Mashirika mengi kupeana kazi kindugu na ukabila

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Hivi haya yasemwayo ni kweli? Kuna maneno nimekuta mahali kuwa mashirika mengi hapa Tanzania hususan NGO's pia mashirika ya umma kuna undugulization tu.

Yaani watu wanapeana kazi kwa kujuana!!Mfano zinaweza kutangazwa nafasi 200 shirika flan halaf watu wakaomba kumbe kutangaza wamefanya kama wajibu ili ionekane walitangaza.

Kumbe tayar watu walishapatikana kwa muda tu tangazo ni zuga tu.

Mashirika mengine yamejaa ukabila na udini pia, kama sio dini fulani hupati kazi, kama sio kabila fulani hupewi kazi na mengine yamejaa kujuana tu kama hujulikani hupati kazi.

Mimi sio mtaalam sana wa masuala ya mashirika hivi hakuna namna taifa linaweza kufanya tukapunguza haya matatizo na huu urasimu?
 
Watu weusi wana huu Upumbavu na Ujinga

Kampuni ya Wazungu wanachoangalia ni Qualifications na Performance,

Ila kampuni ya Mtu mweusi nikuangalia mtoto wa shangazi au wa Baba wa nje au Baba mdg n.k
 
Watu weusi wana huu Upumbavu na Ujinga

Kampuni ya Wazungu wanachoangalia ni Qualifications na Performance,

Ila kampuni ya Mtu mweusi nikuangalia mtoto wa shangazi au wa Baba wa nje au Baba mdg n.k
Ndo ujinga uliyopo Africa
 
Hata mitume wa yesu walikuwa ndugu zake au walipeana michongo alioanza nao wakastua washikaji zao.
 
😂 hivi niwaulize, wewe utajisikiaje kaka yako akiwa bosi wa mradi/kampuni fulani na wewe huna kazi upo mtaani tu, njaa kali.
Si sahihi kufanya undugu lakini tukubali kuwa sisi almost wote tunachangia, tunauchukia pale tu tunapokosa ajira.
 
Wewe ndugu zako walikua wapi? Haya makasiriko inabidi yaende kwa ndugu zako.


download.jpeg
 
Back
Top Bottom