Mashujaa wa kweli Tanzania hawakumuogopa Hayati Dkt. Magufuli

Niwemugizi

Askofu Severine Niwemugizi

Kwa wale wasio mfahamu Askofu Severine Niwemugizi ni Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge-Ngara na ndiye aliyeongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dk John Magufuli nyumbani kwake chato Machi 26, 2021. Taarifa za Askofu Severine Niwemugizi kuhojiwa uraia wake zimekuwepo tangu mwaka 2017, kutokana na shauku na hamu ya umma ya kujua undani wa suala hilo Mwananchi Digital imefanya mahojiano maalum na Askofu Niwemugizi ofisini kwake mjini Ngara ambapo amefunguka mengi kuanzia alivyopata taarifa za kutakiwa kuhojiwa, kuanza kuhojiwa, kutwaliwa na kurejeshwa hati yake ya kusafiria.
 
9 Julai 2020

SHEIKH PONDA : ATAKA UCHAGUZI HURU NA WA HAKI

Sheikh Ponda Issa Ponda, katibu wa jumuiya hiyo leo tarehe 9 Julai 2020 jijini Dar es Salaam, umeitaka serikali kuhakikisha uchaguzi mkuu wa mwaka huu unakuwa huru na haki pia umuhimu wa kuwa na Katiba Mpya.

2 October 2020
Karagwe, Tanzania

UONGOZI BILA HARAKATI SIO UONGOZI ASEMA ASKOFU BENSON KALIKAWE BAGONZA

Mitano tena na Mitano kwanza. Aliyekwisha fanya afanyiwe uchambuzi na Anayeahidi apewe nafasi.

Viongozi watambue kuna maisha baada ya uchaguzi na hata baada ya kutumikia utawala fulani, hivyo watende haki isije kuwa wakajuta baada ya uchaguzi au kuwa nje ya mamlaka ya utawala.
 
9 Julai 2020

SHEIKH PONDA : ATAKA UCHAGUZI HURU NA WA HAKI

Sheikh Ponda Issa Ponda, katibu wa jumuiya hiyo leo tarehe 9 Julai 2020 jijini Dar es Salaam, umeitaka serikali kuhakikisha uchaguzi mkuu wa mwaka huu unakuwa huru na haki pia umuhimu wa kuwa na Katiba Mpya.

Mashujaa ndio hawa sasa. Sio mashujaa uchwara akina Jiwe na genge lake.
 
1,lissu alikimbia na kudai hana imani na usalama alio nao.

3,kibatala ni wakili msomi ambaye anasimamia taaruma yake pekee,labda ungesema kama nayeye ni mwanaisiasa au mwanaharakati.ndio sababu amekuwa si muhanga muda wote.ukichanganya siasa na taaluma umechagua usumbufu.

4,wale mashangazi wawili,inafahamika shida yao ya msingi ni njaa na ulafi wa vyeo.sasa kwa sababu ccm haihitaji watu wasio wavumilivu ndio sababu wameachwa waendelee kuropoka kama warevi,hakuna anayeshughulika nao.
 
Toka Mwaka 2015 mpaka March 17 2021 wanaume walibaki wawili tu,TUNDU ANT-PASS LISSU na JOHN POMBE MAGUFULI.
Mpaka sasa nina uhakika 100% Tundulissu akifa Leo itatuchukua miaka mingi Sana kuzaliwa mtu wa aina yake
Hata Magufuli atamkumbuka huko aliko😆😆😆

Hawa vidume kila mmoja alikuwa tayari kufa kwa kusimamia anachokiamini,bad luck dhaifu zaidi ndio kafariki!Ila hakika wameingia kwenye historia ya Tanzania.
 
Baadae alikwenda kujisalimisha mbele ya Mwendazake pale Ikulu. Hata gari yake haikuruhusiwa kuingia Ikulu. Akashukia mbali kwenye geti, akatembea, huku watu wa Mwendazake wakimpiga picha ya video ili kuitoa baadae kwenye vyombo vya habari kwa namna ya kumdalilisha akijifuta jasho!
Nape Nnauye watu wanamchukulia poa sana sababu yupo CCM, ila huyu kijana alionyesha ujasiri sana kumpinga mwendazake kipindi kile Makonda anavamia clouds, kupinga kunua wapinzani na utumiaji wa task force
 
Wanajamvi,

Kuna watu wanastahili nishani. Kukosa uoga kwao hakuelezeki. Wakati Mwendazake anafungwa watu, kuharibu biashara zao, kuwapakazia makosa yasiyokuwa na dhamana, na wengine kuuawa, hawa jamaa hawakunyaza kimya. Kilikuwa kipindi kigumu cha kuogopesha sana. Watu hawakuwa huru kuongelea serikali na siasa mbele ya watu wasiowafahamu. Hawa jamaa hawakuyumba. Hebu tuwataje:

1) Tundu Lissu - Kwa kifupi tu - Huyu alindamana kupinga udikteta. Alikuwa na jeuri ya kumwita Mwendazake dikteta uchwara. Alifunguliwa kesi zisizokuwa na mashiko. Alipigwa risasi 16 na Mungu akamponya. Baadae akaja kumpinga Mwendazake katika uchaguzi! Katika mazingira na hofu iliyojengwa na Mwendazake, huu ulikuwa ni ujasiri wa kupewa nishani.

2) Lawrence Mafuru - Huyu alikuwa ni Managing Director wa NBC Bank na baadae Msajili wa Hazina. Alikuwa na hali nzuri tu ya maisha na angeweza kunyamaza tu akaendelea na maisha bila bughudha. Wakati Mwendazake anatimua timua watu waliokuwa wanapingana naye, Mafuru alidiriki kupingana na Mwendazake mchana kweupe kwenye TV wakati akijua wazi kuwa atapoteza kazi yake. Mwendazake aliwashutumu watu wa benki kuwa wanweka fedha za serikali katika fixed deposit the kulamba faida kwa manufaa yao. Mafuru akiwa Clouds 360, alimpinga Mwendazake kwa kusema kuwa huo ni uongo kwa vile jambo hilo kwa taratibu za benki haliwezekani. Haikuchukuwa juma moja, Mafuru akafukuzwa kazi na Mwendazake.

3) Wakili Kibatala na jopo lake - Hawa jamaa wamesimama na wapinzani kwa kipindi ambacho Mwendazake alifanya Watanzania kuogopa Upinzani kama ukoma. Hawa jamaa hawakuterereka hata kidogo. Siyo wengi wenye msimamo huu ktk Tanzania. Wengi wanaangalia matumbo yao tu. Hawa jamaa wanastahili nishani kwa kutoogopa udikteta ule.

4) Mashangazi Maria Sarungi na Wakili Fatuma Karume - Hawa wamempinga Mwendazake hata pale ambapo watu waliogopa hata kukohoa katika vyumba vyao vya kulala. Wanastahili kupewa nishani ya ushajaa.

5) Taja wako kama wapo
Tundu Lissu ni kichaa. Maria Salungi na Fatuma Kalume ni mapapalazi wa CCM.
 
Umewaacha viongozi wa dini kama Yule Askofu wa Kagera,Shekh Ponda,Mwamakula na Dr.Shoo
 
Back
Top Bottom