndiyo bara bara kuu waitumiayo
viongozi hawa wakitokea katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro
(KIA).Mara simu yangu ikaita nikaitazama na
kukuta ni Mr Cheleo mmoja kati ya
wanakamati.
?Haloo kaka? nikasema
?Haloo ,uko wapi? Sisi tumeshafika
tunakusubiri wewe tu.?
?Niko njiani kaka si unajua leo njia ilikuwa
imefungwa viongozi walikuwa
wanaondoka.Ndani ya dakika kumi nitakuwa
nimefika hapo Usa river.?
?Ok kaka tunakusubiri?
Hiki kilikuwa ni mojawapo ya kikao cha
maandalizi ya harusi yangu inayotarajiwa
kufanyika muda wa kama mwezi mmoja
ujao.Harusi ambayo kila mmoja wa rafiki
zangu alikuwa akiisubiri kwa hamu
sana.Nimekuwa mchangiaji mzuri wa harusi
za rafiki zangu na kuhakikisha zinafana safari
hii walikuwa wamepania sana kufanya
sherehe ya harusi yangu kuwa ya kihistoria.
Tulipofika maeneo ya madukani gari zikaanza
kwenda kasi na dakika tano baadae nikawasili
usa river katika baa tulivu ya
Roterdam.Nikapaki gari na kuelekea
bustanini.Nikawasalimia wanakamati na
kuwaomba radhi kwa kuchelewa kisha kikao
kikaendelea.Kilikuwa ni kikao kirefu .
Wakati kikao kikiendelea nikachukua simu na
kumtumia mpenzi wangu Emmy ujumbe
mfupi.Kwa siku tatu nilikuwa na shughuli
nyingi na sikupata hata muda wa kuonana
naye.Kwa sasa emmy anasoma digrii ya
sheria katika chuo kikuu cha Tumaini
makumira.Kila jioni huwa ana desturi ya
kupita kwangu na hata kama sipo kwa kuwa
ana ufunguo wa nyumbani kwangu huwa
ananisubiri mpaka nikirudi tunakaa wote
kisha namrudisha kwake.
?Hallow sunshine,niko kwenye kikao hapa
roterdam.Baada ya kutoka hapa nitapita
kwako.Missing you soooo much.? Huu ndio
ujumbe mfupi niliomtumia Emmy kipenzi cha
moyo wangu.
Tukaendelea na kikao.Baada ya kama robo
saa hivi tangu niutume ule ujumbe mfupi wa
maandishi kwa mpenzi wangu Emmy simu
yangu inaita kuangalia zilikuwa ni namba za
emmy.Nikainuka na kwenda mbali kidogo ili
niweze kuongea naye.
?Halloo Darling ?Nikasema kimahaba.kwani
ndivyo tulivyozoea wakati tunaongea simuni.
Nusura moyo unipasuke kwa mstuko pale
nilipoisikia sauti nzito ya kiume ikijibu.
?Mwanaharamu wewe,mpenda wake za
watu.Huna haya unamwita nani Darling?
Kumbe ndio mchezo wako huo wa kudandia
wanawake wa watu.Leo nimekupata.?
Nilibaki nimeduwaa kwa sekunde kadhaa
nisijue nini cha kusema.sikuelewa yule jamaa
alikuwa akimaanisha nini.Huku nikitabasamu
nikauliza
?Mbona sikuelewi wewe.Unasemaje? samahani
kama simu zimeingiliana?
?Simu hazijaingiliana we juha.We si ndio
Wayne? Wayne mkotela?.
?yah ndio mimi? Nikajibu huku mapigo ya
moyo yakinienda kwa kasi baada ya yule
jamaa kulitamka jina langu
? Wewe si ndio umemtumia Sarafina ujumbe
wa maandishi sasa hivi ukisema unakuja
kumuona ukitoka kwenye kikao?
?Mimi nimemtumia ujumbe Emmy na sio
sarafina?
?sasa sikiliza wewe mjinga?.?Nilihamaki
baada ya kuitwa vile lakini nikavumilia
nimsikie alichotaka kusema
?Iwe ni huyo Sara au Emmy kama unavyojua
lakini nakwambia kuwa huyu ni mke wa mtu
na mimi ndio bwana wake.?..
?Unasemaje wewe??..Nikauliza kwa hamaki
?Hebu mpe Emmy simu yake haraka.Mpuuzi
wewe? Nikasema tena kwa hasira
?Mpumbavu wewe ! hivi nikwambie mara ngapi
Hakuna Emmy hapa?Huyu anaitwa
Sarafina.Kama alikwambia anaitwa Emmy
alikudanganya.Huyu ni sarafina na mimi ndio
mumewe,mimi ndio ninayemlipia hii nyumba
anayoishi na ni mimi ndio niliyemtafutia kazi
pale AICC na baadae nikamtafutia nafasi ya
masomo pale Makumira.Mimi ndiye
ninayemlipia ada na kila kitu.Mimi ndiye
ninayemuweka mjini.Nilikuwa nje ya nchi
nilikuwa napata taarifa kuwa kuna mtu
anatembea na mke wangu nikajua ni utani.Leo
ndio nimegundua kuwa ni kweli? akasema Yule
jamaa.
?Mjinga mkubwa wewe,huna haya mimi ndie
ninayemlipia Emmy ada zote za masomo na
hata nyumba anayokaa mimi ndiye
ninayelipa.Na kwa taarifa yako mpumbavu
wewe,sasa hivi tuko katika maandalizi ya
harusi yetu na kesho jumapili kanisani
wanasoma tangazo la kwanza la ndoa
yetu.Hivyo nakuomba usijaribu kwa namna
yoyote ile kuleta upumbavu wako ? Tayari
hasira ilikwisha nipanda nikatamka maneno
yale kwa hasira.
?Sikiliza we mjinga yaani pamoja na kukueleza
kote huku bado hunielewi sasa Emmy huyu
hapa hebu ongea naye?
Nikasikia akimpa mtu simu na kumlazimisha
?Hebu ongea na huyu mbwa mwenzako
mweleze ukweli mimi ni nani na mkanye
akome kuanzia leo kukufuata fuata la sivyo
nitamfanyia kitu kibaya sana ,hanijui mimi ni
nani mjinga huyu? maneno haya nikayasikia
kwa mbali.Mara nikasikia kitu ambacho
sikukitegemea kukisikia maishani
mwangu.Niliomba ardhi ipasuke niingie
ndani.Nilitamani nijimalize pale pale.sikuona
thamani tena ya kuendelea kuishi katika dunia
hii.
Niliisikia sauti ile tamu na nyororo iliyozoea
kuniburudisha kila siku na kunifanya nione
kama niko peponi,sauti ambayo niliamini ni
sauti nzuri kuliko zote duniani,sauti ya
mpenzi wangu,bibi harusi mtarajiwa
Emmy.Huku akilia kwa kwikwi akatamka
maneno ambayo yalinifanya niichukie dunia
na watu wake na hasa wanawake.
?Wayne I?m sorry mimi ni mke wa mtu,na
ninaomba usiendelee tena kumtukana mume
wangu?
Ilikuwa ni kama niko ndotoni nikazubaa kwa
sekunde kadhaa kisha nikajikaza kiume na
kuuliza tena.
?Emmy is that you????.
?Yes Wayne please leave me alone.Usinipigie
simu tena.Mimi nina bwana wangu?
Machozi yalianza kunitoka.Sikuamini kile
nilichokisikia.
?Please Emmy tell me its not true ? Nikasema
tena huku machozi yakinitoka.
?My name is not Emmy?..Akashindwa
kuendelea alikuwa akilia.Yule jamaa
akachukua tena simu
?Sasa umeamini we kijana.Tafadhali
usiendelee kumfuata fuata sarafina.Kitaka
chokupata usije kumlaumu mtu???..?Akamal
izia kwa tusi zito na kukata simu
Nikahisi miguu ikiisha nguvu nikaakaa chini.
Christopher rafiki yangu mkubwa alihisi
lazima nitakuwa na tatizo akanifuata
.Akastuka baada ya kunikuta nimekaa chini.
?Wayne.. ?Akaita nikamuangalia sikuwa na
nguvu za kujibu.
?Wayne una tatizo gani?
Akawaita wanakamati wote wakaja mbio na
kuanza kunipepea.Nikaletewa maji
nikanywa.Dakika kama tano hivi baadae
nikaweza kuongea
?Take me home? Nikamwambia Chris
?Wayne una tatizo gani.Twende hospitali?
Akasema Chris
?No ! take me home? Nikasema huku nikijaribu
kuinuka.Wakanisaidia kutembea hadi garini
kisha Chris akawasha gari na kuondoka
kunipeleka nyumbani.
Picha mbali mbali zikawa zinakuja na
kupotea.Nilihisi kama vile niko ndotoni .Chris
aliendesha kwa kasi bila kunisemesha.Tul
ipofika maeneo ya sanawari nikafungua
mdomo na kumwambia Chris.
?Nipeleke kwa Emmy? Chris alikuwa
akipafahamu anapoishi Emmy hivyo tulipofika
maeneo ya Ilboru akakata kushoto na moja
kwa moja akaelekea nyumbani kwa Emmy.
Alisimamisha gari nje ya nyumba ya
Emmy.Sikuongea kitu nikafungua mlango
nikashuka garini.Mlinzi wa kimasai wa
nyumba ya Emmy alinifahamu hivyo
aliponiona akanisalimia nikapita zangu hadi
ndani.Chris naye alikuwa akinifuata kwa
nyuma.Nilisimama mlangoni na kusikia watu
wakinong?ona kwa ndani.Nilikuwa na funguo
ya mlango nikaufungua bila kugonga na
kuingia ndani.Sebuleni nilimshuhudia Emmy
akiwa kifuani kwa baba mmoja mnene wakiwa
katika mahaba mazito.Nikaanguka na
kupoteza fahamu.
* * * *
Nilizinduka na kujikuta mahala
nisipopafahamu.Nilikuwa katika chumba
chenye harufu ya dawa.Ndani ya chumba hiki
kulikuwa na watu kadhaa.Mtu wa kwanza
kumtambua alikuwa Chris.
?Pole sana Wayne?.Akasema huku akinishika
kichwa.?Tafadhali usiinuke , endelea
kupumzika.? Muda huo huo akaja daktari
akiwa ameongozana na wauguzi
wawili,nikajua hapa nipo hospitali.daktari
akanipima kisha akasema
?Kwa sasa unaendelea vizuri.Itabidi ulale
hapa leo ili tuendelee kukuangalia zaidi?
Sikuwa na ubishi ingawa sikuhisi kuumwa
sehemu yoyote ile zaidi ya kichwa kuwa kizito
mno.Daktari akatoa maelekezo kadhaa kwa
wale wauguzi akaandika pia katika kijikadi
kisha akatoka.Pale mlangoni nilisikia
akiongea kama na kundi la watu.na dakika
hiyo hiyo watu zaidi ya ishirini wakaingia mle
chumbani.Walikuwa ni wanakamati ya
maandalizi ya harusi yangu pamoja na baadhi
ya rafiki zangu.Walinipa pole nami
nikawahakikishia kuwa niko salama
wakanitakia usiku mwema wakaondoka.pale
hospitali nikabaki na Chris
?Chris nini kilitokea mpaka nikaletwa hapa?
Chris akanitazama kisha akajibu
?Wayne ulianguka ukapoteza fahamu ,ikanibidi
nikulete hapa katika hospitali hii .Usijali kila
kitu kinakwenda vizuri.Daktari anasema kesho
asubuhi atakuruhusu?
Niliposikia kuanguka na kupoteza fahamu
,ndipo nikalikumbuka tukio zima
lililotokea.Ghafla fahamu zikanipotea tena.
Nilirejewa na fahamu baadae sikujua ni saa
ngapi.Ukiacha yule daktari mmoja
aliyekuwapo mida ile sasa walikuwapo
watatu.hali hii iliniogopesha sana.Nikaogopa
pengine hali yangu si nzuri.Daktari mmoja
mzee mwenye miwani akanisogelea na
kuniuliza
?Wayne unajisikiaje sasa hivi??
?Najisikia safi ila kichwa ni kizito sana.Nahisi
kama kizungu zungu kwa mbali?
?Ok sawa.Hali yako inaendelea vizuri,vipimo
vyote vinaonyesha uko sawa ila unachotakiwa
kwa sasa ni kujaribu kutokuwaza kitu
chochote kinachoweza kukusababishia
ukapoteza fahamu kwa mara nyingine.Jaribu
kupata mapumziko ya kutosha na jitahidi
sana kutokuwaza?..?
Nilimtazama yule daktari sikuwa na jibu la
kumpa.Nafikiri hakujua kitu gani
kilichonipata.Hakuyaelewa maumivu
yaliyokuwa moyoni mwangu.
?Ok dokta nitajitahidi?.Nilisema huku machozi
yakinilenga.
Madaktari na wauguzi wakatoka na kuniacha
chumbani mimi na Chris.hawakutaka Chris
aniache peke yangu kwa kuwa waliogopa
pengine ningeweza kujidhuru.
Niliinuka na kukaa kitandani.Chris akanisaidia
nikakaa sawa.
?Chris I hate the world?Nikasema kwa sauti
ndogo
Chris akanitazama akasema.
?Wayne jitahidi upumzike.Usiwaze lolote kwa
sasa.Everything will be ok?
?No Chris.Nothing is ok.Emmy lied to
me????????Nikasema huku machozi
yakinitoka.
?Don?t cry buddy,be strong? akasema chris
huku akinipiga piga mgongoni
? I loved her .I loved her Chris more than I love
myself.Lakini ona kitu alichonifanyia?
..Nitauweka wapi uso wangu mimi?.?.Uso
wote ulijaa machozi.Iliniuma kupita kiasi.
?Wayne lala kwanza.Tutaongea asubuhi?
Akasisitiza Chris.
?No Chris siwezi lala wakati mwanamke
niliyempenda amenisaliti?.why me????? Why
this pain????
?Ok brother let it out??let it out?.?Akasema
Chris.
?Emmy amenidanganya muda wote huu kumbe
ni mke wa mtu?.?
?what!!!!!!!!? Akahamaki Chris
?Yah! ana bwana wake.Ndiye yule tuliyemkuta
amelala naye kwenye sofa pale sebuleni
kwake.Kwa mdomo wake mwenyewe
ameniambia nisimsumbue yeye ana mume
wake ?
Chris akainuka na kuanza kuzunguka mle
chumbani huku ameshika kichwa.
?Is this true brother?Akauliza
?Yah..kwa mdomo wake amenitamkia maneno
haya?.It hurt Chris it hurt so much.?
?Mwanaharamu huyu??.?Akasema Chris kwa
hasira
?Kesho ndoa yetu inatangazwa kanisani kwa
mara ya kwanza??.nikashindwa
kuendelea.Nilishindwa kujizuia kuangusha
machozi.
?Wayne its gonna be ok.Jitahidi ulale kesho
tutayaongea mambo haya.Usiwaze sana
kilichotokea.Hii ni mitihani tu ya maisha?
Chris alijaribu kwa kila njia kunibembeleza ili
niweze kuwa katika hali yangu ya kawaida
lakini kwa hali halisi jinsi ilivyo ni ngumu
sana.
Ni Jumatano ya wiki hii tumetoka kuandikisha
ndoa kanisani na kesho tangazo la kwanza
linaanza kusomwa.tayari maandalizi yote ya
harusi yamekamilika .Nitauweka wapi uso
wangu mimi.Nitawaeleza nini watu
wanaoisubiri harusi yangu??Nitawaleleza nini
wazazi na ndugu zangu? Simlaumu
mtu.Emmy nilimchagua mwenyewe.Hakuni
chagulia mtu yeyote.Iwapo ningechaguliwa na
wazazi au mtu mwingine , ningekuwa na kila
sababu ya kuwatupia mzigo wa lawama wao
kwa uchaguzi wao usiofaa.Lakini hili lilikuwa
ni chaguo langu mwenyewe..Huu ni mzigo
wangu na inanibidi nisimame kidete
niukabili.Nilijilaza kitandani na sijui hata saa
ngapi nilipata usingizi.
Saa tano asubuhi tayari nilikuwa nyumbani
kwangu maeneo ya majengo.Nilikuwa najisikia
mzima wa afya isipokuwa kichwa kilikuwa
kikiniuma kwa mbali.Chris ndiye aliyenichukua
hospitali na kunirudisha nyumbani.
Mpaka sasa hivi hakuna mtu mwingine
aliyekuwa akijua nini kilichotokea na
kupelekea kupoteza fahamu na kulazwa
hospitali zaidi yangu na Chris.Sikutaka
kuharakisha kuliweka wazi jambo hili
gumu.Nilitaka kuacha kwanza akili yangu
itulie.Nilikaa kidogo sebuleni ,halafu
nikamwambia Chris aniache nikapumzike.
?Brother naomba nikapumzike,halafu
tutaongea jioni.Ila tafadhali naomba
usimwambie mtu yeyote nini kilichotokea..?
?Ok wayne nenda kampumzike ila tafadhali
don?t do anything stupid?Akasema Chris huku
akitoa tahadhari kwani madaktari walimuonya
asikubali kuniacha peke yangu kwa kuhofia
pengine ninaweza kujidhuru.
?C?mon Chris,I?m not a kid.Haya ni mambo ya
kawaida katika maisha.Let me have a rest
then I?ll know what to do next.?
?Ok wayne..nitapita mchana kukuangalia.Nik
uletee chakula gani mchana?
?Nothing Chris.Usiniletee chochote.I don?t feel
like eating anything.?
?Unatakiwa ule Wayne.unatakiwa uwe na
nguvu.?
Sikumjibu kitu nikamtazama na kuondoka
kuelekea chumbani kwangu.
Nilikaa kitandani,nikalifungua kabati langu na
kutoa albamu kubwa la picha.Humu kuna
picha nyingi ambazo nimepiga na emmy
tangu tulipoanza mapenzi yetu .Picha yetu ya
kwanza mimi na yeye ikanikumbusha
tulikwenda picnic Ziwa Duluti.Ni siku
tuliyofurahi sana.Siwezi kuisahau siku
hii.Nikaendelea na kuzifunua picha
nyingine.Wakati nikiendelea na kuzitazama
picha simu yangu inalia.Alikuwa ni mama
yangu.
?mama shikamoo? nikamsalimu
?Marahaba baba ,hamjambo?
?hatujambo mama,vipi mnaendeleaje?
?Huku wote wazima.Ni baba yako tu kichwa
chake kile kinamsumbua sana lakini
anaendelea vizuri?
?Mpe pole sana ?Nikajibu kwa ufupi.
?Vipi mkwe wangu hajambo?
Nikasita kujibu.
?eenh jamani hajambo mama mkwe? Mama
akauliza tena baada ya kuona sijamjibu
?Hajambo mama?Nikajibu huku nikiuma meno
kwa hasira.Mwanamke huyu amewadanganya
hadi wazazi wangu.Iliniuma sana.
?nashukuru kama ni mzima.Vipi mnaendeleaje
na maandalizi ya harusi?
?mama maandalizi ni mazuri.Tunaendelea
vizuri?
?sawa baba.Leo huku wamesoma Tangazo la
kwanza..Hivi ninavyokwambia watu
wanajiandaa isivyo kawaida,kila ndugu
anataka aje kwenye harusi yako.?
Sikuwa na cha kusema.Machozi yalikuwa
yananitoka.
?Mama nashukuru.Nitakupigia baadae
tutaongea vizuri zaidi?
?Sawa baba?
Nilikata simu na kuitupia kitandani.hasira
zikanipanda.
?Damn you Emmy?..?
Nilizungunguka zunguka mle chumbani
nikijaribu kuwaza na kuwazua bila kupata
jibu.Nikatoka na kurudi sebuleni.Nikafungua
kabati ninamoweka cd na kuchukua moja ya
cd niipendayo sana ya mmoja kati ya
wanamuziki mahiri kwenye mziki wa bongo
fleva,Hamis mwinjuma au Mwana F.A .Huu
wimbo wake niliona ni kama vile alinitungia
mimi kwa sababu ulinihusu mimi.Ubeti wa pili
ndio uliniumiza zaidi ukanifanya niurudie tena
na tena
?hata nikitaka kuoa niambie ntamuoa nani?/
watu wana watu wao wengine toka zamani/
ukiambiwa we ni boyfriend haimaanishi uko
peke yako/
wadogo usoni wanahifadhi wazee wako/
sijui ni dhiki au tamaa tu??/
watoto wanaanika njaa tu/
hawafikirii mapenzi wanachoona wao ni
mkwanja tu/?
Maneno haya yalinichoma moyo.Kijana huyu
aliimba vitu vya kweli kabisa na yote
aliyoyaimba yamenikuta mimi.
Nikarudi tena chumbani sikujua nini cha
kufanya.Nilikuwa kama nimechanganyikiwa
vile.Nikaona ni bora nijilaze kitandani na
kijiusingizi kikanipitia.
Nilistuka na mlio wa simu iliyokuwa kichwani
kwangu,alikuwa ni Chris.
? Haloo? Nikasema
?Wayne umelala??
?Ndiyo nilikuwa nimelala?
?Ok .Sasa wayne naomba uwe na moyo
mgumu na usihamaki tafadhali.Ni kwamba
Emmy amenifuata na hapa nilipo niko naye
na ni yeye ndiye alinisisitiza nikupigie simu
hii.?
?Unasemaje Chris????? ?Nikasema kwa
ukali.Sikutegemea kusikia kitu kama kile.
?Wayne niko na Emmy hapa.amenitafuta na
kuomba nafasi ya kuongea na wewe?
?Chris????..?Nilidakia,sikutaka aendelee tana
kunipa habari za yule baradhuli
?Chris tafadhali.Kama na wewe unataka
tukosane hamna shida ila tafadhali naomba
usinipe habari zozote kuhusu huyu
mwanamke.?
Nikakata simu.Mwili wote ulikuwa
unanichemka kwa hasira.Sikutaka kumsikia
tena emmy katika maisha yangu.Nilikuwa na
hasira mbaya mno kwa kitendo alichonifanyia
na kama angekuwa karibu yangu sijui hata
ningemfanya kitu gani.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO?????????..
 
SEHEMU YA 2
MTUNZI : PATRICK .CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
? Haloo? Nikasema
?Wayne umelala??
?Ndiyo nilikuwa nimelala?
?Ok .Sasa wayne naomba uwe na moyo
mgumu na usihamaki tafadhali.Ni kwamba
Emmy amenifuata na hapa nilipo niko naye
na ni yeye ndiye alinisisitiza nikupigie simu
hii.?
?Unasemaje Chris????? ?Nikasema kwa
ukali.Sikutegemea kusikia kitu kama kile.
?Wayne niko na Emmy hapa.amenitafuta na
kuomba nafasi ya kuongea na wewe?
?Chris????..?Nilidakia,sikutaka aendelee tana
kunipa habari za yule baradhuli
?Chris tafadhali.Kama na wewe unataka
tukosane hamna shida ila tafadhali naomba
usinipe habari zozote kuhusu huyu
mwanamke.?
Nikakata simu.Mwili wote ulikuwa
unanichemka kwa hasira.Sikutaka kumsikia
tena emmy katika maisha yangu.Nilikuwa na
hasira mbaya mno kwa kitendo alichonifanyia
na kama angekuwa karibu yangu sijui hata
ningemfanya kitu gani.
ENDELEA?????????.
?Hana haya mwanamke huyu.Kwa hiki kitu
alichokifanya halafu leo anataka kuongea na
mimi!! Aongee na mimi kitu gani? Kwanza si
ana nguo zake humu .Zote nazipiga
moto.Sitaki kumuona tena machoni mwangu
huyu mwanamke.Amenifanyia kitendo cha
kikatili sana.?
Nikalifungua kabati kwa hasira na kuanza
kutoa ngo zote za Emmy.Nyingi nilimnunulia
mimi mwenyewe na ni nguo za thamani
kubwa.
?Nguo zote hizi nimegharamia hela nyingi
kumbe alikuwa akiniona mimi mjinga namna
hii??.?
Nikazikusanya zote na kwa hasira nikaenda
nazo katika shimo la taka taka na kuzichoma
moto.Sikuondoka mpaka nikahakikisha
zimeteketea kabisa .
Nikarudi sebuleni na kuangalia kama kuna
kitu chochote kinachoweza kumuhusu
Emmy,nikaiskia geti linagongwa.haraka haaka
nikafuta uso na kujiweka vizuri ili mtu asije
gundua nilivyosawajika.
Nilifungua geti na kukuta ni rafiki yangu
anaitwa Erasto.
?karibu Erasto ?ilijilazimisha kuchangamka.
?Ahsante sana wayne?
?Nimekuja kukujulia hali ,niliambiwa na akina
mangi jana ulipata matatizo ukalazwa
hospitali? Akasema Erasto tukiwa tumekaa
sebuleni
?Ndiyo,jana nilipatwa na matatizo ya mstuko
nikaanguka na kupoteza fahamu.Ni mambo ya
uchovu.Si unajua tena ,mambo yamekuwa
mengi sana.? Nikadanganya.Sikutaka mtu
yeyote agundue kilichotokea kati yangu na
Emmy
?Du! Pole sana.lakini hivi sasa unaendeleaje?
?Kwa sasa naendelea vizuri.Madaktari
wamenipima na hakuna tatizo
lolote,wameniomba niongeze muda wa
kupumzika.?
Nilishukuru kwa erasto kuja kunitazama kwani
kidogo kichwa changu kilitulia.Tuliongea na
kucheka nikaona kichwa kinakuwa
chepesi.Mida ya kama saa nane hivi Chris
naye akaja akiwa amefungasha
chakula,tukajumuika wote kula.Kwa masaa
haya machache nilifarijika sana na kujiona
kama vile sina matatizo.
Ilipata saa kumi na moja jioni tukiwa katika
maongezi na rafiki zangu ,geti langu
likagogwa.Nikainuka na kwend akumuona
mgongaji.Nilistushwa na ujio usio wa kawaida
wa mwalimu wangu wa dini.katekista
Nzomola ndiye mwalimu wetu aliyetufundisha
mafundishoya ndoa mimi Emmy na watu
wengine kama nane hivi.
?Ouh Mwalimu,Shikamoo? Nikamsalimia kwa
furaha,sikutaka kuonyesha aina yoyote ya
mstuko kwa ujio wake.hajawahi kuja
nyumbani kwangu hata mara moja.
?Marahaba Wayne.Habari za Jumapili?
?Nzuri katekista.?
?Leo sijakuona kanisani,hata mwenzio naye
sikumuona ?
?Leo sikuwa najisikia vizuri ndio maana
sikuja.Si unajua mwalimu nyakati hizi mambo
yanakuwa mengi ?
Katekista akatabasamu.nikamkaribisha
ndani.Nikamtambulisha kwa Chris na Erasto
amabo baada ya kuona nimepata mgeni
wakaaga na kuondoka.
?Ndio mwalimu karibu sana.hapa ndio
nyumbani kwangu.?
?Ahsante nimeshakaribia.?
Kimya kikapita cha kama dakika moja hivi
,katekista akaanzisha maongezi
?Wayne nimekuja hapa ili tuzungumze juu ya
matatizo yaliyotokea?
Kauli ile inanistua.
?Matatizo?? yapi hayo? ikauliza
?yaliyotokea kati yako na mwenzako?
?nani kakwambia kuna matatizo? Nikauliza
tena
?Mwanzako amenifuata nyumbani .Tangu saa
saba mpaka mida hii ndio tumeachana.Amek
uja analia na kutaka tukae tuyaongee
masuala haya?
Nilimtazama mwalimu yule kwa hasira mpaka
akaogopa.
?Mzee Nzomola nakuheshimu mno kama mzee
wangu,umenijenga sana kiroho.Lakini kwa hili
lililotokea naomba usiingilie kabisa.Hakuna
kitu tunachoweza kuongea hapa.Halafu
mpaka hapa nilipo kichwa changu bado
hakijatulia,bado nina hasira na hatuwezi
kuongea lolote na tukafikia muafaka .Mzee
wangu naomba uniache kwanza nitulie halafu
kwa heshima yako nitakuita mimi mwenyewe
tutakaa ,tutaongea.Usione kama
nimekudharau mzee wangu ,hali niliyonayo
sasa hatuwezi kuongea tukafikia
muafaka.Niachie siku mbili tatu,kichwa kitulie
halafu nitakutafuta mimi mwenyewe.Nakuah
idi hivyo.?
Nashukuru mzee Nzomola alinielewa na
akaondoka.
Jumatatu sikwenda kazini,nilituma taarifa
kwa wakuu wangu wa kazi kuwa
ninaumwa.Mida ya kama saa tano nikiwa
nimepumzika sofani nikitafakari simu yangu
inalia.Nikaangalia mpigaji alikuwa ni baba
mkwe yaani baba yake na Emmy.Niliiangalia
simu ile ikiita na kukata ,ikaanza kuita
tena.Nilikuwa na hasira na sikutaka kusikia
lolote juu ya Emmy.Mwishowe nikakata shauri
niipokee tu.
?Haloo mzee shikamoo?
?Nzuri baba hujambo??
?Sijambo mzee wangu ,sijui nyie
mnaendeleaje?
?Sie huku wazima.Vipi ali yako kwa sasa
unaendeleaje?
?Naendelea vizuri tu mzee.Nashukuru Mungu?
Kimya kikapita cha sekunde kadhaa ,halafu
akasema.
?sasa Wayne nimekupigia simu hii nilikuwa na
maongezi na wewe ya muhimu sana.Tafadhali
ni muhimu mno.Uko kazini?
Nikasita kujibu ,nilijua hakuna kingine
kinachoongelewa hapa zaidi ya suala la
Emmy.
?Niko nyumbani mzee? Nikajibu kwa ufupi.
?Ok vizuri .Basi nitakuja mida ya saa kumi za
jioni ili tuongee mwanangu.Tafadhali naomba
unisubiri?
?Sawa mzee wangu nitakusubiri hapa hapa
nyumbani?
Nikakata simu na kuirushia katika
kiti.Nadhani hata huyu mzee aligundua kuwa
sikuwa katika hali yangu ya kawaida.
* * * *
Saa Tisa kama na nusu hivi za jioni nikasikia
honi ikipigwa nje ya geti langu.Nilikuwa
nimejilaza chumbani nikaamka na kwenda
kufungua mlango.Ilikuwa ni gari ya baba yake
Emmy pamoja na gari nyingine mbili jumla
gari tatu.Nikawakaribisha ndani.Sikutegemea
kama kungekuwa na ujumbe mkubwa
vile.Watu zaidi ya kumi.Wengine nilikuwa
nawafahamu kama shangazi yake zake Emmy
na baba zake wadongo lakini wengine ikawa
ni mara yangu ya kwanza kuwaona.Kwa picha
ile ya ule ugeni nilielewa dhahiri kuwa hapa
linaloongelewa ni suala langu na Emmy
hakuna lingine.
Katika friji kulikuwa na vinywaji,hivyo
nikamkirimu ila mmoja na kinywaji
alichohitaji.
Nilisikia wakiongea kichaga,kana kwamba
walikuwa wakielekezana jambo.Halafu mzee
mmoja mwenye mvi na kitambi akakohoa
kidogo na kusema.
?Bwana Wayne tunashukuru sana kwa
ukarimu wako na kwa jinsi ulivyotupokea.h
atukutegema kabisa kama ungeweza
kutukirimu kwa upendo namna hii.Unaowaona
hapa mbele yako ni baba,mama ,mashangazi
na wajomba wa mchumba wako emmy?
Alipotaja neno ?mchumba wako Emmy?
nikauma meno kwa hasira,nikainama
chini.Nafikiri hata wao waligundua kitu.
?Bwana wayne kwa ufupi tumekuja hapa sisi
kama wazazi wa emmy ili kujaribu kuweka
sawa mambo yaliyotokea.Hatukuwa tunajua
nini kinaendela.Sisi tulikuwa katika
maandalizi ya harusi.hatukujua kilichojificha
nyuma ya pazia.Jana usiku ndio baba yake
akatupigia simu na kutukusanya na kutueleza
kuwa kuna tatizo limetokea.Emmy alitueleza
yote mwanzo hadi mwisho bila kuficha hata
kitu kimoja.Kwa kweli tulistuka sana
sana.mama yake presha ikapanda ikabidi
apelekwe hospitali.Tunashukuru Mungu hali
yake imeendelea vizuri na mpaka sasa tunaye
hapa.Kwa kweli kwanza sisi kama wazazi na
wanafamilia ya Emmy tunakupa pole sana
kwa yaliyotokea na vile vile tunakupongeza
kwa ujasiri na uvumilivu wako.Umeonyesha
uvumilivu na busara ya hali ya juu
sana.Angekuwa ni mtu mwingine sijui
tungekuwa tunaongea nini saa hizi.Ni wazi
angefanya mambo ya ajabu sana.?
Akatulia akakohoa kidogo halafu akaendelea.
? Wayne narudia tena kuwa hata sisi suala hili
limetuuma mno.hatukutegemea kama
tungepata aibu ya namna hii.Hii ni aibu
kubwa na hata kuja kukuona na kuongea na
wewe leo hii ni kwa sababu hatuna jinsi.Lengo
letu kubwa la kuja hapa sisi ni kujaribu kuona
nini tufanye ili kuweza kuokoa kile ambacho
tumekwisha kianza.pamoja na kuwa inauma
na bado una hasira lakini najua ndani kabisa
ya moyo wako bado kuna kiasi Fulani cha
upendo kwa emmy.Emmy Amelia sana na
kuomba msamaha mno na kuahidi kuwa
amekwisha achana na yule mtu wake
aliyemsababishia haya yote.Amelia sana na
ametutuma tuje sisi kama wazee tuombe
msamaha kwa niaba yake .pamoja na shetani
aliyepita kutaka kuvuruga mipango mizuri ya
mbeleni ya maisha yenu lakini nina tumaini
kuwa bado kuna kila dalili ya upendo wa kweli
kati yenu.Suala la nyumba ni gumu na mambo
kama haya huwa yanatokea.hakuna nyumba
inayokosa majaribu na misuko suko.Na
mnapojaribiwa ni wazi yupo atakayeanguka
au mkaanguka wote.lakini sikuzote upendo wa
kweli husimama panapo majaribu na hata
mkijaribiwa mwisho wa siku mtabaki
mnapendana na kusimama imara.Sikuzote
wapendanao kweli hata kama wakianguka
hushikana mikono ,wakasimama na kusonga
mbele.Upendo wa kweli siku zote haushindwi
na lolote.Ninaona picha ya upendo wa kweli
ulio kati yenu.Ni upendo hu wa kweli ndio
uliokuzuia kufanya lolote mpaka leo hii.Roho
wa Mungu yuko pamoja nawe na ndiye
anayekuongoza katika kufanya maamuzi haya
yenye busara.kwa maana hiyo Wayne sisi
wazee wako tumekuja rasmi kama wazazi
kukuangukia na kuomba msamaha na kufuta
kila kilichotokea ,tusimame pamoja tushikane
mikono na tusonge mbele.Tumekosa sisi
tunaomba utusamehe sisi.Emmy yuko tayari
kuja kuomba msamaha mbele yetu sisi wazee
wake.hatukuweza kuja naye mpaka
tutakapoongea na wewe na tuone kama
utakuwa tayari kumsamehe mwenzako?
Akamalizia mzee yule ambaye alikuwa
akiongea kama mchungaji vile.Sijui wazee
hawa walikuja na nini manake nilijisikia
maneno yao yakiniingia moyoni na kujikuta
licha ya hasira nilizokuwa nazo kutaka
kumsamehe Emmy.Kuna wakati ulikuwa
unakuja moyo wa kusamehe lakini papo hapo
inakuja picha ya Emmy akiwa amekumbatiana
na lile libaba.Ikija picha hii hasira zinarudi
tena.
Niliinua kichwa niliposikia baba yake Emmy
akikohoa na kutaka kuongea machache.
?Wayne mwanangu,na mimi naona niongezee
machache katika yale aliyoyasema mkubwa
wangu.Kwa kweli pamoja na uzee wangu huu
nilikuwa nimeishiwa maneno ya kusema ndio
maan nikamuachia mkubwa wangu.Ameeleza
kila kitu na sitaki kurudia yale aliyoyasema ila
nata kusema machache kuwa Emmy ni binti
niliyemlea katika maadili mazuri ya kiroho na
kwa kweli alikuwa ni binti mwenye heshima
kubwa.Sikutegemea kwa jinsi nilivyomlea aje
afanye yale aliyoyafanya.Ndio maana hata
mama yake aliposikia mambo haya presha
ikapanda kwa sababu hatukumlea awe mtu wa
namna hii.Nina imani tabia hii aliyoifanya ni
mambo ya tamaa na kuiga.Tena ni baada ya
kutoka nyumbani.Pale alipoanza maisha yake
ya kujitegemea.Mwanzoni alipotaka kuhama
nyumbani na kwenda kuishi mweneyewe
nilikataa kwa kuhofia asije akaambukizwa
kufanya mambo yasiyofaa katika jamii lakini
aliomba sana kuwa anataka ajifunze maisha
ya kuishi mwenyewe ndipo nikamruhusu.Hii si
tabia yake hata kidogo.Hakuwa na tabia
hizi.Ni tamaa tu ya kuwa na pesa na vitu
vizuri vizuri.Toka akiwa mdogo nilimfundisha
kutambua mara moja anapokosea na kuomba
msamaha.Kweli amelitambua kosa alilolifanya
na kuomba msamaha.Mimi kama baba yake
nilikataa kabisa kabisa kuishughulisha tena
na masuala yake baada ya kusikia aibu
aliyoifanya.Aliniomba sana sana nimsamehe
na nimsaidie kuomba msamaha kwako.Kwa
macho yangu niliona katika macho yake kuwa
alikuwa akimaanisha toba ya dhati.Ni hilo
ndilo lilinisukuma mie nimsamehe na
kunifanya nifike hapa leo pamoja na
wenzangu hawa kuomba msamaha kwa niaba
yake kwanza na baadae yeye mwenyewe
atafika hapa na kuomba msamaha kwako
mbele yetu.Wayne hatutaki katika hatua
kubwa mliyofikia mshindwe kuendelea.Mkisa
meheana katika hili nina imani mtakuwa
mmejenga kitu kikubwa sana na nyumba yenu
itajengwa katika kusameheana hata likitokea
kubwa la aina gani.Kwa hayo machache
Wayne mimi kama baba yake naomba sana
niko chini ya miguu yako msamehe mwenzio
na muendelee na mipango yenu ya ndoa kama
kawaida.?
Baada ya baba yake Emmy kumaliza kuongea
akafuata shangazi yake na baba zake
wadogo.Du ! niliombwa kila aina ya
msamaha.Kila aina ya ushawishi ilitumika ili
niweze kumsamehe Emmy.Kwa kweli sijui
wazee hawa walikuwa na kitu gani manake
niliwasikiliza na kujikuta ninakuwa na moyo
mweupe tena wa kumsamehe Emmy.Pamoja
na kwamba zile picha mbaya zilikuwa bado
zikinijia nilijawa na moyo wa
kusamehe.Hatimaye ikaja zamu yangu
kuongea.Kila mmoja akatulia kutaka
kunisikiliza nitasema nini.
?wazee wangu nimewasikilza vizuri.Ujio wenu
leo umenipa faraja sana.Sijui mmekuja na kitu
gani lakini kwa kweli najiona mwepesi na
mwenye furaha sana.Mmenisaidia kuutua
mzigo mzito niliokuwa nimeubeba.Ahsanteni
sana.Wazee wangu kwa kweli lililotokea ni
pigo kubwa kwa moyo wangu.Nimeumia
sana.Kwa kweli sikutegemea jambo kama lile
kutokea kwa mtu kama Emmy tena kwa wakati
kama huu.kama mzee pale alivyosema ni kwa
maongozi ya Mungu niliamua kutumia busara
zaidi katika suala hili.Sijamueleza mtu yeyote
zaidi ya rafiki yangu wa karibu.Sikuwa na
haraka ya kutaka kuutangazia ulimwengu nini
Emmy kafanya.Sikutaka dunia
imchukie.naamini kama mzee alivyosema ni
tamaa za pesa ,mali na vitu vizuri vizuri ndio
ilmponza.Iwapo ningeamua kumdhalilisha
Emmy kwa kutangaza aliyoyafanya
,nisingekuwa nafanya hivyo kwake tu bali hata
kwa wazee wake waliomlea katika madili
mema,ndugu zake,ndugu zangu na hata
wazazi wangu.Pamoja na yote
yaliyotokea,machungu yote niliyoyapata,ma
umivu ya ndani na nje,bado ninathubutu
kusimama nakutamka mbele yenu wazee
wangu kuwa nimemsamehe Emmy na niko
tayari kurudiana naye tena na mipango ya
ndoa yetu kuendelea kama kawaida?
Hawakuamini ,wakanitaka nirudie tena kauli
yangu.Nikarudia tena na kuwahakikishia kuwa
Emmy nimemsamehe kwa moyo mmoja na
wala sina kinyongo naye tena.
Wazee wakainuka na kuja kunipongeza.Kil
ikuwa ni kipindi cha furaha sana.Baada ya
kupongezana baba yake mkubwa Emmy
akasimama na kusema.
?Wayne wewe ni kijana wa ajabu .Katika
kuishi kwangu mpaka nimefika uzee huu
sijawahi kuona mtu mwenye moyo wa ajabu
kama wako Wayne.laiti dunia ingekuwa na
vijana 100 kama wewe basi pangekuwa ni
sehemu nzuri sana kwa kuishi.Mimi binafsi
sijui hata niseme kitu gani.Sijui hata
nikushukuru vipi kwa ujasiri wa kumsamehe
mwenzako.Narudia tena kijana unaongozwa
na roho wa Mungu.Kwa ulimwengu wa sasa si
rahisi mtu kumsamehe mwenzake
aliyemfanyia kitendo kama alichokufanyia
emmy.Ahsante sana kijana.ahsante sana
wayne?
akanishika mkono tena.Akawageukia wazee
wengine na kuwaambia kuwa ni wakati
muafaka kwa Emmy kuitwa .Ikapigwa simu na
baada ya kama dakika kumi hivi Emmy
akaingia ndani.Moyo wangu ukastuka tena
baada ya kuiona sura ya Emmy ikiwa na
macho mekundu yaliyovimba ikiashiria jisni
alivyokuwa akilia.hakutaka kuniangalia
usoni.Uso wake alikuwa kuinamisha
chini.Nilishindwa kuwa na hasira nikamuonea
huruma.
Baba mkubwa wa Emmy akasimama na
kuongea machache.
?Kijana wetu Wayne,na ndugu wote ambao
mko hapa leo,napenda kuchukua nafasi hii
kuongea machache kwa sababu mengi
yamekwisha semwa na nisingependa
kuyarudia tena.Tumemsikia kijana wetu
alivyosema.Toka ndani ya moyo wake
amekubali kumsamehe Emmy .Kwa kuwa
kijana wetu Wayne si mtenda kosa basi
hatuna budi sasa kumpa nafasi mtenda kosa
yeye mwenyewe kwa mdomo wake akiri kosa
na kuomba msamaha kwa mchumba
wake,wazazi wake na kwa Mungu wake.Emmy
uwanja ni wako ,waangukie wazazi wako
uwaombe msamaha pamoja na mchumba
wako?
Kimya kikatanda mle sebuleni.Emmy huku
akilia akainuka na kwenda kupiga magoti
mbele ya baba yake na kulia akiomba
kusamehewa.Baba yake akamshika kichwa na
kumuombea kwa Mungu amsamehe na
kumtangulia katika kila jambo alifanyalo,hala
fu akatangaza kuwa tayari amemsamhehe
mwanae kwa kosa alilolifanya.Emmy akaenda
tena kwa mama yake na kuomba msamaha
kama alivyofanya kwa baba yake.Naye
halikadhalika akamsamehe.Kazi ikawa
kwangu.Akasita kuja kwangu pale
tulipogonganisha macho.Nadhani ni nafsi
yake ilikuwa ikimsuta kwa mambo
aliyoyafanya.Wazee wake wakamuangalia kwa
ukali hali iliyomlazimu kujikaza kisabuni na
kunisogelea.akapiga magoti mbele yangu na
kunishika miguu.
?Wayne, nakosa hata neno la
kusema.Nashindwa nikwambie kitu gani cha
kuweza kulifuta doa nililoliweka moyoni
mwako kwa tamaa zangu.Nimekuumiza
Wayne,na sistahili hata huruma yako.lakini
pamoja na hayo yote niliyokufanyia naomba
ufahamu kitu kimoja kuwa toka ndani ya
moyo wangu bado nakupenda sana na
ninaomba msamaha wa dhati kabisa
.Naomba unisamehe na tuendelee na mipango
yetu ya ndoa kama tulivyokuwa
tumepanga.naahidi sintafanya tena kosa
kama hili katika maisha yangu.nakuahidi
kuwa mke mwema kama utanisamehe.naomba
msamaha wako Wayne..?
Emmy macho yalikuwa yamejaa
machozi,akilia kwa kosa alilokuwa
amelifanya.Hata mimi ilikuwa ikiniuma sana
na nilikuwa nikijiuliza mara mbili mbili kama
ni kweli nimeamua kwa dhati kumsamehe?
Nikakubaliana na moyo wangu kuwa nikubali
kumsamehe.Nikamshka mkono nikamuinua na
kumtazama usoni.
?Emmy,nakubali ulinikosea.Lakini kama
tunavyofundishwa kila siku nav iongozi wetu
wa dini na kama maandiko yanavyosema
kuhusu kusamehemana,mimi kwa moyo wangu
wote nimekubali kukusamehe.Nakuombea kwa
Mungu naye akusamehe na tuendelee na
mipango yetu ya ndoa kama kawaida ?
Maneno yale machache yakampa Emmy faraja
kubwa na kumfanya ainuke na kunikumbatia
kwa furaha.Sebule yangu ikageuka sehemu ya
furaha kubwa.Watu tukashikana mikono na
kupongezana.Lilikuwa nitukio kubwa na la
kihistioria katika maisha yangu.Vinywaji
vikaletwa tukaendelea kuburudika hadi
ilipotimu saa mbili za usiku tukaagana
wakaondoka.Walipoondoka nikabaki
mwenyewe nikitafakari juu ya kilichotokea.Pa
moja na kumsamehe Emmy lakini bado roho
yangu haikuwa ikimtazama kama nilivyokuwa
nikimtazama hapo zamani.
?Hivi ni kweli roho yangu imekubali kwa dhati
kumsamehe Emmy kwa kitu alichonifanya??
Nikajiuliza tena kwa mara ya pili.Saa chache
zilizopita sikutamanai kkumuona tena Emmy
katika maisha yangu kuokana na kitendo kile
lakini sasa nimeamua kumsamehe.
?Kwa vile nimamua kumsamehe acha tu
nimamehe.Nahisi amekiri toka moyoni
mwake.?Nikajisemea mwenyewe.
Maisha mapya yakaanza tena.Penzi letu
likaonekana kama vile limechipua
upya.Upendo ukaongezeka mara dufu.Enmmy
alionekana kubadilika sana na hiyo
ikanihakikishia kuwa hawezi kurudia tena kosa
alilolifanya.
Taratibu jeraha lililokuwa moyoni mwangu
likaanza kufutika.Nikaanza kusahau yote
yaliyokuwa yamepita.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO???????..
 
