Mashoga WAISHTAKI Tanzania UN | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashoga WAISHTAKI Tanzania UN

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by kanda2, Jul 20, 2009.

 1. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Watetezi wa haki za mashoga na wasagaji nchini wameishtaki Tanzania kwenye kamati ya Haki za Binadamu Umoja wa Mataifa wakidai haki zao hapa nchini zinakiukwa wakati katiba inaruhusu haki sawa kwa wote.

  watetezi hao ni JULIUS KYARUZI,MONICA MBARU NA STEFANO FABENI SOURCE GAZETI LA MWANANCHI TAREHE 18-07-09.

  Habari inayoendana na tukio hili ni hii:

  ------------------------------

  Watetezi wa haki za mashoga waandamwa

  Na Boniface Meena

  WATETEZI wa haki za mashoga na wasagaji nchini, walioishtaki Tanzania kwenye Kamati ya Haki za Binadamu Umoja wa Mataifa (UN), wakidai kuwa haki zao hapa nchini zinakiukwa wakati katiba inaruhusu haki sawa kwa wote wamekumbana na upinzani mkali.

  Viongozi wa dini na wanaharakati wengine wamepinga madai hayo wakisema shughuli za mashoga ni kinyume na mapenzi ya Mungu na ukiukaji wa misingi ya utu wa binadamu.

  Maoni hayo yamekuja baada ya watetezi hao kuwasilisha ripoti yao UN, ikieleza kile wanachodai kuwa sheria za hapa nchini zinazuia uhuru wao katika suala la mahusiano kwa watu wenye jinsia moja.

  Ripoti hiyo ambayo imetumwa na taasisi tatu zisizo za kiserikali ambazo ni Centre for Human Rights Promotion inayojitaja ya Afrika Mashariki, International Gay and Lesbian Human Rights Commission (IGLHRC) na Global Rights inaeleza kuwa, wana matumaini kuwa ripoti hiyo itatoa mwanga kwa jamii juu ya malalamiko yao dhidi ya serikali ili hatimaye wafikiriwe.

  Wawakilishi wa watetezi hao wametaja majina yao kwenye ripoti hiyo kuwa ni Julius Kyaruzi ambaye ni mratibu LGBTI Tanzania, Monica Mbaru mratibu wa programu IGLHRC; na Stefano Fabeni, mkurugenzi wa LGBTI Initiative na Global Rights.

  Taasisi hizo zimedai kuwa, Tanzania bado ina sheria ambazo zinapinga uhuru binafsi wa mtu na kutengeneza matabaka kwa kufanya hisia za mtu kuwa hazikubaliki kisheria na siyo hisia halisi.

  Baada ya ripoti hiyo kutolewa mwezi huu na kuwasilishwa kwa vyombo vya habari wanaharakati wa haki za binadamu na viongozi wa dini hapa nchini, wamekuwa na maoni tofauti kuhusu madai hayo.

  Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Ananilea Nkya amesema kuwa, kama watu hao wanataka haki zao zitambuliwe wajitokeze hadharani kwanza ili jamii iwajue.

  “Tunatakiwa tuwajue, hivyo ni vizuri wakajitokeza na siyo kujificha,” alisema.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia nchini (TGNP), Usu Mallya alisema kuwa watu hao wana haki kwa kuwa jamii ina mifumo mbalimbali ya maisha.

  “Misingi ya katiba inatambua uhuru wa kila mtu, hivyo wana haki kama kikundi na jamii inahitaji kulitambua hilo,” alisema Mallya.

  Alisema jamii inatakiwa kutambua mahitaji yao, kama ilivyoweza kutambua mahitaji ya watu wengine nchini.

  “Kwenye jamii kuna watu tofauti ni kama watu wenye ukimwi, jamii ilivyokuwa haitaki kuwapa nafasi lakini elimu imeonyesha ni jinsi gani mambo yanavyoweza kubadilika,” alisema.

  Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binaadamu (LHRC) Francis Kiwanga alisema kuwa, LHRC inafanya utafiti jinsi gani suala hilo linaweza kushughulikiwa.

  Alisema kama watu hao wanataka wakubaliwe inabidi jamii iulizwe kwa kuwa ni suala ambalo ni tete.

  “Ni suala tete, hivyo watu waulizwe na wabunge wahusishwe ili kuangalia sheria inasemaje katika hilo,” alisema.

  Alisema hata hivyo, suala hilo ni gumu kukubalika katika jumuiya ya Afrika.

  Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa Katoliki, jimbo la Dar es Salaam, Methodius Kilaini alisema kama watu hao ingekuwa ni walemavu wanataka kutambuliwa haki zao ingekuwa sawa, lakini kwa hilo wanalolitaka haiwezi kukubalika.

  “Kama ni walemavu wanataka tuwatambue sawa, lakini kwa sisi hatuwezi kukubali, ni kitu ambacho hakikubaliki na hakiwezi kutambuliwa kwa kuwa Mungu ameumba jinsi mbili na itabaki kuwa hivyo,” alisema Kilaini.

