Masikini kaka huyu


Hata Mimi nahisi hivi
 
Duuhh kazi kweli kweli, wakati mwingine mimi Huwa naamini hakuna ulevi mbaya kama DINI (mnisamehe kwa hili). Maana humwondolea mtu uwezo wa kufikiri kwa mantiki. Kwa hali ilivyo bora waachane (japo wengine huamini alichokiunganisha Mungu.....)

Umeongea kweli tupu
 
Si ndo maana mimi nimegoma kutafuta mchumba ndan ya makanisa ya kilokole,maana wanawake wengi walioko kule ni wale waliostaafu ukahaba,waliostaafu kuua kwa kutoa mimba...awashirikishe washenga na wazee

Aiseee
 
Mwambie arudi huko alipofunga ndoa ambako hata hawaku-bother kuwauliza vyeti vya clearance ya HIV status...

Hao ndio wampe ushauri wa nini cha kufanya...
 
wakati napokea hizi taarifa nilipata shida mnoo kwwa jinsi kijana alivyokuwa anamwamini mkewe

ndio maana kuna semi nyingi zinazopinga uaminifu wa wanawake, sidhani kama binti alikuwa hafaham afya yake au alikuwa ana mahusiano na kidumu chake angali bado yupo na mme mtarajiwa.
 
Huyo mwanamke ana hila

Atalazimishaje ngono bila kondom???

Ila mwanaume nae kiazi.... msimamo wake wa kiume uko wapi???
 
nimeamini hakuna kiumbe kipole duniani nikikumbuka binti alivyokuwa kapole na mstaarabu lakini leo kawa kama mbogo
Mkuu miss chagga hebu nifafanulie kwanza haya maswali yangu. Tatizo hili zito la wanandoa wamekuambia wakiwa wote wawili au unapata maelezo ya upande mmoja,yaani kwa huyo kaka rafiki?? Je! Majibu ya kaka yako umeyathibitisha au anakueleza mwenyewe!? Ukinijibu ntarudi kutoa ushauri.
 
Last edited by a moderator:


Watz bana. Kila kitu kinatafsiriwa kama unyanyapaa..nikisema walioathirika watoe shuhuda zao mtasema nanyanyapaa...
 
Aendelee kusubiri muujiza wa yeye kuambukizwa vvu!! Maana kuna mambo mengine inabidi kujiongeza na siyo kusubiri ushauri!!
 

Waachane kisheria usichezeee ngoma wajameni
 
Duuh! Huyu jamaa sidhani hata kama akiamua kufanya ule mchezo wa baba na mama dude yake itasimama. Hapo ni kama keshapigwa ganzi kisaikolojia.
 
Ukweli hali kama hii inauma sana. Waende kwa kiongizi wao wa kiroho kupata ushauri, pia wazazi wa pande zote mbili nao wahisishwe ili washiriki ktk kuamua.

Miss Chagga, mpe pole nyingi jamaa pia mke wake.
 
Inaonekana alikua hasugui sana. Aendelee aste aste tu.
ila mbona ni sababu tosha kuachana maana ni ushahidi wife alipira diversion.
 
walishauriwa na moja ya njia ni kutumia kinga binti hataki hilo swala la kinga anasema ni dhambi

He! ati kutumia kinga ni dhambi?? mbona walikuwa wanatumia kabla hawajaoana?? Ilikuwa si dhambi walipokuwa wanazuia nazo mimba ila sasa kuzuia VVU ishakuwa dhambi? Haki ya nani kuna mitihani mingine unaweza kufikiri uko ndotoni! Huyo mke hata kumshambulia naogopa maana sipati picha ndo ingekuwa mimi. Huku una VVU, huku una mshtuko, una huzuni, mtu unayemtegemea akufariji anakukimbia... kwa ufupi bidada yuko kwenye "denial" ndo maana hata anadai mngonoko kama kawa tena bila kinga. Na mantiki yake ni kuwa kama wameshangonoka mwaka mzima bila condom leo maambukizi yatatoka wapi? Kijana nae ana mshtuko. Mi ningemshauri asilale sebuleni. Alale kitanda kimoja na mkewe, tena amkumbatie kabisa maana tatizo la mke ni kubwa kuliko la mume. Huyu dada pamoja na VVU pia ni mjamzito. Hatakiwi kuachwa kulia lia hovyo na kukosa matumaini. Kama wanamjua Mungu basi wanajua hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea. Kaka aache kuhukumu maana hakuna ajuaye mke amepataje VVU. Kokote alikopata, sasa wapo wote ndani, ni mkewe, ndo mama mtoto hivyo. Watulie sana, mi naamini watapata suluhisho pengine hata la kuendelea kuishi pamoja na kungonoka na kuendelea kuzaa. Wakipata suluhisho la kutengana basi nalo liwe la heri limuache kila mmoja akiwa na mzigo mwepesi. Mwambie akae kimya kwa sasa, watafakari wenyewe maana hawawezi kuendelea kuchachawa kama maharage yanayochemka. Ifike mahali watulie waongee na habari ya "Uliutoa wapi" isiwepo labda mwanamke mwenyewe aamue kufunguka kama anajua. Namaanisha maongezi yasiwe ya lawama bali ya kutafuta suluhisho. Huyo Mungu wao wakimrudia na kutubu ni mwaminifu, atawapa nguvu ya kuvumilia na atawapa hekima ya kulimaliza hili jambo. Amen.
 

Kuna mtu ananiuliza hapa kwamba huwezi kuongeza herufi moja kwenye hiyo kaka isomeke kakaa ili umsaidie kijana mwenzio? Samahani lakini!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…