BEYOND PAIN
SEHEMU YA 3
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Maneno yale machache yakampa Emmy faraja
kubwa na kumfanya ainuke na kunikumbatia
kwa furaha.Sebule yangu ikageuka sehemu ya
furaha kubwa.Watu tukashikana mikono na
kupongezana.Lilikuwa nitukio kubwa na la
kihistioria katika maisha yangu.Vinywaji
vikaletwa tukaendelea kuburudika hadi
ilipotimu saa mbili za usiku tukaagana
wakaondoka.Walipoondoka nikabaki
mwenyewe nikitafakari juu ya kilichotokea.Pa
moja na kumsamehe Emmy lakini bado roho
yangu haikuwa ikimtazama kama nilivyokuwa
nikimtazama hapo zamani.
?Hivi ni kweli roho yangu imekubali kwa dhati
kumsamehe Emmy kwa kitu alichonifanya??
Nikajiuliza tena kwa mara ya pili.Saa chache
zilizopita sikutamanai kkumuona tena Emmy
katika maisha yangu kuokana na kitendo kile
lakini sasa nimeaua kumsamehe.
?Kwa vile nimamua kumsamehe acha tu
nimamehe.Nahisi amekiri toka moyoni
mwake.?Nikajisemea mwenyewe.
Maisha mapya yakaanza tena.Penzi letu
likaonekana kama vile limechipua
upya.Upendo ukaongezeka mara dufu.Enmmy
alionekana kubadilika sana na hiyo
ikanihakikishia kuwa hawezi kurudia tena kosa
alilolifanya.
Taratibu jeraha lililokuwa moyoni mwangu
likaanza kufutika.Nikaanza kusahau yote
yaliyokuwa yamepita.
ENDELEA????????..
Ni siku yetu ya kufunga ndoa.Sikuweza kupata
usingizi usiku mzima.Nilikuwa nikiwaza kama
ni kweli baada ya kupitia msuko suko mkubwa
hatimaye ninakwenda kufunga ndoa.Ilikuwa ni
kama ndoto.
Asubuhi nilikuwa ni mtu mwenye mawazo na
wasi mwingi.Mpambe wangu aliliona hilo
,akajaribu kunitoa wasi wasi na kunifanya
nichangamke.Kwa mara nyingine tena
nikajikuta niukijiuliza kama ninalokwena
kulifanya leo hii ni sahihi na nina uhakika
nalo.Baada ya tafakari ya kina nikaona
hakuna haja ya kuendelea kujiuliza maswali
mengi.Maji nimekwisha yavulia nguo hivyo
sina budi kuyaoga.
?mwenzangu,pokea pete hii iwe ishara ya
upendo na uaminifu kwako.Kwa jina la baba
nan mwana na la roho mtakatifu.Amina?
Nilitamka maneno haya huku nikimvisha pete
ya Ndoa emmy kama mke wangu halali mbele
ya kanisa lililofurika watu wakiwa kama
mashahidi.Wakati nayatamka maneno haya
bado ndnai ya nafsi yangu kuna kitu kilikuwa
kikiniuliza ?Wayne are you sure with what you
are doing? Sauti ile ilikuwa ikiniuliza kama
ninayatamka manenoyale kwa dhati toka
moyoni mwangu..Sikuijali sana sauti ile ,kwa
sababu nilijua nimekubali kwa dhatiya moyo
wangu kufunga ndoa na Emmy.Niliamini
mwangwi ule ulitokana na tukio lililotokea na
ambalo bado jeraha lake halijapona sawa
sawa..Tukio ambalo kusema ukweli haliwezi
kufutioka kiurahisi.
Baada ya kumalizika kwa shughuli za
kanisanii,shghuli kubwa ikafanyika
ukumbini.Ilikuwa ni sherehe ya aina yake na
kila mmoja aliyehudhuria alisuuzika moyo.Saa
sita za usiku tukaondoka ukumbini na
kuwaacha bado watu wakishereheka,tukaenda
katika hoteli tuliyoandaliwa maalum kwa ajili
ya kulala kwa usiku huo kabla ya kuelekea
katika fungate letu tuliloamua kwenda
Zanzibar.
Huo ukawa ni usiku wetu wa kwanza kama
mke na mume.Ni usiku huo ambao naweza
nikasema kuwa maisha yangu yalianza upya.
* * * *
Maisha ya ndoa yalikuwa mazuri na yenye
furaha.Nilionyesha kila aina ya upendo kwa
Emmy.naye hali kadhalika alionyesha upendo
wa kila namna kwangu ilimradi ilikuwa ni
furaha na mashamsham kila siku.Kila asubuhi
ni kama penzi letu lilianza upya.Miezi hii sita
ya kwanza sikuona kitu chochote kibaya cha
kunikwaza na ambacho kingenifanya niseme
ule msemo uliozoeleka wa ndoa
ndoano.Sikuyaona magumu ya
ndoa.Niliwashangaa wale wote wanaodai
kuumizwa na ndoa zao.Sikuelewa ni kwa nini
wengine hawakutaka kabisa kusikia kitu
ndoa.Kwa furaha niliyokuwa nayo nikwa ndani
ya ndoa sikuweza kufikiri kama iko siku
ninaweza kutembea nje ya ndoa.Niliwashan
gaa wale watu ambao wamekuwa na wapenzi
nje ya ndoa zao.Sikuhitaji mpenzi wa nje kwa
sababu nilipata kila kitu nilichohitaji toka kwa
mke wangu Emmy.Kwa muda huu mfupi
nikanawiri na kuvutia zaidi.Nikawa mshauri
maarufu wa kuwashauri vijana wenzangu
ambao bado walikua wakisita na kuogopa
,kufanya maamuziya kufunga ndoa kwa
sababu ndoa ni tamu ajabu. .Nilitolea mfano
wa raha nizipatazo mimi .
Mwezi wa saba toka tufunge ndoa Emmy
akanitaarifu kuwa tayari alikuwa mjamzito.Hii
ikaongeza furaha na upendo mara dufu ndani
ya familia yetu.
Furaha hii haikuwa tu baina yetu bali hata
kwa ndugu na jamaa zetu.Nilimshukuru
Mungu kwa kunipa mke kama
Emmy.Nilimpenda mno mke wangu na hasa
katika kipindi hiki cha ujauzito.Siku zikazidi
kusonga na hatimaye siku ya kujifungua
ikafika na Emmy akafanikiwa kujifungua
mtoto mzuri wa kiume aliyekuwa na afya
bora.Nilifurahi kupita kiasi kwa zawadi ile ya
mtoto.Ndugu ,jamaa na marafiki wakaungana
nasi katika furaha ile kubwa ya kupata
mtoto.Kwa furaha niliyokuwa nayo
nilimzawadia Emmy zawadi ya gari jipya
kabisa kama shukrani zangu kwake kwa
kumleta duniani mtoto wetu mpendwa ambaye
nilipendekeza aitwe Baraka.niliamini mtoto
yule alikuwa ni baraka za mweneyezi Mungu
kwetu.Emmy akafurahi mno kwa zawadi le
niliyompa.
Ukurasa mpya wa malezi ukaanza nikiwa
baba na Emmy akiwa mama.Nilifurahi
kushirikiana na mke wangu katika malezi ya
mwanetu Baraka.Muda wa mapumziko ya
uzazi ulipokwisha ikatyulazimu kumtafuta
msaidizi atakayetusaidia kumlea mtoto wakati
tukiwa kazini.Tulifanikiwa kumpata msaidizi
kwa msaada wa jiani yetu.
Siku zilikatika kama mvua na ikafika miezi
sita.Tukajadili tukaona kuwa huo ndio muda
unaofaa kwa ajili ya kumbatiza
mwanetu.maandalizi yakafanywa na hatimaye
tukafanikiwa kumbatiza mwanetu kwa jina la
baraka.Mtoto akaendelaa kukua akiwa na afya
njema mno.
* * * *
Miaka minne ilipita.Maisha yakiwa ni yenye
furaha na upendo mkubwa.Mtoto wetu baraka
alikuwa anasoma katika shule ya awali ya
Maria Theresa academy.Baraka alikuwa
akiendelea kukua kwa furaha na upendo
mkubwa.
Kwa muda wa miaka yote hiyo hali ya upendo
ndani ya ndoa yetu ilikuwa kubwa na hii
ilitufanya tuwe mfano wa kuigwa.Nilikwisha
sahau yote yaliyotokea kipindi cha
nyuma.Nilichokuwa nikiangalia kwa sasa ni
malezi ya mtoto wetu na kumtengenezea
maisha mazuri ya baadae.
Ilikuwa siku ya Ijumaa siku ambayo sikuwa na
shughuli nyngi za kufanya nikaamua kuwahi
kurudi nyumbani ili kujumuika na famili na
yangu .Siku zote huwa nikipata nafasi
hupendelea kuwahi kurudi nyumbani na
kuitumia nafasi hiyo nikiwa na familia yangu
tukifurahi pamoja.
Nikiwa mita kadhaa kabla ya kufika nyumbani
kwangu nikaona geti likifunguliwa na gari ya
mke wangu ikitoka.Tulipokutana
akasimamamisha gari,akashusha kioo
tukasalimiana.
?Hello Darling? akasema mama Baraka
?Hello honey? nikajibu
?Mbona leo mapema hivi kulikoni? Akauliza
?Nimeamua kuja kukaa na familia
yangu.Sikuwa na kazi nyingi.Safari ya wapi
tena? Nikauliza
?Kuna mama mmoja jirani yetu ni mjamzito
sasa ameanguka ghafla ndio tunataka
tumkimbize hospitali?
?Ouh ! basi wahini mara moja.? Nikajibu naye
akaliondoa gari kwa kasi kumuwahi
mgonjwa..Nikaingiza gari ndani nikasalimiana
na mwanangu Baraka halafu nikamwacha
akicheza mimi nikaelekea chumbani
kwangu.Kitandani kulikuwa na kompyuta aina
ya Laptop ya mke wangu.Kwa kuwa nilikuwa
nikihitaji kupumzika nikaamua kuitoa na
kuiweka pembeni.Kompyuta ile ilikuwa
imechomekwa katika umeme na ilionyesha
kuwa muda mfupi uliopita alikuwa
akiitumia.Kwa haraka haraka nikaona kama
alikuwa akiwasiliana na watu wake kwa
kutumia Yahoo messenger.Kuna meseji
ilikuwa ikikonyeza kuashiria kuwa haikuwa
imesomwa,nikang?amua kuwa Mama Baraka
alikuwa ameondoka ghafla na kumfanya
asahau kuizima kompyuta yake.Nikaamua
kufunga ile Yahoo messenger ili watu wale
aliokuwa akiwasiliana nao wajue kuwa
hayupo.Kabla sijaifunga kabisa ile Yahoo
messenger,nikaliona jina moja limeandikwa
My special one.nikapata udadisi
Fulani.Nikafungua ule ukurasa waliokuwa
wakiwasiliana nikaanza kuusoma .Meseji ya
mwisho ilisema
?Vipi Darling mbona kimya? Are you there???
Baada ya meseji hiyo zikafuata BUZZ
nyingi..Nilikuwa nimesimama nikaamua kukaa
na kusoma sawa sawa.Nikaanza kuisoma
tokea mwanzo.Kutokana na muda ilionyesha
kuwa walikuwa wameanza kuwasiliana kama
dakika ishirini zilizopita.Mfululizo wa
mawasiliano yao ulikuwa hivi
EMMY: Nimeshafika nyumbani dear
MY SPECIAL ONE : Ouh ! good.Mimi bado
niko ofisini
EMMY: Unatoka saa ngapi leo
MY SPECIAL ONE : Leo nitachelewa kutoka
kidogo.
EMMY: Ok poa Darl ,sasa hebu tuendelee
kujadili lile suala la mtoto manake mimi
linalipa wakati mgumu sana
MY SPECIAL ONE: Darl ni kama nilivyokueleza
kuwa mtoto ni lazima nikamtambulishe kwa
babu zake.Nataka mtoto aanze kunizoea
taratibu ili hata baadae akielezwa kuwa huyu
ndiye baba yako mzazi asishangae.Nataka
aanze taratibu kuwafahamu ndugu zake.
EMMY: Darl unanipa wakati mgumu
sana.Nashindwa hata nifanye nini
MY SPECIAL ONE: Usiogope Darl.Unajua
mtoto anakua kwa kasi na anazidi kupata
akili.Kwa maana hiyo inabidi aanze kujua toka
mapema ,nani baba yake nani siye.Nashukuru
kwa ile safari ya mbuga za wanyama
imeniweka karibu naye sana.
EMMY: Yah hata mimi nimefurahi kwa hilo
kwa sababu kila siku ni lazima akuulizie.
MY SPECIAL ONE: Hivyo ndivyo
ninataka.Jaribu kwa kadiri uwezavyo
kumuweka karibu zaidi na mimi.
EMMY: Nakubali Honey mtoto ni wako lakini
siku huyu jamaa akigundua najua ataumia
mno.Hujui ni jinsi gani anavyompenda Baraka
MY SPECIAL ONE: Yah ! I now that.Ni wazi
ataumia lakini hakuna jinsi.Ni lazima ifike
mahala akubaliane na ukweli kuwa mtoto si
wake.Na kwa kweli darling sitaki tuendelee
kulificha hili kwa muda mrefu.nataka ifike
wakati tuchukue uamuzi wa kumueleza ukweli
kuwa mtoto si wake.Tukiendelea kukaa kimya
tutakuwa hatumtendei haki mtoto.
EMMY: Lakini darling ni wazi siku Wayne
akiufahamu ukweli hakutakuwa na jingine
zaidi ya kuachana.Niliwahi kumuumiza mara
moja miaka kadhaa ya nyuma na nikamuahidi
kuwa sintamuumiza tena.Sasa akigundua hili
sijui nini kitatokea.
MY SPECIAL ONE: Honey usijali kitu
chochote.bado naendelea kuweka mazingira
mazuri ili kama kutatokea la kutokea pindi
utakapomueleza ukweli basi moja kwa moja
unahamia kwangu na tunaanzisha
familia,mimi ,wewe na mtoto wetu baraka.
EMMY : (smiley) Are you sure darling?
MY SPECIAL ONE :Yes baby I?m sure.Lengo
langu mimi sikuzote limekuwa kuishi na
wewe.Nataka kuishi na mwanangu.nataka
mwanangu akasome Ulaya.Nataka siku moja
sisi sote tukaishi Ulaya.
EMMY : Ingawa nakupenda na niko tayari
kufanya lolote kwa ajili yako lakini kila
ninapomfikiria mume wangu nafsi inanisuta
sana.Wayne ananipenda kupita maelezo.
MY SPECIAL ONE: Usijidanganye baby kuwa
mumeo anakupenda.Unachotakiwa ni
kuangalia wapi unapata furaha ya
maisha.Fuata moyo wako unavyokutuma.
EMMY : Ok tuachane na hayo.Umepanga lini
umpeleke mtoto kwa babu zake?
MY SPECIAL ONE: Jumamosi ya wiki
ijayo.Anza kuandaa tararibu mazingira ili
Mumeo asiweze kugundua chochote.
EMMY: Nitajitahidi darling
MY SPECIAL ONE: Vipi weekend hii una ratiba
gani?
MY SPECIAL ONE: BUZZ
BUZZ
BUZZ
BUZZ
MY SPECIAL ONE : ?Vipi Darling mbona
kimya? Are you there???
BUZZ
BUZZ
BUZZ
Mawasiliano yakaishia hapa.nadhani ni
wakati huu Emmy alipopata taarifa ya
ugonjwa wa jirani yetu na kumfanya aondoke
ghafla bila hata kukumbuka kuizima
kompyuta yake.Ilikuwa ni kama ndoto ya
mchana.Sikuamini nilichokuwa
nimekisoma,nikakaa vizuri na kurudia tena na
tena .Nikafungua archive na kukuta
kumbukumbu ya mawasiliano kati ya Emmy
na my special one.Jasho lilikuwa likinitiririka,
mapigo ya moyo yakaanza kwenda kwa kasi
isiyoelezeka.Nikakaa kitandani huku nikihisi
kuishiwa nguvu taratibu.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO??
 
BEYOND PAIN
SEHEMU YA 5
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
I know with all my certainty,
What's going on with you and me,
Is a good thing.
It's true, I believe in you.
I believe in Mom and Dad.
And I believe in you???????
?Honey its enough.This song is so touching.?
Emmy akanikatisha nisiendelee
kuimba.Nilikuwa ninaimba kwa hisia kali sana
huku machozi yakinitoka.Nilipomtazama
Emmy naye alikuwa akifuta machozi.Nadhani
hata yeye wimbo ule ulimgusa.
Usiku ule ulikuwa ni moja kati ya usiku mrefu
ambao sikuwahi kuupata katika maisha
yangu.Sikuweza kupata usingizi.Kichwa
changu kilikuwa kimejaa mawazo.Hostoria ya
maumivu yaliyonipata miaka kadhaa ya
nyuma yakanirudia tena.
ENDELEA?????????..
Siku iliyofuata ilikuwa jumamosi,niliamka
asubuhi na mapema nikamuaga Emmy kuwa
ninaenda ofisini kuna kazi nilitakiwa
nikaifanye asubuhi hii na nisinge chelewa
kurudi.Siku ya leo ni mapumziko hivyo ofisini
nilikuwa mwenyewe.Nikaiwasha kompyuta
yangu nikachomeka ile flash disk niliyokopi
mawasiliano kati ya Emmy na my special
one,mtu ambaye sikumjua ni nani.Nilianza
kupitia tarehe moja baada ya nyingine,nikagu
ndua kuwa mawasiliano yao yameanza muda
mrefu.Kwa mujibu wa mawasiliano yao
ilionesha kuwa walikuwa katika kipindi cha
mapenzi mazito.Walikuwa wakiongea mambo
mengi kuhusiana na raha na starehe
wanazopeana.Nikagundua kuwa huwa
wanakutana katika mahoteli makubwa
makubwa na kupeana maraha.Kumbe mara
zote Emmy akiniaga kuwa wana semina au
makongamano huwa anakwenda kuponda
raha na huyo special one.Yote haya
niliyagundua katika meseji walizokuwa
wakiandikiana.Iliniuma mno siwezi
ficha.Nilitamani kutokuendelea kuzisoma
meseji zile lakini ilinibidi nizisome zote ili
kuupata ukweli wote.
Mpaka nilipomaliza kuzisoma chat history
zote nikajikuta sina hata nguvu za kuinuka
kweye kiti.Jasho lilikuwa likinitiririka.
?God where are you? Please help me?
Nikasema kwa uchungu mwingi.
* * * *
Wiki iliyofuata ilikuwa ni wiki ngumu kwangu
kupita maelezo.Nilijitahidi kutokuonesha dalili
zozote zile kuwa kuna jambo lolote
linanisumbua kichwani kwangu.Kila
nilipomuona Baraka furaha yote
ikapotea.Masikini malaika yule hakuwa na
kosa lolote,hakuwa akifahamu kilichokuwa
kikiendelea.Alifahamu fika kuwa baba yake
mzazi ni mimi.Hata mimi bado niliendelea
kuamini hivyo bado sikuwana na uhakika wa
kutosha kwa yale niliyoyanasa kati ya mke
wangu emmy na my special one ni ya
kweli.Nilihitaji ushahidi wa kutosha..Jumanne
jioni baada ya kazi nikaenda kuonana na
rafiki yangu mmoja aitwaye beka anayefanya
biashara ya kuuza magari.Nilimuomba
anisindikize kwenda Same siku ya jumammosi
tukitumia gari lake.Japokuwa alitaka
kufahamu kwa undani juu ya safari hiyo lakini
sikumpa jibu la moja kwa moja.Kutokana na
ukaribu wetu akakubali kunisindikiza Same
kwa kutumia gari lake.
Siku zikaenda kwa kasi na hatimaye ikafika
siku ya Ijumaa.Usiku tukiwa kitandani Emmy
huku akikichezea kifua changu bila kujua
kama alikuwa akinikera kupita kiasi ,akasema
?darling ,kesho ndio ile safari niliyokwambia
.Nasikitika kukuacha mwenyewe,utakuwa
mpweke sana.?
Nikatabasamu na kusema
?Ni kwa nini usimuache baraka ?
?hapana honey .Unajua Baraka kuna wakati
anakuwa msumbufu sana.Acha tu niende naye
asije akabaki akakusumbua .?
?Hawezi kusumbua.Yupo dada yake wa kazi
atakuwa akimlea.?Nikajibu.
?Siku hizi Baraka amekuwa mtundu
sana.Honey acha niende naye.Siku mbili tu si
nyingi .?
?Mtaondoka na usafiri gani? Nikauliza
?Mimi nitaondoka na gari yangu?
Akajibu Emmy huku usoni akionesha dalili za
kutopendezwa na jinsi nilivyokuwa
nikinga?ngania Baraka abaki.Nilikuwa
nikielewa kila kitu hivyo haikunipa shida
yoyote.
?Ok nadhani hat mimi kesho nitaondoka
asubuhi na mapema kuna kazi ninawahi
kwenda kuifanya ? Nikasema
?Ok baby? Akajibu Emmy akanibusu na
kulala.Alipogeuka upande wa pili nikafuta
mdomo wangu mahala aliponibusu kwa
kiganja cha mkono.
Emmy hakujua kilichokuwa kikiendelea moyoni
mwangu lakini ukweli nilikuwa namchukia
kupita kiasi kwa mambo anayonifanyia.P
amoja na hayo niliendelea kujifanya mjinga ili
niweze kupata ukweli wa mambo.Sikutaka
kuyaendea haraka mambo haya mazito.
Asubuhi na mapema,nikaamka ,nikaoga na
kuagana na Emmy.Nikapanda gari langu na
kuelekea nyumbani kwa Beka maeneo ya
Sakina.Nilimkuta tayari amejiandaa
ananisubiri.
Hatukupoteza muda tukaingia katika gari lake
na safari ikaanza.
?Beka najua bado unajiuliza maswali mengi
toka nilipokwambia kuhusu safari hii.lakini
ukweli ni kwamba kuna gari ambayo itabidi
tuifuatilie inakwenda Same.? Nikasema
?Tunaifuatilia gari??Beka akauliza
?yes..kuna gari tunakwenda kuisubiri
Bomang?ombe na tutaifuatilia mpaka Same.?
Beka akakaa kimya akabadili gia na kulipita
lori la mafuta halafu akanigeukia.
?Wayne whats going on? Toka nimekufahamu
sijawahi hata siku moja kukuona ukiwa katika
hali kama hii.Kuna kitu unanificha .Hebu kuwa
muwazi kama kuna tatizo ili tusaidiane jinsi
ya kulitatua. Wewe ni rafiki yangu na tatizo
lako ni la kwangu?
Ni kweli Beka alikuwa mmoja kati ya marafii
wangu amabao naweza kusemea ni wa
kweli.Sikuona sababu ya kumficha tatizo
langu Nikatabasamu na kujibu
?beka,kusema ukweli nina tatizo kubwa lakini
siwezi kukueleza kwa sasa hadi hapo
nitakapokuwa na uhakika wa kutosha.Kwa
sasa naomba tu unisaidie kulifuatilia hilo gali
nitakalokuonesha.?
Beka hakujibu kitu tena,akakubaliana
nami.Akakanyaga mafuta hadi tulipofika eneo
la Boma,tukasimamisha gari pembeni ya bara
bara.
Mpaka saa nne za asubuhi bado Emmy
alikuwa hajapita ,nikawa na wasi wasi
pengine anaweza akawa amepanda gari
jingine,nikaamua kumpigia simu.
?hallow Emmy,umeshaondoka?
?yes? darling nimeondoka muda si mrefu,kwa
sasa nelekea maeneo ya KIA?akasema Emmy.
?Unatumia usafiri gani,wa kwako au
umepanda basi? Nikauliza ili kupata uhakika
zaidi
?Ninatumia gari yangu?
?Ok honey Mimi ndio natoka kazini muda
huu,msalimu baraka?
Nikakata simu huku beka akiniangalia kwa
jicho kali.
?unaongea na mkeo?
?yah ! ni mke wangu? Nikajibu
?Tunamfuatilia mke wako?
Sikujibu kitu nikakaa kimya
?Wayne tell me please.Tunamfuatilia mke
wako.?
?Yes Beka tunamfuatilia mke wangu.?
?ouh My God whats going on Wayne? Beka
akauliza
?Nitakwambia Beka lakini sio sasa.Ni habari
ndefu sana.?
Beka akajua lazima liko tatizo kati yangu na
Emmy.akawa na subira akisubiri muda ukifika
nimueleze mimi mwenyewe kwa mdomo
wangu nini kinaendelea.Tuliendelea kusubiri
huku tukiburudishwa na muziki ,mara
nikaliona gari la mke wangu mama baraka
likija.Nikamstua Beka aliyekuwa nje akiongea
na simu.Akaingia garini tukaanza kulifuatilia
gari lile.
Beka alilifuatilia gari lie kwa ustadi mkubwa
ili tusije shukiwa kuwa tunawafuatilia.gari la
Emmy likaongoza hadi katika hoteli moja
mpya na ya kisasa sana ijulikanayo kama
Uhuru white peak hotel.Hatukuweza kuingia
mle ndani ya ile hoteli kubwa ya kifahari
tukabana sehemu tukiwasubiri watoke.Baada
ya kama saa moja hivi wakatoka na safari ya
kuelekea Same ikaanza.Nadhani walikuwa
wameenda kupata mlo wa mchana
Tulifika Same saa nane za mchana,.Pale
hatukutaka kuendelea kulitumia gari letu hivyo
ikatulazimu tulipaki mahala penye usalama
tukakodisha gari aina ya Noah,tukaendelea
kuifuatilia ile gari ya Emmy.Gari ya Emmy
ikasimama nje ya nyumba moja kubwa yenye
geti la kijani,na kupiga honi.Mara mlango
ukafunguliwa na akashuka mwanaume mmoja
ambaye sura yake haikuwa ngeni
kwangu.Nikavua miwani myeusi niliyokuwa
nimeivaa ili nimuangalie vizuri mtu yule
.Sikutaka kuamini kuwa akili yangu ilikuwa
sahihi.Sikutaka kuamini mtu niliyemuona toka
ndani ya ile gari ni yeye kweli au
wamefanana.Nilibaki mdomo wazi.
?No Its not true.Chris!!!! Nikasema kwa
uchungu.
Ndugu msomaji aliyeshuka toka ndani ya ile
gari ya Emmy alikuwa ni rafiki yangu wa siku
nyingi aitwaye Chris ambaye alifanya kazi
kubwa katika kufanikisha harusi yangu mimi
na emmy.Ni mmoja kati ya watu ambao
mchango wao kwangu sina uwezo wa
kuulipa.Chris mtu ambaye nilimhesabu kama
mmoja wa ndugu zangu kabla ya uhusiano
wetu kuanza kupungua taratibu kiasi cha
kuweza kumaliza hata mwaka mzima
hatujaonana.
Nikiwa naendelea kushangaa nilichokiona,geti
linafunguliwa na gari linaingia ndani..Nilikuwa
nimelowa jasho mwili mzima.
?Tuondoke eneo hili Wayne? akasema Beka
Tuliondoka eneo lile na kurudi hadi mahala
tulipoacha gari letu.Tukamlipa yule jamaa
mwenye ile gari tuliyoitumia akaondoka zake
?Tunaelekea wapi baada ya hapa? Beka
akauliza
Sikujibu kwa haraka.Nilitafakari nini kifuate
baada ya hapo.Niendelee kumfuatilia Emmy
au nirudi nyumbani? Nikajiuliza mwenyewe na
mwishowe nikaamua kurudi nyumbani.
?Twende turudi nyumbani Beka.tayari
nimeshaujua ukweli? Nikasema huku Beka
akiniangalia na kisha akaondoa gari.
Safari yetu ilikuwa ya kimya kimya .Nilikuwa
na mawazo mengi mno .Tulipofika maeneo ya
kwa Sadala Beka akauvunja ukimya.
?Wayne najua si vizuri kuingilia mambo
yasiyonihusu lakini wewe ni rafiki yangu na
kama una jambo lolote linalokusumbua basi
hata mimi linanihusu.Hebu niambie kuna
tatizo gani?
Sikuona sababu yoyote ya kumficha Beka juu
ya tatizo linalonikabili.Nikaamua kumweleza
ukweli wote ulivyo.Beka akasimamisha gari
pembeni ya bara bara baada ya kuusikia
ukweli.Hata yeye alistuka sana.
?Wayne ni ya kweli hayo unayonieleza? Beka
akauliza
?kwa nini nikudanganye Beka.Haya yote ni ya
kweli kabisa.?Nikasema.Beka akavuta pumzi
ndefu na kusema kwa sauti ndogo
? I cant believe this.?
Akanyamaza kidogo halafu akasema
?Kwa jinsi ninavyomfahamu mke wako
niliamini ni mmoja kati ya wanawake waadilifu
mno katika ndoa zao.?
?hata mimi nilikuwa naamini hivyo na sikujua
kama anaweza akanifanyia kitu kama
hiki.Namsikitikia mtoto kwa sababu hajui
lolote.Ninampenda mno Baraka.Niliamini yeye
ndiye mrithi wangu na ndiye furaha ya maisha
yangu.baada ya kugundua kuwa si mwanangu
sijui hata nifanye nini.Ninampenda mno mtoto
yule Beka? Nikasema kwa uchungu.
?Kwa hiyo umepanga kufanya kitu gani? Beka
akauliza.Swali hili kwangu lilikuwa moja kati
ya maswali magumu kujibu.Sikuwa nimepanga
kufanya chochote na wala sikujua ningefanya
nini.Kwa kitendo alichokifanya Emmy sikuona
hata adhabu gani inayomstahili.
?Beka sijapanga bado nifanye kitu gani.bado
nahitaji ushahidi wa kutosha ili niweze
kujiridhisha na hatua nitakazozichukua..I
think I need more time? Nikasema
?More time??.Beka akauliza kwa mshangao.
?More time? Akarudia tena.
? Wayne naona kama unafanya utani na suala
kama hili.Hili si suala dogo kama
unavyolichukulia.Ni suala zito mno.Mkeo
ameisaliti ndoa yenu na ushahidi wa uhakika
unao.Umemfuatilia mkeo hadi Same na
umegundua kuwa anaetembea na mkeo ni
rafikiyo sasa ushahidi gani tena unaouhitaji?
Hebu chukua hatua stahili mapema? Beka
akasema kwa hasira.Beka alikuwa sahihi kwa
upande Fulani lakini bado moyo wangu
ulikuwa mzito kuchukua hatua za haraka.Beka
alikuwa ameukunja uso kwa hasira.Kitendo
kile ni wazi kilikuwa kimemuumiza mno.
?Beka uko sahihi kuwa ushahidi unajitosheleza
kwa kiasi kikubwa.lakini bado nahitaji muda
zaidi wa kufikiri nini cha kufanya.Sitaki suala
hili limuumize baraka.Nataka suala hili
niliendee taratibu? Nikasema
?Taratibu? Beka akauliza tena.
?Wayne sidhani kama suala hili
linakuumiza.Naona unalifanyia
mzaha.Taratibu wakati mkeo bado
anaendelea kukudanganya ,bado anakuona
hayawani,anatembea na rafiki zako halafu
unasema unachukulia mambo taratibu..Be
serious my friend? beka akasisitiza.
?nakuelewa Beka,lakini hizo hatua
unazonisisitiza nichukue ni hatua zipi? Hebu
nishauri? Nikasema
?Hakuna ushauri hapa.Fukuza tu aende kwa
huyo hawara yake.? Beka akajibu kwa hasira
kali.
Nilishindwa kukasirika ikanibidi nicheke .
?sasa unacheka nini Wayne? Wanawake wa
namna hii dawa yao ni kuwatimulia mbali ili
wakafunzwe na dunia.Sipendi watu wasiokuwa
na hisani?
?Huo ndio ujinga wa wanawake.kwa jinsi
ninavyofahamu ni kwamba Chris ana
mchumba wake na tayari amezaa naye mtoto
mmoja.Kwa sasa binti huyo yuko nje ya nchi
kimasomo.Kwa maana hiyo ahadi kwamba
atamuoa Emmy na kwenda kuishi naye nje ya
nchi ni uongo mtupu.Chris akisafiri na kwenda
nje ya nchi huwa anakwenda kumtazama
mchumba wake na si vinginevyo.Iwapo
nikimtimua Emmy hatakuwa na mahala pa
kwenda kwa sababu ninamfahamu vizuri
Chris.Hii ndiyo tabia yake kuwahadaa
wanawake.Ninayemuonea huruma hapa ni
Baraka.?
Beka bado hakuridhika na maelezo yangu
?Wayne mimi nakuonya ,mwanamke huyu si
mzuri na hafai katu kuishi naye.Sikushauri
uendelee kuishi naye.Mtimue haraka sana.?
?Beka najua unachokiongea lakini kumbuka
Emmy bado ni mke wangu wa ndoa na kama
tulivyoelezwa siku tunakula kiapo cha ndoa
kuwa kilichofungwa duniani kimefungwa na
mbinguni.Hilo ndilo tatizo kubwa
linalonifanya nisite kuchukua
maamuzi.Nitawezaje kutengua ndoa hii? ?
Nikasema huku nikishika kichwa.
?Hivi Wayne huyu mwanamke amekupa kitu
gani? Kuna dawa amekulisha wewe si
bure.Haiwezekani ugundue mtu amekufanyia
kitendo kama hiki halafu bado unamruhusu
kulala ndani ya chumba chako.? Beka
akasema kwa hasira
?hahahaha Beka achana na mambo ya
dawa.Unajua mimi huwa sipendi kuchukua
maamuzi ya haraka haraka.Hili ni jambo zito
linahitaji utulivu na busara ya hali ya juu
kulitatua.usiwe na wasi wasi rafiki yangu
suala hili litakwisha.Suala kama hili ni lazima
washirikishwe wazee,viongozi wa dini
n.kTwende tuendelee na safari tutaongea zaidi
tukifika.?
Beka akawasha gari tukaendelea na safari ya
kurudi Arusha huku akionyesha dhahiri
kuchukizwa na msimamo wangu.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO???????
 