  Alisema kuwa suala la usawa ambalo wanadai limekiukwa kutokana na katiba kuruhusu, ni kitu ambacho hawaelewi kwa kuwa usawa unaoelezewa kwenye katiba ni wa jisia ya kike na kiume na siyo ya uhusiano wa kimapenzi kwa watu wa jinsi moja.

  “Usawa hauwezi kupinga uhalisia, mwanamke atabaki kuwa mwanamke na mwanamume atabaki kuwa mwanamume kama Mungu alivyoumba,” alisema.

  Kilaini alisema kuwa katiba inatambua hivyo na haitambui mwanamume kujigeuza kuwa mwanamke na mwanamke kujigeuza kuwa mwanamume.

  Katika ripoti yao taasisi hizo tatu zimetaka marekebisho yafanyike katika sheria ya makosa ya jinai (Penal Code) ambayo inazuia masuala hayo kwa kuyafanya kuwa jinai.

  Hata hivyo, Msemaji wa Wizara ya Sheria na Katiba, Omega Ngole alikiri kuona ripoti ya watetezi hao wa mashoga, na kufafanua kuwa sheria za nchi siyo tu zipo kwa ajili ya kulinda haki za watu wote, bali pia kulinda utu wa mtu.
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tanzania kuna gay rights movement napo pia? Ni haki gani hizo wanazodai na kuona wana nyimwa? Wanaishtaki Tanzania kwa lipi haswa? Ila Mods nashauri hii isiwekwe hapa kwenye jukwaa la siasa ambapo kuna mijadala ya more serious issues.
   
 3. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  hii issue ni very serious kwanini hutaki tuijadili hapa? unaona ni jambo dogo hili? soma gazeti la mwananchi,co.tz mimi nimeshangazwa na kuona kuwa tayari tumevamiwa na haya mambo nchini na kuna vyama kama vitatu vilivyopeleka mashitaka UN.
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hapa ndipo hasa pahala pake pa kujadiliwa.

  mwenye kujua sheria za tanzania tungeomba atuwekee wazi, sheria zetu zinapinga vipi ushoga?
   
 5. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Safi sana, ubaguzi wa aina yoyote lazima upingwe.
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ubaguzi gani?
   
 7. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Ubaguzi huo.
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ubaguzi ambao hauna madhara..Hivi bongo hatuna ishu za maana mpaka tuwe tunadakia mambo ya dunia ya kwanza kila mara?
   
 9. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #9
  Jul 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Hauna madhara kivipi? Kwanini watu waishi maisha ya woga na kujificha bila sababu maalum?
  Haya si mambo ya dunia ya kwanza, bongo yapo na kila mtu anajua.
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Jul 20, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hakuna uhuru kwa kila jambo..sometimes ubaguzi ni muhimu ktk ku-maintain society ktk muelekeo sahihi. Sio kila uhuru unaifaidisha jamii, ndio maana Bush aliliona hili mapema.
   
 11. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Bush amewafunga watu bila kesi na ameruhusu torture itumike. So sidhani kama Bush ni mfano mzuri kwenye discussion ya uhuru.

  Uhuru wenye vipimo ni pale tu ambapo unawazuru/unawagusa watu wengine, watu wawili wanachofanya kati yao halimhusu mtu yoyote.
   
 12. N

  Natasha Ismail JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Kang !
  Leo mbona nakuwa sikuelewi elewi,kweli uhuru wa watu wawili wajinsia moja kupumuliana .Ndio unaoutaka? Please nakuamini sana badilisha kauli zako hujachelewa.
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mimi naona uhuru wa watu kutumiliana kihivyo ni ufujaji na una madhara makubwa ki-afya na kiuchumi. Uhuru wa watu wa jinsia moja kufujana kuna athiri uwiano wa uzazi, unaleta mitafaruku kijamii na kwenye familia.

  Dunia inahitaji watu wazaliane ili kuhimili mahitaji ya nguvu kazi ili kuendeleza ukuaji uchumi na maendeleo.

  Kiafya..watu wanaofujana wao kwa wao wanakuwa prone na magonjwa mbalimbali ya kingono nk. Takwimu zipo wazi.

  Kijamii, watu hawa wamekuwa wakisababishia familia zao kukumbwa na sintofahamu na kuwanyong'onyesha wanafamilia na hasa wazazi. 

  Pia watu wanaofujana wamejipenyeza hadi kwenye mambo ya kuabudu na hivyo kusababisha waumini kuopunguza ucha Mungu na matokeo yake uovu kuongezeka ktk jamii. Gharama za kuongezeka maovu ktk jamii kila mtu anazijua.

  Hizi ni baadhi ya sababu zinazonifanya kuamini hawa watu ni kama kansa ktk jamii yetu na wanapaswa kushughulikiwa kimuundo and systematically.
   
