Wanasiasa ndio kundi la kwanza kwa ubinafsi na wasio na huruma na upande mwingine

conductor

JF-Expert Member
May 29, 2013
718
569
Kadri umri wa mwanadamu unavyosogea mbele ndivyo uona kasoro nyingi ambazo ama anazijutia mwenyewe au anamuonea Huruma aliyeko kwenye msimu huo.

Kiwango cha hatari ambacho mwanasiasa yeyote ujitwika nje ya pazia ni kubwa kiasi kwamba kisaikilojia hana tena kitu cha kumtisha katika ulimwengu wake mpaka pale majibu ya risk alizozibeba wakati ule zitakapomletea madhara ya afya kama pressure, kisukari, msongo wa mawazo au sonona.

Siasa ni Ajira iliyobeba tabia za laana maana Uongo ni kielelezo cha kuonekana mwanasiasa na huku ukijua unachosema unamdhuru binadamu mwenzako ila kwasababu we na ukoo wako au familia yako wataishi salama unasahau hawataishi milele (Mtu Pesa-Banza Stone).

Mtaji wa mwanasiasa ni kupata wale wasio na uwezo wa kuhoji au kundi lililofundishwa kutii sheria kwanza halafu kujitetea badae (wale tuliosoma seminar tunajua padre akikupa adhabu basi hata Padre mwingine akikuondoa unafukuzwa wewe bila utetezi) Majeshi na Polisi hii tabia ipo.

Si njia nzuri kama itatumika pasipo pahala pake. Kwanza mwanasiasa anajua kabisa:

1. Ni mnafiki
2. Dikiteta
3. Muongo
4. Na hana nia njema na wenzie.

Ila atatumia njia ya:

1. Udhaifu wa jamii yake kuonekana mwema na ana nia njema

Ukitaka kufanya biashara baadhi ya nchi za Ulaya na Marekani ukishaonyesha kuna mkono wa mwanasiasa kwenye proposal yako, kuna mawili wataangalia wanafaidikaje kwa muda mfupi nawe ila hawatakaa nawe muda watakufukuza kwani wanajua unaendesha mambo kwa mhemko wa upepo wa kusiasa. Mwana siasa haoni aibu kukupangia mshahara anajua hutofika week mbili bado upo alafu yeye anajipangia mshahara wa miezi mitatu ndani ya mwezi mmoja.

Mwanasiasa anaweza kuharibu mfumo mzima uliobora wa nchi yake kisa tu aneemeshe watoto wake, Yuko tayari aingie mkataba feki ilimradi tu kama huo mkataba hautadhuru familia yake.

Duniani Hamna mwizi kutoka mbali ya mji wako akaja kuiba bila connection ya mwenyeji. Katika uwekezaji wa nchi mdhamini namba moja ni mwanasiasa, sasa shida inakuja mwanasiasa ana elimu gani katika huo mradi, kuna tabia mbaya nilioona kwenye miradi unayotaka kuingia na Muhindi kama anataka akuwin kwa kukurubuni anakuita maeneo anayoyamumudu yeye alafu anakufanyia round table na wale woote ambao hutoweza ku-argue nao.

Na atakuelezea faidi tu za uongo na kweli ili ukubari mkataba wake basi umeisha, hii mbinu ndo ya mwanasisa.

Mwanasiasa yuko tayari kuwekeza kwenye kundi lililodhaifu ili adhoofishe wengine yeye asonge mbele (chawa), ila sijawahi ona kampuni binafsi inaajiri au ina nia ya nikuajiri mtu aliye dhaifu katika field yake, kampuni binafsi ndo sekta inatamani kuwa na wafanyakaz wanomzidi uzoefu na akiri, ndio maana mwanasiasa ukioona anadhoifisha elimu ya nchi yake kwa kutoa baadhi ya msingi, jua kabisa ana hatarisha ata Muwekezaji kuja na watu wake na akaacha wazawa.

Leo hii vyuo vinalalamikiwa kutoa wanafunz wasiokidhi hata challenge ya kujieleza pale mpakani Namanga huyo ataweza visiki vya strong paper ya njia bora yakupata umeme wa uhakika nakuwapa IMF kutoa pesa,huyo ataweza kupambana na negotiation za mhindi aingize dawa yenye kiwango kidogo cha kutibu ugonjwa, huyo ataweza kupamba na nijeria inayopambana na Ajira za bill gate?

Nguvu imeelekezwa Sana kupofusha elimu ili mwanasiasa apite, Motivation speakers watatokea kwenye misiba kumuongelea aliyekosa vigezo huko jikoni Leo unapambana kwanini? Hiyo ndio siasa, kama kuna taaluma inabidi inyimwe ufadhiri ni kusomea political science, ila mwanasiasa anasema hutopata mikopo kama utapata admission ya ustawi wa JAMII, ualimu na history.

Laiti jamii ingepata upeo wa nafasi ya mwanasiasa na namna anavyoweza kusaliti maendeleo ya jamii flani, basi watafiti wangebuni namna bora yakumkwepa mwanasiasa, yaani "Pure segregation" minimise attention to them" wengi si watu wanaojifunza utu.

Unawezaje kujimilikisha Mali ambayo hutoweza kuitumia ardh, pesa, kila deal umo Tu, bandle imekuwa shida bei kila siku inapanda ukichunguza ama kuna kanjubai au mwanasiasa, nauli kila siku juu, ukija kuchunguza mabasi maroli kuna mwanasiasa au kanjubai deal, sasa mchina kaingia mjini mbinu zake anaami hata kupiga mzawa Kofi (dharau kubwa Sana)kwao huwez fanya na kwakuwa Mchina kakuajiri ana anakiburi cha mwanasiasa hutofurukuta.

Neno Uzalendo vyuoni vimelifuta kiasi kwamba hata maisha ya debate yamekufa, Mwalimu mwenyewe akijifanya mjuaji huku anaishi nyumba ya chuo kesho wanamuondoa akasote mitaani apambane na madaladala kwenda kazini, unapewa cheo kwa kiwango chako kikubwa cha kuwa CHAWA na kufunika upuuzi sio weredi.

Nchi zilioendelea zimetenga Biashara na Siasa, je nchi yako iko upande gani.
Mwanasiasa ndo anaweza kustaafu kazi kwa mujibu wa katiba analipwa mafao yake anastaafu , kwasababu uwezo wake kitaalam umechoka alafu anaingia jimbon kutafuta ubunge ili awongoze wale VIPANGA waliorithi nafasi yake iliyoonekana apumzishwe, (why wakati mfumo unaonyesha hutoshi tena) hiyo ndo tabia ya mwanasiasa.
Kigezo cha kustaafu hakimuhusu mwanasiasa ndo ubinafsi mwenyewe.
Hivi miiko ya MAJAJI nitofauti?, sijawahi sikia jaji mstaafu anakuwa Mbunge, Kama kweli tuige WASOMI hao kwa KURIDHIKA.
 

Attachments

  • image_66a6fe81-800e-41ed-b63e-603093f8fa3820231010_112041.jpg
    image_66a6fe81-800e-41ed-b63e-603093f8fa3820231010_112041.jpg
    60.4 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1708429492203.jpg
    FB_IMG_1708429492203.jpg
    92.9 KB · Views: 1
Back
Top Bottom