SEHEMU YA 6
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
?Beka najua unachokiongea lakini kumbuka
Emmy bado ni mke wangu wa ndoa na kama
tulivyoelezwa siku tunakula kiapo cha ndoa
kuwa kilichofungwa duniani kimefungwa na
mbinguni.Hilo ndilo tatizo kubwa
linalonifanya nisite kuchukua
maamuzi.Nitawezaje kutengua ndoa hii? ?
Nikasema huku nikishika kichwa.
?Hivi Wayne huyu mwanamke amekupa kitu
gani? Kuna dawa amekulisha wewe si
bure.Haiwezekani ugundue mtu amekufanyia
kitendo kama hiki halafu bado unamruhusu
kulala ndani ya chumba chako.? Beka
akasema kwa hasira
?hahahaha Beka achana na mambo ya
dawa.Unajua mimi huwa sipendi kuchukua
maamuzi ya haraka haraka.Hili ni jambo zito
linahitaji utulivu na busara ya hali ya juu
kulitatua.usiwe na wasi wasi rafiki yangu
suala hili litakwisha.Suala kama hili ni lazima
washirikishwe wazee,viongozi wa dini
n.kTwende tuendelee na safari tutaongea zaidi
tukifika.?
Beka akawasha gari tukaendelea na safari ya
kurudi Arusha huku akionyesha dhahiri
kuchukizwa na msimamo wangu.
ENDELEA????????
Jumapili jioni nikiwa nimepumzika bustanini
nikitafakari Emmy akarudi.Baraka aliposikia
niko bustanini akaja mbio akanikumbatia na
kunisalimu.Emmy naye akaja bustanini haraka
.Nilipomuona tu nikahisi hasira kali
moyoni.Picha ya Chris ikanijia tena.Nikabadili
ka ghafla.Emmy akanibusu shavuni
.Nilitamani nimkate shingo kwa hasira
nilizokuwa nazo.Alionyesha mapenzi mazito
kumbe ulikuwa ni unafiki mtupu.Huku
akinipapasa kifuani akamwamuru Baraka
aende ndani akapumzike .Nadhani hii ilikwa ni
janja yake ili nisiweze kumuuliza Baraka
kuhusu safari yao.
?Honey habari ya toka juzi? Akasema kwa
sauti laini ya kimahaba.
?Nzuri .Pole kwa safari? Nikasema
?Safari nzuri.Jamani honey I missed you so
much.? Akasema na kunibusu tena.
?Unajua kukaa mbali nawe hata kwa siku moja
naumia sana.Nilipata wakati mgumu mno kwa
kuwa mbali nawe.? Akasema huku moyoni
akinizidishia hasira.
?Mwanamke shetani huyu..? Nikasema moyoni
kwa hasira.
?baby are you ok? Akauliza baada ya kuniona
nimekaa kimya
?yah I?m ok? Nikajibu kwa kifupi.Akainua
kichwa na kunitazama usoni halafu akakilaza
kifuani kwangu.Sikuwa na msisimko wowote
kama alivytarajia.Laiti angejua kilichokuwa
moyoni mwangu katu asingethubutu
kunisogelea karibu.
Baada ya mlo wa usiku nikamuaga baraka na
kumtaka aende akalale ili kesho asichelewe
shule.Haikuwa kawaida yangu kuingia
chumbani kulala mapema vile.Dakika chache
baadae Emmy akanifuata.Akavaa nguo za
kulalia na kuja kujilaza pembeni yangu.
?baba baraka una tatizo gani? Akauliza
Nilimtazama kwa makini usoni nikaona jinsi
alivyokuwa na wasi wasi.
?Sina tatizo lolote ? Nikajibu
?hapana mume wangu .nakufahamu vizuri una
tatizo.Kuna kitu kinakusumbua.Hebu nieleze
mume wangu.haipendezi kama una kitu
kinakuumiza halafu hutaki kukisema.Mimi
ndiye mke wako sasa usiponiambia mimi
utamwambia nani tena?
Nilitamani kucheka kwa jinsi alivyokuwa
akijibalaguza pale kitandani.
?Ni kweli nina tatizo.? Nikasema.
?tatizo gani hilo mume wangu? Akauliza huku
akinishika kichwa.
Nilikaa kimya kwa sekunde kadhaa
nikatafakari kisha nikasema
?Jumamosi ijayo tunasafari ya kwenda dar es
salaam.nataka tukafanye DNA test?
Emmy akastuka kama vile ameona
jini.Akainuka kwa kasi na kukaa huku kijasho
kikianza kumtoka usoni.Akaniangalia kwa
macho makali.
?DNA test? Akauliza kwa ukali.
?Yes DNA test.Nataka nijue Baraka ni
mwanangu au si mwanangu? Nikasema
?Unajua bado sijakuelewa baba
Baraka.Unamaanisha nini unaposema unataka
ujue Baraka ni mwanao au si mwanao?
?Kwani kuna tatizo gani la kutaka kuwa na
uhakika wa mwanao? Nikauliza
?baba Baraka hivi umepatwa na kitu gani?
Iweje ukampime mwanao wa kumzaa ? Ina
maana umefikia mahala pa kutokuniamini
hata mimi mkeo wa ndoa?
?si hivyo mama baraka.Ni katika kujiridhisha
tu.Nakuamini sana mke wangu lakini kwa hili
utanisamehe kwa sababu nahitaji kufahamu
kama Baraka ni mwanangu au si mwanangu?
Emmy akakaa kimya.akainuka pale kitandani
akasimama na kuanza kuzunguka mle
chumbani.Ghafla akageuka huku uso wake
umejaa machozi.
?Nasema hivi kama mimi ni mke wako wa
ndoa hufanyi hiyo test.Hivi mimi nitakuwa
mjinga kiasi gani nikudanganye kuwa Baraka
ni mwanao wakati si mwanao?Nasema baraka
ni mwanao na hiyo Test haifanyiki?
?na mimi nasema hivi ,kama mimi ni mumeo
wa ndoa nitafanya hiyo Test.Lazima nijue
Baraka ni mwanangu au si mwanangu?Nikase
ma kwa ukali.
?Kitu gani kinachokupa wasi wasi kuwa
Baraka anaweza kuwa si mwanao? Emmy
akauliza.
?Hakuna kitu chochote Emmy nimeamua tu
nifanye hivyo ili niwe na uhakika?
Emmy akaanza kulia kwa kwikwi huku
akilalama kuwa nimevuka mipaka kwa
kumuona yeye ni msaliti wa ndoa
yetu.Sikumjali nikavuta shuka nikajifunika na
kulala.
* * * *
Ni wiki ambayo naweza kusema ilikuwa ni
nyeusi ndani ya nyumba yangu.Maongezi na
vile vicheko vilivyozoeleka vilikuwa nadra sana
kusikika.Emmy hakutaka maongezi na mimi
kwani muda mwingi alipotoka kazini alikuwa
analala chumbani kwa kisingizio cha kazi
nyingi.Sikuijali hali hiyo ,ila nilikuwa makini
sana ili hali kama ile isije kumuathiri
Baraka..Mtoto hakuwa na kosa na hakutakiwa
kusulubishwa kwa makosa ya wazazi
wake.Nilijitahidi kuwa naye karibu,kumsaidia
kazi za shuleni zilizomshinda,na wakati
mwingine tulikwenda bustanini kupiga
magitaa yetu.Sikutaka aone kama kuna
tofauti yoyote imetokea kati ya wazazi
wake.Siku ya ijumaa usiku tukiwa mezani
tunapata chakula nikakumbushai juu ya safari
ya Dar es salaam kesho yake na kuuliza kama
kila kitu kiko tayari..
?Kila kitu umekwisha kiweka tayari kwa safari?
Nikauliza
Emmy hakujibu kitu akaniangalia kwa jicho
kali .
?Hivi ni kweli umemaanisha kwenda kufanya
hiyo DNA test au unanitania? Emmy akauliza
?mama baraka sikutanii.Kesho tunasafri
kwenda Dar kwa ajili ya DNA.It?s a serious
issue.?Nikasema
?Kama unakwenda nenda mwenyewe.Mimi
wala mwanangu Baraka hatutakwenda? Emmy
akasema kwa kiburi
?Mama Baraka ,mimi ndiye mwenye kauli ya
mwisho katika nyumba hii na ndiye mwenye
kuamua nini kifanyike na nini kisifanyike.Kwa
maana hiyo basi nasema kuwa kesho alfajiri
na mapema wote tunakwenda Dar es
salaam.Hili halina kipingamizi na wala sihitaji
mjadala tena? Nikasema kwa sauti iliyoashiria
hasira ndani yake .Nilifahamu ni kwa nini
Emmy hakutaka kwenda kufanya kipimo cha
vinasaba.Nina uhakika mkubwa kuwa Baraka
hakuwa mwanangu wa damu lakini nilikuwa
nataka kuwa na ushahidi mkubwa zaidi wa
kibaolojia.
?Kama mnakwenda nyie nendeni lakini mimi
sintakwenda Dar es salaam.Mimi ndiye
mwenye ukweli wote na hata kama ukienda
kupima bado ukweli hautabadilika ?Emmy
akasema huku akiubetua mdomo wake kwa
dharau akakiweka kijiko chini na kuondoka
mezani kwa hasira.Niliumia sana moyoni kwa
majibu yake ya kiburi namna ile lakini
sikutaka kuonyesha mbele ya mtoto.
* * * *
Siku ya jumanne nilirejea toka jijini Dar es
salaam nilikokuwa nimekwenda kwa ajili ya
kufanya kipimo cha vinasaba ili kubaini kuwa
Baraka ni mwanangu au si mwanangu.Emmy
alikataa kata kata kuungana nasi kwenda Dar
kwa ajli ya vipimo hivyo ikanuilazimu kwenda
mimi na Baraka.Majibu niliyopewa yalinitoa
machozi kwani yalionyesha dhahiri kuwa
Baraka hakuwa mwanangu wa
damu.Japokuwa nilikuwa naelewa kabla kuwa
Baraka hakuwa mwanangu lakini sikuwa na
uhakika sana hadi majibu haya yaliponidhihiri
shia wazi .Majibu haya yalinifanya nifikie
hatua ya mwisho ya kuutafuta ukweli kama
Baraka ni mwanangu au sivyo.Kila
nilipomuangali mtoto yule niliyempenda kuliko
kitu chochote kile roho iliniuma sana.Emmy
alinifanyia unyama mkubwa sana.Ni bora
Emmy angenieleza toka mapema nikafahamu
kuwa yule si mwanangu.Ameuficha ukweli
miaka hii yote na kwa sasa Baraka amekwisha
kuwa mkubwa na ana akili za kutosha na
hivyo kuambiwa ukweli kuwa mimi si baba
yake ni kitendo ambacho kitamchanganya
akili na kumuathiri kisaikolojia.
Saa moja za za jioni tukawasili Arusha na
kuelekea moja kwa moja nyumbani.Nyumbani
alikuwepo mtumishi wa ndani peke
yake.Nikamuuliza alikoenda Emmy akasema
kuwa siku tulipoondoka kwenda Dar es salaam
na yeye akaondoka na hajarudi tena hadi leo
hii na wala hakusema anaelekea
wapi.Sikushangaa wala kuumia rohoni kwa
kitendo kile kwa sababu kuendelea kumuona
Emmy machoni pangu kungeniongezea
hasira.Nikaingia chumbani na kukuta baadhi
ya vitu vyake havipo.Nadhani alitambua kuwa
kwenda kwangu Dar es salaam kungeweka
ukweli wa mambo kuwa baraka hakuwa
mwanangu na kwa maana hiyo akaamua
kuondoka mapema kabla sijarudi ili kuepusha
matatizo..
Nilikaa kitandani nikitafakari kwa kina juu ya
maisha yangu na matatizo ambayo Emmy
amenisababishia.Toka nimegundua uchafu
alionifanyia Emmy nimekuwa nikijipa ujasiri
mkubwa kuwa haya ni masuala madogo
ambayo katu hayawezi kuniumiza kichwa
lakini nikiwa pale kitandani kwa mara ya
kwanza nikahisi kitu kama kisu kikali
kikiupenya moyo wangu .Nilihisi maumivu
makali ya moyo.pamoja na ujasiri wangu
wote nilioahidi kuwa nao lakini nilishindwa
kuyazuia machozi kunitoka.Hayakuwa
maumivu ya kawaida.Ilikuwa ni zaidi ya
maumivu..
Kesho yake nikadamka asubuhi na mapema
na kujiandaa kumpeleka Baraka shule.Emmy
hakurejea na wala sikusumbuka kumtafuta
katika simu na kumuuliza yuko wapi ingawa
nilipaswa kujua aliko akiwa kama mke
wangu.Kwa hasira niliyokuwa nayo moyoni
sikuwa tayari kumuona tena akitia mguu
nyumbani kwangu.Macho yalikuwa
yamevimba na mekundu kwa kukosa usingizi
.Baraka alipokuwa tayari akaingia garini
nikampeleka shule halafu nikaelekea
ofisini.Japokuwa nilijitahidi kuuficha ukweli
kuwa kuna jambo linanisumbua lakini
wafanyakazi wenzangu walihisi sikuwa
sawasawa.Nikiwa ofisini niliegemea kitini na
kuanza kutafakari kwa kina juu ya maisha ya
furaha niliyoishi na Emmy kumbe nyuma yake
kumejaa usaliti na uchafu wa hali ya juu
mno.Niliufikiria pia urafiki kati yangu na
Christopher ulivyokuwa wa karibu.Tulikuwa ni
marafiki tulioshibana sana na tuliishi kama
ndugu.Ni Christopher ndiye aliyesaidia mpaka
mimi na Emmy tukarudiana tena baada ya
Emmy kunifanyia usaliti miaka ya nyuma
kabla hatujaoana.Leo mke wangu wa ndoa
anadiriki kuzaa na rafiki yangu wa
karibu.Sikuwa tayari kuendelea kuteseka na
kuumia moyo kwa ajili yao tena.Nikaamua
kuliweka wazi suala hili.Nikachukua simu na
kumpigia baba mkwe wangu yaani baba yake
Emmy na kumuomba kama ana nafasi
nionane naye jioni yeye pamoja na
mama.Hakuwa na tatizo mzee yule ,halafu
nikampigia tena simu rafiki yangu Beka na
kumuomba aje nyumbani kwangu jioni kwa
ajili ya maongezi mafupi , nikampigia pia
simu mwalimu wa dini ambaye amekuwa
karibu nasi na kutulea kiroho kwa muda
mrefu.Niliwataarifu vile vile wasimamizi wetu
wa ndoa kuwa wafike jioni hiyo kuna masuala
muhimu ya kuongea.Nilihitaji na Emmy awepo
katika kikao cha jioni hiyo wakati nikiusema
ukweli mbele ya wazee na mashahidi lakini
sikuwa na hamu hata ya kuongea naye
simuni.Baada ya kufikiri mara kadhaa
nikaamua kumpigia simu japokuwa moyo
ulikuwa hautaki .
?Unasemaje wewe? Akauliza kwa ukali mara tu
alipoipokea simu.Nilistushwa na ukali ule na
kauli ile ya dharau kwani hakutaka hata
kunisalimu.Nilisita kidogo kuongea kutokana
na hasira zilizonipanda ghafla.Leo emmy
amefikia hatua ya kuniita mimi ?wewe?
?Sema unachokitaka kama husemi nitakata
simu? Akasema tena kwa ukali baada ya
kuona nimekaa kimya.
?nakuhitaji nyumbani jioni? Nikasema
?Nije kufanya nini? Hivyo vipimo ulivyoenda
kufanya si vimeshakupa ukweli sasa unataka
nije kwako kufanya nini tena?
?nataka uje tuongee?
?Tuongee nini tena? Hatuna cha kuongea
wayne.tayari ukweli unaufahamu kwa hiyo
sioni kama kuna kitu tunatakiwa kuongea
mimi na wewe.Umeshatambua Baraka siyo
mwanao kwa hiyo hata mimi si mkeo.Sifikirii
tena kuishi na wewe .Nimechoka mimi maisha
ya kubanwa banwa na kufugwa fugwa ndani
kama njiwa.Nahitahi maisha ya uhuru,maisha
ya kufanya nitakacho.Naomba uniache
Wayne.Mimi sifai kuwa mkeo.Unahitaji
mwanamke bora wa kuishi naye na si mimi.?
Nilivuta pumzi ndefu baada ya maneno yale
mazito.Sikutegemea Emmy mwanamke
niliyempenda na mbele ya mashahidi kanisani
akala kiapo cha kuwa nami katika maisha
yote mpaka kufa lakini leo ananitamkia
maneno kama haya.Ni shetani gani
amemwingia mwanamke huyu hadi
akabadilika na kuwa namna hii?
?Emmy mimi sina ugomvi na wewe na hata
kama ukitaka kuondoka kwangu mimi sikuzuii
kwani ni uamuzi wako.Ninaujua ukweli
wote.Ninafahamu Baraka si mwanangu wa
damu.Ninafahamu Baba yake ni nani kwa hiyo
ninachotaka tukae chini tuongelee suala la
huyu mtoto .Tukilimaliza hilo mimi sina tatizo
na wewe hata kidogo.You can do anything you
want? Nikasema huku moyo ukiniuma kupita
maelezo.
?Ok kama nitapata muda nitakuja.? Emmy
akajibu kwa dharau na kukata simu.Nilihisi
kama dunia inazunguka .sikuwa nimetegemea
kama itatokea siku mimi na Emmy tungefikia
mwisho wa namna hii.
* * * *
Saa kumi na moja za jioni Baba mkwe akiwa
ameongozana na mkewe wakawasili nyumbani
kwangu.Niliwakaribisha kwa furaha japokuwa
nyuso zao zilikuwa na wasi wasi
mwingi.Nadhani mwito ule wa dharura
ulikuwa umewastua sana.Tayari
Beka,mwalimu wangu wa dini na wasimamizi
wetu wa ndoa walikuwa wamekwisha fika
muda mrefu na waliokuwa wakisubiriwa ni
wakwe.Zaidi ya Beka hakuna aliyekuwa akijua
nini niliwaitia jioni ile,hali iliyowafanya wote
wazidi kuwa na wasi wasi .Baada ya salamu
na maongezi mafupi,nikafanya utambulisho
kwa wageni wote halafu nikafungua kikao.
?Baba na mama mkwe,kwanza kabisa
ninapenda kuchukua nafasi hii kuwaomba
samahani kwa kuwasumbua jioni hii.Najua
mna majukumu mengine mengi ya kufanya
.Nashukuru sana kwa kuitikia mwito wangu na
kufika hapa.Nawashukuru pia wengine wote
mliofika,rafiki yangu Beka,mwalimu wangu wa
dini, na wasimamizi wetu wa ndoa.?
Kabla sijaendelea mbele zaidi,baba mkwe
akadakia.
?Samahani kwa kukukatisha Wayne.Mbona
simuoni Emmy hapa?
Swali lile linanipa wakati mgumu kidogo
kulijibu.Nikafikiri kwa sekunde chache na
kusema
? Emmy atakuja si muda mrefu.amepata
dharura kidogo? Nikadanganya.Sikutaka
kuharakisha mambo.Nilitaka kwanza niwape
picha kamili ya mambo jinsi ilivyo.Nikawata
zama wote na kila mmoja alikuwa na sura
iliyoniashiria niendelee na maongezi.
?Nimewaiteni jioni hii ya leo kuna mambo
muhimu ya kuongelea.Nadhani nyote
mnafahamu kuwa ndani ya ndoa
migongano,mikwaruzano huwa
haikosekani.Kunapotokea mikwaruzano au
migongano ndani ya ndoa na wanandoa
mkashindwa kuisuluhisha basi hamna budi
kuwashirkisha watu wa karibu kama wazazi
na ndugu wengine wa karibu.Kwa ufupi ni
kwamba ndani ya ndoa yetu kumetokea
matatizo kidogo ambayo sisi kama wanandoa
tumeshindwa kuyatatua ikanilazimu kuwaita
na kuwashirikisha katika suala hili.?
Nikanyamaza na kuwaangalia wote mle ndani
,kila mmoja alikuwa na hamu ya kutaka kujua
nini kimetokea.
?nafikiri nyote mnakumbuka kuwa kipindi
kifupu kabla ya ndoa yangu na Emmy
kulitokea mtafaruku ambao ulichangiwa na
mwenzangu kutokuwa mwaminifu katika
uchumba wetu.Sitaki kurudia kulielezea hilo
kwa sababu lilikwisha pita na limesahaulika,i
la nimelisema tu ili kuweka kumbukumbu
sawa.Baada ya usuluhishi wa wazazi na
ndugu tulilimaliza suala lile na ndoa
ikafungwa.Tumeishi vizuri na mwenzanguu
hadi tukabahatika kupata mtoto
mmoja.Maisha yetu yamekuwa ni ya furaha
kubwa siku zote.?
Nikanyamaza tena na kuvuta pumzi halafu
nikaendelea
?Siku chache zilizopita,niligundua kuwa
mwenzangu amekuwa si mwaminifu katika
ndoa yetu.Labda kwa kuelezea tu ilimpate
picha halisi ni nini ninakiongea ni kwamba
kuna siku niliwahi kutoka kazini,sikuwa na
kazi nyingi za kufanya hivyo ikanibidi kuwahi
kazini na kuja kukaa na familia yangu
.Nilipofika getini nikakutana na mke wangu
akitoka nikamuuliza alikokuwa akielekea
kasema kuwa wanampeleka jirani yetu
hospitali.Nikaingia ndani na kuikuta kompyuta
yake iko kitandani,nikaona ni bora
niizime.Kabla sijaizima nikagundua kuwa
kabla hajatoka alikuwa akiwasiliana na mtu
.Kwa kuligundua hilo nikaona ni bora mtu
huyo aliyekuwa akiwasiliaana naye nimjibu
kuwa asubiri hadi baadae.Nilipatwa na
udadisi wa kusoma zaidi baada ya kuona jina
la mtu aliyekuwa akiwasiliana mke wangu
limeandikwa my special one.Nikajiuliza huyu
my special one ni nani? Hata kama ungekuwa
ni wewe ni lazima ungepatwa na udadisi wa
kutaka kujua huyo special one ni nani.kwa
sababu mimi kama mume mke wangu ndiye
mtu wangu muhimu,ndiye my special one.Kwa
mantiki hiyo hata mke wangu mimi ndiye
special one wake kwa sababu aliamua
kuwaacha wanaume wote na kuolewa na
mimi.Sasa nikastuka baada ya kujua kuwa
mwenzangu ana special one mwingine ambaye
si mimi.?
Nikatulia na kuwaangalia watu wote mle
sebuleni.walikuwa kimya kabisa
wakiniskiliza.mama yake Emmy alikuwa
ameinama ameshika shavu .Nikaendelea.
?Baada ya uchunguzi nikagundua kwamba
walikwisha anza kuwasiliana muda mrefu toka
Emmy akiwa kazini,na aliporudi nyumbani
wakaendelea tena kuwasiliana.Na hiyo
haikuwa mara yao ya kwanza kuwasiliana.Baa
dae nikagundua kuwa kulikuwa na message za
kimapenzi walizokuwa wakitumiana.Nikabaini
kuwa Emmy ana uhusiano na mtu huyu wa
kimapenzi kwa sababu kwa mujibu wa meseji
wanazotumiana walikuwa wakikumbushana
juu ya siku za nyuma wanazokutana katika
mahoteli makubwa na kufanya mapenzi.Si
mara moja Emmy huwa ananiaga kuwa
anakwenda semina au katika makomngamano
au kikazi nje ya mji kumbe huwa anautumia
muda huo kukutana na huyo mtu wake
muhimu.Ushahidi wa meseji zote hizo ninao
toka walipoanza kuwasiliana.?
Mama mkwe akainama chini kwa aibu .Baba
mkwe yeye akatoa kitambaa na kufuta jasho
lililoanza kumtoka.Kila mmoja mle sebuleni
sura yake ikabadilika.Sikutaka kumung?unya
maneno,nikaendelea.
?Niliumia sana baada ya kuligundua hilo
lakini nashindwa hata kuelezea maumivu
niliyoyapata baada ya kugundua kuwa ???.?
Kabla sijaendelea mbele mlango
ukagongwa.Nikaomba samahani na kwenda
kuangalia ni nani aliyekuwa akigonga.Alikuwa
ni jirani yetu mama Mwantumu.Mama yule
akaniambia kuwa Emmy alikuwa akihitaji
kuonana na mimi nje ya nyumba.Amegoma
kuinia ndani baada ya kuliona gari la baba
yake liko mle ndani.Nikaingia ndani na
kumwita mama mkwe nje.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO????????
 
BEYOND PAIN
SEHEMU YA 7
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Baadae nikagundua kuwa kulikuwa na
message za kimapenzi walizokuwa
wakitumiana.Nikabaini kuwa Emmy ana
uhusiano na mtu huyu wa kimapenzi kwa
sababu kwa mujibu wa meseji wanazotumiana
walikuwa wakikumbushana juu ya siku za
nyuma wanazokutana katika mahoteli
makubwa na kufanya mapenzi.Si mara moja
Emmy huwa ananiaga kuwa anakwenda
semina au katika makomngamano au kikazi
nje ya mji kumbe huwa anautumia muda huo
kukutana na huyo mtu wake muhimu.Ushahidi
wa meseji zote hizo ninao toka walipoanza
kuwasiliana.?
Mama mkwe akainama chini kwa aibu .Baba
mkwe yeye akatoa kitambaa na kufuta jasho
lililoanza kumtoka.Kila mmoja mle sebuleni
sura yake ikabadilika.Sikutaka kumung?unya
maneno,nikaendelea.
?Niliumia sana baada ya kuligundua hilo
lakini nashindwa hata kuelezea maumivu
niliyoyapata baada ya kugundua kuwa ???.?
Kabla sijaendelea mbele mlango
ukagongwa.Nikaomba samahani na kwenda
kuangalia ni nani aliyekuwa akigonga.Alikuwa
ni jirani yetu mama Mwantumu.Mama yule
akaniambia kuwa Emmy alikuwa akihitaji
kuonana na mimi nje ya nyumba.Amegoma
kuinia ndani baada ya kuliona gari la baba
yake liko mle ndani.Nikaingia ndani na
kumwita mama mkwe nje.
ENDELEA????????.
?Mama samahani,Emmy amekuja yuko nje
lakini amegoma kuingia humu ndani baada ya
kuliona gari la baba.Ninaomba ukamshawishi
aingie ndani kwa sababu kama nikienda mimi
hatakubali kuingia ndani? Mama mkwe
akakubali na akaenda nje ya nyumba kuonana
na Emmy.
?Wayne vipi,uko salama? Kuna tatizo lolote?
Akauliza baba mkwe baada ya kuniona
nimerudi ndani na kukaa kimya kimya
?Hapana mzee.Ni mambo ya kawaida ,mama
anayashughulikia? Nikasema
Baada ya dakika tano hvi mlango
unafunguliwa,mama mkwe akiwa
ameongozana na Emmy wanaingia
ndani.Emmy akiwa ni mwenye sura ya aibu
akamsalimu baba yake na mwalimu wa dini
halafu akakaa sofani huku amekiinamisha
kichwa chake chini.hakutaka kumuangalia mtu
yeyote usoni.
?Nadhani tunaweza kuendelea.? Nikasema na
kuwatazama watu wote mle ndani.Baba mkwe
alikuwa akimuangalia Emmy kwa jicho la
hasira mpaka nikaogopa .
?Endelea Wayne? Akasema baba mkwe.
?Kabla hatujasimama nilikuwa nasema
kwamba,niliumia sana baada ya kugundua
kuwa mwenzangu alikuwa akitoka nje ya ndoa
yetu.Mwenzangu hakuwa mwaminifu hata
kidogo.Kikubwa zaidi ya yote ni kwamba
niligundua kuwa mtoto Baraka hakuwa
mwanangu wa damu.Alikuwa na baba
yake???
?Yarabi toba?.? Mama mkwe akasema kwa
sauti kubwa huku ameshika kichwa
chake.baba mkwe akamshika mkono na
kumtoa nje.Mama mkwe ana matatizo ya
shinikizo la damu.Baba mkwe aliamua kumtoa
nje baada ya kuona hali yake inanza
kubadilika.
Baada ya dakika kadhaa,baba mkwe akarudi
ndani.
?Tuendelee?mama yenu huwa ana matatizo
ya shinikizo la damu na habari kama hizi
huwa zinamstua sana ndiyo maana nimemtoa
nje apumzike.?
?Mwanzoni sikuamini hata kidogo kuwa ni
kweli Baraka anaweza kuwa si mwanangu.Kwa
mujibu wa meseji nilizozipata ,walizokuwa
wakitumiana Emmy na My special one ni
kwamba kwa kuwa Baraka tayari amekwisha
kuwa mkubwa, anapaswa kuanza kuwafahamu
ndugu zake na kwa kuanzia walipanga waanze
kumpeleka kwa babu zake huko Same.Ni kweli
siku hiyo kama walivyokuwa wamepanga
Emmy aliniomba ruhusa kuwa anamsindikiza
rafikiye kwenye sherehe ya ndugu
yake.Nilimfuatilia bila ya yeye kujua mpaka
Same ndipo nilipogundua kuwa huyo mtu
aliyemuita kama special one alikuwa ni rafiki
yangu wa siku nyingi sana aitwaye
Chris.Nilipolitambua hilo nikataka nipate
uhakika zaidi nikamuomba emmy tuende
tukapime DNA ili tuwe na uhakika mtoto ni
wangu au si wangu.Emmy alikataa kata kata
ikanilazimu kuondoka mimi na Baraka hadi
Dar es salaam na kufanya kipimo hicho cha
DNA na majibu ylidhihirisha kuwa ni kweli
Baraka si mwanangu.Niliporudi toka dar es
salaam nikiwa na majibu ya vipimo vya DNA
Emmy tayari alikwisha ondoka nyumbani na
nilipompigia simu ni kwa nini aliondoka
nyumbani bila ruhusa yangu akaniambia
kwamba kwa sasa sina nguvu yoyote ya
kuweza kumzuia,na akaenda mbele zaidi kwa
kunitaka nisiendelee kumfuatilia.Nilimuelewa
lakini nikamuomba aje katika kikao hiki cha
jioni ya leo kwa ajili ya kujadili kuhusu suala
la mtoto.Kwa ufupi hayo ndiyo niliyowaitia
jioni hii ya leo na imekuwa vyema mhusika
mkuu naye amefika?
Nikamaliza na kuwatazama watu wote mle
ndani.Kila mmoja alikuwa kimya .Ukimya
mkuu ukatanda mle sebuleni halafu
babamkwe akasema kwa hasira.
?Emmy ,japokuwa umechelewa ,lakini
umeyasikia yote aliyoyaongea mwenzio.Je una
lolote la kuongea?
Emmy hakujibu kitu akakaa kimya huku
machozi yakimtoka
?nakuuliza tena Emmy una lolote la kuongea
kutokana na haya aliyoyasema mwenzio?
Naomba usikae kimya nijibu haraka? baba
mkwe akasema kwa ukali
Emmy akiwa ameuficha uso wake kwa viganja
vya mikono akasema
?Yote aliyoyasema ni kweli baba?
Baba mkwe akashika kichwa kwa mstuko.
.Alipatwa na mstuko wa ghafla.Kila mtu mle
ndani alikuwa amepigwa na butwaa.baba
mkwe akainama akatafakari kwa sekunde
kadhaa halafu akainua kichwa na kusema
?Emmy naomba urudie tena,haya
aliyoyatamka mwenzako ni mambo ya kweli?
Huku akifuta machozi akiwa ameinama chini
akasema bila kusita
?Ni ya kweli baba?
Ghafla baba mkwe akainuka kwa kasi ya
ajabu na kutaka kumvaa Emmy kwa
kipigo,nashukuru mwalimu wa dini alikuwa
karibu akawahi kumshika na kumketisha
chini.
?Mtoto una laana wewe.Unawezaje kufanya
upuuzi kama huu ? Baba mkwe akasema kwa
hasira
?Mzee.Punguza hasira tuyaongee haya mambo
kiutu uzima tuyamalize.Najua inauma kama
mzazi lakini jitahidi kujizuia mzee wangu ili
tuyamalize mambo haya magumu kwa
amani?Mwalimu wa dini akasema taratibu
akijaribu kumtuliza baba mkwe aliyekuwa
amewaka kwa hasira.
?Mwalimu hebu niachieni nafasi nimshikishe
adabu baradhuli huyu .Amenitia aibu kubwa
.Tutaziweka wapi sura zetu sisi? ..Ouh My
God?..? Akasema kwa hasira baba mkwe.
?Aibu hii si yako peke yako.Suala hili
limetugusa sisi sote.Wote tunaumia mioyoni
mwetu.lakini tunajitahidi kujizuia .Nakuomba
mzee wangu tuliza hasira tuyaongee mambo
haya na kuwasaidia hawa vijana.?
Baba mkwe akatulia lakini alikuwa akihema
kwa hasira.Emmy uso ulikuwa umejaa
machozi.Mambo haya mimi niliyaona kama
ya kawaida kwa sababu nilikwisha yazoea
tayari.Nilikwisha umia vya kutosha kwa hiyo
sikuwa mgeni wa maumivu haya.Wote
tulikuwa kimya tukisubiri kusikia baba mkwe
atasema kitu gani.
?Emmy nataka uniambie.Ni kitu gani
kimepelekea wewe ukafanya uchafu wa namna
hii.Nataka uwe wazi ili tujue na tuone jinsi
gani tunaweza kulimaliza suala hili?
Emmy alikuwa ameinama akilia.Hakuweza
kuinua uso wake kwa aibu.Sebule yote ikawa
kimya ikimsubiri yeye aweze kujibu swali
aliloulizwa na baba yake.
?Emy nimekuuliza,na ninataka unijibu sasa
hivi ni kitu gani kimepelekea wewe ukafanya
uchafu wa namna hii ? Hii ni aibu kubwa
kwetu kama familia,umetuumiza sana siwezi
kukuficha na hasa mama yako ameumia
mno.Umemuumiza mwenzako pia kiasi
ambacho hakielezeki.Bado kuna mtoto Baraka
ambaye ataumia kupita kiasi atakapoelezwa
kuwa huyu si baba yake mzazi.Tafadhali
usikae kimya hebu tueleze ni kwa nini ulifanya
mambo kama haya? Baba mkwe akauliza tena
huku hasira zikianza kumpanda. Emmy
akafuta machozi kwa kitambaa chake halafu
akainua sura yake na kusema kwa kwikwi.
? baba ?kusema ukweli..nilifanya hivi kwa
sababu???? Emmy akashindwa kuendelea
akaanza kulia.
?Emmy naomba tafadhali usipoteze muda
wetu hapa.hebu tueleze ni kitu gani
kimekufanya wewe ukamfanyia mwenzako
namna hii? Baba mkwe akasema kwa sauti
kali
?baba ..niliamua kutoka nje ya ndoa kwa
sababu sikuwa naridhika?.Wayne
haniridhishi??.
Kauli ile inanifanya nihisi kama vile moyo
wangu unataka kupasuka kwa jinsi
ulivyoyabadilisha mapigo yake na kuanza
kwenda kasi.Katika maisha yangu sikuwa
nimetegemea kama iko siku Emmy atakuja
kutamka kitu kama kile.Nilijitahidi kwa kila
niwezavyo kumridhisha kwa kila kitu
alichokihitaji bila kujali gharama yake.na hata
katika mapenzi ya kitandani nilikuwa mjuvi
wa mambo na kila tulipofanya mapenzi siku
zote hunisifia na kuniita kidume huku akiapa
na kuwatukana wanaume wengine kuwa
hawana hadhi ya kumgusa mtu kama yeye
kutokana na raha ninazompatia.Sasa iweje
tena leo mbele ya wazee atamke kuwa sikuwa
namridhisha?Baada ya tafakari fupi
nikagundua kuwa alisema vile kama utetezi
wake.Uongo ule ukaniuma sana.baba mkwe
akamtazama Emmy kwa hasira na kuuliza.
?Emmy unadai kuwa ulifanya uchafu huu kwa
sababu mumeo hakuwa akikuridhisha,je kuna
siku yoyote uliwahi kukaa naye na
ukamueleza kuhusu suala hilo?
Emmy hakujibu kitu akakaa kimya.Nilijua
alikuwa akiongopa ndiyo maana hakuwa na
jibu.Alipoona Emmy amekaa kimya hana jibu
baba mkwe akanigeukia mimi
?wayne hebu tuelze.Kua siku yoyote mkeo
alikwisha wahi kukueleza kuwa humridhishi?
?Hapana baba hakuna hata siku moja
aliyowahi kuneieleza kuwa haridhiki.Kinac
honishangaza ni kwamba mara zote amekuwa
akinisifia kuwa hajawahi ona mwanaume
kama mimi ,kwa maana hiyo ni kwamaba
alikuwa akiridhika saa iweje leo atamke
kwamba hakuwa akiridhika? Zaidi ya yote
hakuna kitu alichowahi kukitaka mke wangu
akakosa hata cha gharama gani.Kuna siku
nyingine akiwa nyumbani huwa ananipigia
simu na kunieleza kuwa ananihitaji,kwa
kumridhisha huwa natoroka kazini na kuja
kukaa naye.Hebu muulizeni kama ninasema
uongo?
?Emmy umemsikia mwenzio alivyosema.Ni
kweli?
Emmy hakujibu kitu.Baba mkwe akawagekia
wasimamizi wa ndoa yetu na kuwaliza.
?Au alikuwa kushitaki kwenu wasimamizi?
?hapana baba.Hakuna hata siku moja Emmy
amewahi kuja kushitaki kwetu kuhusu jambo
lolote lile linalohusiana na masuala ya ndani
ya ndoa yao?
baba mkwe akatafakari kwa muda na kusema
?Inaonekana Emmy umeamua kutunga
uongoHuna sababu yoyote ya msingi
iliyopelekea wewe kuamua kutoka nje ya ndoa
yako,na hata kufikia hatua ya kuzaa nje ya
ndoa na kumdanganya mumeo.Mara ya
kwanza mwenzio alikufuma na mwanaume
akakusamehe na mkafunga ndoa.Niliamini
kuwa ulijifunza na ukabadilika .Siku zote hizi
umekuwa ukiishi kama mke mwema kumbe ni
chui ndai ya ngozi ya kondoo.Inaonekana hii
tabia ya umalaya imekwisha kuingia ndani ya
damu yako na hautaweza kuiacha.Sasa
nakuambia hivi kwa kosa hili ulilolifanya mimi
sintakuwa na kusema .Nitamuachia wayne
yeye ndiye atakaye amua afanye nini.? Baba
mkwe akasema kwa ukali.mwalimu wa dini
ambaye alikuwa amekaa kimya muda wote
akakohoa kidogo na kusema.
?Jamani naomba na mimi niseme
kidogo.Nakubali kuwa Emmy amefanya kosa
kubwa sana.Amemkosea mwenzake na hata
kuvunja ahadi ya ndoa aliyoiweka mbele ya
altare ya bwana.Lakini kama Mungu
anavyotuagiza kwamba tusiwe na mipaka
katika kusamehe kama yeye anavyowasamehe
hata wale wanaomkosea kupita kiasi.kwa
maana hiyo kabla hatujaendelea mbele na
kikao hiki ningeomba kwanza tujenge
mazingira ya kusameheana.Ni kwa njia hiyo
pekee tunaweza kuyamaliza mambo haya kwa
amani.Halafu kitu kingine ni kwamba
tunataka Emmy atueleze nani ni baba wa
mtoto ili tuone ni vipi tutafanya kuhusu mtoto
huyu.? Mwalimu wa dini akasema lakini kabla
hajaendelea zaidi baba mkwe akadakia
?Mwalimu,nafahamu wewe ni mtu wa Mungu
na siku zote kazi yenu ni kuhubiri upendo na
kusameheana.Lakini nadhani wewe hujaguswa
na jambo hili.maumivu ya kufanyiwa kitu
kama hiki hayapimiki..Suala la kusameheana
naona tumuachie Wayne yeye ndiye
atakayeamua kama atamsamehe huyu mke
wake au vipi.Tuendelee na kikao chetu.Emmy
hebu tueleze huyu mtoto Baraka baba yake ni
nani?
Kwa upande Fulani nilimuunga mkono baba
mkwe kwa kauli yake.Kumsamehe Emmy
ilihitaji moyo wa ajabu sana.haikuwa rahisi
kusamehe .Emmy hakuwa tayari kusema nani
alikuwa ni baba wa Baraka.ote tukakaa kimya
tukimsubiri.
?Emmy tunakusubiri wewe ,hebu tueleze ni
nani baba wa mtoto ?
Emmy hakuwa tayari kusema lolote kuhusiana
na mtu aliyezaa naye.Kwa kuwa nilikuwa
nikimfahamu ni nani baba wa Baraka nikaona
ni bora niwe wazi.
? Baba mkwe hawezi kutujibu huyu.Lakini
tayari ninamfahamu baba wa mtoto.?
?unamfahamu baba wa mtoto? Baba mkwe
akauliza kwa mshangao
?Ndiyo tayari ninamfahamu? Nikajibu
?Hebu tutajie ni nani huyo?
?Ni rafiki yangu Chris? Kimya kikatanda mle
sebuleni.Kila mmoja hakuamini kama Emmy
angeweza kuzaa na rafiki yangu.
?Yaani Emmy anadiriki kuzaa na rafiki yako?
Baba mkwe akauliza.
?Si tu rafiki yangu,bal ni mtu aliyekuwa rafiki
yangu wa karibu sana.Ni Chris ndiye
aliyekuwa muandaaji mkuu wa harusi yangu
na Emmy.Nilimwamini na kumuona kama
ndugu.Sikujua kama iko siku anaweza
akafanya kitu kama hiki alichokifanya.?
Nikasema kwa uchungu.Ilikuwa inauma sana.
?mambo haya yanazidi kuwa magumu.Na
huyo rafikiyako mmekwiha wasilia ana kwa
siku za hivi karibuni? Aba mkwe akauliza
?Hapana baba.Ni kitambo kirefu sijawasiliana
naye.Mawasilaiano baina yangu na yeye
yalianza kufiifia na hatimaye kufa kabisa.Kwa
sasa sina mawasilano naye yoyoite yale?
Baba mkwe akamgeukia Emmy
?Emmy ni kweli umezaa na rafiki wa Wayne?
Kwa sauti yenye kitetemeshi Emmy akajibu
?Ni kweli baba,nimezaa na Chris? jibu lile
linampandisha baba mkwe hasira
?Mtoto una laana wewe.Unawezaje kuzaa na
rafiki wa mumeo?
?baba Chris ninampenda .Sitaki kuendelea
kuishi na Wayne.Nataka nikaishi na Chris
tulee mtoto wetu.?
Chumba chote kikawa kimya kwa kauli ile ya
Emmy.Kila mmoja alikuwa amepatwa na
mshangao mkubwa .Kwa wale waliokuwa pale
sebuleni ilikuwa ni kama wanaangalia mchezo
wa kuigiza lakini ilikuwa kweli.
?baba wewe una mawazo gani ? Baba mkwe
akanigeukia na kuniuliza.Watu wote mle
sebuleni macho yao yakanielekea mimi ili
kunisikia ninatoa wazo gani.Kila mmoja
alikuwa akikwepa kutoa hukumu kwa kesi ile
ngumu.Nililitambua hilo na nikaamua kuweka
wazi yaliyokuwa moyoni mwangu
?baba nadhani nyote mmesikia kwa kauli yake
kuwa hana haja ya kuishi tena na mimi.Hili
amelitamka mbele yako wewe baba ambaye ni
mzazi wake na mbele ya mashahidi ambao
walishuhudia ndoa yetu.Mpaka hapa ilipofika
mimi nina imani huyu mke wangu amekwisha
nichoka na hana mpango na mimi tena.hata
kama tukiamua kuyamaliza mambo haya kwa
kusameheana na kuanza maisha mapya ni
wazi ndani ya nyumba hakutakuwa na amani
yoyote wala upendo tena.Mimi kwa moyo
mweupe mbele yenu ninyi wazazi na
mashahidi ninapenda kuweka wazi lililo
moyoni mwangu.?
Nikatulia kidogo huku kila mmoja akisikiliza
kwa makini sana ili kusikia nitaongea kitu
gani
?Kama tulivyoapa siku ya ndoa yetu na padri
akatamka kwamba kilichofungwa duniani
kimefungwa pia mbinguni kwa maana hiyo
ndoa yangu mimi na Emmy haitaweza
kuvunjika hadi pale kifo kitakapotutenga
nisha.Pamoja na yote aliyonitendea lakini
bado Emmy ni mke wangu na siku zote
sintalisahau hilo.Pamoja na hayo lakini yeye
kwa upande wake amelisahau hilo na kutamka
wazi kwamba hajisikii tena kuwa na mimi
mume wake wa ndoa na kwamba anahitaji
kwenda kuishi na mwanaume mwingine ili
walee mtoto wao.Natamka wazi kwamba yuko
huru kwenda huko atakako kwenda.siwezi
kumzuia kufanya atakavyo hata kama
tunafungwa na ahadi ya ndoa.Kwa hiyo Emmy
mimi nakuruhusu uende huko unakotaka
kwenda,ukaishi kwa amani.Inaniuma sana
lakini sina namna nyingine ya
kufanya.Naamini mateso haya
uliyonisababishia Mungu anayaona na iko
siku atanipa faraja.Kwa hiyo mama uko huru
kwenda unakotaka kwenda.Una ruhusa ya
kuchukua chochote ukitakacho humu
ndani.Mimi ya kwangu ni hayo tu? Nikasema
na kuinama.Nilihisi maumivu makali ya moyo.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO?????????.
 
