Mashujaa wa kweli Tanzania hawakumuogopa Hayati Dkt. Magufuli

Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
7,105
18,005
Wanajamvi,

Kuna watu wanastahili nishani. Kukosa uoga kwao hakuelezeki. Wakati Mwendazake anafungwa watu, kuharibu biashara zao, kuwapakazia makosa yasiyokuwa na dhamana, na wengine kuuawa, hawa jamaa hawakunyaza kimya. Kilikuwa kipindi kigumu cha kuogopesha sana. Watu hawakuwa huru kuongelea serikali na siasa mbele ya watu wasiowafahamu. Hawa jamaa hawakuyumba. Hebu tuwataje:

1) Tundu Lissu - Kwa kifupi tu - Huyu alindamana kupinga udikteta. Alikuwa na jeuri ya kumwita Mwendazake dikteta uchwara. Alifunguliwa kesi zisizokuwa na mashiko. Alipigwa risasi 16 na Mungu akamponya. Baadae akaja kumpinga Mwendazake katika uchaguzi! Katika mazingira na hofu iliyojengwa na Mwendazake, huu ulikuwa ni ujasiri wa kupewa nishani.

2) Lawrence Mafuru - Huyu alikuwa ni Managing Director wa NBC Bank na baadae Msajili wa Hazina. Alikuwa na hali nzuri tu ya maisha na angeweza kunyamaza tu akaendelea na maisha bila bughudha. Wakati Mwendazake anatimua timua watu waliokuwa wanapingana naye, Mafuru alidiriki kupingana na Mwendazake mchana kweupe kwenye TV wakati akijua wazi kuwa atapoteza kazi yake. Mwendazake aliwashutumu watu wa benki kuwa wanaweka fedha za serikali katika fixed deposit the kulamba faida kwa manufaa yao. Mafuru akiwa Clouds 360, alimpinga Mwendazake kwa kusema kuwa huo ni uongo kwa vile jambo hilo kwa taratibu za benki haliwezekani. Haikuchukuwa juma moja, Mafuru akafukuzwa kazi na Mwendazake.

3) Wakili Kibatala na jopo lake - Hawa jamaa wamesimama na wapinzani kwa kipindi ambacho Mwendazake alifanya Watanzania kuogopa Upinzani kama ukoma. Hawa jamaa hawakuterereka hata kidogo. Siyo wengi wenye msimamo huu ktk Tanzania. Wengi wanaangalia matumbo yao tu. Hawa jamaa wanastahili nishani kwa kutoogopa udikteta ule.

4) Mashangazi Maria Sarungi na Wakili Fatuma Karume - Hawa wamempinga Mwendazake hata pale ambapo watu waliogopa hata kukohoa katika vyumba vyao vya kulala. Wanastahili kupewa nishani ya ushajaa.

5) Taja wako kama wapo
 
List hii inaonesha kuwa Mbowe na Zitto sio mashujaa, bali ni wanafiki na wachumia tumbo wa kisiasa, wanaotumiwa na mfumo kujifanya ni wanasiasa... Walishindwa hata na kina shangazi.

Asante sana mleta mada kwa kuuweka wazi msimamo wako ambao upo tofauti na wenzako.
 
Back
Top Bottom