Ushindi wa Dkt. Tulia, hakika hayati Magufuli hajawahi kukosea

yvegenc prymacov

JF-Expert Member
Jan 22, 2023
1,527
1,913
Dkt Tulia Akson juzi alishinda ushindi wa kishindo, na kwa kweli kaliheshimisha taifa letu. Tulia Akson ni rais wa Ipu Mdogo kbs kuwahi kutokea ktk historia ya bunge hilo.

Ninapoushangilia ushindi wa Dkt Tulia, namkumbuka hayati John Pombe Joseph Magufuli. Hakika jicho lake halijawahi kukosea. JPM ndiye alimwibua Tulia kutoka chuo kikuu, alikiona kipaji chake na kumvuta kumwingiza kwenye siasa. JPM alitikiswa sana, mpaka watu wa kulee wakawa wanasema ni hawala yake, lakini leo tunaona jicho la JPM mbali.

Ninaamini JPM huko aliko anasherekea ushindi wa kijana wake.
 
Dkt tulia akson juzi kashinda ushindi wa kishindo,na kwa kweli kaliheshimisha taifa letu. Tulia akson ni rais wa ipu mdogo kbs kuwahi kutokea ktk historia ya bunge hilo.
Ninapo ushangilia ushindi wa dkt tulia,namkumbuka hayati John pombe Joseph magufuli,hakika jicho lake halijawahi kukosea,jpm ndie alimwibua tulia kutoka chuo kikuu,alikiona kipaji chake na kumvuta kumwingiza kwenye siasa,jpm alitikanwa sana,mpk watu wa kulee wakawa wanasema ni hawala yake,lkn leo tunaona jicho la jpm mbali.

Ninaamini jpm huko aliko anasherekea ushindi wa kijana wake,
Watu tunawaza tule nini wewe unatuletea ya spika kuchaguliwa? Kuna chakula ataniletea huko? Badala utoe elimu hizi mvua za elnino tuzitumie vipi bei vyakula viwe vingi wewe unahangaika na wanasiasa ambao wameshashiba?
 
Swala la chakula ni jukumu la wewe binafsi mkuu,ukilala njaa wengine wanatupa makombo.labda useme kama kuna kikwazo kinaletwa na huyu spika juu ya wewe kujipatia chakula,lkn kama hakuna basi,tuna haki ya kushangilia ushindi wake mkuu.
 
Dkt tulia akson juzi kashinda ushindi wa kishindo,na kwa kweli kaliheshimisha taifa letu. Tulia akson ni rais wa ipu mdogo kbs kuwahi kutokea ktk historia ya bunge hilo.
Ninapo ushangilia ushindi wa dkt tulia,namkumbuka hayati John pombe Joseph magufuli,hakika jicho lake halijawahi kukosea,jpm ndie alimwibua tulia kutoka chuo kikuu,alikiona kipaji chake na kumvuta kumwingiza kwenye siasa,jpm alitikanwa sana,mpk watu wa kulee wakawa wanasema ni hawala yake,lkn leo tunaona jicho la jpm mbali.

Ninaamini jpm huko aliko anasherekea ushindi wa kijana wake,
Acha uongo we kilaza

Dkt. Tulia aliteuliwa na Kikwete kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali mwaka 2014/2015
 
Dkt tulia akson juzi kashinda ushindi wa kishindo,na kwa kweli kaliheshimisha taifa letu. Tulia akson ni rais wa ipu mdogo kbs kuwahi kutokea ktk historia ya bunge hilo.
Ninapo ushangilia ushindi wa dkt tulia,namkumbuka hayati John pombe Joseph magufuli,hakika jicho lake halijawahi kukosea,jpm ndie alimwibua tulia kutoka chuo kikuu,alikiona kipaji chake na kumvuta kumwingiza kwenye siasa,jpm alitikanwa sana,mpk watu wa kulee wakawa wanasema ni hawala yake,lkn leo tunaona jicho la jpm mbali.

Ninaamini jpm huko aliko anasherekea ushindi wa kijana wake,
JPM ndiye aliyempa cheo cha ukurugenzi wa mamlaka ya anga ndugu Hamza Said Johari mwaka 2016 mwanzoni baada ya mawaziri wa Jakaya Kikwete kuliweka kabatini jina lake baada ya Kikwete mwenyewe kuidhinisha apewe cheo kikubwa zaidi kuliko kile alichokuwa nacho kabla akiwa ni mwanasheria anayesimamia haki za wasafiri wa anga Tanzania.