BEYOND PAIN
SEHEMU YA 8
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
?Kama tulivyoapa siku ya ndoa yetu na padri
akatamka kwamba kilichofungwa duniani
kimefungwa pia mbinguni kwa maana hiyo
ndoa yangu mimi na Emmy haitaweza
kuvunjika hadi pale kifo kitakapotutenga
nisha.Pamoja na yote aliyonitendea lakini
bado Emmy ni mke wangu na siku zote
sintalisahau hilo.Pamoja na hayo lakini yeye
kwa upande wake amelisahau hilo na kutamka
wazi kwamba hajisikii tena kuwa na mimi
mume wake wa ndoa na kwamba anahitaji
kwenda kuishi na mwanaume mwingine ili
walee mtoto wao.Natamka wazi kwamba yuko
huru kwenda huko atakako kwenda.siwezi
kumzuia kufanya atakavyo hata kama
tunafungwa na ahadi ya ndoa.Kwa hiyo Emmy
mimi nakuruhusu uende huko unakotaka
kwenda,ukaishi kwa amani.Inaniuma sana
lakini sina namna nyingine ya
kufanya.Naamini mateso haya
uliyonisababishia Mungu anayaona na iko
siku atanipa faraja.Kwa hiyo mama uko huru
kwenda unakotaka kwenda.Una ruhusa ya
kuchukua chochote ukitakacho humu
ndani.Mimi ya kwangu ni hayo tu? Nikasema
na kuinama.Nilihisi maumivu makali ya moyo.
ENDELEA?????????..
Wote wakakaa kimya ni baba mkwe pekee
aliyethubutu kufungua kinywa chake na
kusema
?Wayne tumeyasikia mawazo na maamuzi
yako.Wote tulikuwa tukisubiri kusikia kauli
yako ya mwisho kwa sababu wewe ndiye
mwenye mke na sisi ni washauri tu.Wayne
najua ni maumivu kiasi gani uliyoyapata kwa
kitendo hiki alichokufanyia mwenzio.najua
umeumia kupita kiasi japokuwa ni wewe
mwenyewe unayejua ni kiasi gani
umeumia.Pamoja na hayo yote Wayne
napenda nipendekeze jambo moja kwamba
bado kuwe na fursa ya majadiliano na
kusameheana.Sisi sote ni binadamu na sote
tunakosea.Baba wa mbinguni anaagiza
kwamba mara zote tuishi kwa kusameheana
hata pale ambapo mioyo yetu inakuwa
migumu kusamehe.Sijui wenzangu mnalionaje
suala hili? Baba mkwe akauliza
Mwalimu wangu wa dini akasema kwa haraka
?Mzee hata mimi nakuuunga mkono kwa
hilo.Japokuwa masuala haya bado ni
magumu na yanaumiza moyo lakini bado
tunapaswa kusameheana kwa kila jambo.Hata
mimi napendekeza hivyo kwamba tupate fursa
ya kulijadili suala hili kwa undani na
kusameheana ili maisha yaendelee na mtoto
asiweze kuathiriwa na haya yaliyotokea kwani
yeye ndiye atakayekuwa muathirika mkubwa?
Mawazo yao yalikuwa mazuri lakini moyoni
sikuwa hata na hamu ya kumuona tena
Emmy.Nikainua kichwa na kusema kwa
haraka.
?wazee wangu mna wazo zuri lakini naomba
niweke wazi kwamba mimi nilikwisha
msamehe Emmy siku nyingi.Najua aliteleza
kitu ambacho kila binadamu kinaweza
kumtokea.Pamoja na kufanya hayo yote
aliyoyafanya , bado Emmy ndiye aliyekuwa wa
kwanza kuondoka hapa nyumbani bila
kufukuzwa.Kwa maana hiyo ni kwamba hata
tukikesha usiku na mchana tunajadili tayari
mwenzangu hana mpango wa kuwa na mimi
tena.Angekuwa ni mtu mwenye busara na
mwenye kulitambua kosa lake angeweza
kuomba msamaha lakini mpaka leo hajafanya
hivyo.Ninyi wenyewe mmekuwa mashuhuda
wa majibu anayoyatoa hapa mbele yenu.Mzee
tusipoteze muda yeye aende tu anakotaka
kwenda.? Nikasema huku hasira tayari ikianza
kunipanda.Baba mkwe akamgeukia Emmy
?Emmy umeyasikia aliyoyasema mwenzako?
Baba mkwe akauliza .Emmy kwa sauti ndogo
akajibu.
?baba mimi nimekwisha sema siwezi tena
kuishi na Wayne.hakuna haja ya kupoteza
wakati kwa usuluhishi.Yeye amekwishanipa
ruhusa niende kwa hiyo hakuna kitu cha
kuendelea kujadili hapa.hata mkisema nini
mimi siwezi kurudiana na Wayne.? Emmy
akasema kwa kiburi.
Baba mkwe akatafakari kwa sekunde chache
halafu akasema
?sawa Emmy tumekusikia.Tumekuelewa
unataka kitu gani.nenda unakotaka kwenda
lakini ukumbuke kwamba hii ni dunia.mambo
uliyomfanyia mwenzio leo na wewe yatakukuta
kesho.Siku zote asiyefunzwa na mamaye
atafunzwa na dunia.nakutakia kila la kheri
huko uendako.? Baba mkwe akasema kwa
hasira
Baada ya kama dakika moja hivi ya ukimya
baba mkwe akasema.
? Wayne vipi kuhusu mtoto Baraka.Kuna
utaratibu gani kuhusu yeye?
?Baraka ana haki ya kumfahamu baba yake
mzazi.Haitakuwa jambo la busara kama
tutamficha ukweli mtoto.Ni jambo zuri ikiwa
atafahamu mapema kwamba baba yake si
mimi.Iwapo tutamficha na akaja kufahamu
tayari akiwa amekuwa mkubwa sana
itamuumiza mno.Mimi naona ni bora kama
tutafanya utaratibu ili aweze kufahamishwa
na kwa baba yake.Hata kama nikiendela
kumlea lakini awe akifahamu kwamba mimi si
baba yake mzazi.Bado nampenda sana
Baraka.Na endapo wazazi wake watakubali
wanaweza wakamuacha hapa mimi
nikaendelea kumlea???
Sikumaliza sentensi yangu emmy akajibu kwa
haraka
?Siwezi kumuacha mtoto wangu
hapa.Ninapoondoka hapa leo ninaondoka na
mwangu.Siwezi kuruhusu mwanangu aje
kulelewa na mwanamke mwingine.Mwanangu
nitamlea mimi mwenyewe.?
Emmy alisema kwa ukali halafu akainuka na
kuelekea chumbani kwa baraka.Kila mmoja
alikuwa akishangaa
?Wayne hivi huyu mwenzio amepatwa na
matatizo gani? Kwa sababu naona si yule
Emmy niliyemlea mimi.Amebadilika ghafla?
Baba mke akauliza
?baba hata mimi mwenyewe ninashangaa kwa
mabadiliko haya .?
Wakati tukiendelea kujadiliana kule sebuleni
nikasikia Baraka akipiga kele chumbani
kwake.Nikainuka na kuelekea chumbani kwa
Baraka
Emmy alikuwa akipakia nguo na vitu vya
Baraka katika begi huku Baraka akilia kwa
nguvu.
?Baraka kuna nini ? Nikauliza baada ya
kumkuta Baraka akigalagala chini.
Aliponiona akakimbia na kunikumbatia.
?Daddy ,mama anasema eti leo tunahama
mimi na yeye tunakuacha peke yako.Halafu
anasema eti anataka kunipeleka kwa baba
yangu? Nilimuonea huruma malaika yule asiye
na kosa. Nikambembeleza akanyamaza kulia
halafu nikamwambia.
?Baraka ni kweli mama yako anakupeleka
ukamfahamu baba yako mzazi.Hatukukut
aarifu toka mapema kwamba mimi si baba
yako mzazi.Kwa hiyo B??.? kabla sijamalizia
sentensi yangu baraka akachoropoka na
kukimbia akajifungia bafuni akilia.
Nikamfuata na kukuta tayari amekwisha
ufunga mlango kwa ndani.Alikuwa akilia kwa
nguvu
?Baraka fungua mlango..Nikasema.
?Sifungui mlango hadi uniambie wewe ndiye
baba yangu.?
Nikakosa jibu la kumpa.Roho ikaniuma sana
kwa malaika yule kuteseka bila kosa.
?Fungua mlango Baraka? Nikasema tena .
?daddy sifungui mlango hadi uniambie wewe
ndiye baba yangu.Mimi simtaki baba
mwingine zaidi yako???.?
Nilichomwa na maneno yale ya Baraka
nikasimama na kuuma meno kwa hasira
?Kwa nini Emmy unafanya hivi? Nikajisemea
moyoni.
.Kwa jinsi nilivyokuwa ninampenda mtoto yule
sikutazamia kama itakuja tokea siku ambayo
ataumia kama hivi.Nilisimama pale mlangoni
nikiwa na hasira huku Baraka akiendelea kulia
mle ndani bafuni.
?Baraka fungua mlango ,nataka kuongea na
wewe.Fungua mlango mwanangu? Nikaendelea
kumbembeleza Baraka afungue mlango.Bado
aliendelea kulia.
?Baraka mwanangu nyamaza kulia na ufungue
mlango.? Nikasema tena
?baba sifungui hadi uniambie kwamba
hautanipeleka huko mama anakotaka
kunipeleka.Simtaki baba mwingine.wewe ndiye
baba yangu? Baraka akasema.
Wakati nikiendelea kumbembeleza baraka
afungue mlango wa bafuni baba mkwe
akatokea.
?Wayne nini kinaendelea huku? Akauliza baba
mkwe.
?Mzee,Baraka amekimbia na kujifungia huku
bafuni.Hataki kwenda sehemu yoyote
ile.Nimejaribu kumbembeleza afungue mlango
lakini amekataa hadi nitakapomuhakikishia
kwamba mimi ni baba yake?
baba mkwe akainama na kufikiri kwa sekunde
kadhaa halafu akasema
?Emmy amesababisha mambo makubwa
mno.Sikutegemea kama itakuja tokea siku
Emmy atakuja fanya mambo kama haya.?
Baba mkwe akanong?ona.
Kwa muda wa kama dakika moja tulikuwa
tumesimama pale mlangoni huku Baraka
akiendelea kulia mle bafuni.
?Kwa hiyo umeamua nini Wayne? Baba mkwe
akauliza.
?Ni kama tulivyoamua pale sebuleni.Emmy
ataondoka na Baraka na kwenda kumkabidhi
mtoto kwa baba yake mzazi,halafu taratibu
nyingine za kisheria na kikanisa zitafuata
baadae.lakini kwanza baraka amfahamu baba
yake?Nikasema
?Sawa Wayne mimi siwezi kupingana na
uamuzi wako japokuwa Emmy ni mwanangu
lakini kwa dharau aliyoionyesha leo kwetu sisi
wazazi wake na kwako wewe mume wake wa
ndoa sina budi kukubali uamuzi wako huo
kwamba aende anakotaka kwenda lakini ni
dunia ndiyo itakayomfundisha.Mpaka
umefikia uamuzi huu nina imani atakuwa
amekufanyia mambo mengi ambayo huwezi
kuyaweka wazi.lakini pamoja na hayo nina
wazo moja.?
?wazo gani baba?Nikauliza
?Nataka nimpeleke Emmy huko anakotaka
kwenda.Nataka nikamkabidhi kwa huyo mume
wake mpya ambaye yeye ametamka mbele
yetu kwamba ndiye anayemfaa kuishi
naye.Kwa sababu yeye ameamua kuachana na
kiapo chake cha ndoa alichoapa mbele ya
mwenyezi Mungu,nitampeleka kwa huyo
mwanaume ambaye yeye anamuona ni wa
muhimu kwake .Inaniuma sana kufanya hivyo
kama mzazi ambaye nilipaswa kuhakikisha
mambo haya yanakwisha na mnakuwa
pamoja tena lakini hata kama tukijaribu
kuyaweka sawa mambo haya ili muishi
pamoja Emmy atakuumiza sana na anaweza
hata kukutoa uhai wako.Wayne acha tu
niende nikamkabidhi huko halafu nitanawa
mikono.Huyo Chris ndiye atakayekuwa ni baba
na mama yake.? Baba mkwe akasema
Nikakaa kimya kwa muda halafu nikasema
?Baba tutakwenda sote?
?Hapana Wayne nadhani ingekuwa vizuri kama
ungebaki hapa halafu mimi na huyu mzee wa
kanisa tutampeleka Emmy huko anakotaka
kwenda.?
?Nalijua hilo baba.Lakini ninaomba
niongozane na ninyi .Hakuna chochite
kitakachoharibika.Chris alikuwa rafiki yangu
mkubwa sana.Sintamweleza chochote
isipokuwa nataka aione sura yangu ili
aendelee kuikumbuka katika maisha yake
yote.?
?sawa wayne kama umesisitiza basi hakuna
shida.Sasa tunafanyaje kuhusu huyu mtoto
aliyejifungia humu bafuni? Muda unazidi
kusonga.?Baba mkwe akauliza
?Nimekumbuka kuna ufunguo wa akiba.Ngoja
nikauchukue ? Kwa haraka nikaelekea
chumbani nikauchukua ufunguo wa akiba
.Emmy bado alikuwa akikusanya nguo pamoja
na vitu vyake vidogo vidogo.Sikusumbuka
kumsemesha nikatoka chumbani na kurudi
kule bafuni alikokuwa amejifungia
Baraka.Nikachomeka ufunguo na kuufungua
mlango.Baraka alikuwa amejikunyata katika
pembe ya bafu akilia.Nilimuonea huruma
sana mtoto yule lakini sikuwa na namna
nyingine ya kufanya.
Nilimfuata pale chini alipokuwa amekaa
nikapiga magoti na kumfuta machozi.
?baba naomba usinipeleke huko mahala
mama anakotaka kunipeleka.? Baraka
akasema
?Nyamaza kwanza kulia baraka?
Nikambembeleza
?Baba mimi sitaki kuwa na baba
mwingine.wewe ndiye baba yangu? Baraka
akasisitiza
?Nalijua hilo Baraka ,lakini huko mama yako
anakotaka muende ni muhimu sana.Ila usijali
tutakwenda wote.Mimi pia ninakwenda.?
?na wewe unakwenda baba? Akauliza Baraka
?Ndiyo Baraka.hata mimi ninakwenda
huko.Inuka basi twende ukajiandae?
Baraka akakubali ,akainuka nikamshika
mkono na kumuongoza kwenda chumbani
kwake.Nguo zake pamoja na vitu vyake
vilikuwa tayari vimepakiwa katika masanduku
.Niliumia sana moyoni .Sikutegemea kama
ingetokea siku ningeachana na mtoto huyu
niliyempenda kupita kitu chochote.Machozi
yalikuwa yakinilenga lakini nikajikaza ili
baraka asigundue chochote.Alipokuwa tayari
nikamfuata mama yake kule chumbani.
?baraka yuko tayari.Vipi uko tayari?
Nikamuuliza Emmy lakini hakunijibu kitu.
?kama kuna vitu vitabaki kesho nitamtuma
dereva akuletee kila kitu unachohitaji?
Nikasema
?Sihitaji kitu chochote toka kwako
Wayne.Nilichokuwa nikihitaji nimeshakipata.N
ilikuwa nahitaji kuondoka tu hapa ndani.na
tafadhali wayne nakuomba nikitoa mguu
ndani ya nyumba hii usiendelee kunifuata
wala kunipigia simu.Forget if I exist.Na wala
usimfuate fuate Chris.hana kosa lolote mimi
ndiye niliyemchagua?
Emmy akasema huku amenikazia
macho.Sikutaka kuendelea kubisha
naye.Nikainua mabegi yake mawili nikaanza
kuyatoa nje na kuyafungia katika gari
lake.Mama yake aliyekuwa amekaa ndani ya
gari baada ya kutolewa mle sebuleni kutokana
na hali yake kuanza kubadilika alianza kulia
aliponiona nikitoka na mabegi na kuyapakia
katika gari la Emmy.nadhani alifahamu fika
kwamba mambo yalikwisha haribika.
?wayne baba usijali Mungu atakulipia.Mambo
aliyokufanyia huyu mwenzio ni mambo
mabaya sana? Akasema mama mkwe.
?usijali mama hii ndiyo dunia na hii ni
mitihani ambayo hatuna budi kuishinda.Nitak
uwa salama mama usijali? Nikasema huku
nikipiga hatua kurudi tena ndani.Nilijitahidi
kutokuonesha hali yoyote ya huzuni japokuwa
nilikuwa na maumivu makubwa ndani ya
moyo.Nikachukua mabegi ya Baraka na
kuyapakia pia ndani ya gari ya Emmy.
?baba naona kila kitu kiko tayari.nadhani
tunaweza kuondoka sasa? Nikamwambia baba
mkwe.
?Emmy tunakwenda wote hadi kwa huyo
mume wako mpya.Tunataka tukakukabidhi
huko? baba mkwe akamwambia Emmy
aliyekuwa amesimama mlangoni akiwa na
Baraka.
?baba mimi nakwenda peke yangu.Sitaki mtu
yeyote anifuate? Emmy akasema na kumfanya
baba mkwe akunje uso kwa hasira
?Emmy nakuonya kwa mara ya mwisho
kwamba sintaendelea kuvumilia dharau zako
kwetu.Umetudhalilisha kiasi ambacho wewe
huwezi jua,lakini kama haitoshi bado
unaendelea kutudharau.Nakwambia
sintavumilia zaidi dharau zako.Kuanzia sasa
nataka unisikilize mimi kama baba
yako.Nakuonya usiendelee kunijaribu tena??
baba mkwe akasema kwa hasira huku akitoa
kitambaa na kujifuta jasho.
?wayne kama hakuna tunachokisubiri tena
,funga nyumba twendeni ? baba mkwe
akaamuru.tayari alikuwa amekasirika
.Nilimsifu sana baba huyu kwa ustahimilivu
wake mkubwa kwa dharau za mtoto wake wa
kumzaa.Dharau za Emmy hazikuwa
zikimithirika.Sikujua sababu ya mabadiliko
yale ya tabia ya Emmy.
Nilifunga milango ya nyumba yangu huku
roho ikiniuma kila nikimfikira baraka.Mimi na
Beka pamoja na wale wasimamizi wetu wa
ndoa tukaingia katika gari la Beka,halafu
mzee wa kanisa akapanda gari moja na baba
na mma mkwe ,Emmy akapanda gari lake
akiwa na Baraka.Safari ikaanza ya kuelekea
Njiro mahala anakoishi Chris.
Usiku huu hakukuwa na msongamano mkuwa
wa magari katika barabara iendayo Njiro.Kwa
wakazi wa Arusha wanaufahamu
msongamano mkubwa wa magari uliopo siku
hizi katika barabara za jiji hili linalokua kwa
kasi. Haikutuchukua muda mrefu sana toka
maeneo ya Majengo ninakoishi mimi hadi
maeneo ya Njiro. Safari yetu ilikuwa ni ya
kimya kimya.Kila mtu alikuwa akiwaza
lake.Tulikuwa tukilifuata gari la Emmy ambaye
ndiye aliyekuwa akituongoza njia.Hatimaye
gari ya Emmy ikasimama nje nyumba moja
yenye geti kubwa jeusi.Akafungua mlango na
kushuka garini.Baba mkwe naye akashuka
garini.Kuona hivyo na sisi ikatubidi tushuke.
?nadhani ni hapa? baba mkwe
akasema.Nilipatazama mahala pale
nikapatambua kwamba pale hapakuwa kwa
Chris.
?Mzee hapa si nyumbani kwa Chris.Ninapafah
amu nyumbani kwake.Emmy anataka
kutuchezea mchezo? Nikasema.Ni wazi pale
hapakuwa nyumbani kwa Chris.Haraka haraka
baba mkwe akamwita Emmy ambaye alikuwa
getini akisubiri geti lifunguliwe.
?Emmy nilikuonya toka mwanzo kwamba
sintavumiia tena dharau na michezo yako ya
kijinga.Hebu niambie hapa ndipo nyumbani
kwa Chris?
Babamkwe akauliza.Emmy hakujibu kitu
akabaki kimya.Tukiwa hatuna hili wala lile
tulitahamaki baba mkwe akimchapa Emmy
kofi kali la shavuni linalompeleka Emmy
chini.Alitaka kumfuata tena pale pale chini ili
aendelee kumuadhibu lakini kwa jitihada
zangu na Beka tukafanikiwa kumtuliza.
?Haya ingia garini sasa hivi tunaelekea kwa
Chris.Wayne ongoza njia kwenda kwa huyo
mshenzi mwingine? baba mkwe akatamka kwa
hasira.Emmy akasimama huku akilia akaingia
garini na kuligeuza gari lake.Mimi
nikatangulia mbele halafu gari la Emmy
likafuatia na mwisho lilikuwa ni gari la baba
mkwe.Dakika chache baadae tukawasili katika
nyumba ya Chris.Gari zikasimama nikashuka
na kumfuata baba mkwe.
?baba ,Chris anakaa hapa? Nikasema
?una uhakika Wayne? Baba mkwe akauliza
?Nina ukakika baba? Nikajibu.Baba mkwe
akashuka na kumfuata Emmy ambaye alikuwa
ameuinamia usukani akilia
?Hebu tuambie hapa ndipo nyumbani kwa
Chris? Baba mkwe akauliza kwa ukali
?Ndiyo .Ni hapa? Akajibu huku akijifuta
machozi.
?haya wapigie simu ndani watufungulie
mlango?
Sekunde chache geti likafunguliwa tukaingiza
magari ndani.Baada tu ya kushuka ndani ya
Gari Baraka akaja na kuung?angania mkono
wangu.hakutaka kuniachia.Emmy
akatuongoza na kuelekea sebuleni.Mara tu
tulipoingia sebuleni nilipatwa na kitu
ambacho siwezi kukielezea kama ni hasira au
ni nini baada ya kumuona aliyekuwa rafiki
yangu mkubwa Chris akiwa amekaa sofani
akiangalia luninga huku mezani kukiwa na
chupa kubwa ya mvinyo. Mapigo ya moyo
yalibadilika na kuanza kwenda kwa kasi ya
ajabu.Nikahisi jasho likilowanisha shati langu
jepesi.Kichwa kiliwaka moto kwa hasira.Chris
aliponiona nimesimama alipatwa na mstuko
mkubwa akainuka na kusimama huku akiwa
na wasi wasi mwingi.Niliushuhudia uso wake
ukivuja jasho jingi.
?Hallow?W..way.ne..? Akasema kwa sauti
yenye kutetemeka.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO??????
 