 14. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #14
  Jul 20, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Ndio kusema DUNIA KWISHA KAZI.
  Vp ingekuwepo gharika nyingine tofauti na hii ya UKIMWI,TUNGEKUWA WAPI LEO?
  Kama serikali kwa kushirikiana na wadau wengine,wameshindwa kuzuia ushoga na uchangudoa basi ni heri wakaruhusu na kuwe na sheria za kusimamia uchafu huo kwa lengo la kupata mapato yatokanayo na kodi zao hao mashoga na changudoa kama zilivyo biashara nyingine halali.
   
 15. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mkuu Kang,kwenye tamaduni zetu hili la kupumiliana watu wa jinsia moja halipo.Na ni ujinga kudai haki ya aina hii. Unaweza ukawa wewe ni pro-ushoga kwasababu ya kutetea haki za binadamu ama vinginevyo lakini ukweli unabaki kwenye hili serikali ya tanzania hakiuki haki zozote za binadamu.

  Uhuru una mipaka,na miongoni mwa mipaka ndiyo hili la kutopumuliana watu wa jinsia moja.
   
 16. C

  Chuma JF-Expert Member

  #16
  Jul 20, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
 17. TinyMonster

  TinyMonster JF-Expert Member

  #17
  Jul 20, 2009
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Wapuuzi hao, as far as i know ushoga na usagaji ni kosa kwa sheria zetu.
   
 18. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #18
  Jul 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Naamini sio nafasi ya serikali kujaribu kupanga sex lives za watu, leo serikali ikasema hauruhusiwi kuwa na demu mpaka uoe kwa vile "Sio utamaduni wetu" au "Dini zinakataza" utasemaje?

  Homosexuality haiambukizi, so sioni jinsi itakavyoathiri watu kuzaliana sio kwamba watu wote duniani watageuka mashogo ghafla. Na hata mashoga nao wana njia za kuzalisha kama artificial insemination etc.

  Wanawake wanaosagana wana chance ndogo zaidi kupata magonjwa, kwa sabau hakuna penetration, kwa hiyo usagaji utaukubali kwa kuwa itapunguza ukimwi?

  Kuna vitu vingi vinaleta matatizo kwenye familia, sio nafasi ya serikali kujaribu kuvitungia sheria vyote, tutajikuta kila kitu kina sheria tukienda huko.

  Well kwanza sina uhakika kama kweli hakuna hii kitu kwenye tamaduni zetu, kuna sehemu fulani zinasifika kwa hili!
  Pia kitu kuwa au kutokuwa kwenye utamaduni haina maana kuwa ni positive au negative. Kwa mfano tohara kwa wanawake nao ni utamaduni, ambao sasa hivi (wengi)tunaupinga.


  Mwisho naomba tukumbuke, sheria haibadilishi sexuality ya mtu! Kama wewe ni shoga wakati sheria inaruhusu bado utakuwa shoga HATA SHERIA ISIPORUHUSU. So hii sheria haina maana zaidi ya kuwanyanyasa watu.
   
 19. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #19
  Jul 20, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Tatizo sio homosexuality..tatizo ni u-active gayism, na matakwa yake, na matokeo na athari zake kwa jamii. Suala la kupungua watu duniani sijasema linasababishwa solely na hawa active gays,la..Kuna factors nyingine lakini pia wao vitendo vyao vinachangia. Suala la artificial insemination ni kujiongezea majukumu yasiyo na tija, natural process zipo kwanini watu wasizitumie ?

  Kuhusu magonjwa hilo halina pingamizi, maana lipo wazi. Wanawake wasagaji wana chance sawa ya kuambukizana sawa na wengine depending na njia wanayotumia kufujana..

  Vicious cycle ya hawa gays sio tu inakuwapo ktk familia, bali hata wao wenyewe..na wengi wao wanakuwa ma-drug addicts kutokana na psychological problems ambazo ni causes au effects au both. Kutokana na hilo wengi wao hawawezi kuji-control kufanya safe sex na ndipo unaona cycle inarudi palepale kuwa vitendo hivi havina maslahi kwa jamii.
   
 20. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #20
  Jul 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  No, wasagaji wana chance ndogo sana ya kuambukizwa ukimwi. Ndio inategemea na njia wanayotumia kama heterosexuals lakini on average chance zao ni ndogo zaisi ya heterosexuals.

  Sasa ni mtu yupi ambaye yuko kwenye hatari zaidi ya kupata matatizo ya kisaikolojia, mtu anayeishi kwenye jamii inayombagua au mtu mwenye usawa kwenye jamii?
  Hizi sheria za kibaguzi zitaongeza matatizo ya kisaikolojia na si kuyapunguza.

  Sana sana watu wanafanya mambo kwa kujificha kitu ambacho kinasababisha matatizo mengi sana yakiwemo wanaume mashoga kwenda kuwaambukiza wake/mademu zao ngoma.
  Hili ni tatizo kubwa sana kwa wamarekani weusi, wanaita kuwa "On the down low".
   
Loading...