Mashine za EFD sasa kutolewa bure na Serikali!

Mashine za EFD sasa kutolewa bure na Serikali!

Sawa. Hebu tuambiane je elimu hiyo imetolewa kwa mnunuzi au muuzaji, maana bila mnunuzi kupewa hiyo elimu itaonekana muuzaji anamuibia mnunuzi. Pili je hiyo vat inakatwa mara ngapi mpaka imfikie mlaji wa mwisho. Kwa mfano kule kiwandani imelipwa vat wakati wa duka la jumla ananunua, halafu anamuuzia wa duka reja reja na vat inalipwa, nk. Mwisho wa siku unakuta bidhaa moja mpaka inamfikia mlaji wa mwisho imelipiwa vat kama mara tatu au zaidi, je hii ni sahihi!!?

sio sahihi kabisa ktk mazingira yetu labda huko ulaya mifumo iko kamilifu, hiyo ni theory tu ya madarasani nikipata muda ntawaelezeni nini kinatokea
 
nadhani tatizo sio mashine, ni mfumo mzima wa ulipaji kodi, mtu kama bhakresa anapotengeneza syndicate ya wakwepa kodi wanaingiza mataili wanasambaziana wao kwa wao ni dhahiri mfanyabiashara anaelipa kodi halali hawezi kushindana nao na hatimae watabaki pekeyao.

TRA wakifanyakazi yao kwa usahihi na kila mtu akalipa kodi stahiki basi hakuna mtu atakaekwepa kulipa kodi kwani patakuwa na ushindani uliosawa wa kibiashara. Mfano mtu aliyeuziwa matairi ambayo hayajalipiwa kodi hawezi toa risiti na atakayeenda nae hatatoa risiti, sasa huyu aliyepanga dukani tukamlazimisha atoe risiti huku jamaa yake bhakresa tukimwacha ni dhahiri hii kazi itakuwa ngumu kweli kwa tra

lakini bhakresa akilipa kodi stahiki na akatoa risiti hata huyu mangi wa kariakoo mwenye tairi kumi nae atatoa risiti na kulipa kodi stahiki na kazi ya tra itakuwa rahisi pia.
 
Acha kulalamika inakatajwe kwenye mtaji? au huelewi maana ya vat, vat registered ni wakala wa kukukusanya kodi zile 18% zote unakusanya kwanini usiwakilishe serekalini tuache biashara za ujanja ujanja.

sio sahihi kabisa ktk mazingira yetu labda huko ulaya mifumo iko kamilifu, hiyo ni theory tu ya madarasani nikipata muda ntawaelezeni nini kinatokea
 
Wanajamvi,

Kilio cha muda mrefu cha wafanyabiashara nchini waliokuwa wanalalamikia Serikali kwamba mashine za EFD's zinauzwa ghali, kwa sasa tatizo hilo limetauliwa kwani zitatolewa bure na Serikali.

Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Philip Mpango, ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam na kwamba mashine hizo za EFD hazitauzwa, wafanyabiashara nchini watapewa vifaa hivyo bure.

Nadhani sasa Serikali imeamua kujielekeza kuondoa vikwazo vyote vilivyokuwa vinalalamikiwa ili kufanikisha zoezi la kukusanya mapato.
Hilo sawa,ila pia TRA waangalie utaratibu wa jinsi ya ukokotoaji kodi wa hizo maahine.Vinginevyo mgogoro bado ni uleule.
 
Wanajamvi,

Kilio cha muda mrefu cha wafanyabiashara nchini waliokuwa wanalalamikia Serikali kwamba mashine za EFD's zinauzwa ghali, kwa sasa tatizo hilo limetauliwa kwani zitatolewa bure na Serikali.

Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Philip Mpango, ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam na kwamba mashine hizo za EFD hazitauzwa, wafanyabiashara nchini watapewa vifaa hivyo bure.

Nadhani sasa Serikali imeamua kujielekeza kuondoa vikwazo vyote vilivyokuwa vinalalamikiwa ili kufanikisha zoezi la kukusanya mapato.

Naomba kuuliza, hivi baada ya kupewa Mashine ya EFD ishu ya makadirio ya kodi inakuwaje?
 
wabongo kwa kuchakachua...!! watazichakachua hizi pia
 
Watu wanashindwa kuelewa kwamba Ishu sio Bei ya hizo Mashine ishu kubwa Watu hawataki kuzitumia kwa sababu zinawabana sana,

Hizo mashine zinawabana vilivyo sasa swala la bei ya mashine hutumika kama kisingizio tu, Hakuna mfanya biashara atakaye shangilia kusikia kwamba mashine hizi zinatolewa bure, kwanza ndo watasikitika sana make kisingizo kikuu kimeondolewa
 
Upatikanaji wa hizo EFD kwa wafanyabiashara hiyo ni hatua moja, hatua ya pili ni kutumika kwake, je watazitumia ipasavyo??? na je, serikari itahusika pia na matengenezo ya hizo EFD endapo zikipata hitilafu?
Ni hayo tuu kwa leo
 
Kwa anaefanya biashara zake kiuhalali Mashine za-EFD sio tatizo..
Na anaesema mfumo wa ukataji kodi wa EFD ni tatizo nadhani hajaelewa kuhusu hizo mashine, binafsi tatizo nililo liona ilikua ni mfanya biashara kuikopesha serikali pesa ya kununulia EFD machine.