SEHEMU YA 10
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
?Chris usiseme chochote.kwa kuwa
wamekwisha nikataa kuwa mimi si mtoto wao
sasa ya nini uendelee kuwabembeleza?
Achana nao Chris.Let them go.?
Nilimtazama Emmy kwa hasira.Alikuwa
akiongea kwa kiburi sana.Sikutegemea kama
ni kweli Emmy niliyemfahamu leo hii anadiriki
kutamka maneno yale kwa kiburi kikubwa na
tena mbele ya wazazi wake.Baba mkwe
hakutaka kuongea tena neno lolote
akatuongoza tukatoka nje.Nilimuona Chris
akiwa amesimama pale sebuleni akiwa
haamini kilichokuwa kimetokea.
?Wayne baba, nenda nyumbani
kapumzike.Tutaongea zaidi kesho.Ninachoku
omba usiwaze sana kuhusu haya
yaliyotokea.Hii ni mitihani ya dunia na huna
budi kuishinda.Ninachokusihi jitahidi sana
kuomba Mungu ili aweze kukupa nguvu ya
kuweza kuyashinda majaribu haya.Muda si
mrefu mambo haya yatakwisha na utasahau
kabisa? baba mkwe akaniambia huku
akinipiga piga mgongioni wakati tukijiandaa
kuingia katika magari yetu .Sikujibu kitu
nilikuwa nimeinama chini nikitafakari..S
ikutegemea kama mwisho wangu na Emmy
ungekuwa namna hii.
ENDELEA????????..
?Wayne anayosema baba yako mkwe ni ya
kweli kabisa.Jipe moyo na Mungu
atakusaidia.Jitahidi sana kudumu katika
maombi na Mungu atakusikia.Inawezekana
Mungu ana mpango mwingine na wewe.Mimi
binafsi nitakuombea sana kila siku ili upate
nguvu uweze kuendelea na maisha yako.Ila
kesho nitaonana na baba Paroko na
kumweleza kuhusu suala hili ili tuone ni kitu
gani anaweza akafanya kwa sababu kwa
mahali ndoa yako ilipofikia ni pagumu sana.?
Mwalimu wangu wa kanisa naye akasema
machache.Niliwashukuru sana wazee wale
kwa nasaha zao na kwa jinsi walivyoniunga
mkono ,tukaingia magarini na kuondoka zetu.
?Beka sikutegemea kama mwisho wangu na
Emmy ungekuwa namna hii.mwanamke
niliyempenda na kumthamini leo amenifanyia
kitendo kama hiki du ! sikutegemea
kabisa.Nilikuwa mjinga sana kwa kumuamini
Emmy kupita kiasi .Alinitenda mara ya
kwanza nikamsamehe na kurudiana naye
tena.Nilifanya kosa kubwa sana kuamua
kurudiana naye baada ya kosa lile la
kwanza.Nimepoteza muda mwingi katika
kulihudumia penzi lisilokuwa na matunda
yoyote zaidi ya maumivu kila kukicha.?
Nilisema kwa hisia kali wakati tukiendelea na
safari ya kurudi nyumbani.Nilikuwa na
uchungu mwingi.
?Wayne najua ni jinsi gani ulivyoumizwa na
suala hili.Hata mimi ninapata wakati mgumu
sana kuamini kama ni kweli yametokea
haya.Ni kweli kama mambo haya ameyafanya
Emmy ninayemfahamu mimi.kama
nisingeshuhudia mwenyewe kwa macho yangu
nisingeamini katu kama Emmy angeweza
kufanya mambo kama yale.Kitu cha msingi ni
kukubali kilichotokea.Jipe moyo na maisha
yaendelee.Jipange na uanze maisha
mapya.Msahau kabisa Emmy katika maisha
yako.Bado hujachelewa Wayne katika
kuyapanga upya maisha yako.Jipange vizuri
na mwisho wa siku utasahau kila kitu kuhusu
Emmy? beka akasema.
?Beka hakuna mtu anayeweza kuyaongelea au
kupima maumivu niliyoyapata kwa kitendo hiki
cha Emmy.Amenisababishia majeraha
makubwa moyoni ambayo si rahisi kufutika
mapema.Itanichukua muda mrefu sana
kumsahau Emmy na mambo yote
aliyonitendea.Kinachoniuma zaidi ni ukatili
alioufanya kwa mtoto Baraka.Inaniwia vigumu
kuamini kwamba mtoto yule si
mwanangu.Bado ninampenda kupita maelezo
na sijui hata nifanye kitu gani ili niweze
kuyaondoa maumivu haya makali kuhusiana
na mtoto huyu .? Nikasema huku Beka
akikanyaga mafuta na kuongeza mwendo wa
gari
?Huwezi kumsahau kwa haraka namna hiyo
Wayne.Nakushauri uchukue likizo ndefu na
uende mbali na hapa ukae huko kwa muda
.Utakapokuwa mbali na mazingira haya
utajifunza ni jinsi gani ya kuanza maisha
mapya.Nadhani hii itakuwa njia bora sana ya
kuweza japo kwa asilimia chache
kukusahaulisha na mkasa huu wa kuumiza.?
Beka akasema.Ushauri wa Beka ulikuwa mzuri
nikauona unafaa
?nakubaliana nawe Beka.Hilo ni wazo
zuri.Itanibidi nilifanyie kazi mapema
iwezekanavyo.I need to go far away from
here.I need to forget everything.?
Nikasema.Wazo lile la Beka lilikuwa ni wazo
zuri ambalo hata mimi nilikuwa bado
sijalifikiria.Ni kweli ,ningezidi kuumia sana
kama ningeendelea kukaa ndani ya nyumba
ambayuo kila siku kumbu kumbu ya Emmy na
baraka zingekuwa zinanijia.
Beka alinipeleka nyumbani akaniacha pale na
yeye kuondoka.Nikaingia ndani na kukaa
sebuleni.Ukutani kulikuwa na picha kubwa
niliyopiga na Emmy siku ya harusi
yetu.Niliiangalia picha ile kwa umakini
mkubwa .Emmy alikuwa amejaa tabasamu
zito,alikuwa amependeza sana.Ni kipindi
ambacho tulikuwa katika mapenzi
makubwa.Tulikuwa katika mahaba mazito
sana.Ni katika kipindi hicho nilikuwa ni
mmoja kati ya wanaume wenye furaha kubwa
duniani.Sikutaka tena kuendelea kuiangali a
picha ile,nikaitoa na kuiweka chini,nikaanza
kukusanya vitu vyote ambavyo
vitanisababisha nimfikirie Emmy .Nilikusanya
kila kitu chenye uhusiano na Emmy kuanzia
picha hadi vyombo nikavifunga pamoja katika
boksi kubwa na kwenda kuvihifadhi stoo.Saa
nane za usiku nikapanda kitandani na kulala.
* * * *
Niliamka saa nne za asubuhi.Kichwa kilikuwa
kizito sana.Nyumba yote ilikuwa kimya
kabisa.Nilizoea kuamka asubuhi na kuikuta
nyumba ikiwa imechangamka kwa muziki
,maongezi na vicheko lakini leo hii hali ilikuwa
tofauti kabisa.Hakukuwa na sauti yoyote
iliyokuwa inasikika.Mtu pekee niliyeamini
angekuwapo ndani muda ule ni mtumshi wa
ndani .Kwa kuwa nilikuwa nimedhamiria
kuchukua likizo ndefu na kuondoka kabisa
Arusha niliamua kumpa likizo binti yule wa
ndani akapumzike hadi hapo nitakapomuhitaji
tena.Nilijizoa zoa pale kitandani nikaenda nje
na kumkuta Sharifa akifua nguo.
?Shikamoo kaka? akanisalimu kwa adabu.
?marahaba Sharifa hujambo?
?Sijambo kaka? akajibu msichana yule
mwenye adabu nyingi.Msichana yule
aliyekuwa akitokea mkoani Singida nimeishi
naye kwa muda mrefu na ninamchukulia kama
mmoja kati ya ndugu zangu.
?Sharifa kuna jambo ninataka kuongea na
wewe? Nikamwambia na kumfanya astuke na
kuacha kazi aliyokuwa akiifanya.
?Sharifa nadhani unafahamu kila kitu
kilichotokea hapa nyumbani.Hali hapa
nyumbani si shwari.Dada yako ameondoka na
kwa sasa niko mwenyewe hapa
nyumbani.Kutokana na mambo yaliyotokea
hata mimi nimeamua kuchukua likizo na
kusafiri ,kwa maana hiyo nimeona nikupe
likizo uende nyumbani ukapumzike kwa muda
halafu nitakaporudi nitakuita tena..Kwa hiyo
leo ungejiandaa na kesho uanze safari?
Nilimpatia kiasi cha shilingi laki tatu kwa ajili
ya maandalizi ya kwenda nyumbani
kwao.Ingawa hakuwa na pingamizi lakini
niliamini moyoni hakuwa amependezwa na
suala lile la kumtaka arudi nyumbani kwa
muda hadi hapo nitakapomuita tena.Sikulijali
hilo .Baada ya kuoga nikapata kifungua
kinywa halafu nikarudi tena chumbani kwangu
kulala.Sikuwa na hamu ya kwenda mahala
popote.Niliutumia muda huo kutafakari
mustakabali mzima wa maisha yangu
yaliyopita na yajayo.Nilijaribu kuitumia nafasi
hiyo katika kuyapanga maisha yangu yajayo
bila ya kuwa na Emmy na Baraka.
Saa kumi za jioni niliamua kutoka na kwenda
sehemu tulivu kwa ajili ya kupata upepo na
kupunguza mawazo.Sikutaka kwenda sehemu
zenye mkusanyiko mkubwa wa watu.Nilihitaji
kwenda mahala ambako ni tulivu
,nitakapopata wasaa wa japo muda mfupi
kuyasahau maisha yangu ya nyuma.Arusha
tulivu garden ni moja kati yua sehemu tulivu
sana kama lilivyo jina lake.Ni sehemu ambayo
imekuwa inapendwa sana na wageni toka nchi
mabalimbali.nafikiri mahala hapa
panapendwa kutokana na utulivu wake na
mandhari ya kuvutia mno.Ninaifahamu
sehemu hii na ndiyo maana nikachagua kuja
huku kwa sababu ni sehemu pekee niliyoamini
ingeweza kunisaidia kunisahaulisha na
dhahama iliyonikumba japo kwa masaa
machache
Niliwasili katika geti la sehemu hii tulivu na
kuingia ndani.Nilikuwa nikitabasamu kwa
mandhari safi na tulivu ya mahala
hapa.Ndani ya bustani hii tulivu kulikuwa na
sura nyingi za wageni ambao kama
nilivyosema wanapapenda sana mahala
hapa.Niliegesha gari na kushuka nikatafuta
mahala nikaketi.Ukimya ulikuwa umetawala
sehemu hii.Ni milio ya ndege na muziki laini
wa ala ndivyo vilivyokuwa vikisikika.Hakika
nilipafurahia mno mahala hapa.Muhudumu
aliyevalia nadhifu,suti safi nyeusi na tai
nyekundu akafika na kwa adabu
akanikaribisha na kuniuliza kile ambacho
ningependa kutumia.Nilimuomba aniletee
wine safi aina ya Lion hills.Mkononi nilikuwa
na kitabu cha hadithi tamu ya kusisimua
nilichokinunua majuma kadhaa yaliyopita,kita
bu kilichoandikwa na mmoja kati ya
waandishi wa riwaya ninaopenda kusoma
riwaya zao kiitwacho ?Before I die? Kwa siku
hii niliamua kutumia muda huu niliouapata
kwa ajili ya kuisoma hadithi hii tamu na ya
kusisimua.Nilikuwa nikisoma huku nikiendelea
kupiga mafunda kadhaa ya wine ile
nzuri.Nilijisikia furaha sana kwa muda ule
niliokuwa pale.
?habari yako kaka? Nilistuliwa na sauti tamu
na nzuri ya mwanamke.Kwa kuwa nilikuwa
nimezama katika simulizi nzito ya kitabu hiki
cha ?before I die? nilionesha kama kustushwa
kidogo na sauti ile.Nikainua kichwa na
kukutana na sura ya mwanamke mmoja
mrembo sana aliyekuwa amesuka nwele zake
katika mtindo wa rasta zilizokuwa zimemkaa
vyema.Alikuwa mwembamba wa wastani na
mwenye sura nzuri .
?Nzuri dada habari yako? Nikasema huku
nikimtazama mwanadada yule .
?habari yangu nzuri. Naruhusiwa kukaa?
Akauliza dada yule mwenye sauti tamu .
?Hakuna shida unaweza kukaa? Nikasema na
dada yule akavuta kiti na kuketi.Mara moja
muhudumu akafika dada yule akamuomba
amletee kinywaji chake alichokiacha katika
meza aliyokuwa amekaa.
?Sahamani kaka kama nimekusumbua
,nilikuwa nimekaa kule peke yangu lakini
nikaona ninazidi kuboreka.Nimekuona muda
mrefu uko hapa mwenyewe nikaona nisogee
hapa walau nione kama ninaweza kupata mtu
wa kuongea naye mawili matatu.Sahamani
kama nimekukwaza.? Akatamka dada yule na
kunifanya nitabasamu kutokana na adabu na
ustaarabu wake
?Bila samahani dada yangu.Mimi mwenyewe
nilikuja hapa kwa ajili ya kupumzika na
kupoteza mawazo lakini kwa kuwa sikuwa na
mtu yeyote wa kuweza kubadilishana naye
mawazo nikaamua kujisomea kitabu changu
hiki cha hadithi ilimradi siku iende? Nikasema
huku nikikifunika kitabu changu nilichokuwa
nakisoma na kukiweka mezani.
?Wow ! ?before I die? ! Nimesikia kwamba
kitabu hiki kimetoka.Nilikuwa nakitafuta
sana.Napenda sana riwaya za huyu
kaka.mara nyingi nisomapo riwaya zake huwa
nahisi msisimko wa ajabu sana? Akasema
dada yule.
?Kumbe hata wewe ni mpenzi wa mtunzi
huyu? Nikauliza huku nikitabasamu.
?Mimi ni shabiki wake mkubwa.Kinachon
ifurahisha ni kwamba amekuwa akiandika
simulizi tamu ambazo mara nyingi ni vitu
vinavyotokea katika jamii yetu.Kuna kitabu
aliwahi kukitoa kinaitwa Malaika wa
Valentine,kwa kweli kitabu kile kila
ninapokisoma huwa ninatoa machozi kwa
sababu hadithi ile inanigusa mno kwani
mambo yaliyomo katika kitabu kile yaliwahi
kunitokea hata mimi.Tokea wakati huo siachi
kusoma hadithi yake hata moja.? Akasema
mwanadada yule ambaye tayari muhudumu
alikwisha mletea kinywaji chake alichokuwa
anakitumia.Nilipotazama alikuwa akitumia
Miami 24 whisky.Nilistuka kidogo kwa sababu
kutokana na umbo lake na jinsi alivyo
sikutegemea kama angeweza kutumia kinywaji
kikali kama kile.Nilipatwa na shauku ya
kutaka kumfahamu zaidi yule
dada.Akamimina mvinyo kidogo katika glasi
halafu akanywa yote akainua kichwa na
kunitazama.
?Nimefurahi sana kumpata shabiki mwingine
wa simulizi za Patrick.? Nikasema huku
nikitabasamu.
?Hata mimi ninafurahi sana kila ninapokutana
na mtu ambaye anapenda kusoma hadithi za
watunzi mbali mbali.Itabidi tufanye mpango
wa kuanzisha klabu ya wasomaji wa riwaya
,wewe mwenyekiti mimi katibu ,au unasemaje?
Akauliza na kufanya wote tuangue kicheko
kikubwa.Hiki kilikuwa ni kicheko changu cha
kwanza toka nimekumbwa na masahibu ya
Emmy.
?Hiloni wazo zuri sana.Tunaweza tukaanzisah
kitu cha namna hiyo ambacho kinaweza
kusaidia sana kuamsha ari ya usomaji vitabu
hapa nchini.Katibu wewe unaitwa nani?
Nikauliza na kumfanya dada yule acheke
kicheko kikubwa kinachosababisha na mimi
nicheke.Akatoa kitambaa katika pochi yake
ndogo na kujifuta machozi yaliyotokana na
kucheka.
?naitwa Clara.na wewe mwenyekiti wangu
unaitwa nani? Akauliza
?Mimi naitwa wayne?
?Ouh Jina zuri sana wayne.Nafurahi mno
kukufahamu.? Akasema Clara huku
akitabasamu.
?Wayne wewe ni mkaazi wa hapa Arusha?
Akauliza.
?Haswaa.Mimi nimkaazi wa hapa hapa
Arusha.Ninaishi maeneo ya Majengo.wewe
unaishi wapi?
?Kwa sasa mimi makazi yangu ni Pretoria
afrika kusini japokuwa wazazi wangu wanaishi
Dar es salaam.Hapa Arusha nimekuja kwa siku
chache kwa ajili ya kutoa mada katika semina
ya mitindo na mavazi inayoendelea katika
hoteli ya Naura spring.Siku ya leo nimeamua
kuja hapa kwa ajili kupata hewa safi na
kutuliza kichwa.? Clara akasema.
?Ouh kumbe unajishughulisha na masuala ya
mitindo na mavazi? Nikauliza
? ndiyo .Ninajishughulisha na mambo ya
ubunifu na mitindo kwa ujumla.? Akajibu.
?Nilipokuona nilijua ni lazima ungekuwa
mwanamitindo? Nikasema na kumfanya
atabasamu.
?Unaionaje fani ya mitindo na mavazi hapa
Tanzania ukilinganisha na afrika ya kusini?
Nikauliza. Clara akamimina mvinyo katika
glasi akanywa halafu akasema.
?Kwa hapa Tanzania fani hii ya mitindo bado
iko chini japokuwa kuna wanamitindo wazuri
na wabunifu wazuri.Wenzetu wamepiga hatua
kubwa sana.Kuna kila sababu ya kuongeza
juhudi ili kuweka kufikia hatua waliyopiga
wenzetu kama afrika kusini .Wenzetu wakojuu
sana.Ninachokifanya kwa sasa ninajaribu
kuwatafutia wanamitindo na wabunifu wa
kitanzania nafasi katika majukwaa makubwa
ya kimataifa na kuwafanya wajulikane.Ni kazi
kubwa lakini tunajitahidi na maendeleo si
mabaya? Clara akasema.
? Nimefurahi sana kusikia hivyo Clara.Unajua
hata mimi hapo awali nilikuwa na ndoto za
kuwa mbunifu lakini baadae nikajikuta
nikiingia katika masuala mengine kabisa na
kuamua kuachana na mawazo ya kuwa
mbunifu? Nikasema
?Unayoyasema ni kweli kabisa Wayne.Wengi
wanakuwa na ndoto za kuwa watu Fulani
lakini si wote wanaoweza kuzifanya ndoto zao
kuwa kweli.Mimi sikuwa na wazo la kuwa
mwanamitindo na wala sikuwahi kuota
kwamba iko siku nitajulikana katika majukwa
makubwa ya mitindo na mavazi.Kitaaluma
mimi ni daktari lakini kwa sasa nimeachana
na shughuli za udaktari na kuamua kujikita
zaidi katika mitindo.Ilikuwa mwaka juzi wakati
nikiwa katika mapumziko nchini afrika kusini
nilipokutana na mtu ambaye alinishawishi
nijaribu fani ya mitindo kwani aliona nina
vigezo vyote vya kuwa mwanamitindo.Ni
likuwa nataka kuyabadili maisha yangu kwa
hiyo nikaona niingie katika mitindo.Nashukuru
Mungu kwani baada tu ya kuingia katika
mitindo maisha yangu yalibadilika na mpaka
sasa ni mmoja kati ya wanamitindo
wanaofahamika na kuheshimika sana nchini
afrika kusini.? Clara akasema na kuzidi
kuniongezea udadisi juu yake.
?amesema alitaka kuyabadili maisha yake?
Kwa nini alitaka kuyabadili maisha yake?
Lazima kuna sababu iliyomlazimu afanye vile
Aliwezaje kufanikiwa kuyabadili maisha yake?
Hata mimi ninahitaji kuyabadili maisha yangu
na kuyasahau maisha yangu yaliyopita.Nata
kiwa kuwa karibu na Clara ili aweze kunisaidia
kuyabadili maisha yangu kama yeye
alivyofanikiwa? Nikawaza huku nikimuangalia
Clara usoni.
? Kwa hiyo wayne usishangae kwamba
ulikuwa na ndoto za kuwa mbunifu lakini
ukajikuta ukifanya kazi nyngine tofauti kabisa
na ubunifu .? Clara akasema na kunifanya
nitabasamu
?Una bahati sana Clara .Umeweza kufanikiwa
katika fani ambayo hukuwahi hata kuota
kama siku moja ungekuwa mmoja kati ya
wanamitindo wakubwa.? Nikasema
?Nashukuru Wayne.Niliweza kufanikiwa kwa
sababu nilikuwa najituma sana na nilikuwa
nahitaji kufanya kitu ambacho kingenifanya
niyasahu maisha yangu ya nyuma na kuanza
maisha mapya.Hii ndiyo sababu iliyonifanya
nijitume mno kitu kilichopelekea kufanikisha
ndoto zangu.? Akasema
?nafurahi jinsi ulivyojituma na ukafanikiwa.Ila
ninachofurahi zaidi katika jitihada zako za
kuyasahu maisha ya nyuma kama unavyodai ,
hujasahau nyumbani? Nikasema na wote
tukaangua kicheko kikubwa.
?You are so funny wayne..Siku zote nyumbani
kutabaki nyumbani.Nilizaliwa Tanzania
,nimekulia Tanzania.Afrika ya kusini
nimekwenda miaka minne iliyopita.Kwa hiyo
Tanzania ni nyumbani na siwezi kusahau
nyumbani na ndiyo maana unaniona niko
hapa mida hii.Niko nyumbani? Clara akasema
huku akitabasamu.Natamani ungesikia
mrembo huyu akiongea.Hutatamani amalize
kuongea.Alijua kupangilia maneno na sauti
Kama angekuwa mtangazaji katika redio au
televisheni nina imani angejizolea maelfu ya
wapenzi.
? Ulitaka kusahau kitu gani Clara? Nikauliza
kwa umakini na kumfanya Clara acheke kwa
sauti.Kitu kingine alichojaaliwa mrembo huyu
ni ucheshi.Kwa muda huu mchache niliokaa
naye nimegundua kwamba ni mmoja kati ya
wasichana wachache wenye mafanikio na
ambao hawana ile silica ya kujivuna au
kujiona wao ni bora zaidi kuliko wengine.Clara
ni mcheshi na mchangamfu sana.
?Wayne hilo swali la kichokozi? akasema huku
akiendelea kucheka.
?Si vibaya kufahamu Clara kwa sababu
unapoamua kufanya mabadiliko fulani basi ni
lazima kuwe na sababu fulani .Wewe ni
sababu gani zilikupelekea kuamua kuyabadili
maisha yako na kuanza maisha mapya?
Nikauliza na kumfanya acheke tena.
?wayne wewe ni mwandishi wa habari? ?
akauliza na kunifanya na mimi nicheke.
?Hapana Clara mimi si mwandishi wa habari?
Nikajibu.
Clara akatoa kitambaa chake cha mkononi na
kujifuta macho halafu akaniangalia
?Ni hivi Wayne,katika haya maisha tunapitia
mambo mengi sana .Kuna nyakati tunapitia
mambo ambayo kwa kweli yanatusababishia
tuweze kuyachukia maisha ,kuichukia dunia na
watu waliomo ndadni yake.Kuna nyakati vile
vile tunaamua kuyabadii maisha yetu na
kuamua kuwa wapya tena kutokana na
maisha tuliyoishi huko nyuma..Kwa sasa
mimi ni mtu mwenye furaha na amani
maishani mwangu tofauti na maisha
niliyokuwa nikishi hapo awali.Kuhusu ni kitu
gani kilipelekea mimi kuamua kubadili maisha
yangu..its uhh?something personal.I?m sorry
for that? Clara akasema
?Usijali Clara.Ila nakubaliana nawe kwamba
kuna mambo yanayotutokea katika maisha na
ambayo yanatulazimu kuachana kabisa na
maisha yetu ya nyuma na kuishi maisha
mapya.? Nikasema na mara kumbukumbu za
Emy zikanijia kichwani na kunifanya nikae
kimya ghafla.
?Wayne are you ok? Clara akanistua.
?Yah I?m ok ?Nikajibu.
?Unaonekana kama umezama katika mawazo
ghafla? Clara akasema.Sikujibu kitu
nikatabasamu
?Thinking of your wife? Akauliza
tena.Nikamtazama usoni na kusema
?I don?t have a wife? Clara akanikazia macho
na kuniuliza.
?whats that ring for?
?A ring? Nikauliza kwa mshangao.Ni kweli
katika kidole changu cha mkono pete ya ndoa
bado ilikuwa iko kidoleni.Nilighafirika sana
baada ya kugundua ujinga niliokuwa
nimeufanya wa kumdanganya mrembo
yule.Midomo ilikuwa ikinitetemeka na
kunifanya nishindwe kutamka neno.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO?????
 
BEYOND PAIN
SEHEMU YA 11
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
?Usijali Clara.Ila nakubaliana nawe kwamba
kuna mambo yanayotutokea katika maisha na
ambayo yanatulazimu kuachana kabisa na
maisha yetu ya nyuma na kuishi maisha
mapya.? Nikasema na mara kumbukumbu za
Emy zikanijia kichwani na kunifanya nikae
kimya ghafla.
?Wayne are you ok? Clara akanistua.
?Yah I?m ok ?Nikajibu.
?Unaonekana kama umezama katika mawazo
ghafla? Clara akasema.Sikujibu kitu
nikatabasamu
?Thinking of your wife? Akauliza
tena.Nikamtazama usoni na kusema
?I don?t have a wife? Clara akanikazia macho
na kuniuliza.
?whats that ring for?
?A ring? Nikauliza kwa mshangao.Ni kweli
katika kidole changu cha mkono pete ya ndoa
bado ilikuwa iko kidoleni.Nilighafirika sana
baada ya kugundua ujinga niliokuwa
nimeufanya wa kumdanganya mrembo
yule.Midomo ilikuwa ikinitetemeka na
kunifanya nishindwe kutamka neno.
ENDELEA????????
Clara akaona jinsi nilivyobadilika ghafla
akasema
?Usijali Wayne ,its ok.Sikuuliza kwa ubaya?
Picha za Emmy zilikuwa zikija kwa kasi
kichwani kwangu
?baba mimi nimekwisha sema siwezi tena
kuishi na Wayne.hakuna haja ya kupoteza
wakati kwa usuluhishi.Yeye amekwishanipa
ruhusa niende kwa hiyo hakuna kitu cha
kuendelea kujadili hapa.hata mkisema nini
mimi siwezi kurudiana na Wayne.?
Ni maneno ambayo aliyatamka Emmy mbele
ya wazazi wake,yalinifanya nikae kimya na
fundo kunijaa rohoni.Siwezi kuyasahau
maneno yale yaliyojaa kiburi.Nikakumbuka pia
siku niliyompigia simu na kumtaka afike
nyumbani kwa ajili ya kikao alinijibu majibu
ambayo sintaweza kuyasahu kama yalitoka
kwa aliyekuwa mke wangu wa ndoa.
?Tuongee nini tena? Hatuna cha kuongea
wayne.tayari ukweli unaufahamu kwa hiyo
sioni kama kuna kitu tunatakiwa kuongea
mimi na wewe.Umeshatambua Baraka siyo
mwanao kwa hiyo hata mimi si mkeo.Sifikirii
tena kuishi na wewe .Nimechoka mimi maisha
ya kubanwa banwa na kufugwa fugwa ndani
kama njiwa.Nahitahi maisha ya uhuru,maisha
ya kufanya nitakacho.Naomba uniache
Wayne.Mimi sifai kuwa mkeo.Unahitaji
mwanamke bora wa kuishi naye na si mimi.?
Uchungu na maumivu niliyokuwa najaribu
kuachana nayo vikarudi upya.
?Nilizama katika penzi la mtu asiyependeka.Ni
likuwa kipofu.Nilipoteza muda kupalilia penzi
ambalo halikuwa na faida wala manufaa
yoyote.She was right.may be I wasn?t a man
enough for her.I wasn?t her choice.Its time to
let her go.Its time to forget her?
Nikawaza.Nikauinua mkono na kuitazama
pete ile ambayo toka emmy amenivisha siku
tunakula kiapo cha ndoa yetu haijawahi
kutoka mkononi mwangu.Nilisikia uchungu
mwingi kwa jinsi alivyoweza kuivunja ahadi
aliyoiweka mbele ya madhabahu ya
Mungu.Aliahidi kunipenda katika kila hali
lakini ameshindwa kutimiza ahadi
yake.hakuwa na thamani yoyote tena
kwangu.Bado niliendelea kuitazama pete ile
kwa uchungu huku machozi yakinitoka.Siku
ona tena ulazima wa kuendelea kuivaa pete
ile kidoleni.Taratibu nikaanza kuizungusha na
kuitoa kidoleni kwangu.Niliitoa kidoleni na
kuishika mkononi.Clara alikuwa
amenitumbulia macho asiamini alichokuwa
amekiona.Niliitazama pete ile kwa hasira
nikainuka na kelekea moja kwa moja
lilipokuwa bwawa kubwa ambalo ndani yake
kulikuwa na bata wazuri weupe
wakiogelea.Nikaishika mkononi pete ile
nikaitazama na kunong?ona
? I have t do this to forget you Emmy.As from
today I erase every memory of you in my
heart.You ?ll have no chance in my heart.
From today I don?t know you,..from today I
never married you?from today you are out of
my life.I?m moving forward with my life?
Nilisema maneno yale kwa uchungu mwingi
huku machozi yakinitoka.Nikainua mkono na
kuirusha pete ile mbali kati kati ya
bwawa.Niliitazama pete ile ikidumbukia kati
kati ya bwawa lile.Nilibaki nimeishikilia nguzo
iliyokuwa pembeni ya bwawa kwa dakika
kadhaa.Bado machozi yalikuwa yakinitoka.
?Wayne its ok.? Ilikuwa ni sauti ya upole ya
Clara aliyekuwa akinitazama kwa wasi
wasi.Alinishika mkono na kuniongoza
kunirudisha mahala tulipokuwa tumekaa.
?Calm down Wayne ,its gonna be fine?
akasema Clara kwa sauti ya upole huku
akinisugua bega.
?Whysky please? Nikasema na kulisogeza glasi
karibu na Clara ili animimie mvinyo
Clara akanitazama kwa mshangao.Akanim
iminia mvinyo katika glasi nikaunywa wote
kwa mara moja.
?One more please? Nikasema.Clara
akanimiminia tena mvinyo katika glasi
nikanywa na kuweka glasi mezani.
?I?m sorry Wayne? Clara akasema
?Usijali Clara,ni mambo ya kwaida.?
Kimya kikapita cha dakika mbili hivi halafu
nikasema
?Clara samahani kwa hali ilivyobadilika
ghafla,lakini nimeshindwa kuvumilia.I feel so
much pain inside.This is beyond pain Clara.?
Nikasema kwa uchungu mwingi huku Clara
akinisugua sugua
?Its ok Wayne.You are gonna be fine.You are
gonna be ok? Akasema Clara.
?I don?t think so Clara.No body knows how I
feel inside.? Nikajibu.Kikapita kimya kidogo
Clara akauliza
?Wayne what happened? Can you tell me? ?
?Clara sijui hata nikueleze kitu gani.Lets not
talk about it now.Lets not ruin our
evening.Tumekuja hapa kupoteza mawazo na
si kuongeza mawazo.Lets drink and have fun?
Nikasema na kujimiminia mvinyo katika glasi
nikanywa.Clara naye akamimina mvinyo
akanywa..
Muda ulizidi kwenda na kiza kikaanza
kuingia.Tulikuwa tukiongea na kucheka kwa
furaha sana .Kwa mara ya kwanza toka
matatizo ya Emmy yamenikuta nilikuwa na
furaha iliyopitiliza.Tuliongea mambo mengi
huku tukicheka na kupata mvinyo.Ilikuwa ni
siku nzuri . Kwa muda wa masaa haya
machache nilisahau kabisa kama muda mfupi
uliopita nilikuwa nimezama katika dimbwi la
matatizo.Nilistaajabia uwezo wa Clara wa
kuweza kunisahaulisha japo kwa masaa
machache machungu yote yaliyonisibu
.Mwanamke huyu alikuwa na uwezo wa ajabu
sana.Alikuwa miongoni mwa wale watu
wachache mno ambao wana uwezo wa
kutamka neno moja likasababisha mabadiliko
makubwa katika maisha ya watu.Nilivutiwa
mno kuwa karibu na Clara .Japokuwa hapo
kabla niliweka ahadi kwamba kwa jinsi
alivyonitenda Emmy sintathubutu kuwa na
mwanamke mwingine tena maishani .Nilikuwa
nikiamini kwamba wanawake wote ni
sawa.Baada ya kukutana na Clara msimamo
wangu umeanza kutetereka na nimeanza
kuamini bado wapo wanawake wazuri na
wenye kunifaa na mmoja wao ni huyu mrembo
aliyekaa nami mezani,ambaye
amenisahaulisha machungu yote niliyoyapata
.Clara alikuwa mwanamke mcheshi,mkarimu
,na mwenye uelewa wa mambo wa kiasi cha
juu mno.Ni mwamanke msomi,mzuri na
mwenye ndoto za kufanya kazi kwa bidii na
kufikia malengo aliyojiwekea.Nilipata shauku
ya kutaka kumfahamu Clara kiundani zaidi
.Sikufichi ndugu msomaji nilikuwa nimevutiwa
mno na Clara.Mvuto huu haukutokana na ya
pombe tulizokuwa tunakunywa lakini nilihisi
kuna kitu kipo moyoni ambacho ni vigumu
kukielezea.Nilihisi kuna kitu kipo kati yetu sisi
wawili .Nilikuwa na hisia na furaha ya ajabu
sana ambayo sijawahi kuipata wakati nikiwa
na Emmy.
?Nilipoteza muda mwingi kwa Emmy na
kumbe wako wanawake wengine wazuri wenye
kujiheshimu ? niliwaza huku nikimuangalia
Clara usoni.
?Wayne nimekuona unaniangalia sana usoni
kwa muda mrefu sasa.Whats wrong? Clara
akauliza baada ya kugundua kwamba
nilikuwa nikimuangalia usoni.Ni kweli nilikuwa
nikimuangalia.Sikuisha hamu ya kuitazama
sura ile nzuri .
Nilitabasamu na kujibu
?Clara imenibidi nikuangalie tena na tena
usoni ili nithibitishe kama mwanamke
niliyenaye mezani ni binadamu wa kawaida au
ni roho.? Nikasema na kumfanya Clara acheke
kwa sauti.
?Kwa nini unasema hivyo Wayne? Clara
akauliza
?Its ..uhhmm ?I feel something strange with
you?kwa muda wa masaa haya machache
tuliyokaa pamoja hapa najiona kama mtu
mpya.Najisikia huru na mwenye furaha kupita
kiasi.Kwa muda huu mfupi nimeweza
kuyasahau matatizo yangu yote
niliyonayo.Kwa muda huu mfupi ninajiona ni
kama vile ninaishi katika dunia isiyokuwa na
matatizo ya aina yoyote..I feel like you have
some power..a magic power which makes
people forget their problems.?Nikasema huku
Clara akiwa hana mbavu kwa kucheka.Alichek
a sana na kunifanya nami nicheke
pia.Akachukua kitambaa na kujifuta machozi
yaliyotokana na kucheka.
?Wayne umenifurahisha sana leo.Sijawahi
kukutana na mtu aliyenifurahisha kama
wewe.Hebu leta mkono wako hapa? Clara
akasema nami bila kukawia nikaunyoosha
mkono wangu akaushika na kuupeleka katika
bega lake.
?Hiki umeshika ni kitu gani? Akauliza
?Hili ni bega? Nikajibu.
?Una hakika umeshika bega?
?Ndiyo Clara hili ni bega?
?Ok Good..kama una hakika kwamba hili ni
bega basi mimi si mzimu.Mzimu ni roho na
hauna nyama and above all mzimu haunywi
mvinyo? Akasema Clara na wote tukajikuta
tukiangua kicheko kikubwa.
?I wish like I could be this happy everyday?
Nikasema
?Me too? akasema Clara huku akitabasamu.
?Bado nina muda wa wiki nzima wa kuwapo
hapa Arusha.Kama na wewe utakuwa na
muda wa kutosha bado tunaweza kuendelea
kukutana na kuwa na furaha kila siku.Siwezi
kukataa Wayne kwamba leo nimefurahi sana.
I had a very great time with you.Nimeipenda
kampani yako? Nilitabasamu kuisikia kauli ile
ya Clara .Akainua mkono wake na kuitazama
saa
?wayne inakaribia saa tano za usiku.Nikiendel
ea kukaa na wewe hapa tunaweza tukafika
asubuhi.Its time to go now.I had a very great
time Wayne.? Clara akasema kwa sauti ya
chini ambayo ilionyesha wazi ni kwamba
alipenda kuendelea kukaa nami.
?Clara sipati neno la kukushukuru kwa jinsi
ulivyoifanya siku yangu ya leo kuwa yenye
furaha .Nashukuru sana Clara.? Nikasema
huku nikimalizia mvinyo uliokuwa ndani ya
glasi.
?Hapa arusha umefikia wapi? Nikauliza
?Nimefikia SEAN 11 Lodge wewe unaishi
maeneo gani???? Akasema
?.Mimi ninaishi Majengo? Nikasema huku
nikisimama
?Nashukuru kukufahamu Wayne.You are such
a wonderfull guy?? Clara akasema na kunipa
mkono.
?Hata mimi nafurahi sana kukufahamu
Clara.Sikutegemea kama siku ya leo ingeisha
nikiwa na furaha ya ajabu namna hii.uhhm .if
its ok with you can you give me your phone
number ? Nikasema.
?Nipe wewe namba yako kwa sababu bado
sina namba ya simu ya Tanzania.Nitakupigia
mimi? Clara akasema.Nikamuandikia namba
zangu na kumpa.
?Kesho tutaonana wapi? Nikamuuliza.
?Ratiba yangu ya kesho inaonyesha nitakuwa
na shughuli nyingi lakini nitakutaarifu kama
nitapata nafasi ama vipi? Clara akasema huku
akianza kupiga hatua kuondoka na mimi
nikiwa pembeni yake.Nilihisi msisimko wa
ajabu kutembea na mlimbwende yule.Mwendo
wake wa maringo ulinifanya nijione kama
ninatembea na malaika.
?Are you sure you can drive? Kama hujisikii
kuendesha let me take you to a hotel?
Nikamuuliza
?No thank you Wayne.I?m a bit drunk but I can
manage?
Nilimsindikiza Clara katika gari lake akaingia
na kuliwasha.Sikuondoka pale hadi
alipoligeuza na kuliweka tayari kwa
kuondoka.Akashusha kioo na kunipungia
mkono.
?Good night Wayne? Akasema .
?Good Night Clara? Nikajibu .Clara akafunga
kioo na kuliondoa gari.Nililitupia macho gari
lile likiondoka hadi lilipopotea kabisa machoni
pangu.Nikaelekea katika gari langu nikaingia
na kukaa nikiwa nimeuinamia usukani
?What a wonderfull woman?sidhani kama
atakuwa binadamu wa kawaida yule..si
mzimu kweli yule? Lakini hapana, nimeushika
mkono wake na kuhakikisha ni binadamu wa
kawaida.Mwanamke huyu mbona ameuteka
moyo wangu ghafla namna hii? Gosh hizi ni
hisia za kweli au ni hizi pombe nilizokunywa?
?Nikawaza.?
?Yeroo?..Mbona unainamia sukani..umesidiwa
tukupeleke sipitali?? Sauti ya mlinzi wa
kimasai aliyekuwa akilinda eneo lile ndiyo
inanistua katika mawazo .
?Ouh Rafiki..niko mzima siumwi kitu?
Nikawasha gari na kuondoka
**********
Saa tisa za usiku bado nilikuwa sijapata
usingizi.Toka nimerudi nimekuwa nikihangaika
kitandani kujaribu kutafuta usingizi bila
mafanikio.Sikuelewa sababu ilikuwa ni pombe
nilizokunywa au ni mawazo niliyokuwa
nayo.Mawazo mengi sana yamekuwa yakinijia
kichwani .Kubwa ilikuwa ni kumbukumbu ya
mambo yaliyotokea jioni ya siku
iliyotangulia.Kumbukumbu hii ilikuwa
ikijirudia kichwani kama filamu na kunifanya
nitabasamu.
?Clara?? Nilisema kwa sauti ndogo huku
nimekaa kitandani
?You are such an amazing woman.? Nikasema
huku nikitabasamu.
? hatimaye nimekutana na mwanamke wa
ndoto zangu.Clara is a perfect woman for
me.Ana kila kitu ninachokihitaji kwa
mwanamke wa ndoto zangu? Nikajilaza tena
kitandani.
? I think like I?ve lost her.Itakuwaje kama
sintaonana naye tena? Vipi kama hatanipigia
simu tena? Ouh Mungu wangu ninakufa na
mawazo ya huyu mwanamke.?
Nikainuka kitandani na kwenda kuketi sofani.
?Sintasafiri tena kama nilivyokuwa
nimepanga.Kuonana na Clara kumenifanya
nimsahau Emmy ghafla.Nilazima nionane
tena na Clara.Siwezi kukubali
kumpoteza.Nitamsaka dunia nzima hadi
nimpate??..? Nikawaza huku nikiwa
nimejilaza sofani.
Sikumbuki saa ngapi usingizi ulinichukua
.Nilistushwa na mvumo wa simu iliyokuwa
pembeni yangu.Nikafumbua macho
yaliyokuwa mazito kutokana na
usingizi.Nikaichukua simu na kuangalia
mpigaji.Alikuwa ni baba mkwe.
?baba shikamoo? Nikamsalimu.
?marahaba Wayne habari za leo?
?nzuri tu baba habari za kwenu?
?Huku kwema.Nimekupigia ili nijue unaendelea
vipi ? baba mkwe akauliza
?Ninaendelea vizuri baba Nashukuru? Nikajibu
?Ok Nashukuru sana kama unaendelea
vizuri.Ukiwa na tatizo lolote lile tafadhali
tupigie simu sisi wazee wako tupo
tutakusaidia?
?Sawa baba nashukuru? Nikajibu na baba
mkwe akakata simu.
Niliyafikicha macho ili niweze kuona
vizuri.Nilitazama saa ilipata saa tatu za
asubuhi.Haikuwa kawaida yangu kulala kwa
muda mrefu namna hii .Nadhani hii ilitokana
na pombe tulizokuwa tumekunywa jana
yake.Tulimaliza chupa nzima ya mvinyo
mkali.Mvinyo ule tuliokunywa jana yake
ukanifanya niikumbuke sura ya kuvutia yenye
nuru na tabasamu muda wote,sure yenye
macho mazuri meupe ambayo ungependa
yakuangalie muda wote,sura yenye midomo
laini na mizuri ambayo kila anapotasamu
huanikiza meno meupe yaliyojipanga vyema
kinywani,ni sura ya mwanamke wa kipekee
kabisa Clara ambaye toka nimekutana naye
jana yake amenikosesha usingizi na kunifanya
usiku mzima nikeshe nikimuwaza yeye.
Niliipekua simu ili kuangalia kama Clara
alipiga wakati nikiwa usingizini au alituma
ujumbe wa maneno lakini hakukuwa na simu
yoyote iliyopigwa wala ujumbe toka kwa
Clara.Nikaitupa simu pembeni.
?Laiti kama ningezifahamu namba za simu za
hoteli aliyofikia ningempigia walau kumjulia
hali.Nina hamu ya kutaka kuisikia tena sauti
yake nzuri.Lakini bado mapema ndiyo kwanza
saa tatu.Ni lazima atanipigia .Kwa namna
nilivyokuwa nimemgusa ni lazima
atanipigia.Ngoja niendelee kusubiri?
Nikawaza.
Mwili ulikuwa mzito kuinuka pale
kitandani.Nilihisi njaa kali.Nikaenda jikoni
nikatazama katika friji lakini sikupata
chochote cha kuweza kula..Nikaamua nioge
halafu nitoke kwenda kutafuta supu safi.Kisha
oga niliigia garini na kuondoka kwenda
kutafuta chochote cha kutia tumboni asubuhi
ile hususan supu .Bado sura ya Clara ilikuwa
ikinijia akilini kila mara na kuniweka katika
fikara nzito.
?This is what they call love at first sight.Yaani
kumuona jana tu tayari ameniteka akili namna
hii.Sina shaka na hisia zangu.Ninaamini moyo
wangu haunidanganyi kwamba Clara ndiye
mwanamke anayenifaa maishani.? Nikawaza
huku nikipata supu.
Mpaka saa nne za usiku Clara hakuw
amenipigia simu kama alivyokuwa
ameahidi.Niliumia sana kwa kitendo
hiki.Mishale ya saa ilizidi kusonga kwa kasi
hadi ilipofika saa sita za usiku lakini sikuwa
nimepokea simu yoyote au hata ujumbe wa
maneno toka kwa Clara.Kichwa kilijaa
mawazo mengi.Mwishowe nikaamua kulala.
Siku ya pili ikakatika bila ya kupokea tena
simu toka kwa Clara.Nilijiuliza maswali mengi
kulikoni asipige simu wakati alikwisha ahidi
kunipigia? Nini kimetokea? Ndugu msomaji
nilikuwa na mawazo mengi mno kwa Clara
kushindwa kunipigia simu.Nilianza kupatwa
na mawazo pengine hakuwa na nia ya kweli
ya kunipigia simu na aliongea vile kwa ajili ya
kuniridhisha.Nilianza kukata tamaa ya
kuonana tena na Clara .Nilijiona kama ni mtu
nisiyekuwa na bahati katika suala la urafiki
na watoto wakike.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO???
 
