Sisi wajasiliali si ugomvi wetu ni mfumo uliomo ktk mashine hizo...KWAMBA HATUUTAKI MFUMO....SIO MASHINE...narudia tena ..HATUUTAKI MFUMO WA MSHINE HII KUKATA KODI KWENYE MAUZO..TUNAOMBA MASHINE IKATE KODI KWENYE FAIDA
Mkuu hizo ni kodi mbili tofauti, na kwa kisheria ya sasa, lazima zilipwe. Ninacho kubaliana na wadau ni kwamba hizi sheria zinataka marekebisho makubwa tu kwa faida ya pande zote mbili kwa kutizama hali ya uchumi ya sasa kwa nchi yetu.
1. Kodi ya mtumiaji (VAT). Mutaniwia radhi kwa vile sina uhakika ni kiasi gani ya mauzo kwa mwaka ukifikisha unatakiwa ukusanye kodi hii katika mauzo. Lakini, lets say, ni 50,000,000 approx US$23,000 kwa mwaka ni sawa na 4,166,000 (US$1920) kwa mwezi ikiwa ni sawa na 140,000 (US$64) kwa siku. Ukiitizama hii hesabu ni masihara kwa serikali yetu kuweka sheria kama hii. Hata muuza machungwa na madafu na wanaotembeza soda na chinga wote wanafikisha mauzo haya kwa siku. Jee na wao wapewe mashine za EFD? Kwa hali ya sasa ingetakiwa angalau mauzo ya mwaka 360,000,000 yaani ikiwa sawa na 1,000,000 kwa siku ndio ulazimishwe kukusanya VAT.
2. Jee wateja wa nje ya nchi, Rwanda, Zambia, Msumbiji nk wataipataje VAT yao kwa vile hawatakiwi walipie? TRA watakaa na marundo ya hela mipakani kuwalipa marehesho yao au wafanyabiashara watatakiwa wasiwatoze VAT hawa. Sifikirii kama TRA wako tayari kuwalipa hawa mipakani na sifikirii kama wafanya biashara watakuwa waaminifu katika mauzo yao kwa kutumia mwanya huu kutowatoza kodi watumizi wa ndani kwa kutumia details za foreigners katika risiti. Hapo ndio mwanzo wa kuibiana.
3. Jee faida ya mfanya biashara itachukuwa vigezo gani kwa vile huduma nyingi tu nchi hii hazitolewi risiti kama vile uchukuzi wa local, kwenye vi carry na mgongoni pamoja na trolleys. Hizi zote ni gharama ambazo mashine haziwezi kuzitambua.
4. Msongamano wa mfumo katika kutoa ripoti ya marejesho. Kwa sasa tunaona namna gani mitandao inavyosumbua ofisini kwa TRA. Inaweza kusumbua kwa siku mbili nzima. Na hizi mashine haziwezi kukuruhusu kuitumia kufanya mauzo siku ya pili mpaka utume ripoti ya mauzo ya siku ya nyuma. Jaalia unatuma hongera za mwaka mpya saa sita usiku on New year eve. Nini kinatokezea? Sms haiendi kwa msingamano. Jaalia machine 1,000,000 moja zinatumika ndani ya mkoa wa Dar maduka yanapifungwa (saa 11 -12) kila siku. Nafikiria hiyo server ya TRA itaungua.
5. Kufanya marudisho mwisho wa mwaka itakuwa msongamano mkubwa ofisi za TRA. Kwa vile mfumo mzima ni automated, itachukuwa muda mrefu kwa kila mteja kumaliza huduma ya marejesho kutokana na miundo mbinu isyoaminika. Na sababu nyengine nyingi tu itakuwa usumbufu kuzitaja zote hapa.
Kwa sasa rates zetu za kodi ni kubwa mno, in theory atleast, na tunashindwa kukusanya hata 25% ya kodi. Tungezipunguza nusu yake tujakusanya 75% tu ya kodi basi tungekusanya kodi nyingi kuliko tunavyokusanya sasa.
Kwa muono wangu, kwa nini tutumie mifumo iliyokuwa hatujaibuni sisi wenyewe na kuwapa faida Wachina na Wazungu kwa kununua vifaa vyao na kulipia huduma za matengenezo kwao. Tutumie mfumo wetu wenyewe, na kwa sasa ni makadirio, manually, tuajiri vijana wengi tu wawe wanapita kuhakikisha kila mfanya biashara analipa kodi aliyokadiriwa kila mwezi. Ukimpa kijana mmoja maduka 200 ahakikishe mfanya biashara amelipa bank lets say 200,000 kila mwezi. Atakuwa kakusanya 40,000,000 na yeye mshahara wake ni 1,500,000. Itakuwa TRA imekosa nini? Vijana wanamaliza masomo hawana kazi, tunawatajirisha Wachina kwa kununua mashine zao mbovu kutiana hasara tu, kwa nini? Halafu eti Wachina wameendelea! Wasiendelee na sisi tunajizarau wenyewe. Kwetu tuseme hatuna mafundi wanaoweza kushona sare za jeshi, polisi etc?. Kama rates kubwa za kodi ndio maendeleo, basi Dubai ingekuwa mkiani kimaendeleo. Kama EFD machines ndio maendeleo, basi India na China wangekuwa tiro kimaendeleo. Tubadilike.