Kwa sababu kiuhalisia ile gharama uliyoitumia kununua mashine unatakiwa uikate katika kodi unayotakiwa kuipeleka serikalini-TRA, kwa mfano kama umekusanya kodi(VAT) ya Million 2 kwa December 2015 katika mauzo yako na ulilipa kodi (VAT) ya laki7 katika mahitaji yako ya kibiashara, na ulinunua mashine ya EFD kwa shilingi laki5, itakapofika January 2016 badala ya kupeleka TRA-Serikalini shilingi million2 utatakiwa upeleke laki 8 (yaani kodi(VAT) uliyokusanya 2,000,000-700,000-500,000).

Pili sio kila mwenye mashine ya EFD anaweza akatoza kodi ya VAT (ni mpaka usajiliwe), kwahiyo kama hujasajiliwa utatumia mashine ya EFD kwa ajili ya kumbukumbu zako za kibiashara na pia itakusaidia usitozwe kodi zaidi ya mauzo yako...kwahiyo inampunguzia uonevu kwa sababu mauzo yako ya mwaka mzima yataonekana na sio kukadiriwa (KAMA UTATII SHERIA YA UKIUZA TOA RISITI NA UKINUNUA DAI RISITI).

:angry::angry:Tatizo tulizoea kununua vitu vya jumla toka kwa wafanyabiashara WALIOKUA WANATOA MAKONTENA BILA KULIPA KODI:angry::angry:

Ili tufike katika huo uchumi wa kati EFD-NI LAZIMA.

Tutakua ni wazalendo na wapenda mabadiliko ya kweli..kama tutaiomba serikali itupunguzie viwango vya kodi zote kama VAT, PAYE, na WHT...lakini sio kuzipinga mashine za EFD

Ushauri kwa TRA- itoe elimu zaidi juu ya hizi mashine, na usimamizi wa matumizi yake uongezwe ikiwezekana uanzie serikali za mitaa..na pia ikusanye kodi kwetu sisi tunaopangisha nyumba zetu huku sinza badala ya kuendelea kuwabana maaskari magereza, walimu n.k katika mishahara yao.
 
...wafanyabiashara wa nchi hii nawachukia sana, wafanyakazi kodi wanayokatwa kila mwezi ni sawa na kodi ya mauzo ya duka moja kubwa kinyama, then wafanyakazi hao hao wanaenda maduka ya wafanyabiashara ambao mosi wanakwepa kodi, then bado wanalalamika wakikatwa kodi na serikali!
 
Kwanza inaonekana huelewi kitu na hiyo machine hukuwa nayo. Kwani mkataba na tra c kwamba mtakuwa mnalipana ktk hiyo kodi kdgo kdgo?? Maana yake unaikopesha tra.... we sio mlipa kodi

Stup.i.d, bill nunua mashine hii kutoka kampuni Fulani. Na kwa shughuli ninazofanya naweza kutoa Z report miezi mitatu mfululizo na mwezi utaofuata nalipa ninachodaiwa.
Hujui unachosema wewe.
 
sio sahihi kabisa wanadanganya watu ktk mazingira yetu uongo mkubwa labda huko ulaya mifumo iko kamilifu, hiyo ni theory tu ya madarasani nikipata muda ntawaelezeni nini kinatokea

Tunasubiri mkuu utudadavulie hili la vat na efd, usichelewe.
 
we kweli unaumwa...ttcl ndio ISP active pale tra acha kuropoka km huna data kenge ww

Huna lolote unalojua kuhusu VAT achilia mbali hizi Electronic Fiscal Devices. Sidhani kama unaelewa mlipa VAT Ni wewe!
Malaya we
 
Completely free EFD-where is the catch? Inaingia akilini kuzitoa bure? Nani atagharamia matengenezo yake?
 
Tatizo kubwa lililopo ni matumizi ya EFD machines. Kuna scenario mbili; Kukey in amount kidogo ili kuonesha mashine inatumika na kutoitumia kabisa. Tatizo hili litapungua pale ambapo Watanzania i.e. mfanyabiashara na mnunuzi watakapoona na kufahamu umuhimu wa kodi. Ikifikia ikawa fahari kulipa kodi, basi EFD machine zitakuwa na maana. Lakini kwa mindset iliyoko kwa wafanyabiashara ya kukwepa (evasion ) bado machine hizi zitakuwa mapambo.
 
Back
Top Bottom