BEYOND PAIN
SEHEMU YA 12
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
?This is what they call love at first sight.Yaani
kumuona jana tu tayari ameniteka akili namna
hii.Sina shaka na hisia zangu.Ninaamini moyo
wangu haunidanganyi kwamba Clara ndiye
mwanamke anayenifaa maishani.? Nikawaza
huku nikipata supu.
Mpaka saa nne za usiku Clara hakuw
amenipigia simu kama alivyokuwa
ameahidi.Niliumia sana kwa kitendo
hiki.Mishale ya saa ilizidi kusonga kwa kasi
hadi ilipofika saa sita za usiku lakini sikuwa
nimepokea simu yoyote au hata ujumbe wa
maneno toka kwa Clara.Kichwa kilijaa
mawazo mengi.Mwishowe nikaamua kulala.
Siku ya pili ikakatika bila ya kupokea tena
simu toka kwa Clara.Nilijiuliza maswali mengi
kulikoni asipige simu wakati alikwisha ahidi
kunipigia? Nini kimetokea? Ndugu msomaji
nilikuwa na mawazo mengi mno kwa Clara
kushindwa kunipigia simu.Nilianza kupatwa
na mawazo pengine hakuwa na nia ya kweli
ya kunipigia simu na aliongea vile kwa ajili ya
kuniridhisha.Nilianza kukata tamaa ya
kuonana tena na Clara .Nilijiona kama ni mtu
nisiyekuwa na bahati katika suala la urafiki
na watoto wakike.
ENDELEA?????????..
Siku ya alhamisi saa tatu za usiku nikiwa
nimepumzika nyumbani nikiangalia
filamu,mara simu yangu ikaita.Nikaichukua na
kutazama mpigaji.Zilikua ni namba ngeni
katika simu yangu.Nikabonyeza kitufe cha
kupokelea simu.
?Hallo? Nikasema
?Hallo naongea na Wayne? Sauti ya kike
ikauliza ambayo moja kwa moja niliitambua
ilikuwa ni sauti ya Clara.Nikapatwa na furaha
ya ghafla.
?yah hapa unaongea na Wayne.Nani
mwenzangu? Nikauliza huku nikijifanya
kutoifahamu sauti ile .
?Unaweza ukaikumbuka sauti hii? Akauliza
Clara huku akicheka kicheko cha chini chini
kama kawaida yake
?yah ?nadhani?uhhm hii itakuwa ni sauti ya
Clara..? Nikasema halafu Clara akacheka
kicheko kikubwa.
?Nilitegemea utakuwa umeshaisahau sauti hii?
Clara akasema huku akicheka
?katika sauti zote za dunia hii sauti hii
sintaweza kuisahau hata sekunde moja.hata
Ukiwa katika kundi la watu elfu moja sauti
yako nitaitambua tu kwa sababu ni sauti ya
kipekee sana?.? Nikasema huku sura yangu
ikiwa imepambwa na tabasamu zito.Clara
akaendelea kucheka
?Wayne habari za toka tulipoonana?
?habari nzuri Clara.Sijui wewe.Niliona kimya
kingi nikajua pengine umeshazipoteza namba
zangu? Nikasema
?Ouh No Wayne..siwezi kuipoteza namba
yako.Nilishindwa kukupigia nilikuwa
nimebanwa mno na ratiba.Unajua siku
zenyewe ni chache na mambo yalikuwa mengi
sana kwa hiyo ikanibidi kufanya kazi hadi
usiku wa manane kila siku.Nasuhukuru Mungu
tunamalizia leo? Clara akasema kwa sauti
tulivu
?Ouh kumbe mnamaliza leo?
?Ndiyo Wayne leo tunamaliza .Lakini kesho
kutakuwa na sherehe za kuchangia kituo cha
watoto wanaoishi katika mazingira magumu
cha Future generation Hafla hiyo itafanyika
kuanzia saa moja za usiku.Ninaomba kama
utakuwa na nafasi twende wote?
?Clara nitakuwa na nafasi ya kutosha hivyo
usihofu tutakwenda wote.?
?Nashukuru sana kwa kukubali kwenda nami
katika hafla hiyo.Nitakutegemea unipitie hapa
hotelini kwangu saa kumi na mbili za jioni.?
Clara akasema
?Hakuna tatizo Clara nitafika hapo hotelini
kwako mida hiyo uliyosema.?
?Ok Wayne goodnight?
?Goodnight Clara? Nikajibu na simu
ikakatwa.Nilipatwa na furaha ya aina
yake.Nilikwisha kata tamaa ya kuonana tena
na Clara.Simu hii aliyopiga ilinirudishia
furaha na matumaini ya kumuona tena
mrembo yule.
* * * *
Saa kumi na mbili juu ya alama ilinikuta
katika geti la kuingilia SEAN 11 LODGE
alikofikia Clara.Sikutaka kuchelewa miadi na
mrembo huyu wa kutukuka.Nilishuka katika
gari nikajiangalia na kujiona niko safi kabisa
kwa ajili ya shughuli ya usiku huu.Nilikuwa
nimependeza kupita maelezo.Nilikuwa
nimevaa suti kali nyeusi .Ukiwa umeambatana
na mrembo kama huyu inakubidi na wewe uwe
umependeza isivyo kawaida ili
muendane.Nilitembea kwa mikogo hadi
mapokezi.Nikawasalimu akina dada wawili
waliokuwa pale wenye nyuso za
furaha.Nikawaomba wamtaarifu Clara
kwamba mgeni wake amekwisha fika.dada
mmoja akachukua simu akapiga halafu
akaiweka simu chini akaongea na mwenzake
ambaye akaja akanichukua na kunipeleka
katika ukumbi.Nilionyeshwa meza moja
iliyokuwa na viti viwili ambayo ilikuwa
pembeni kabisa mwa ukumbi ule uliokuwa na
mwanga hafifu na watu wachache.Muhudumu
yule akanivutia kiti na kunikaribisha.
?Clara amesema ukae hapa utumie chochote
kile unachoona kitakufaa kwa muda huu
unapomsubiri.yeye bado anajiandaa.?
Akasema dada yule mwenye lafudhi ya
kichaga
Nilimwambia aniletee mvinyo mwepesi
.Nilikuwa na mawazo mengi juu ya
Clara.Niliwaza jinsi muonekano wake
utakavyokuwa usiku wa leo ,niliwaza jinsi
tutakavyoongozana katika shughuli
hiyo.Niliwaza mambo mengi sana.Dakika
ishirini toka nifike pale mara kwa mbali
nikamuona mtu akija kwa mwendo wa
madaha mno.Toka kwa mbali niliweza
kumtambua alikuwa ni Clara.Mrembo yule
alikuwa aking?aa usiku huu.Kadiri alivyopkuwa
akisogelea pale mezani ndivyo moyo wangu
ulivyoongeza kasi ya mapigo yake. Alikuwa
amevaa gauni refu jekundu lililokuwa likingaa
kila limulikwapo na mwanga wa taa.Shingoni
alikuwa amevaa mkufu mdogo wa dhahabu
wenye kung?aa na mkononi alikuwa na pochi
ndogo nyekundu.Chini alikuwa amevaa viatu
virefu vyekundu.kwa ujumla alikuwa
amependeza isivyo kawaida.
?Waoo !! Wayne you are amazing
tonight?.samahani sana kwa kuchelewa?
Akasema Clara akiwa amesimama pembeni ya
ile meza huku akinipa mokono.
?Bila samahani Clara.You look like a heaven
angel tonight ? Nikajibu huku nikitabasamu.Cl
ara akacheka na kusema
?Angels don?t wear high hills ? Tukacheka
wote kicheko kikubwa.
?nadhani tunaweza kuondoka..? akasema
Clara.Tukatoka na kuingia katika gari langu
tukaondoka kuelekea katika hafla ya
uchangiaji wa kituo cha watoto wanaoishi
katika mazingira magumu.
?Nimefurahi sana kukuona tena Clara?
Nikaanzisha mazungumzo ndani ya gari.
? I missed you Wayne?did you miss me?
Akauliza Clara .
?I missed you so badly.Siku zilivyokuwa
zikikatika bila ya kupata simu yako nilikuwa
na mawazo mengi mno.Niliwaza pengine
labda umepoteza namna yangu,au pengine
??.?
?Pengine nini? akauliza Clara huku
akitabasamu
?pengine labda hukujisikia kunipigia kwa
kuogopa usumbufu wa namna moja au
nyingine?
?Pole sana Wayne kwa usumbufu huo
ulioupata .Sikufanya makusudi kutokukupigia
simu.Nilikuwa nimebanwa sana na ratiba
ndiyo maana sikuweza kupata muda wa kukaa
na wewe.mambo yalikuwa mengi na siku
zilikuwa kidogo.?
Tuliendelea na maongenzi na kutaniana huku
tukicheka kwa furaha na hatimaye tukafika
mahala inapofanyikia hafla hiyo.Hapo nje
palikuwa na magari mengi ya watu waliokuwa
wamekuja katika kuchangia.
Tuliposhuka garini Clara akaukamata mkono
wangu na kisha tukaanza kuingia ukumbini
kama wapenzi.
?Do you mind? Akaniuliza iwapo nitajali kwa
kitendo kile cha kunikamata mkono.Sikujibu
kitu nikatabasamu naye akatabasamu
.Nilikuwa nimefurahi moyoni kupita kiasi kwa
kitendo kile cha kuingia ukumbini huku
tumeshikana mikono kama wapenzi.Yeyote
ambaye angetuona angefikiri kwamba sisi ni
wapenzi tena tunaopendana mno.Nilifarijika
mno kwa kitendo kile.Nilijiona ni mwanaume
mwenye thamani tena.
Watu walikuwa ni wengi ndani ya ukumbi huu
mkubwa.Watu walikuwa wakitukodolea macho
wakati tukipita kutafuta meza.Wengine
walikuwa wakinong?onezana.Sikuelewa ni kwa
nini ilitokea vile.labda ni namna tulivyokuwa
tumependeza.Ghafla bila kutegemea niliona
kitu ambacho sikuwa nimekitegemea kukiona
mahala pale.Katika meza moja nilimuona
Emmy akiwa amekaa na Chris pamoja na
watu wanaofanya kazi kampuni moja na Chris
ambao baadhi yao niliwafahamu kupitia kwa
Chris.Macho yangu na Emmy
yakagongana.Niliuona mstuko wa wazi
uliompata.Akainamisha kichwa chake chini
kukwepa macho yangu.Chris alistuka baada
ya kuona jinsi mpenzi wake alivyo badilika
ghafla.Alipogeuka kuangalia tukagonganisha
macho.Amani ikamtoweka ghafla.Sikuwajali
nikamshika mkono Clara tukaendelea kwenda
mbele katika meza zilizokuwa wazi.
Sikuwa nimefikiria kama ningeweza kuonana
na Emmy mapema namna hii.Niliamini
kwamba kwa sasa mwanamke yule hayuko
moyoni mwangu kwa sababu pamoja na
kugonganisha macho katu sikuwa na mstuko
wowote .Nilijisikia amani kubwa moyoni.Hiki
kilikuwa ni kipimo tosha kwamba tayari hana
nafasi yoyote tena moyoni mwangu.Kilichok
uwa kikinijia mara kwa mara na kunipa
mawazo mengi ni sura ya Baraka.Sikujua
mpaka sasa hivi atakuwa katika hali
gani.Nilizoea kucheza naye kila
siku,nilikumbuka jinsi tulivyokuwa tukikaa
bustanini hasa nyakati za usiku tukipiga
magitaa yetu na kuimba.Zilikuwa ni nyakati
za furaha sana.Sikutegemea kama huko aliko
alikuwa akipata furaha kama aliyokuwa
akiipata alipokuwa na mimi.Sikuwa na namna
ya kufanya ili niweze kuonana naye
tena.Sikutaka kuwa karibu na Emmy kwa
namna yoyote ile.Sikutaka kumbughudhi
katika maisha yake mapya.Nilichokifanya ni
kuomba Mungu siku moja anikutanishe na
Baraka japo kwa dakika mbili ili niweze
kufurahi naye tena.
?Wayne mbona huagizi vinywaji? Akauliza
Clara baada ya kurudi toka katika meza ya
jirani alikokuwa amekwenda kuwasalimia
wanamitindo wenzake.
?Ninakusubiri wewe ili tuagize kwa pamoja?
Nikasema na mara muhudumu akafika
tukaagiza vinywaji.
?Nilikuwa nawasalimia marafiki zangu.?
Akasema Clara.
?Nimewaona.They are so pretty? Nikatania.
?Shhhhhhh!!! Don?t ever say that to me
Wayne.I?m so jelousy?don?t talk to any woman
tonight..I wont allow any woman to steal you
from me tonight ..I?m gona kill the one who
try? Clara akasema huku akicheka kwa nguvu
sana na mimi pia nikacheka.
?Kusema ukweli umependeza sana Wayne.You
are the cutest man tonight.Naogopa nisije
nikaibiwa? Clara akasema huku akiendelea
kucheka.Kama hujamfahamu Clara unaweza
ukadhani labda amekwisha lewa lakini hivi
ndivyo alivyo.Ni mtu mcheshi ,mchangamfu
na mwenye utani mwingi.Manenoyale ya utani
aliyoyaongea yanazidi kunipandisha joto la
mwili.Nilitamani kama angekuwa akimaanisha
kile alichokuwa anakisema.Nilitmani kuwa na
Clara muda wote.Ni mwanamke ambaye ana
heshima,mstaarabu ,mwenye kujipenda,mweny
e kujali watu,mcheshi na mkarimu.Sifa zote
hizi zilinifanya nivutike kutaka kuwa naye
muda wote.
?Ok here?s the deal.I?m not going to talk to
any woman and you don?t talk to any
man..deal?
?Deal? akajibu Clara huku akicheka kicheko
kikubwa.Watu waliokuwa meza za karibu
walikuwa wakitushangaa kwa jinsi
tulivyokuwa tunafurahi.
?mwanaume yeyote akikaribia meza hii
ninamtoa kwa makofi? Nikasema na
tukaendelea kucheka.
?Wayne umeshawahi kupigana katika maisha
yako?
?Yes ! ? nikajibu kwa ufupi
?Sura yako ya upole haionyeshi kama ni mtu
wa vurugu.? Akasema huku akitabasamu
Sherehe zilifunguliwa na mgeni rasmi
aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha
mjini.Baadae shughuli za uchangiaji
zikaanza.Baadhi ya makampuni yaliyokuwa
yamealikwa yalikuwa yametuma wawakilishi
wao kuleta michango yao ambao walikuwa
wakipita mbele na kukabidhi kiasi
kilichotolewa na kampuni husika.Kampuni
zilikuwa ni nyingi na mara nikasikia kampuni
anayofanyia kazi Chris ya Amazora safari
ikitajwa.Chris ndiye aliyekuwa akiongoza
kundi la wafanyakazi wa Amazora safari
kwenda kukabidhi michangoya kampuni
.Miongoni mwao alikuwepo Emmy.Sikutaka
kuwatazama tena nikayarudisha macho na
mawazo yangu mezani.
Michango bado iliendelea kutolewa
Makampuni na watu mbali mbali walikwisha
toa michango yao na ndipo muongoza
shughuli akachukua kipaza sauti na
kumkaribisha muandaaji wa shughuli ile
mama Blandina chokasi ambaye alifika pale
mbele akakabidhiwa kipaza sauti ili aweze
kuongea jambo.Ukumbi wote ukakaa kimya ili
kumsikiliza mama yule.
?Ndugu mgeni rasmi,mheshimiwa mbunge
wetu wa Arusha mjini,wawakilishi wa
makampuni mbali mbali,ndugu wageni
waalikwa mabibi na mabwana ninapenda
kuchukua nafasi hii kuwashukuru kwa namna
mlivyojitokeza kwa wingi kuchangia kituo hiki
cha watoto wanaoishi katika mazingira
magumu cha future generation.Kujitokeza
kwenu kunaonyesha ni jinsi gani nyote
mnavyoguswa na matatizo ya watoto hawa
ambao wengi wao hawana wazazi au wazazi
wao hawana uwezo wa kuwatunza.Najua
nyote mna majukumu mengi lakini mmejibana
na kutoa kile mlichokuwa nacho kwa ajili ya
kuwasaidia watoto hawa masikini.Sisi
hatutaweza kuwalipa chochote il
tunawaombea kwa Mungu awazidishie wote
mara mbili ya mlicho nacho na awape moyo
wa kuweza kujitolea zaidi kwa ajili ya watu
masikini na wasio na uwezo.? Akatulia na
ukumbi wote ukalipuka kwa makofi na vigere
gere halafu akaendelea.
?Ndugu wageni waalikwa mabibi na
mabwana,bado shughuli yetu inaendelea lakini
nimesimama hapa kwa ajili ya jambo maalum
kabisa.Nimesimama hapa kwa ajili ya kutoa
shukrani za kipekee kwa mtu ambaye kampuni
yake ndiyo imefanikisha jambo hili muhimu la
leo.Ni mwanadada wa kitanzania ambaye kazi
zake za mitindo na urembo zimevuka mipaka
ya nchi yetu na kufika mbali .Kwa sasa
mwanadada huyu anafanya kazi za mitindo
na ubunifu nchini afrika ya kusini.Ni mbunifu
mkubwa wa kimataifa na kampuni yake
inafahamika kote duniani.Amekuwa akishiriki
katika matamasha na majukwaa mbali mbali
makubwa ya urembo duniani.Mbunifu huyu
amekuwa akifanya juhudi kubwa katika
kuhakikisha kwamba wabunifu na
wanamitindo wa kitanzania wanafahamika
duniani.Kupitia kampuni yake ya Black angels
amekwisha wasaidia wanamitindo zaidi ya 30
kupata mikataba na kufanya kazi na
makampuni makubwa ya urembo duniani,vile
vile amefanikisha kuwatangaza wabunifu wa
kitanzania katika majukwaa makubwa ya
mitindo duniani.Mbunifu huyu amekuwa na
mchango mkubwa sana katika umoja wa
wabunifu na wanamitindo wa Tanzania.Mara
kwa mara amekuwa akija na kutoa semina
kwa wabunifu na wanamitindo wachanga.Kwa
muda wa wiki mbili sasa tumekuwa naye
hapa Arusha akiendesha semina ya mambo
haya ya ubunifu na urembo.Kwa kuifanya fani
hii ya mitindo na urembo izidi kukua hapa
nchini aliona haitakuwa vizuri kama semina
ile itaisha hivi hivi ,akabuni lifanyike jambo
hili la kuichangia jamii.Kila mwaka tutakuwa
tunafanya kitu kama hiki na kuichangia jamii
yetu katika matatizo mbali mbali iliyokuwa
nayo.Mabibi na mabwana naomba sasa
nimtambulishe kwenu rais wa kampuni ya
Black angels Bi Clara msikongo.Kokote uliko
tafadhali Clara simama uwasalimu wageni
waalikwa.?
Clara akasimama na kupunga mikono,ukumbi
wote ukalipuka kwa makofi na vigere
gere.Nilikuwa nimestuka sana.Sikujua kama
nimekaa na mtu mkubwa na maarufu namna
ile.Nilimtazama Clara akiwapungia mikono
wageni mle ukumbini huku akiwa na
tabasamu zito Sikuamini macho yangu.
?Clara tafadhali naomba upite uje huku mbele
ili uongee neno lolote kwa hadhira hii
iliyokusanyika hapa usiku huu? mama
Blandina akasema.
Clara akachukua pochi yake pale mezani
halafu akanisogelea akaniinua
mkono.Nilielewa alikuwa akitaka niinuke pale
kitini.Moyo ulikuwa ukinienda mbio
sana.Alitambua kwamba nilikua mzito
kusimamam akaniinamia na kuninong?oneza
sikioni.
?Don?t be nervous..smile? akasema.Nikainuka
na kuanza kutabasamu.Akanishika mkono
tukaanza kutembea kwa madaha kuelekea
jukwaani.Makofi na vigere gere vilikaribia
kulichana paa la ukumbi ule mkubwa.Miguu
ilikuwa ikinitetemekaSikuelewa hofu ile ilikuwa
imetoka wapi.Tulipanda jukwaani nikasimama
pembeni ya Clara ambaye akapewa kipaza
sauti ili aongee machache
?mabibi na mabwana habari zenu.?
?Nzuriiii? Ukumbi wote ukaitikia huku makofi
yakipigwa.
?Awali ya yote napenda kuwashukuru sana
kwa kuitika mwito wetu.Japokuwa ilikuwa ni
taarifa ya muda mfupi lakini mmeweza
kujitokeza kushirikiana nasi katika kuchangia
jambo ili muhimu.Kila siku tunashuhudia
ongezeko la watoto wanaoishi mitaani katika
mazingira magumu.Kama wana jamii tuna
jukumu la kuwasaidia watoto hawa ambao
wengi wao hawana wazazi au kama wana
wazazi basi ni masikini sana.Ni jukumu la kila
mwanajamii kuhakikisha kwamba anatoa kile
kidogo alicho nacho kwa ajili ya kuwasaidia
watoto hawa .Kuna makundi mengi
yanayohitaji msaada kama vile wanawake
wenye maradhi ya Fistula,wanawake
wanaosumbuliwa na kansa ya matiti n.k Sisi
kama jukwaa la wanamitindo tumeamua
kuanza kwanza na kundi hili la watoto hawa
na kisha tutachangia makundi mengine.? Clara
akatulia na ukumbi wote ukalipuka kwa
makofi
?Ndugu zangu uwingi wenu usiku huu wa leo
umenipa faraja sana kwamba sasa fani hii ya
urembo imeanza kueleweka katika jamii
kwamba si uhuni kama ilivyokuwa ikidhaniwa
hapo awali bali ni kazi kama kazi nyingine
zozote.Fani hii ya urembo kama ikitiliwa
mkazo inaweza kuwa ni mkombozi wa ajira
kwa vijana wetu wengi.Tunaiomba serikali
iitazame fani hii kwa upana wake kwa sababu
ni fani ambayo inaweza ikatutangaza sana
kimataifa kama tunavyojitahidi kufanya hivi
sasa japokuwa mchango wa serikali bado ni
mdogo mno.Ndugu zangu sitaki kuchukua
muda mrefu wa kuongea kwa sababu bado
kuna mambo mengine yanaendelea.napenda
kabla ya kumaliza niseme kwamba pamoja na
kwamba mimi ni mmoja wa waandaaji wa
shughuli hii lakini mimi na mwenzangu hapa
tunao mchango wetu ambao tunautoa kwa
ajili ya watoto hawa.Kwa pamoja tunatoa
cheki yenye thamani ya fedha za kitanzania
shilingi millioni hamsini.? Ukumbi wote
ukalipuka kwa kelele za shangwe.Nilistuka
sana.Sikuwa nimeongea na Clara kuhusu
jambo lolote lile kuhusiana na fedha zile
alizosema tumetoa kwa pamoja mimi na
yeye.Clara akatoa cheki akaikabidhi huku
makofi na vigere gere vikizidi.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO?????.
 
SEHEMU YA 13
MTUNZI :pATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
?Ndugu zangu uwingi wenu usiku huu wa leo
umenipa faraja sana kwamba sasa fani hii ya
urembo imeanza kueleweka katika jamii
kwamba si uhuni kama ilivyokuwa ikidhaniwa
hapo awali bali ni kazi kama kazi nyingine
zozote.Fani hii ya urembo kama ikitiliwa
mkazo inaweza kuwa ni mkombozi wa ajira
kwa vijana wetu wengi.Tunaiomba serikali
iitazame fani hii kwa upana wake kwa sababu
ni fani ambayo inaweza ikatutangaza sana
kimataifa kama tunavyojitahidi kufanya hivi
sasa japokuwa mchango wa serikali bado ni
mdogo mno.Ndugu zangu sitaki kuchukua
muda mrefu wa kuongea kwa sababu bado
kuna mambo mengine yanaendelea.napenda
kabla ya kumaliza niseme kwamba pamoja na
kwamba mimi ni mmoja wa waandaaji wa
shughuli hii lakini mimi na mwenzangu hapa
tunao mchango wetu ambao tunautoa kwa
ajili ya watoto hawa.Kwa pamoja tunatoa
cheki yenye thamani ya fedha za kitanzania
shilingi millioni hamsini.? Ukumbi wote
ukalipuka kwa kelele za shangwe.Nilistuka
sana.Sikuwa nimeongea na Clara kuhusu
jambo lolote lile kuhusiana na fedha zile
alizosema tumetoa kwa pamoja mimi na
yeye.Clara akatoa cheki akaikabidhi huku
makofi na vigere gere vikizidi.
ENDELEA????????.
?Kabla hatujaondoka nadhani mwenzangu
hapa na jambo la kusema? Clara akasema
akiwa na maana ya mimi.Sikuwa nimejiandaa
kusema lolote na sikujua niseme nini.Nilihisi
kutetemeka.Sikuwa na uzoefu wa kuongea
mbele ya hadhira kubwa kama ile iliyobeba
watu mashuhuri na matajiri.Clara akanipa
kipaza sauti huku akitabasamu.Nilikipokea
japo mikono ilikuwa ikinitetemeka.Nilikishika
kipaza sauti nikakisogeza karibu na mdomo
wangu.Clara akaniangalia kwa tabasamu.Sijui
nilipata wapi nguvu na uwezo wa kuongea
ghafla nikajikuta nikisema
?Mabibi na mabwana,sina mengi ya kuongea
kwa sababu mengi amekwisha yaongea
mwenzangu hapa.Ninachotaka kukisema ni
kwamba kadiri muda ulivyokuwa ukienda mimi
binafsi nimejikuta nikizidi kuguswa na maisha
ya watoto hawa.Nimejikuta nikitaka kuchangia
tena na tena lakini uwezo unakuwa
hauruhusu.Kwa namna nilivyoguwa naomba
kama mimi nitoe ahadi ya kuchangia tena
shilingi millioni thelathini pesa ambayo
nitaitoa kesho.? Ukumbi wote ukalipuka kwa
shangwe .Nikatabasamu baada ya kuiona
furaha ile ya watu.Nikamrudishia Clara kipaza
sauti lakini kabla hajakikabidhi kwa mama
Blandina akaniomba nisogee karibu
yake.Nikasogea akauinua mkono wake na
kuuzungusha shingoni kwangu akaniangalia
kwa tabasamu na kusema.
?Mabibi na mabwana na mimi naongeza tena
shilingi millioni ishirini .Jumla mimi na
mwenzangu hapa tunatoa shilingi za
kitanzania millioni mia moja.Ahsanteni sana?
Ukumbi ukalipuka kwa kelele za
shangwe.Clara akanishika mkono tukaanza
kushuka ngazi huku ukumbi wote ukiwa
umesimama ukitushangilia .Nilihisi kama
miguu inagongana wakati tukirudi katika
meza yetu.Sikuwa nimetegemea kitu kama kile
kutokea.Mambo yale makubwa yalitokea kwa
haraka sana.Niliona ni kama ndoto vile.
?You did great..I didn?t expect you could be
such a smart guy?.Wayne you are
amazing..congraturations? Clara
akaninong?oneza sikioni wakati tukikaa
kwenye viti vyetu.Sikujibu kitu nilikuwa
nikitabasamu.Nikatoa kitambaa na kujifuta
jasho lililokuwa likinitoka kama nimemwagiwa
maji.
Mambo yaliyokuwa yametokea pale ukumbini
yalikuwa ni kama ndoto .Sikuwa nimetarajia
kuwa mambo yangekuwa kama vile.Siwezi
kuelezea ni jinsi gani nilivyokuwa nimefurahi
moyoni.
Baada ya kushuka toka jukwaani meza yetu
ilikuwa haikauki watu waliokuja kutupa
mikono ya pongezi..Huu ulikuwa ni usiku wa
kipekee sana kwangu.Nilifurahia sana kwa
namna Clara alivyonifanya niyasahau
masahibu yote yaliyokuwa yamenikumba .Kila
nilipomtazama Clara usoni nilishindwa
kuamini kama ni yeye kweli ndiye aliyeweza
kunifanya nikawa na furaha kubwa namna
ile.Katika usiku ule nilikuwa nimepata
heshima kubwa na ya kipekee kwanza kwa
kuongozana na mwanamke mwenye sifa
kubwa kama Clara, na pili kitendo cha
kusimama jukwaani na kuongea na hadhira ile
kubwa ya watu na kuwafanya wote walipuke
kwa shangwe kilinipa heshima kubwa mno
ambayo sikuwa nimetarajia kuipata.Emmy
alinidharau na kuniona si mtu mbele ya watu
lakini leo Clara amenirudishia heshima yangu
iliyopotea..Nilipokumbuka kwamba Emmy
naye alikuwepo pale ukumbini nikatabasamu
Sikujua nimshukuruje Clara kwa namna
alivyoirudisha tena furaha yangu iliyopotea.
?Ninaamini Clara ndiye mwanamke ambaye
Mungu ameniandalia.Moyo wangu umekuwa
rahisi mno kumkubali na kumpa nafasi
kubwa.Sina shaka na moyo wangu kwani
naamini safari hii haunidanganyi kama
ulivyofanya kwa Emmy.Lakini Clara si kama
Emmy.Utofauti wao ni kama ardhi na
mbingu.Safari hii sitaki kufanya
makosa.Nitaenda naye taratibu na mpaka
niuteke moyo wake.Ninachotakiwa kukifanya
kwa sasa ni kuanza kumfahamu kiundani
Natakiwa niwe na subira kwa sababu iwapo
nitaanzisha masuala ya mapenzi mapema
namna hii ninaweza kumpoteza malaika
huyu.Natakiwa nianze kwa kujenga urafiki
mkubwa na baadae ndipo masuala ya
mapenzi yafuate.Sitaki kumpoteza mtu
muhimu kama huyu.? Niliwaza huku
nikimtazama Clara kwa kuibia akiwa
anazungumza na wanamitindo wenzake.
Saa saba za usiku ndipo tulipopata nafasi ya
kuondoka pale ukumbini.Hatukuweza
kuondoka mapema kutokana na Clara kuwa na
maongezi na watu wengi ambao wengi wao
walikuwa ni wanamitindo na wabunifu.Mpaka
anaingia garini bado walikuwepo wasichana
waliokuwa wanamfuata ili kujaribu kupata
walau namba yake ya simu kwa sababu
hawakujua ni wapi wangeweza kumuona tena
baada ya semina ile kumalizika.
?Pole na kazi nzito? Nikasema wakati
tukiondoka maeneo yale
Clara akaniangalia na kusema huku
akitabasamu
?ahsante sana Wayne.Sikutegemea kama watu
wangekuwa wengi namna hii.Nasikitika muda
umekuwa mdogo sana na sijaweza kuonana
na wote waliokuwa wakihitaji kuniona.Nitataf
uta muda nirudi tena Arusha.Nimepapenda
sana?
?Kwa hiyo unategemea kuondoka lini ?
Nikauliza
?Kesho kutwa natakiwa niwe nimeondoka
Tanzania.Kuna shughuli moja muhimu
natakiwa kwenda kuifanya afrika kusini? Clara
akasema na kunifanya nistuke na
ninyong?onyee ghafla.Katika mawazo yangu
nilitegemea kwamba pamoja na semina
kumalizika lakini angeendelea kubaki arusha
kwa siku kadhaa .Laiti kama ningekuwa na
uwezo ningeweza kumzuia asiondoke kwa
sababu bado nilihitaji kuwa naye.
?Mbona kimya hivyo Wayne? Clara
akauliza.Nadhani aligundua kwamba nilikuwa
kimya ghafla.Kwa kweli kutoka moyoni
sikutaka Clara aondoke,lakini uwezo wa
kumzuia asiondoke sikuwa nao.
? Nilidhani baada ya kumaliza semina ile
ungebaki Arusha japo kwa siku mbili
tatu.Nilikuwa nimepanga nikupeleke
ukatembelee hifadhi ya Ngorongoro.?
Nikasema .Clara akanitazama halafu akasema
?Wayne hata mimi sikuwa nimepanga
kuondoka mapema namna hii.Nilipanga kuwa
na siku kadhaa za mapumziko baada ya
semina kumalizika lakini nilipigiwa simu jana
usiku na mmoja wateja wangu wakubwa kuwa
kuna kazi moja muhimu sana ambayo
natakiwa kwenda kuifanya.I?m sorry Wayne
kwa kuikosa ofa hii ya kwenda kutembea
Ngorongoro lakini usijali nitatafuta nafasi
nitakuja tena Arusha.Nimepapenda sana
.Kuna hewa safi,warembo wazuri and above
all I?ve met with so wonderfull people
especially you Wayne.Toka siku tumekutana
umekuwa ni mmoja kati ya watu wangu
muhimu sana japokuwa hatujapata muda
mwingi wa kukaa na kufurahi pamoja.Wayne
naomba ufahamu kwamba uko katika orodha
ya watu wangu muhimu wanaonifanya niwe
na furaha katika maisha haya.You are so
wonderfull.I?ll miss you a lot but don?t worry
I?ll come back I promise? Clara akasema kwa
ile sauti yake nzuri yenye kuvutia.Nilifarijika
mno kwa maneno yale ya Clara.Kuwa
miongoni mwa watu wake ambao yeye
anawaita ni wa muhimu ilikuwa ni faraja
kubwa kwangu.Japokuwa hakunifahamu
kiundani lakini alitokea kuniamini na kunweka
miongoni mwa watu muhimu.Ulikuwa ni
mwanzo mzuri ambao sikutaka kuuharibu.
?Usijali Clara.Siku yoyote ukitaka kuja Arusha
naomba unitaarifu tafadhali ili nikufanyie
maandalizi kama mwenyeji wako? Nikasema
na kumfanya Clara acheke kicheko kikubwa.
?hakuna haja ya maandalizi Wayne.Hapa ni
kama nyumbani.Hata nikija bila taarifa
nafahamu nina watu wangu wa muhimu.?
Clara akasema huku akicheka
?Kwa hiyo Clara kama umepanga kuondoka
kesho kutwa,siku ya kesho utakuwa na kazi
gani? Nikauliza ili kujua kama ninaweza
kupata walau nafasi ya mwisho ya kuwa na
mwanamke huyu mrembo.
?kesho nitaondoka na ndege ya saa saba
mchana kwenda kuwaaga wazazi Dar es
salaam halafu kesho kutwa ndiyo nitaondoka
kuelekea South Afrika.?Akajibu.
Nilimpeleka Clara hadi katika hoteli aliyokuwa
amepanga.Nilimsindikiza hadi katika chumba
chake akanikaribisha ndani,sikujivunga
nikaingia ndani na kuketi sofani.
?Clara kwa kuwa muda umekwenda sana na
kesho unatakiwa kusafiri ,mimi naomba
nikuage ili nikupe nafasi ya kujiandaa kwa
safari ya kesho.? Nikasema huku nikijiandaa
kuinuka.
?Wayne please sit down.? Clara akasema
,nikakaa chini.
?Mbona una haraka namna hiyo? Kesho
ninaondoka lakini zitapita siku nyingi kabla
hatujaonana tena ,Don?t you like to spend
sometimes with me? Don?t you wanna talk
about it? Clara akauliza
?about what? Nikauliza na mimi
?about what happened at the party? akasema
Clara na kunifanya nicheke .
?Please Wayne just for tonight,stay with me
and we can have wine,talk,laugh and have
fun.I know after I?m gone I?ll miss someone to
laugh with.? Clara akasema Hakujua ni jinsi
gani nilivyokuwa nimefurahi kwa kuniomba
niendelee kukaa pale.
?Ok Nitabaki kwa saa moja au mawili halafu
nitaondoka? Nikasema
?Thank you so much Wayne.It means a lot to
me.Now wait there and I?ll be back in a
second? Akasema Clara huku akifungua
mlango na kuingia katika chumba cha
kulala.Baada ya kama dakika mbili akarudi
akiwa amevaa suruali ndefu ya kitambaa
chepesi pamoja na koti jeusi lenye manyoya
laini.Akalifungua friji na kutoa chupa za
mvinyo akazipanga mezani.
?Nina furaha ya ajabu sana leo
Wayne.Naomba tunywe na tufurahi mpaka
tuchoke? Akasema Clara.Tulipoanza kunywa
Clara akasema
?Wayne naomba nichukue nafasi hii kukuomba
samahani kwa kilichotokea pale ukumbini?
?Nothing wrong happened Clara? Nikasema
?Najua utasema hakuna kilichotokea lakini
nilikupandisha jukwaani bila ridhaa
yako.Haukuwa umepanga kuongea na hadhira
kubwa kama ile.najua vile vile hata zile fedha
ulizochangia hukuwa umepanga kuzitoa kwa
hilo usijali nitakurudishia zile fedha zote?..?
?no no no Clara? Niliingilia kati kabla
hajamaliza sentensi yake.
?Nimetoa fedha zile kwa moyo mmoja na wala
sihitaji unirudishie.Uliponiomba niambatane
nawe katika uchangiaji wa kituo kile
nilikwisha andaa mchango wangu kama
mshiriki.Tafadhali Clara mchango ule niliutoa
kwa moyo wangu wote kwa ajili ya watoto
hawa wenye mazingira magumu,na kuhusu
kunipandisha jukwaani yah ! I was a bit
nervous lakini kwa kuwa karibu nawe nilipata
ujasiri mkubwa hata nikaweza kuongea na
umati ule mkubwa wa watu.? Nikasema kwa
msisitizo na kumfanya Clara atabasamu,akani
angalia kisha akasema
?Wayne you are amazing.Nilifanya makusudi
kukuomba nipande nawe jukwaani.Lengo
langu lilikuwa kukupima ni jinsi gani
unavyojiamini.I know you were nervous but
what you did was wonderfull.Nimefurahi sana
Wayne kwa sababu hukuweza
kuniangusha.Kwa dakika kadhaa tuliweza
kuziteka akili za kila mmoja pale
ukumbini.Wayne sijawahi kuwa na furaha
kama siku ya leo.Na furaha yote hii
imechangiwa na wewe.You made my evening.?
Clara akasema huku akiinua glasi yake
tukagonganisha maglasi yetu
?cheers!! Tukasema kwa pamoja.
Kitu kimoja ambacho sikuwa na uwezo nacho
ni kusimamisha muda uliokuwa ukienda kwa
kasi ya ajabu.Nilitaka niendelee kubaki na
mrembo yule asiyechosha kuwa naye.Nilihisi
kuipata furaha ya ajabu ambayo sikuwa
nimeipata kwa miaka mingi.
?Wayne mbona kimya? Unawaza nini?
? .akauliza Clara baada ya kuniona nikiwa
kimya ghafla nikimtazama
?Nothing Clara? Nikajibu
?Wayne do you have a family? Clara
akauliza.Sikujibu swali lile kwa haraka.Sikujua
nimpe jibu gani.Swali lile likanikumbusha
mateso aliyonipa Emmy ,papo hapo
nikamkumbuka mtoto Baraka.
?Not anymore? Nikajibu kwa sauti iliyoonyehsa
kuwa na chembe za hasira ndani yake
?You had one? Clara akauliza tena.
?Clara it?s a very log story.Nisingependa
kuiongelea hadithi hii kwa usiku huu wenye
kila aina ya furaha,sipendi kuufanya usiku huu
mzuri uwe ni usiku wa simanzi? Nikasema
huku nikiongeza mvinyo katika glasi
?can you be strong enough to tell me? Clara
akaendelea kusisitiza.
?Clara I?m sorry but its not a nice story to
hear tonight.There is nothing interested in
it.It?s a beyond pain story.So why don?t we
skip this and talk some other sweet things like
nice places in South Africa..your handsome
boyfriend..?
?Hahahahaaaa??.hahahaa??.? Clara
akacheka kicheko kikubwa mara tu
nilipomaliza sentensi yangu.
?Boyfriend? .. akauliza
?yes you boyfriend,Don?t you have one?
Nikauliza na kumfanya acheke tena kicheko
kikubwa.Sikushangaa kwa sababu toka
nimemfahamu nimegundua kwamba Clara
anapenda mno kucheka.
?Wayne unamaanisha nini unaposema
boyfriend? Akauliza huku akipiga funda la
mvinyo
?I mean someone you love,someone whom
your heart belong to????? sikumalizia
sentensi yangu Clara akaanza tena kucheka
?wayne unanifurahisha sana.I don?t have a
boyfriend or believe in love.Kama
unamaanisha mpenzi,mpenzi wangu mimi ni
kazi yangu ninayoifanya kwa mapenzi yote
toka moyoni.After what I got from men,I don?t
think I will ever love again.Ninaishi maisha
yangu ya furaha,I have lots of friends,I have a
job,I do whatever I want to do,I drink,I dance I
sing and I?m happy.so what do I need a man
for? ???Clara akasema huku akiinuka na
kwenda katika friji kuchukua vipande vya
barafu.Maneno yale yalikuwa mazito sana
kiasi kwamba nilianza kukata tamaa kama
ningeweza kumpata mwanamke kama yule
maishani.Manenoyale yalionyesha wazi
kwamba aliwahi kutendwa huko nyuma na
kumfanya asione tena thamani ya
mapenzi.Kwa sasa alikuwa na maisha yake
mazuri yaliyojaa furaha na amani hivyo
hakutaka kupata tena matatizo.Kwa upande
Fulani nilikubaliana na mawazo yake kwa
sababu hata mimi kwa jinsi nilivyokuwa
nimetendwa na Emmy sikutaka tena kujiingiza
katika masuala ya mahusiano kwa sababu
niliamini wanawake wote ni sawa.Sielewi ni
kitu gani kilichonikutanisha na Clara ambaye
kwa muda mfupi niliokutna naye ameweza
kuufuta mtazamo huo kichwani kwangu na
kunijengea mtazamo mpya kwamba wanawake
wote si sawa.kwa mbali nilisikia kitu kama
sauti ikininiambia nisikatishwe tamaa na
maneno yale ya Clara.
? You can have all that Clara,money,friends
job,cars and everything,but are you happy??
Nikamuuliza Clara.Akachukua glasi
yake,akapiga funda kubwa la mvinyo
akaliweka chini na kukaa kimya kwa sekunde
kadhaa akiniangalia.
?Mbona hunijibu? Nikamwambia
Clara.Akanitazama na kusema
?Sorry Wayne, this conversation brings me lots
of things in my mind..Uliniuliza swali gani?.?
Clara akasema .Nilimtazama usoni
nikagundua kuna mambo aliyokuwa
akiyawaza.
?Nilikuuliza kwamba ,unasema una kila
kitu,pesa,marafiki,kazi na kila kitu
unachokitaka unakipata.Lakini je una furaha
moyoni mwako?
?Furaha ipi unayoizungumzia Wayne? Clara
akauliza
?nazungumzia furaha ya moyo.Pamoja na
kuwa na vitu vyote hivyo maishani lakini moyo
wako una furaha? Nikauliza
?Wayne nina furaha.Kwa sababu kila kitu
ninachokitaka ninakipata Nina
furaha.Kikubwa kinachonifanya niwe na
furaha maishani ni kwamba niko huru,moyo
wangu una amani.Nina uhuru wa kufanya
chochote nikitakacho.Hebu niambie kuna
furaha zaidi ya hiyo? Clara akauliza
?Nafahamu hilo Clara ,nazungumzia ndani ya
moyo wako una furaha? Nikauliza tena
?Wayne nimeshakwambia nina furaha moyoni
mwangu? Clara akajibu akanitazama na
kusema
?Please Wayne can we change the subject.Can
we talk of something else like..uhhm tell me of
your love life,about your girfriend? Clara
akasema huku akitabasamu,akainua glasi
yake na kupiga funda la mvinyo.Nilifikiri
kidogo nimweleze nini nikaamua kusema
ukweli
? I don?t have a girlfriend.?
Clara akanitazama kwa makini usoni baada
ya kauli ile na kusema
?Wayne ,tell me what happened? Kila
ninapokutajia kuhusu masuala ya mahusiano
yako unabadilika ghafla.Kitu gani
kimekutokea? Tafadhali naomba
uniambie.Nitakusaidia? Clara akasema kwa
msisitizo huku amenikazia macho
Nilivuta pumzi ndefu na kusema
?Clara ni hadithi ndefu sana na nisingependa
kuongelea masuala hayo kwa sasa?
?C?mon Wayne mimi ni rafiki yako.naomba
uniamini.Nieleze nini kilikutokea ?
Usiponieleza leo utanieleza lini? Clara
akauliza
?Sawa Clara kwa vile umesisitiza kutaka kujua
ukweli ,nitakueleza ukweli.?
Nilimweleza Clara kila kitu toka tulipoanza
mahusiano yetu mimi na Emmy na hadi
tulipokuja kuachana..Nilipomaliza kumsimulia
mkasa ule ulionipata niliona michirizi ya
machozi machoni pa mrembo yule.
?Wayne hadithi yako imenichoma moyo
sana.Kwa nini binadamu wengine wanakuwa
na ukatili wa namna hii? Pole sana
wayne.Nafahamu kwa sasa uko katika wakati
mgumu mno.Jipe moyo na yatakwisha? Clara
akasema huku akifuta machozi
?Usijali Clara,nimemwachia Mungu ndiye
atakayenilipia.Sihitaji kulipa ubaya kwa
Emmy..Nashukuru hata hivyo kwa kukutana
nawe kwa sabahu umenifanya kwa siku hizi
chache tulizofahamiana niwe mtu mwenye
furaha na kusahau yote yaliyonipata.Nakiri
kwamba wewe ni mwanamke wa pekee
sana.Mwanaume atakayekuwa nawe atakuwa
na bahati kubwa mno?
Clara akacheka sana baada ya kuongea vile.
?Wayne kila mara unaongelea kuhusu
mwanaume.Ninayafurahia maisha yangu bila
mwanaume kwa hiyo sifikirii kuwa na mume?
Clara akasema
?what about children? Nikauliza.Clara akakaa
kimya akafikiri kwa muda na kusema
?Kids ?
?Yes.Hujawahi kufikiri kuwa na watoto siku
moja?
?I love children and I?d like to have two
.Nafikiri furaha yangu itakamilika siku nikiwa
na mtoto wangu?
?Good . kama ni hivyo utawapataje hao watoto
bila kuwa na mume? Nikauliza
?Ouh Wayne please just forget about that..lets
talk of something else..? Clara akasema
akionyesha wazi kulikwepa swali langu.Lengo
langu lilikuwa kutaka kufahamu undani wake
kuhusu maisha yake ya kimapenzi.Toka
nimekutana naye Clara amekuwa mgumu sana
kunieleza kuhusu maisha yake ya
kimapenzi.Kila ninapoanzisha mazungumzo
hayo huwa anapenda tubadilshe
maongezi.Nilisimama,nikamsogelea karibu na
kumshika bega lake la kulia kwa mkono
wangu
?Nisikilize Clara,pamoja na kwamba umekiri
kuwa una furaha ya kutosha maishani,lakini
ukweli ni kwamba hauna furaha ya
moyo.Kusema kwamba haufikirii kuwa na
mpenzi hauutendei haki moyo wako.Moyo
wako unahitaji upate mwenza na hivyo
kuufanya uwe na furaha maishani.Clara you
are a great woman.You deserve to be loved
and be happy.You need someone who can
complete your happiness.Don?t lie to yourself
Clara that you have happiness.You
don?t..Utakuwa mwanamke mwenye furaha
pindi utakapompata mwanaume wa maisha
yako.Tafadhali naomba usilisahau hilo?
TUKUTANE SEHEMU IJAYO??????..
 