JPM alikuwa na maono makubwa, aliweza kumuona mtu ambaye wengi wetu hatuna uwezo wa kumuona atakuwa vipi huko mbeleni. Aendelee kupumzika kwa amani.
 
Jana ilikuwa birthday yangu.(Good God !,Dr. Tulia Ackson amechaguliwa wadhifa wake siku ya birthday yangu).
Anyway,jana ilikuwa birthday yangu,na nilikuwa nawasubiri wageni waalikwa wafike. Wageni walichelewa kigodo kufika,na kwa muda mfupi nilidhani wameisusia party yangu. Lakini baadaye wakafika.
Wakati nawasubiri wageni kufika ndio nikayaona haya matokeo Tulia ameshi da. Basi nikasema,sihitaji hata kula keki kuwa na furaha siku ya leo.
 
JPM ndiye aliyempa cheo cha ukurugenzi wa mamlaka ya anga ndugu Hamza Said Johari mwaka 2016 mwanzoni baada ya mawaziri wa Jakaya Kikwete kuliweka kabatini jina lake baada ya Kikwete mwenyewe kuidhinisha apewe cheo kikubwa zaidi kuliko kile alichokuwa nacho kabla akiwa ni mwanasheria anayesimamia haki za wasafiri wa anga Tanzania.

JPM alikuwa na maono makubwa, aliweza kumuona mtu ambaye wengi wetu hatuna uwezo wa kumuona atakuwa vipi huko mbeleni. Aendelee kupumzika kwa amani.
Shikamooo
 
Dkt Tulia Akson juzi alishinda ushindi wa kishindo, na kwa kweli kaliheshimisha taifa letu. Tulia Akson ni rais wa Ipu Mdogo kbs kuwahi kutokea ktk historia ya bunge hilo.

Ninapoushangilia ushindi wa Dkt Tulia, namkumbuka hayati John Pombe Joseph Magufuli. Hakika jicho lake halijawahi kukosea. JPM ndiye alimwibua Tulia kutoka chuo kikuu, alikiona kipaji chake na kumvuta kumwingiza kwenye siasa. JPM alitikiswa sana, mpaka watu wa kulee wakawa wanasema ni hawala yake, lakini leo tunaona jicho la JPM mbali.

Ninaamini JPM huko aliko anasherekea ushindi wa kijana wake.
Amepita Kwa sababu ya Ushawishi wa Rais Samia ila Rais angekuwa Mwendazake hakuna mtu angempa kura huyo ambae alikuwa hajumuiki na wenzie full ugomvi na kununa.

Chini ya Samia hakuna kitu Tanzania inafeli kuanzia Afcon hadi kuwa na Makao Makuu ya Sekretarieti ya mambo ya soko Arusha na Tanznaia ilichaguliwa mapema mwaka huu.
 
nakushauri ukamfufue uzikwe wewe chizi mkubwa wewe
 
JPM asingeweza kuuza bandari, sasa hilo jicho lake limeuza bandari?
JPM aliingizwa choo cha kike kuhusu suala la bandari ya Bagamoyo na alipogundua akamtimua kazi Kipilimba boss wa TISS.

Angeelimishwa kuhusu mikataba inakuwaje kwa kina, angekubaliana na huu uwekezaji wa TPA. Bosi wake wa zamani hayati Mkapa aliwakodisha TICTS mwaka 2000 sioni ni kwa namna gani yeye JPM aje akatae kuwakodisha DP World.
 
Amepita Kwa sababu ya Ushawishi wa Rais Samia ila Rais angekuwa Mwendazake hakuna mtu angempa kura huyo ambae alikuwa hajumuiki na wenzie full ugomvi na kununa.

Chini ya Samia hakuna kitu Tanzania inafeli kuanzia Afcon hadi kuwa na Makao Makuu ya Sekretarieti ya mambo ya soko Arusha na Tanznaia ilichaguliwa mapema mwaka huu.
Samia ana spirit nzuri sana kimataifa, hana majivuno wala haonekani kutaka kushindana na taasisi za kimataifa hivyo anachukuliwa kuwa ni rais msikivu na mwepesi kufanya nae biashara.
 
Back
Top Bottom