BEYOND PAIN
SEHEMU YA 14
MTUNZI:pATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
?Ouh Wayne please just forget about that..lets
talk of something else..? Clara akasema
akionyesha wazi kulikwepa swali langu.Lengo
langu lilikuwa kutaka kufahamu undani wake
kuhusu maisha yake ya kimapenzi.Toka
nimekutana naye Clara amekuwa mgumu sana
kunieleza kuhusu maisha yake ya
kimapenzi.Kila ninapoanzisha mazungumzo
hayo huwa anapenda tubadilshe
maongezi.Nilisimama,nikamsogelea karibu na
kumshika bega lake la kulia kwa mkono
wangu
?Nisikilize Clara,pamoja na kwamba umekiri
kuwa una furaha ya kutosha maishani,lakini
ukweli ni kwamba hauna furaha ya
moyo.Kusema kwamba haufikirii kuwa na
mpenzi hauutendei haki moyo wako.Moyo
wako unahitaji upate mwenza na hivyo
kuufanya uwe na furaha maishani.Clara you
are a great woman.You deserve to be loved
and be happy.You need someone who can
complete your happiness.Don?t lie to yourself
Clara that you have happiness.You
don?t..Utakuwa mwanamke mwenye furaha
pindi utakapompata mwanaume wa maisha
yako.Tafadhali naomba usilisahau hilo?
ENDELEA????????
Nilimwambia Clara ambaye alikuwa ametulia
akinisikiliza.Akachukua glasi yake ya mvinyo
akapiga funda moja akainama na kufikiri
kisha akasema
?Wayne katika wanaume niliowahi kukutana
nao,sijawahi kukutana na mwanaume
aliyeniambia maneno yaliyonigusa kama
uliyoniambia leo hii.Maneno yako yamenigusa
sana moyo.Umeamsha kitu kipya ambacho
sikuwa nikikifikira katika maisha
yangu.Namkabidhi Mungu ndiye atakayejua
hatima ya maisha yangu .Kama itampendeza
mimi kupata mwanaume wa maisha yangu na
iwe hivyo? Clara akasema taratibu akiwa
ameinamisha kichwa.Nilitabasamu baada ya
kuisikia kauli ile.
Nilitazama saa na kukuta ni saa tisa za usiku.
?Clara muda umekwenda sana.Nahitaji
kukuacha upumzike na ujiandae kwa safari ya
kesho? Nikasema huku Clara akinitazama
?No Wayne you cant go now and leave me
alone.Stay with me just for tonight..? Clara
akaomba.Niimtazama machoni na kugundua
kwamba alikuwa akimaanisha
alichokisema.Hakujua ni furaha kiasi gani
nilikuwa nayo kwa kuniomba nibaki naye
usiku ule kitu nilichokuwa nikikiomba kila
siku.Nilitabasamu na kumsogelea,akasimama
na kunishika shingo yangu kwa mikono yake
laini.
?I?ll stay with you tonight? Nikasema kwa
sauti ya tayatibu yenye kukwama kwani
nilihisi msisismko wa ajabu baada ya
kuguswa shingo yangu na mrembo
yule.Msisimko ule ukanifanya niichukue
mikono yangu na kuizungusha kiunoni mwake
na kumfanya astuke ghafla na kuanza
kuhema kwa kasi.
?Wayne what do you want from me tonight?
Clara akauliza kwa sauti laini
?I just want a wonderfull night with
you..unforgetable night? Nikasema na kwa
kasi ya ajabu akanivuta kwake na kunipiga
mabusu mfululizo.Nilihisi kama napaa
mawinguni kwa mpasuko wa furaha
nilioupata.Ulikuwa ni usiku wa aina yake.Kwa
miaka mingi sikuwa nimepata usiku niliohisi
kama niko peponi kama huu.
* * * *
?Wayne you are amazing? Ilikuwa ni sauti ya
laini ya Clara iliyonistua toka usingizini.Nili
yafumbua macho na kujikuta nikiwa pembeni
ya mrembo mwenye uzuri uliotukuka.Nilijihisi
kama vile niko ndotoni.Kiumbe aliyekuwa
amelala pembeni yangu alifanana na wale
wanaopatikana katika simulizi mbali mbali au
kwenye picha za kuchora.
?Wayne..thank you for the wonderfull night ?
Akasema Clara na kunitoa katika fikra kuwa
nilikuwa ndotoni.Sikuwa nikiota.Ni kweli
nilikuwa nimelala na Clara.Nilimtazama Clara
ambaye alikuwa amenigeukia akinitazama
usoni huku macho yake mazuri yakifanya
mwili wangu uhisi msisimko wa ajabu
?Wayne sikutegemea kama ningekuja kukutana
na mwanaume ambaye angenipa furaha kama
uliyonipa usiku wa kuamkia leo.Katika maisha
yangu sijawahi kukutana na mwanaume wa
shoka kama wewe.Nilichokipata katika maisha
yangu ya kimapenzi ni karaha na mateso kiasi
kwamba niliwachukia wanaume wote na
kuwaona ni wanyama,wabinafsi na hakuna
mwanaume ambaye angeweza kunipa raha
niliyokuwa nikiihitaji.Wayne naomba nikiri
kwamba umenibadilisha mtazamo
wangu.Umenifanya niamini kwamba bado
wako wanaume ambao Mungu amewajaalia
uwezo mkubwa wa kuwaridhisha
wanawake.Wayne you are one of those few
men hard to find in this world.I don?t know
what I should do to make you forever
mine.Sikujua kama itatokea siku nitatokea
kumuhusudu mwanaume kama ilivyonitokea
kwako.Wayne naomba usinielewe vibaya lakini
toka nimekutana nawe nimejikuta nikiwa
tofauti sana na nilivyokuwa awali.Nimejikuta
nikiwa na furaha ya ajabu kitu ambacho
hakijawahi kunitokea hapo kabla.Nimejikuta
nikitoka nje ya msimamo wangu kwa mara ya
kwanza na kuhisi kwamba ninahitaji kuwa na
mtu wa kunifanya niendelee kuipata furaha hii
ya ajabu niipatayo sasa.Wayne sihitaji kuwa
mbali nawe tena kuanzia sasa.Kwa mara ya
kwanza toka nimezaliwa ninathubutu kupiga
magoti na kuomba nafasi ndani ya moyo wa
mtu.Wayne tafadhali naomba unipe nafasi
ndani ya moyo wako.Sintakuumiza kama
alivyokufanya mwanamke uliyekuwa
naye.Nitakupenda na kuwa nawe daima kwa
sababu you are so special Wayne.? Clara
akashindwa kuendelea akakiangusha kichwa
chake kifuani kwangu.Nilihisi joto la
ghafla.Nilihisi ile ilikuwa njozi na si kitu cha
kweli.Clara mwanamke mrembo anayeupeleka
mbio moyo wangu toka nimekutana naye leo
hii kwa mdomo wake anatamka kwamba
anahitaji kuwa nami maishani.Niliona ni kama
muujiza mkubwa ulionitokea.
Sikuwa na kitu cha kujivunga tena.Sikuwa na
kipingamizi wala sababu yoyote ya kukataa
ombi lile la Clara.Niliamini yale yalikuwa ni
majibu ya maombi yangu niliyomuomba
Mungu baada ya kutendwa na Emmy.
Siku mpya ikaanza kwa penzi zito kati yangu
na Clara.
? Wayne nasikitika sana kwa sababu sitaki
kubanduka pembeni yako lakini kazi hii
inayonilazimu kwenda afrika kusini leo ni
muhimu mno.Itanilazimu kwenda na baada ya
muda mfupi nitarejea.Nahisi miguu mizito
kuondoka hapa lakini sina namna nyingine ya
kufanya.Wayne umeniteka ghafla kiasi
kwamba sijielewi.nini kimenitokea.Kabla
sijaondoka ningependa nikapafahamu
nyumbani kwako ili nikija kwa mara nyingine
nisifikie tena hotelini? Clara akasema .
Sikuwa mbishi kwa kila alichokuwa akikiongea
Clara.Nilimsikiliza kama malkia wangu.Kwa
kuwa alikuwa na safari mchana wa siku
hiyo,hatukuwa na muda wa kupoteza
tukaingia garini na kuelekea nyumbani
kwangu.
Tulifika nyumbani kwangu na kwa ghafla
nilipatwa na mstuko wa ajabu kwa
nilichokiona katika geti la kuingilia ndani
.Nilisimamisha gari na kushuika kwa haraka.
Katika geti la nyumbani kwangu alikuwepo
Baraka amekaa juu ya tofali.Nilimwinua na
kumkumbatia kwa furaha kubwa.
?baraka umekuja saa ngapi? Nikamuuliza
?Nimekuja asubuhi ,nimekuta geti limefungwa
kwa kufuli nikajua haupo nikaamua kukaa
hapa nje nikusubiri? Baraka akajibu
?Mama na baba wamekuruhusu uje huku
asubuhi hii?
?hapana hawajaniruhusu.Nimetoroka
nyumbani.Simtaki uncle Chris.Kila siku
ananilazimisha nimuite yeye baba.Nataka
kuendelea kukaa na wewe.Sitaki tena kurudi
kule kuishi na mama.Nataka kuishi na wewe.?
Baraka alisema huku akitoa machozi.Mtoto
huyu aliniumiza sana na kukitonesha tena
kidonda kilichoanza kupona.Niliendelea
kumlaani Emmy kwa kitendo alichokifanya na
kumfanya mtoto mdogo kama yule kuteseka
namna ile.
?basi usilie baraka.Tutakaa wote siku ya leo
halafu jioni nitakupeleka nyumbani na kama
mama yako atakubali uishi huku basi tutaishi
wote.? Nilimwambia Baraka ambaye
alionyesha wazi kutokuridhika na uamuzi
wangu wa kumrudisha nyumbani kwao
jioni.Nilimtambulisha Baraka kwa
Clara,akamshika mkono nikaingiza gari
ndani.Kwa muda mfupi Clara na Baraka
wakazoeana na kuwa marafiki .Dakika zile
chache za kuwa pamoja zilileta furaha kubwa
miongoni mwetu.
Tukiwa bado katika maongezi na vicheko pale
sebuleni mara ghalfa mlango unafunguliwa na
anaingia Emmy akiwa ameongozana na askari
wanne .Alikuwa amefura kwa hasira.Wote
tukapigwa na butwaa kwa hali ile.Moja kwa
moja Emmy akaninyooshea kidole mimi na
mmoja wa wale askari akanikaribia.
?Ndugu wewe ndiye Wayne??
?Ndiye mimi.Kuna nini afisa? Nikauliza kwa
mshangao
?Wayne tunakuhitaji kituoni.Unatuhumiwa
kumchukua mtoto aitwaye Baraka bila ridhaa
ya wazazi wake.Tafadhali tunaomba
tuongozane kwenda kituoni kwa ajili ya
maelezo zaidi.?
Mwili wote ukajikuta ukilowa jasho na
midomo kunitetemeka kwa hasira.
?Afande nafahamu kwamba mko kazini lakini
naomba mnieleweshe ninakamatwa kwa kosa
lipi? Sielewi nimefanya kosa gani ?
Nikawaambia wale askari ambao walionyesha
hawakuwa na muda wa kupoteza.
? Bwana Wayne,huyu mama unamfahamu?
Akauliza yule askari aliyeonekana ndiye
kiongozi wa msafara ule
?Ninamfahamu.Alikuwa mke wangu? Nikajibu
huku nikimtazama Emmy kwa macho makali
?Huyu mama ndiye mlalamikaji ,na ameleta
malalamiko kwamba mtoto wake amepotea na
moja kwa moja akakuhisi wewe kwamba ndiye
uliyemchukua mtoto huyo bila ridhaa ya
wazazi wake kitu ambacho ni kosa
kisheria.Tumekuja hapa na kumkuta mtoto
huyo anayedaiwa kupotea yuko hapa
kwako.Kwa hiyo tunakuhitaji hapa tuende
wote kituoni ili ukatoe maelezo yako
kuhusiana na suala hili? akasema afande yule
ambaye sikuweza kuzisoma namba zake kwa
sababu ya sweta alilokuwa amevaa.Niliuma
meno kwa hasira nikawatazama wale
maaskari kisha nikasema
?naomba tusikilizane maafande.Mimi
siwaelewi mnaongea kitu gani kwa sababu
mimi ndiyo kwanza nimefika hapa nyumbani
sina hata nusu saa,sasa huyo mtoto
nimemuiba saa ngapi? Isitoshe nimefika hapa
na kumkuta Baraka amekaa getini.Nikamuul
iza amefikaje fikaje hapa akaniambia kwamba
ametoroka nyumbani kwao basi nijkamchukua
na kuingia naye ndani.Kama hamuamini
ninachokisema hebu muulizeni mtoto huyu
hapa yeye mwenyewe atasema ukweli?
Nikasema kwa msisitizo
?Afande msimuamini huyo.Amemuiba mtoto
wangu na kuja kumficha huku.Tafadhali
afande tusizidi kupoteza muda mchukueni
tuelekee kituoni,atajitetea mahakamani?
Emmy akasema akiwa amefura kwa
hasira.Nilitamani nimrukie na kumpa kipigo
kikali mwanamke yule lakini nikajitahidi
kujizuia ili nisifanye jambo kama hilo
japokuwa nilikuw ana hasira zisizomithilika..
?Afande samahani naomba na mimi niongee
kidogo? Clara aliyekuwa ameduwaa akiangalia
mambo yanavyokwenda akafunguka na
kusema
?Nyamaza kimya hasidi wewe?.? Emmy
akasema kwa ukali akimwambia Clara lakini
afande akamzuia
?Emmy hebu nyamaza tumsikilize na mwenzio
anataka kusema nini.Endelea mama?? afande
akampa ruhusa Clara aongee
?Afande mimi sioni kosa ambalo Wayne
anatuhumiwa nalo.Nimekuwa na Wayne toka
jana jioni,tulihudhuria wote hafla ya
uchangishaji fedha za kusaidia kituo cha
watoto wanaoishi katika mazingira
magumu.Tumetoka pale ukumbini na kuelekea
hotelini kwangu.Nimekuwa na Wayne usiku
mzima na hakurejea nyumbani kwake.Asubuhi
hii tumeongozana wote kuja hapa kwake na
tulipofika getini tumemkuta mtoto
amekaa,Wayne akamuuliza kama
ameruhusiwa kuja huku na mama yake
,Baraka akasema kwamba hakuruhusiwa na
mtu yeyote kuja huku ila ametoroka yeye
mwenyewe baada ya kutokuridhishwa na
maisha anayoyaishi huko kwao.Nimeona
niongee ukweli kwa sababu inaonekana huyu
mwanamke hana uhakika na anachokiongea.?
Clara akasema na ghafla Emmy akakurupuka
na kutaka kumvaa Clara,akazuiwa na askari.
?Niacheni nimfundishe adabu huyu mwanamke
naona bado hajanifahamu mimi ni
nani.nakuonya wewe mwanamke usiingilie
mambo yasiyokuhusu.kama unahitaji mtoto
zaa wa kwako na si kusubiri wengine
wakuzalie ili uibe.Ninakwambia wewe na huyu
baradhuli mwenzio mtanikoma mwaka huu.?
Emmy akaongea kwa sauti kali.Niliitazama
sura ya Clara nikaona ni jinsi gani
alivyoumizwa na maneno yale ya
Emmy.Hasira zikanipanda nikashindwa
kujizuia nikataka kumvaa Emmy na kumpa
kipigo lakini askari wakafanya kazi yao na
kunizuia.
?Afande sintakubali hata siku moja
mwanamke huyu akaja na kuanza
kuporomosha matusi ndani ya nyumba yangu.
Kama ni kutukana anitukane mimi na hata
siku moja asije akamgusa Clara.Hahusiki na
kitu chochote .?Nikasema kwa ukali.
?Anhaa kumbe huyu ndiye anayekupa
kiburi,basi nitakula naye sahani moja.Yeye si
ndiye anayeona fahari kuchukua mabwana za
watu, nakwambia nitamfundisha
adabu.Nitamuonyesha mimi ni nani.Wayne
fahamu kwamba wewe bado ni mume wangu
halali wa ndoa na ninakuonya kwamba
sintakupa muda wa kupumzika.Nitak
ufundisha adabu? Emmy akaongea kwa
kujiamini sana.Chuki ya wazi wazi
ikajidhihuirisha machoni pake.Sikuelewa nini
sababu ya chuki ile kubwa na ya dhahiri
aliyokuwa nayo Emmy kwangu.Alitaka kuwa
huru na nikamruhusu aende anakotaka
kwenda .Kwa ulimi wake alitamka kwamba
hanitaki tena katika maisha yake sasa kwa
nini aanze kunifuatilia maisha yangu wakati
kila mmoja amekwisha anza maisha yake?
Nilikasirika sana
?jamani hapa hatukuja kwa ajii ya
kugombana.Sasa sikilizeni.Wayne na
mwenzio,wote tunaelekea kituoni kwa ajili ya
kupata maelezo ya kina juu ya suala hili lenye
utata.Mambo yote yatajulikana huko huko
kituoni? Afande akasema.
?Sawa hakuna shida afande.Lakini huyu
mwenzangu Clara naomba mumuache aende
zake kwa sababu kwanza hahusiki kwa namna
yoyote na masuala haya na pili ana safari ya
kwenda Dar es salaam saa tano asubuhi ya
leo kwa ndege na tayari amekwisha kata
tiketi.? Nikawaomba wale maaskari lakini kwa
haraka Clara akasema
?wayne usijali nitakuwa nawe mpaka
mwisho.Siwezi kukuacha peke yako katika
tuhuma ambazo si za kweli.Safari yangu
ninaweza kwenda siku yoyote ile lakini
sintakubali kuona ukinyanyaswa na mijitu
yenye roho za kishetani? Clara akasema huku
ameukunja uso wake kwa hasira.Moyoni
nilisikitika sana kwa kumuingiza Clara katika
matatizo yangu na Emmy,mwanamke mwenye
roho ya shetani.Maneno yale ya Clara
yalionyesha kumchoma moyo Emmy ambaye
alibetua midomo na kusonya kisha kwa
ghadhabu akamuendea Baraka aliyekuwa
sofani akilia ,akamchukua kwa nguvu.
?hebu twende ,wewe ndiye unayesababisha
mpaka mimi natukanwa namna hii? Emmy
akaongea kwa hasira huku akimvuta mkono
baraka ambaye alikuwa akipiga kelele
akigoma kuondoka.
?Bwana wayne tafadhali ingia garini wewe na
mwenzio twende kituoni ? Afande akaniamuru
nipande gari la polisi lililokuwa imeegeshwa
pale nje kwangu.
?Afande sijakataa kwenda kituoni.Nimetii bila
shuruti na ninaomba niruhusiwe kuongoza
kituoni mimi mwenyewe na gari yangu.Siwezi
kupanda gari moja na huyo mwanamke?
Afande akanitazama na kukubaliana nami
kwamba nitumie gari langu.Mimi na Clara
tukaingia katika gari langu na kuongoza
kuelekea kituoni.Clara alikuwa kimya na
hakuongea kitu chochote.Ni wazi alikuwa
ameumizwa sana na kitendo alichokifanya
emmy.Nilikuwa nikimtazama kwa kuibia .
?Clara samahani sana kwa yote
yaliyotokea.Sifahamu nini sababu ya
mwanamke yule kunifanyia mambo kama
haya..Kama uhuru nimekwisha muachia na
anaishi na mtu ambaye yeye mwenyewe
alitamka kwamba ndiye anayempa furaha
maishani sasa iweje tena aanza kunifuatilia
katika maisha yangu? Ameniumiza sana lakini
nitamuonyesha mimi ni nani? Nikasema
?Wayne tafadhali usiendelee kugombana na
yule mwanamke kichaa.Utajikuta ukipoteza
muda mwingi kwa mambo yasiyokuwa na
maana yoyote.Kitu cha msingi jaribu
kujipanga na kuangalia maisha yako ya
mbeleni.Mtu kama yule usimuweke katika akili
yako.Ukisema upambane naye utapoteza
muda wako bure.Nakushauri achana naye
kabisa na wala usijishughulishe naye hata
kidogo? Clara akasema huku akiweka mkono
mmoja begani kwangu
?Vipi kuhusu safari yako ya Afrika kusini?
Itakuwaje iwapo hautaonekana? Nikauliza
?Usijali kuhusu hilo wayne.safari yangu si
muhimu kwama ulivyo wewe.Mimi ninafahamu
thamani yako kwangu na ndiyo maana niko
tayari kufanya lolote lile kwa ajili yako.Niko
tayari kwenda hadi mwisho wa dunia kwa ajili
yako.Kwa hiyo kuhusu hilo la safari lisikupe
shida kabisa Wayne.? Maneno yale
yakanifanya nitabasamu .Clara alimaanisha
alichokuwa amekisema.Aliiona thamani yangu
kwake na hivyo kuwa tayari kufanya chochote
kile kwa ajili yangu.Niliapa moyoni kufanya
kila niwezalo kwa ajili ya kuwa na mwanamke
kama huyu ambaye ananijali na kunithamini .
Tulifika kituoni na kushuka kisha tukawasubiri
askari wale wafike kwa sababu tulikuwa
tumewatangulia kufika.Walipofika
tukaongozana wote hadi ndani ambako
nilichukuliwa maelezo.Nilipomaliza Clara naye
akaomba atoe maelezo yake kama nyongeza
kwa yale ya kwangu akakubaliwa.
Baada ya masaa manne ya mjadala mkali
baina yetu na maafisa wa polisi ikaonekana
wazi kwamba sikuwa na kosa lolote
nililolifanya ila zilikuwa ni hila za Emmy
kutaka kunichafua.Alipewa onyo kali kwanza
kwa kusumbua chombo cha dola na pili kwa
kutaka kunichafua.Vile vile ikaamriwa kwamba
aniombe radhi mimi pamoja na Clara kwa
usumbufu aliotusababishia na mwisho
akakanywa kwamba kama tumeachana
asijaribu tena kuyafuatilia maisha yangu.
Baada ya kikao kile tukaagana na maafisa wa
polisi tukatoka na kuelekea lilipo gari letu
huku tumeshikana mikono.Nikamfungulia
Clara mlango aingie garini lakini kabla
hajaingia nikamuona Baraka akija mbio kule
kwenye gari letu.
?daddy naomba usiniache nirudi tena kwa
mama.naomba tuondoke wote? Baraka
akasema huku akilia.Nilimuonea huruma sana
mtoto yule kwa namna alivyokuwa akiteseka
lakini sikuwa na jinsi ya kumsaidia.Nilibaki
nikimtazama.Clara akainama na
kumbembeleza
?Baraka nenda kwa mama .Mimi na baba
yako tutakuja kuomba kwa mama yako ili
akuruhusu ukae nasi..? Clara akamwambia
Baraka ambaye akanigeukia na kuniuliza
?Eti daddy ni kweli ?
?kweli Baraka.Tutakuja kuongea na mama
yako ili akuruhusu uje kukaa kule kwetu?
Nikajibi na ghafla akatokea Emmy na
kumnyakua Baraka kwa nguvu toka kwa Clara
?Nakwambia hivi wewe mwanamke,lazima
nikuonyeshe kazi.Nitakufundisha adabu.Wewe
ndiye unayempa kiburi huyu kunguru,basi
jiandae kupambana na mimi? Emmy akasema
kwa shari.Clara akamtazama na kutabasamu
kisha akanisogelea akanikumbatia na kunipa
busu moja zito.
?Let?s get out of here darling.She is crazy?
Clara akasema huku akicheka kichini chini
kisha tukaingia garini na kuondoka
tukimuacha Emmy amevimba kwa hasira.
?Darling ,sababu iliyopelekea wewe ukaachana
na yule mwanamke ni ile ile uliyonieleza au
kuna sababu nyingine? Clara akauliza tukiwa
garini
?Kwa nini umeuliza hivyo Clara?
?Kwa sababu naona chuki aliyokuwa nayo
yule mwanamke ni kubwa sana na ya wazi.Ni
kama vile anataka kukuangamiza kabisa.Ni
kama vile anataka kulipiza kisasi kwa jambo
baya ulilomfanyia? Clara akasema na
kunifanya nitabasamu
?Clara yule mwanamke sijui anachokitafuta
kwangu ni kitu gani.Kama ni chuki nilipaswa
kuwa nayo mimi kwa sababu yeye ndiye
aliyenifanyia mambo ya ajabu sana.Mimi
sijamfanyia jambo lolote lile baya na wala
hastahili kuwa na chuki na mimi.Alihitaji
uhuru na nikampatia uhuru sasa tatizo liko
wapi? Clara nakuomba umpuuze hayawani
yule.Hana chochote cha kukufanya? Nikasema
na kumfanya Clara atabasamu,akanisogelea
karibu na kubusu
TUKUTANE SEHEMU IJAYO?????.
 
BEYOND PAIN
SEHEMU YA 15
MTUNZI:pATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
?Let?s get out of here darling.She is crazy?
Clara akasema huku akicheka kichini chini
kisha tukaingia garini na kuondoka
tukimuacha Emmy amevimba kwa hasira.
?Darling ,sababu iliyopelekea wewe ukaachana
na yule mwanamke ni ile ile uliyonieleza au
kuna sababu nyingine? Clara akauliza tukiwa
garini
?Kwanini umeuliza hivyo Clara?
?Kwa sababu naona chuki aliyokuwa nayo
yule mwanamke ni kubwa sana na ya wazi.Ni
kama vile anataka kukuangamiza kabisa.Ni
kama vile anataka kulipiza kisasi kwa jambo
baya ulilomfanyia? Clara akasema na
kunifanya nitabasamu
?Clara yule mwanamke sijui anachokitafuta
kwangu ni kitu gani.Kama ni chuki nilipaswa
kuwa nayo mimi kwa sababu yeye ndiye
aliyenifanyia mambo ya ajabu sana.Mimi
sijamfanyia jambo lolote lile baya na wala
hastahili kuwa na chuki na mimi.Alihitaji
uhuru na nikampatia uhuru sasa tatizo liko
wapi? Clara nakuomba umpuuze hayawani
yule.Hana chochote cha kukufanya? Nikasema
na kumfanya Clara atabasamu,akanisogelea
karibu na kubusu
ENDELEA????????..
Niliendelea kumshukuru Mungu kwa kunisaidia
kushinda tuhuma zile nzito alizokuwa
ameziibua Emmy.Bado sikuelewa ni kwa nini
Emmy alikuwa na chuki ya namna ile
kwangu.Sikufahamu nilimkosea jambo gani
baya kiasi cha kumfanya anichukie namna
ile.Kama ni kuachana na mimi yeye ndiye
aliyetaka tuachane sasa ni kwa nini anifanyie
vile? Kwa nini aliahidi kuendelea kupambana
na mimi? Pengine labda kile kitendo cha
kuniona niko na Clara kilimuuma sana
.Yawezekana alikuwa akiugulia moyoni kwa
wivu.Lakini wivu wa nini kwa sababu ni yeye
ndiye aliyeyaanzisha mambo yote haya.
Mawazo haya yaliendelea kuniumiza kichwa
sana na mara Clara akanistua
?wayne unawaza nini?
?Mambo mengi Clara.Nawaza ni namna gani
ulivyoumia moyoni kwa jambo alilolifanya
Emmy.Nawaza ni namna gani nitakuomba
msamaha kwa jambo la aibu kama lile.Ni siku
yetu ya kwanza tu kuwa pamoja halafu
unakutana na jambo kama lile na kupelekea
ukafika hadi polisi na kikubwa zaidi
amekufanya uahirishe hadi shughuli zako
muhimu.Kila nikifikiria suala hili ninaumia
sana Clara?
Clara akanitazama akatabasamu na
kuunyoosha mkono wake ,akasugua sugua
shingo yangu kidogo huku akisema
?Wayne naomba usikwazike kwa kitendo
alichokifanya Emmy.Kwangu mimi sikuumia
kwa mambo aliyoyafanya bali nilimuonea
huruma sana kwa sababu hana amani moyoni
kwa mambo aliyoyafanya.Kama hatabadilika
basi hatakuwa na amani maishani mwake
hadi siku yake ya mwisho.Mimi sina tatizo
naye hata kidogo na nina imani kwamba
hawezi kunifanyia kitu chochote kibaya kama
alivyoahidi.Yale yalikuwa ni maneno ya kujipa
moyo.Ninachokushauri kwa sasa inabidi
uondoke hapa Arusha kwa muda wa mwezi
mmoja au zaidi ili umsahau kabisa
Emmy.Utakapofanya hivyo utakuwa umempa
nafasi hata yeye mwenyewe ya kuweza
kuendelea na mambo mengine yanayomuhusu
kwa sababu kila atakapokuwa akijaribu
kukutafuta hatakupata.?
?wazo lako zuri Clara.Hata hivyo nilikuwa na
mawazo kama hayo toka zamani na
niliahirisha baada ya kukutana nawe.?
?Uliahirisha safari kwa ajili yangu? Clara
akauliza
?Ndiyo Clara .Nilikwisha andaa safari ya
kuelekea Zanzibar mahala ambako niliamini ni
sehemu nzuri na ambayo ingenifanya nisahau
kabisa yote yaliyonitokea lakini nilipokutana
nawe siku ile mipango yote ikavurugika.?
Clara akacheka kicheko kikubwa kama
kawaida yake halafu akasema
?kama uliahirisha safari kwa ajili yangu,na
mimi leo nimeahirisha safari kwa ajili
yako.Ngoma droo? wote tukacheka kicheko
kikubwa.
?Ulikuwa umepanga kwenda Zanzibar? Clara
akaniuliza
?Ndiyo Clara nilikuwa nimepanga kwenda
kupumzika Zanzibar.Nilitaka nikaishi mbali
kabisa na hapa na nikaona kwamba Zanzibar
ni sehemu nzuri na salama sana kwa
mapumziko.?
?hata mimi sijawahi kufika Zanzibar.Unaonaje
kama tukienda wote kupumzika Zanzibar?
Clara akauliza.Nikamtazama na kusema.
?Kokote utakakotaka twende ,nitakuwa
tayari.hata ukisema leo hii tunywe sumu tufe
wote mimi niko tayari? Nikasema na
kumfanya Clara acheke sana .Akafunua pochi
yake na kutoa kitambaa cha mkononi na
kufuta machozi yaliyotokana na kucheka
?Wayne unanifurahisha sana.You make me
feel a very special woman in this
world.Najisikia furaha sana.You are very
special to me?
Sikujibu kitu zaidi ya kutabasamu ,halafu
nikapunguza mwendo wa gari na kukata kona
ya kuelekea nyumbani kwangu.
?Wayne naomba usinielewe vibaya kwa haya
nitakayokwambia ? akasema Clara tukiwa
tumejipumzisha kitandani nyumbani kwangu
?Nakusikiliza Clara? Nikamwambia huku
nikilisugua bega lake la kulia kwa mkono
wangu
?Ni muda mrefu sana nimeishi maisha yangu
nikiwa mwenyewe bila kuwa na mpenzi na
niliweka nadhiri kwamba sintakuwa na mtu
aitwaye mpenzi katika dunia hii hadi kifo
changu.Nilikuwa nikiwachukia
wanaume.Niliamini wanaume wote baba yao
mmoja kwa hiyo wote wako sawa.Wayne
sifahamu kilinitokea kitu gani lakini baada ya
kukutana na wewe nimejikuta nikiivunja
nadhiri yangu.Nimejikuta nikibadili msimamo
na matazamo wangu.Kilichotokea hata mimi
bado nashangaa.Hata marafiki zangu
wakifahamu kuhusu uhusiano wetu huu
watanishangaa sana kwa sababu walielewa
fika ni jinsi gani nilivyokuwa nikiwachukia
wanaume.Wayne nimevunja nadhiri yangu ya
kutokuwa na mwanaume na nimeamua
kukukabidhi moyo wangu wewe pekee kwa
kuamini kwamba uko tofauti sana na
wengine.Nimekupa moyo wangu kwa sababu
nakupenda sana.Nakukabidhi moyo na mwili
wangu uvitunze.Nakuahidi nitakupenda hadi
mwisho wa maisha yangu.Nitakuwa
mwaminifu kwako hadi kifo kitutenganishe.
Nitaishi nawe katika kila hali ,iwe masika
kiangazi,kwenye jua na mvua.Ugonjwa na
faraja sintakuacha Wayne.Pamoja na hayo
yote nakuomba kitu kimoja tu?
Clara akasema kwa hisia kali huku macho
yake yamejaa machozi
?Chochote utakachoomba Clara nitakutimizia.?
Nikasema taratibu huku nikishika mikono
yake.
?Wayne don?t ever make me cry. Promise me
that you?ll never hurt me.Promise me that
you?ll make me a happiest woman? Clara
akasema huku amenikazia macho.Nilimtaza
ma mrembo yule mwenye macho ya
kimalaika.Macho yake yalinieleza kila kitu
kilichokuwamo moyoni mwake.Nikamshika
mikono yake na kumsogeza zaidi
kwangu.Nikambusu na kusema
?Clara My angel naomba nikueleze ukweli
kwamba hadi sasa najihisi kama vile niko
ndotoni kwa sababu sikutegemea kama
wanawake kama wewe bado wanaishi katika
dunia hii.Baada ya kutengana na Emmy
niliumia sana na sikufichi kwamba
niliwachukia wanawake kupita kiasi.Kila
mwanamke niliyemuona nilijenga picha
kwamba ana tabia kama za Emmy.Siku ile
nilipokutana nawe nilijikuta nikibadili kabisa
mtazamo wangu kuhusu wanawake.Nilijikuta
nikipata furaha ya ajabu na kusahau kama
nilikuwa nimeumizwa muda mfupi
uliopita.Toka siku ile nilikuwa naota ni namna
gani ningeweza kuwa na furaha kama
ningekuwa na mwananke kama wewe.Nilisali
na kumuomba Mungu anirejeshee tena furaha
yangu iliyopotea na leo hii amesikia sala
zangu na niko nawe hapa kitandani.Clara
nakupenda na ninakuahidi kwamba
nitakuheshimu na kukutunza kwa sababu
wewe ni kitu cha thamani kubwa maishani
mwangu .Thamani yako inazidi hata ile ya
Lori zima la almasi.Siku zote nitakuwa nawe
na kukuenzi kama malkia wangu.Sintakuum
iza na wala kukutoa machozi.nakuahidi hivyo
? Clara akanivuta kwake na kunikumbatia kwa
nguvu..
Tulishinda nyumbani kwangu hadi jioni
,nikampeleka Clara hotelini alikofikia akabadili
mavazi kisha tukaelekea katika klabu moja ya
usiku ambako kulikuwa na muziki wa
bendi.Tulicheza na kufurahi hadi saa nane za
usiku kisha tukarejea hotelini kwa Clara
tukalala hadi asubuhi.Sikuwahi kupata raha
za namna hii katika maisha yangu.Nilimuona
Clara kama malaika aliyeshushwa ili kunipa
furaha maishani mwangu.
Asubuhi ya siku iliyofuata tulirejea nyumbani
kwangu kwa ajili ya kubadili nguo kisha
tuelekee matembezini.Tulipanga tukatembee
katika bustani ya nyoka .Clara alikuwa
akisikia kwamba kuna nyoka wanafugwa na
hivyo alihitaji kwenda kuangalia. .
Baada ya kuingia chumbani kwangu nilihisi
kama vile chumba hakikuwa sawa.Sikutilia
maanani sana nikalifungua kabati na kutoa
nguo nikavaa.Nikiwa naendelea kuvaa simu
yangu ikaita.Nikaangalia namba za
mpigaji,zilikuwa ni namba ngeni kabisa katika
simu yangu.
?hallow? Nikasema baada ya kuipokea simu
ile
?hallow Wayne.Ni mimi Emmy?
?Bastard ! unanitafutia nini wewe baradhuli ?
Nikajikuta nikisema kwa ukali.Nilipatwa na
hasira za ghafla
?Ama kweli umenichoka.Umefikia hatua ya
kuniita baradhuli ? Akasema Emmy
?Emmy nakuonya . Acha kabisa kunifuata
fuata katika maisha yangu.Naomba hii iwe ni
mara ya mwisho kuisikia sauti yako ?
? Nafurahi kusikia hivyo Wayne.Nafahamu
sihitaji kukusumbua tena katika maisha
yako.Nakuacha ule raha na mwanamitindo
wako.Sintakupigia tena simu lakini nadhani
wewe ndiye utakayenipigia simu na
kunitafuta.Kabla sijakata simu na kuachana
nawe kabisa kuna jambo naomba nikueleze ?
?unataka kunieleza nini wewe mwanamke ?
nikauliza
?usiwe na haraka hivyo Wayne.Mimi ndiye
niliyekupigia simu na ninaomba
unisikilize.Nakuomba tafadhali unisikilize kwa
makini kwa mara ya mwisho.Nafahamu una
shilingi millioni mia moja na arobaini katika
benki ya kimataifa ya European Africa
Bank.Nafahamu ni jinsi gani ulivyozipata
fedha zile na ninaufahamu mtandao wenu
wote.Sitaki kukuchosha sana lakini ninakupa
masaa ishirini na manne uhamishe shilingi
millioni mia moja katika akaunti yangu benki
ya Stanbic. Iwapo hautatekeleza hilo fahamu
kwamba utakwenda mahakamani na
ninakuhakikishia kwamba ni lazima
utafungwa kifungo kirefu gerezani kwa sababu
ushahidi wote ninao.kama huamini angalia
kabati lako unalohifadhi kumbukumbu
zako.Kumbuka masaa ishirini na nne Wayne
ama la utafia gerezani na utamuacha mrembo
wako akiponda raha na wanaume
wenzako.hahahahahaa bye Wayne?
Nilikuwa nimepigwa na butwaa nikashindwa
hata kufunga mkanda wa suruali nikaiacha
ikaanguka chini.Jasho lilianza kunitoka.
?wayne whats wrong? Akasema Clara ambaye
alistuka kutokana na mabadiliko yangu ya
ghafla.
?Documents !! documents ! ??? Nikasema
huku nikilivuta kabati kubwa la nguo na kwa
nyuma yake nikaanza kubonyeza namba za
sefu ambalo huwa natunzia kumbu kumbu
zangu muhimu.Sefu hili huwa linafunguliwa
na namba maalum na kwa bahati mbaya
Emmy alikuwa akizifahamu
Nilitamani ardhi ipasuke niingie ndani baada
ya kulifungua sefu langu na kukuta nyaraka
zangu muhimu hazimo.
?damn you Emmy..? Nikaishiwa nguvu na
kukaa chini.
Clara alistuka sana kwa hali niliyokuwa nayo
akanisogelea na kuniuliza
?Wayne whats wrong? Sikumjibu kitu
.Akakimbia na kuniletea glasi ya maji
?Kunywa maji Wayne.? Nikaishika glasi ile
nikanywa maji kisha akaniinua na kunipeleka
kitandani.
?My documents? Nikasema kwa uchungu
?what documents? Clara akauliza
Niliendelea kutikisa kichwa kwa hasira
?wayne document zipi hizo? Clara akaendelea
kuuliza
?She was here..that bastard was here last
night !! Nikasema kwa sauti kali
?Wayne nani alikuja hapa? Clara akauliza
? Emmy? Nikajibu na kumfanya Clara astuke
?Emmy ?
?Ndiyo Emmy alikuja hapa jana usiku na
amechukua nyaraka zangu muhimu sana?
?Ouh Emmy why are you doing this to me?
Nikasema huku nikiuma meno kwa uchungu.
?Calm down Wayne.? Clara akasema huku
akinipiga piga mgongoni.
?Wayne nyaraka hizo zilikuwa zinahusu nini?
Akauliza Clara.Nilishindwa nimjibu
nini.akanitazama tena na kuuliza
?Wayne hebu niambie nyaraka hizo zilikuwa
zinahusu nini?
?mshenzi yule alifahamu mahala nilipokuwa
naweka nyaraka zangu muhimu na amekuja
kuzichukua? Nikasema
?wayne please answer me.Nyaraka hizo
zilikuwa ni za nini? Pengine ninaweza
kukusaidia kuzipata?
?Clara nyaraka hizo ni za muhimu sana na
kama nikifanya mchezo ninaweza kufungwa.?
Clara akastuka na kuniangalia kwa macho
makali
?Kufungwa ?? akauliza
?Ndiyo Clara.Ninaweza kufungwa? Nikajibu
?Ufungwe kwa kupoteza nyaraka ? Clara
akauliza
?Its not simple as you think Clara.This is
something very serious? Nikasema huku
nikiinuka pale kitandani na kwenda kusimama
dirishani.Nilikuwa nikihema kwa kasi kutokana
na hasira nilizokuwa nazo.
?Wayne kama amekuja Emmy na kuingia
ndani mwako bila ruhusa yako na kisha
akachukua nyaraka zako,basi tunaweza
kusema kwamba mtu huyo ni mhalifu.Amevunj
a na kuiba.Twende tukamshitaki polisi haraka
ili wamkamate? Clara akasema
?No Clara hili si suala la polisi.Ndiyo maana
amenipigia simu na kunifahamisha kwamba
nyaraka zangu anazo kwa sababu anafahamu
kwamba sintaweza kwenda polisi kushitaki.?
?Why Wayne? Kwa nini usiende kumshitaki
polisi wakati ameingia nyumbani kwako
,akachukua nyaraka zako na kuondoka.Huo ni
uhalifu.Lets report her to the police.That?s the
best way to teach her a lesson.Huwezi
kumuacha mtu kama huyu .Huyu ni mhalifu
na huwezi kujua anaweza hata akakuua.Ouh
Wayne I?m so sacred.lets go to police? Clara
akasema.Uso wake ulionyesha wasi wasi.
?hapana Clara .Hili si suala la kwenda
kushitaki polisi.Hili ni suala langu mimi na
yeye?
?Wayne tell me why ?? kwa nini tusimshitaki
polisi ili achukuliwe hatua?
? No Clara we cant do that? Clara
akanisogelea na kusema
?Wayne niambie ni kwa nini Emmy
asichukuliwe hatua kwa kosa alilolifanya?
Sikujibu kitu nikainama chini
?Whats going on Wayne? Don?t tell me you are
scared of her.? Nilinyamaza kimya na
kumtazama Clara ambaye alianza kupata
mashaka.Niliogopa kumweleza ukweli kwa
sababu ilikuwa ni mapema sana kuanza
kukumbana na mambo kama haya.hakupaswa
kuanza kuumizwa na masuala yangu kwa
muda huu mfupi.Nilimchukia Emmy kupita
kiasi kwani sasa niliamini lengo lake lilikuwa
ni kunifanya niishi maisha magumu .Nikiwa
nimezama katka dimbwi la mawazo nikastukia
bega langu likiguswa na Clara.Nikainua
kichwa na kumtazama
?Wayne do you real love me? Clara akauliza
?Clara I love you more than you think?
Nikajibu
?kama kweli unanipenda Wayne tell me the
truth.Whats going on here.If you love and
trust me tell me the truth and I?ll understand
you.Hata kama umeua mtu,niambie ukweli.As
far as I love you I will understand.? Clara
akasema huku akinitazama usoni.
Nilimtazama usoni,nikajisikia vibaya
sana.Clara hakustahili kuteseka kwa ajili
yangu.macho yake yalikuwa yakitoa machozi
,nikamuonea huruma nikaamua kumweleza
ukweli.
?Clara nitakueleza ukweli? Nikasema huku
nikimshika mkono na kumpeleka
kitandani,.Tukaa na kutazamana.
?I?m listening Wayne.? Clara akasema.Nikakoh
oa kidogo kusafisha koo langu kisha
nikasema
?Hapo awali nilikuwa nafanya kazi katika
halmashauri ya jiji la Arusha nikiwa katika
kitengo cha ukarabati wa miundombinu.Mimi
ndiye niliyekuwa nikiratibu shughuli zote za
ukarabati wa miundombinu mbalimbali ya
halmashauri ya jiji kama vile barabara
n.k.Miaka mitatu iliyopita aliletwa mkurugenzi
mpya ambaye kwa sasa ni marehemu.Mkurug
enzi huyu ambaye naweza kusema kwamba
ndiye aliyenifundisha namna ya kubuni miradi
hewa na kuingiza mfukoni pesa ya
halmashauri.Akiwa kama kiongozi ,aliunda
mtandao wa watu ambao kwa pamoja
tulishirikiana katika kubuni miradi mingi
ambayo haikuwepo au kama ilikuwepo basi
ilikarabatiwa au kujengwa kwa kiwango cha
chini sana tofauti na gharama zilizoainishwa
katika taarifa za mradi.Tulitengeneza fedha
nyingi sana.Tulibuni miradi mingi iliyogharmu
mabilioni ya shilingi lakini mingi kati ya hiyo
haikuwepo na au ilikuwa ya kiwango cha chini
sana.Haikuwa rahisi kugunduliwa kwa sababu
mkaguzi mkuu wa ndani wa halmashauri na
wahasibu wote walikuwa katika mtandao wetu
hivyo kila ripoti za ukaguzi zilipohitajika
zilipelekwa ripoti nzuri na za kufurahisha.Ili
tokea bahati mbaya mkaguzi wetu wa ndani
alihamishwa na kuletwa mkaguzi mwingine
ambaye hakuweza kushirikiana na sisi hivyo
kutaka kutibua mambo.Ili kulizima sakata hilo
ikatulazimu kuwanyamazisha huyo mkaguzi
pamoja na mkurugenzi .Baada ya hapo
nikaacha kazi halmashauri na kutafuta kazi
mahala kwingine.Wakati mambo yote haya
yanafanyika nilimshirikisha Emmy kama mke
wangu katika kila kitu.Alichokifanya Emmy
,jana usiku amekuja na kuchukua nyaraka
zangu zote muhimu na anazo kwa
sasa.Alikuwa akifahamu kwamba nina shilingi
millioni mia moja na ishirini benki ambazo
nilizipata wakati ninafanya kazi
halmashauri.Anataka nihamishie shilingi
milioni mia moja katika akaunti yake ya benki
na nisipofanya hivyo ataripoti suala hili
polisi.Amenipa saa ishirini na nne niwe
nimetekeleza hilo agizo?
Nilimaliza kumweleza ukweli Clara ambaye
akainuka na kushika kichwa chake kwa
mikono yake miwili.
?Ouh my god ! what a scandal.Why me? ?
Clara akasema kwa hali ya kukata
tamaa.Nilihisi kuchanganyikiwa.
Clara akavuta pumzi ndefu akaenda kukaa
kitandani,akainama na kujishika kichwa kwa
mikono yake miwili.Sikuelewa alikuwa akiwaza
kitu gani lakini ni wazi alikuwa katika hali ya
kukata tamaa.Aliumizwa mno na maneno
niliyomwambia.Nilimtazama kwa makini
huruma ikaniingia.Clara alikuwa akiishi
maisha yake kwa raha mustarehe na hakuwa
na matatizo .Aliogopa kuingia katika
mahusiano tena baada ya kutendwa katika
uhusiano wake wa awali.Japokuwa hajawahi
kunieleza ni kitu gani kilimtokea hapo kabla
kiasi cha kumfanya awachukie wanaume lakini
ni wazi kitu alichofanyiwa kilimuumiza sana
kiasi cha kumfanya awachukie wanaume wote
.Baada ya miaka kadhaa kupita ameamua
kumuamini na kumpa mwanaume mwingine
nafasi katika moyo wake,mwanaume huyo ni
mimi.Siku mbili tu tangu awe na mimi
amekutana na mambo ambayo yametonesha
donda lililokwisha pona muda mrefu.Clara
amejikuta akiuumiza tena moyo wake.Jana
nilituhumiwa kumchukua mtoto Baraka bila
ridhaa ya wazazi wake kitu kilichopelekea
kushikiliwa na polisi kwa masaa kadhaa
tukihojiwa.Kutokana na sakata hilo Clara
aliahirisha safari yake ya muhimu sana.Leo
hii limeibuka tena jambo jingine
jipya.Sikuhitaji kumuumiza Clara namna ile
lakini sikuwa na namna nyingine ya kufanya
zaidi ya kumueleza ukweli.Sikuona umuhimu
wa kumficha kitu kwa sababu hata kama
ningeficha ingekuja kufahamika tu.
 
Mkuu una sehemu zote?? Naogopa kuanza kuisoma halafu baadae naishia njiani
 
SEHEMU YA 16
MTUNZI:pATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Clara akavuta pumzi ndefu akaenda kukaa
kitandani,akainama na kujishika kichwa kwa
mikono yake miwili.Sikuelewa alikuwa akiwaza
kitu gani lakini ni wazi alikuwa katika hali ya
kukata tamaa.Aliumizwa mno na maneno
niliyomwambia.Nilimtazama kwa makini
huruma ikaniingia.Clara alikuwa akiishi
maisha yake kwa raha mustarehe na hakuwa
na matatizo .Aliogopa kuingia katika
mahusiano tena baada ya kutendwa katika
uhusiano wake wa awali.Japokuwa hajawahi
kunieleza ni kitu gani kilimtokea hapo kabla
kiasi cha kumfanya awachukie wanaume lakini
ni wazi kitu alichofanyiwa kilimuumiza sana
kiasi cha kumfanya awachukie wanaume wote
.Baada ya miaka kadhaa kupita ameamua
kumuamini na kumpa mwanaume mwingine
nafasi katika moyo wake,mwanaume huyo ni
mimi.Siku mbili tu tangu awe na mimi
amekutana na mambo ambayo yametonesha
donda lililokwisha pona muda mrefu.Clara
amejikuta akiuumiza tena moyo wake.Jana
nilituhumiwa kumchukua mtoto Baraka bila
ridhaa ya wazazi wake kitu kilichopelekea
kushikiliwa na polisi kwa masaa kadhaa
tukihojiwa.Kutokana na sakata hilo Clara
aliahirisha safari yake ya muhimu sana.Leo
hii limeibuka tena jambo jingine
jipya.Sikuhitaji kumuumiza Clara namna ile
lakini sikuwa na namna nyingine ya kufanya
zaidi ya kumueleza ukweli.Sikuona umuhimu
wa kumficha kitu kwa sababu hata kama
ningeficha ingekuja kufahamika tu.
ENDELEA????????..
Clara alikuwa akitoa machozi na kwa mbali
nilisikia kilio cha chini chini.Nafikiri alikuwa
akilia kwa mambo niliyoyafanya kwa sababu
ni kinyume kabisa cha maadili ya mfanyakazi
wa umma.Niliiba fedha ya serikali ambayo ni
kodi za wananchi.Fedha zile nyingi zingeweza
kutumika katika miradi ya maendeleo kama
zahanati na kununua vifaa vya shule n.k. Kwa
mara ya kwanza nilihisi uchungu kwa kuliibia
taifa namna ile.Nilisikia uchungu mkubwa
moyoni.Kingine nilichohisi kinamliza Clara ni
namna jina lake litakavyochafuka.Clara ni mtu
mwenye jina na heshima kubwa sana katika
jamii kwa hiyo kitendo cha Emmy kulipeka
suala lile mbele ya sheria na yeye kuonekana
nami ni wazi kingelichafua jina lake zuri lenye
heshima kubwa ndani na nje ya nchi.Roho
iliniuma nikamuonea huruma mrembo yule
aliyekuwa ameketi kitandani akilia kwa
kwikwi.
?Kama ni kuchafuka ni bora nichafuke mimi
na Clara abaki na heshima yake .Kwa mambo
niliyoyafanya sistahili kuwa karibu na mtu
kama Clara.Itakuwa vizuri kama nikibaki
mwenyewe na kuendelea kuubeba msalaba
wangu mwenyewe.? Nikawaza na kuanza
kupiga hatua za taratibu na kumsogelea
Clara.Nilikuwa na wasi wasi mwingi ni jinsi
gani ningeweza kuongea naye .Kwa sasa
sikutegemea kama angetaka hata kuzungumza
nami.Nikajikaza na kumshika bega.
?Clara ? Nikamuita taratibu akainua uso wake
uliokuwa umelowa machozi.Nikamtazama
nikasikia uchungu mwingi .Nilimuahidi Clara
kwamba sintamliza lakini leo hii uso wake
umelowa machozi kwa sababu yangu.
?Clara najua sistahili hata kuongea na wewe
tena lakini tafadhali naomba unisikilize japo
kwa dakika chache ? Nikasema na kutulia
kidogo,nikamtazama Clara aliyekuwa ametulia
kimya .
?Clara nakumbuka nilikuahidi kwamba
sintathubutu hata siku moja kukutoa chozi na
wala kuumiza moyo wako. Ahadi niliyokupa
nimeshindwa kuitimiza na tazama sasa hivi
uso wako umejaa machozi,na moyo wako
umeumia kwa sababu yangu.Nimesikia
uchungu sana kukuona ukitoa machozi kwa
jambo ulilolisikia.Kwa mara ya kwanza
ninajutia kitu nilichokifanya.Chozi lako
ulilomwaga limenifanya nisikie uchungu
mwingi na kuuona ujinga nilioufanya.Kitu
nilichokifanya nitakijutia katika maisha yangu
yote yaliyobaki kwa sababu kimenifanya
nikampoteza mwanamke niliyempenda kwa
moyo wangu wote.?
Clara akaonyesha mstuko baada ya kutamka
maneno yale ya mwisho.
? Clara narudia tena kukiri kwamba nilifanya
kosa kubwa sana kuchukua fedha zile za
serikali ambazo ni kodi na majasho ya
wanachi wanyonge. Fedha ile ingeweza
kufanya shughuli mbali mbali za maendeleo
.Chozi ulilolimwaga limenifanya nitambue
kosa langu.Ninastahili kufikishwa mbele ya
sheria na kupata adhabu.Ni kweli ninastahili
adhabu kwa kosa hili.Clara wewe ni mtu safi
uliyezitumia nguvu na vipaji vyako hadi
ukafika hapa ulipo sasa hivi.Jina lako ni
kubwa na heshima yako katika jamii ni kubwa
sana.Siko tayari kuona jina lako likichafuliwa
kwa sababu yangu.Japokuwa inaniuma
kusema lakini ni lazima niseme kwamba
kutokana na hali halisi ilivyo siko tayari
kuyakubali matakwa ya Emmy.Siko tayari
kumpatia kiasi hicho cha pesa
anachokitaka.Kama alivyokuwa ametishia
kwamba endapo nisipotimiza matakwa yake ni
lazima atanifikisha katika vyombo vya
sheria.Niko tayari kwa hilo..Kwa mambo
niliyoyafanya napenda kukiri kwamba sistahili
kuwa na mtu kama wewe.Ninaomba uhusiano
wetu Clara uishie hapa ili niweze kuyakabili
mambo haya mimi mwenyewe bila
kumuhusisha mtu yeyote .Hii itakuwa njia
pekee ya kukuepusha na aibu hii kubwa na
kulilinda jina lako safi.? Nikasema na kutulia
kidogo.Clara akafuta machozi na kunitazama
kisha akanivuta mkono na kunifanyia ishara
niketi kitandani.
?Wayne tafadhali usiseme hivyo.Ukisema
hivyo unazidi kunifanya niumie zaidi ?Clara
akasema
? Inaniuma kusema hivyo Clara lakini huo ndio
ukweli halisi ambao lazima tuukubali siko
tayari kuona jina lako likichafuka kwa ufisadi
nilioufanya..Ninastahili kuubeba msalaba
wangu mwenyewe?
?Wayne naomba unisikilize.? Akasema Clara
na kuinama chini kidogo akatafakari.
?Ni kweli nimeumia sana.Siwezi kuelezea ni
kwa kiasi gani lakini nimeumia mno.Ni muda
mfupi sana tumekuwa pamoja lakini kwa
muda huu mfupi yameanza kujitokeza mambo
ambayo yamesababisha uhusiano wetu
kutetereka.Wayne siku zote nilikuwa nikikwepa
kujiingiza katika mahusiano kwa kuogopa
kuumiza moyo wangu kwa mara nyingne
tena.Pamoja na yote yaliyotokea lakini
kuachana si suluhisho.Haya yote ni majaribu
ambayo hatuna budi kuyashinda.Mimi siwezi
kukuacha hata uniambie kitu gani.Tayari
nimekwisha ufungua moyo wangu na
kuuruhusu upende tena kwa hiyo siwezi kurudi
nyuma.Niko tayari kusimama na wewe katika
sakata hili.Sintajali kama jina langu
litachafuka ama la.Ninachokijua ni kwamba
niko na wewe na moyo wangu unahitaji kuwa
na wewe pekee.kwa hiyo sahau suala la
kuachana kwa sababu siyo suluhisho la tatizo
hili.Nikikuacha leo hii mimi ndiye
nitakayeumia zaidi .? Clara akasema na
kunivuta kwake ,akanikumbatia halafu
akaniachia na kusema
?Pamoja na yote uliyoyafanya Wayne lakini
bado hayanizuii mimi kukupenda au kuwa na
wewe.Wote tunafanya makosa katika maisha
yetu na tujapogundua baadae makosa
tuliyoyafanya huwa tayari tumeshachelewa.
Wayne nafurahi kama umeligundua kosa lako
na kulijutia.Kinachotakiwa kwa sasa ni
kuangalia namna tutakavyoweza kulimaliza
suala hili? Clara akasema.Nikamtazama
mrembo yule na kumwambia
?Kuna jambo nimekuwa nikilifikiria pengine
labda linaweza likasaidia ili suala hili libaki
kama lilivyo?
?jambo gani hilo Wayne? Clara akauliza
?nafikiria kukubaliana na matakwa ya Emmy.?
Nikasema na kumfanya Clara astuke
?Yaani kumpatia Emmy pesa zote kama
alivyotaka?
?Ndiyo Clara.Nadhani hii itakuwa njia pekee
itakayomfanya anyamaze na asilipeleke suala
hili katika vyombo vya usalama?
?Wayne hapana.Huwezi fanya hivyo.Hutakiwi
kukubaliana na matakwa ya Emmy.Kukubali
anachokitaka kutaonyesha ni jinsi gani ulivyo
dhaifu na atautumia udhaifu huo kukufanyia
kila aina ya vituko.Leo atataka ufanye
hiki,kesho atakuambia ufanye kile.Usikubali
kamwe kumpa hiyo nafasi.Unachotakiwa
kukifanya ni kumpigia simu na kumtaarfu
kwamba hauko tayari kukubaliana na vitisho
vyake na kwamba hutampatia hata senti moja
katika zile fedha.Muonyeshe kwamba uko
imara na hauko tayari kuyumbishwa na kama
anataka kupeleka nyaraka hizo katika vyombo
vya kisheria mpe ruhusa afanye hivyo.? Clara
akasema na kunifanya nizidi kumshangaa.
?Unashangaa nini Wayne? Chukua simu na
umpigie sasa hivi na umweleze hayo
niliyokwambia halafu nitakueleza nini
kitafuata.? Nikachukua simu na kupiga namba
zile alizonipigia Emmy.
?hallo Wayne.Mbona umenipigia simu
mapema namna hii? Umeshanitumia hizo
fedha kama nilivyokuambia? Akasema Emmy
baada ya kupokea simu.
?Emmy tafadhali naomba unisikilize?
Nikasema huku uso wangu umekasirika.
?Nakusikiliza Wayne? Akasema Emmy
?Nimekupigia simu kukuonya kwamba iwe ni
mwanzo na mwisho kunipigia simu na kunipa
amri.Naomba ufahamu kwamba siko tayari
kuendeshwa na mwanamke mwenye upeo
finyu kama wewe.Ninakupa masaa kumi na
mbili ,nyaraka zote ulizoziiba hapa nyumbani
kwangu ziwe zimerudi na kama hutatekeleza
utanitambua mimi ni nani.Nimechoshwa nawe
Emmy...? Nikasema kwa ukali.Emmy akacheka
na kusema
?Wayne,kumbe kuna nyakati huwa unakuwa
jasiri namna hii? Hahahaaa nafurahi kuona
huyo mwanamitindo wako anakupa ujasiri wa
namna hiyo.Mpe salamu zangu .Na wewe kwa
kuwa umeonyesha kiburi basi naomba
tupambane mimi na wewe na tuone ni nani
atakayechukua ushindi.Bado nakusisitizia
kwamba masaa ishirini na manne yakipita
bila fedha niliyokwambia kuingia katika
akaunti yangu basi ujue kwamba mwisho
wako utakuwa ni gerezani na pesa yote
nitabaki naimiliki mimi.Kwa hiyo wakati bado
una nafasi tafadhali fanya vile
nilivyokuamuru.Jambo la mwisho nakuomba
usinipigie simu kama huna kitu cha maana
cha kuniambia.? Emmy akasema kwa jeuri na
kukata simu
Nilipandwa na hasira kasi kwamba kama
angekuwa karibu ningemshushia kipigo
kikali.Nilikuwa nikihema mfululizo kwa hasira
nilizokuwa nazo.Sikuelewa sababu ya Emmy
kuwa na uadui mkubwa na mimi kiasi kile.
?You did great? akasema Clara huku akinipiga
piga mgongoni
?Kwa sasa hata yeye atakuwa akijiuliza ni kwa
nini umekuwa jasiri namna ile.Hata kama
alikuwa na wazo la kwenda katika vyombo vya
sheria itambidi ajiulize mara mbili.?
?Clara nina wasi wasi baradhuli huyu anaweza
akakusababishia matatizo makubwa.?
?Usijali kuhusu hilo Wayne kwa sababu huyu
mtalaka wako anaonekana bado ana akili za
kitoto na haniwezi mtu kama mimi.Sasa
sikiliza Wayne.Mimi nitakusaidia katika
kulitatua tatizo hili kwa sababu bado liko
ndani ya uwezo wangu kulimaliza.Nitalimaliza
suala hili lakini naomba unipe ahadi kwamba
baada kumalizika hautajihusisha tena na
masuala ya uhujumu wa uchumi wala aina
yopyote ya ufujaji wa fedha za umma au
kujipatia fedha kwa njia isiyo halali.?
?Clara ninajutia kosa nililolifanya na ninataka
kuyabadili maisha yangu na kuishi maisha
mazuri ya kujitafutia fedha za halali.?
Nikasema na kumfanya Clara atabasamu
?Nafurahi kusikia hivyo.Kwa sababu
nakupenda nimeamua kulibeba mimi suala
hili.Mpango mzima utasomeka kwamba mimi
na wewe ni washirika wa kibiashara toka
muda mrefu na una kiasi Fulani cha hisa
katika kampuni yangu ya mavazi kwa hiyo
fedha zile zilitoka katika kampuni
yangu.Nitawasiliana na wahasibu wa kampuni
yangu ili waandae nyaraka ambazo
zitakuonyesha kwamba wewe ni mshirika
wangu kibiashara na kwamba kwa nyakati
tofauti ulipokea fedha toka katika kampuni
yangu.Vile vile nitawaelekeza waingize leo
kiasi fulani cha pesa katika akaunti yako
yenye fedha anazozitaka Emmy ili ionekane ni
kweli umekuwa unapokea fedha toka kampuni
yetu.Kokote atakakokwenda Emmy ataonekana
mwongo na tutamtaka athibitishe hilo
analolisema na itakuwa ni aibu kubwa kwake.?
?Ouh Clara sijui hata nikushuruje kwa msaada
huu mkubwa unaonisaidia.? Nikasema huku
nikimkumbatia
?Bado sijamaliza Wayne.Kuna jambo ambalo
ninataka kuliweka sawa.Nina uhakika suala
hili litamalizika kwa sababu litasimamiwa na
wanasheria wangu ambao ni wanasheria
wakubwa na wenye uzoefu .Baada ya suala
hili kumalizika nitakuwa nimeingia katika
dhambi kubwa.Nimeshiriki katika kufunika
uovu.Kwa maana hiyo sintakuwa na amani
daima.Ninachotaka kukisema hapa ni kwamba
fedha ile yote uliyoichukua inabidi tuirudishe
kwenye jamii. Sina maana ya kufanya
mkutano na waandishi wa habari na kusema
kwamba ulichukua fedha za serikali na
unataka kuzirudisha bali tutazitumia katika
mradi wowote wa maendeleo.Tunaweza
tukazitumia fedha hizo kujenga darasa au
kuchimba kisima cha maji katika sehemu
ambayo kuna shida ya maji au kununua
vitabu mashuleni ili mradi tufanye kitu
chochote chenye faida kwa jamii kupitia fedha
ile.Iwapo utakubaliana nami kuhusu suala hilo
nitaamini kwamba ni kweli unajutia kosa lako
na kwamba una lengo la dhati la kubadilika
na kuanza kuishi maisha mapya kabisa .Je
uko tayari kwa hilo? Clara akauliza
Lilikuwa ni swali gumu sana kulijbu kwa
haraka. Nikatafakari kwa sekunde chache ili
nione nitamjibu nini. Ni kweli nilikuwa na
mamilioni ya fedha ambazo zote zilitokana na
ufisadi tulioufanya mimi na wenzangu kwa
fedha ya walipa kodi wa Tanzania.Swali lile
lilikuwa ni mtego wa mimi kuchagua ama
fedha ama clara.Kwa sasa Clara ndiye
aliyekuwa kila kitu kwangu .Fedha zote
nilizokuwa nazo hazitakuwa na maana kama
nitaikosa furaha hii ya maisha
yangu.Nikakata shauri ni bora nikose fedha
lakini niwe na Clara.
?Clara nashukuru sana kwa kukutana nawe
kwani ni wewe pekee ambaye umenifanya
nifahamu nini nimefanya na nini ninapaswa
kufanya .Nimejifunza kitu kikubwa sana toka
kwako.Kwa moyo wote nakuahidi kwamba
baada ya mambo haya yote kuisha fedha zile
zote tutazirudisha kwa wananchi.? Nikasema
na kumfanya Clara atabasamu ,akanikumbatia
?Nimefurahi sana kusikia hivyo Wayne.Basi
usiumize kichwa tena na huyu kichaa Emmy
.Vaa nguo zako tutoke na kuendelea na siku
yetu kama tulivyokuwa tumepanga.Wakati
ukijiandaa naomba niitumie nafasi hii
kuwasiliana na watu wa kampuni yangu
pamoja na wanasheria ili waanze
kulishughulikia suala hili haraka.? Clara
akasema akanibusu na kutoka mle
chumbani.Nilibaki nimesimama kwa dakika
tatu nikitafakari kisha nikaanza kuvaa nguo
tayari kwa kutoka.Baada ya muda Clara
akaingia tena chumbani.
?Kuwa na amani mpenzi wangu,usiumizwe
kichwa na Emmy.Mimi nimeamua kulisimamia
suala hili na litakwisha.Naomba uniamini.?
Clara akaniambia huku akilirekebisha shati
nililokuwa nimevaa.
?Clara sioni hata nitamke neno gani
kukushukuru kwa namna ulivyoamua
kunisaidia katika suala hili.Nina deni kubwa
ambalo ninahitaji kukulipa? nikasema na
kumfanya Clara atabasamu ,akanisogelea
karibu zaidi akanibusu.
?Wayne ni kweli una deni kwangu na
nitakuomba unilipe kitu kimoja tu?
?Clara niko tayari kukulipa kitu chochote kile
utakachoomba.Niambie unahitaji kitu gani na
sinta sita kukupatia.Niko tayari kufika hadi
pembe ya mwisho wa dunia kwa ajili ya
kukutafutia kitu unachokihitaji.Niambie
tafadhali unataka nikulipe nini?
Clara akanitazama kwa macho yake mazuri na
kunifanya nisisimkwe mwili
?Una uhakika utanipatia ninachokihitaji?
Akauliza Clara
?Nina uhakika Clara.Nitakupatia chochote kile
unachokihitaji.? Nikajibu kwa kujiamini
?nafurahi kusikia hivyo Wayne.Kitu
ninachotaka toka kwako ni kidogo sana na
ambacho hakikulazimu kwenda hadi mwisho
wa dunia kukipata.Ninachohitaji ni nafasi
ndani ya moyo wako.?
Nikamuangalia Clara na kutabasamu baada
ya kutamka vile.Nikamvuta karibu yangu zaidi
nikamuangalia usoni na kumwambia.
?Clara huna haja ya kuomba nafasi ndani ya
moyo wangu.Toka siku nimezaliwa tayari
nafasi yako ilikwisha wekwa moyoni
mwangu.Moyo wangu umejazwa na sura yako
pekee.hakuna tena mwanamke mwingine
anayeweza kuipata nafasi hii iliyojazwa
nawe.Mapenzi yangu yote yameishia kwako
pekee Sina mapenzi tena kwa mwanamke
mwingine .? Nikasema na kumbusu Clara
ambaye alikilaza kichwa chake kifuani kwangu
na kunikumbatia kwa mahaba mazito.
?Wayne naomba uelewe kwamba ninakupenda
kuliko kitu chochote katika dunia hii.Wewe
ndiye kila kitu kwangu.tafadhali nahitaji
nafasi ya kudumu ndani ya moyo
wako.Nataka uwe wangu peke yangu.Nahitaji
muda wako uliobakia wa kuishi hapa duniani
uumalize ukiwa na mimi.Nataka tuishi
pamoja,nataka tuzae watoto na kutengeneza
familia yenye furaha na upendo.Nnakuhitaji
Wayne katika maisha yangu? Mrembo huyu
adhimu alikuwa akiongea toka nani kabisa
mwa moyo wake.Ni kweli alikuwa akinipenda
na hata mimi nilikuwa nikimpenda kupita
kiasi.Nilijilaumu sana kwa kupoteza muda
mwingi kwa mtu kama Emmy mwanamke asiye
na shukrani ambaye katika kipindi cha maisha
niliyoishi naye amenisababishai maumivu
ambayo naweza kusema ni zaidi ya maumivu
ya kawaida.
?Clara my angel.Nakuhakikishia kwamba wewe
ni wangu pekee,na mimi niwako pekee.Sijui
nitampa nini Mungu kama shukrani zangu
kwake kwa kuniletea furaha hii kubwa ya
maisha yangu.Amenirudishia furaha ya
maisha iliyokwisha toweka.Clara nitakupenda
milele na milele na ninakuahidi kwamba
hakuna mtu yeyote katika dunia hii
atakayeweza kututenganisha.Ni kifo pekee
kitakachoweza kututengansiaha mimi na
wewe.Nitaishi nawe na kukupenda hadi katika
pumzi yangu ya mwisho ? maneno yale
yakamfanya Clara ashindwe kujizuia
kudondosha machozi.
?tafadhali usilie Clara.Huu ni wakati wa
kufurahi na si wakati wa kudondosha
machozi? nikamwambia huku nikimfuta
machozi
?Wayne ninalia kutokana na furaha
niliyonayo.Nimekaa miaka mingi nikijihisi ni
mwenye furaha lakini sikuwahi hata mara
moja kuipata furaha kubwa kama niipatayo
sasa kwa kuwa nawe.Ni wewe ndiye uliyenipa
furaha hii kubwa maishani.? Akasema
Clara.na kuniangalia usoni.
?Darling twende tukaendelee na ratiba yetu ya
siku.Tuna kila sababu ya kufurahi? Tukatoka
na kuingia garini tukaelekea eneo la meserani
ambako kuna hifadhi ya nyoka.Mimi si mpenzi
kabisa wa nyoka na ni moja kati ya vitu
ninavyoviogopa sana katika hii dunia lakini
niliamua kwenda huko kwa sababu Clara
alipenda kwenda kutazama nyoka wa aina
mbali mbali wanaofugwa.Amekuwa akisikia
hifadhi hii ya nyoka na alipanga siku moja
aitembelee na sasa ameipata nafasi hiyo
hakutaka kuipoteza.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO?????
 
Back
Top Bottom