Mashine za EFD sasa kutolewa bure na Serikali!

Mashine za EFD sasa kutolewa bure na Serikali!

Hakuna mtanzania asiyetaka kulipa kodi ila kuna mazingira yasiyo rafiki yanayompelekea mfanyabiashara kukwepa kulipa kodi

Efds ni janga hata zikitolewa bure. Impact ya hizi ndude kwenye biashara ni hatariiii.
 
Tangu awali hizo mashine hawakuuziwa wafanyabiashara. ila serikali ilichofanya ni kuwaambia wagaramie garama za ununuaji halafu watarudishiwa taratibu wakati wakilipa kodi mpaka hela yao waliyolipia itakapotimia. hela yenyewe kama sikosei ilikuwa laki 8. kwa lugha rahisi ni kuwa hela yao ingerudi kwa kulipa kodi pungufu ya ili waliyostahiki kufidia hela ya hiyo mashine.
bila shaka mmeelewa.

Na hao waliokwisha nunua warudishiwe mishiko yao

sasa walionunua watarejeshewa pesa yao?

Na rais wa zamani arudishwe madarakani. ndo hayo watu wanaanza kusema kuhusu serikali iliyopita. tutafika kwa hayo yaliyotendeka huko?
ngoja afanye kuanzia anapoanzia. tumpe suport tu.

na mm nilienunua je

]sasa walionunua watarejeshewa pesa yao?##Ikiwa hivyo na raid aliepita arudi madarkan kama haliwezekani lililopita limepita tugange lililopo

Wanakopesha hawagawi alonunua bado ana faida.

Itasaidia kukusanya kodi na kupunguza malalamiko, maana wafanyabiashara walikuwa wakizilalamikia zinauzwa kwa bei kubwa. Kazi ya kukusanya kodi itafanyika bila malalamiko. Tanzania ijengwe kwa kodi zetu pamoja na rasirimali zetu, kwa Dunia ya sasa hakuna msaada wa bure.

Will TRA make a refund for my old machine?
Magufuli anavamia syndicate kwa pupa. Matatizo ya uchumi wetu SI mashine hizi Ni watu kama Kinana, Ritz1, Ben etc
Ubavu Hana hata WA kuwaambia tra watumie network ya ttcl....
 
Safiiiii safiiiiiiii safiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii....

So, now wafanyabiashara watakuwa wanafurahi kidogo.... lilolobaki ni kuangalia kodi, je ni rafiki kwa mfanyabiashara.....? Usikute mtu aba turnover ya 20 mil kwa mwaka... alafu kodi ni 10 mil.. hapo utamuua na KUMZIKA KABISAAA MFANYABIASHARA....

EFD.. hii ni hatua kubwa sana kwa Magufuli kafanya vema... tumpongeze... kwenye ukweli tumpe CREDIT JAMANI...!!

👏👏👏👏👏👏

Hapana jamani, wafanyabiashara wanalalamikia mfumo mzima unaoizunguka sio rafiki kabisa.Mfano,unapopata dharura na ukashindwa kufungua duka unatakiwa uandike barua kwa meneja wa T. R. A. kuhusu udharura huo. Sasa ikitokea umefiwa? au asubuhi umeamka na tumbo la kuhara?(kumradhi).

Na usipofanya hivyo ni adhabu ya milioni 3 kwa kukwepa kutoa risiti na sababu kuu hapa kila risiti unayoiandika taarifa zake zinakuwa T. R. A kwa sababu ya mfumo huo wa mashine kuunganishwa na wa T. R. A..

Lingine ni ubora hafifu wa mashine hizi pamoja na Network kuwa mbaya kwa muda mrefu, haya tu pekee yanaifanya mashine kukataa kutoa risiti. Hivyo faini(adhabu) tu zinatosha kuuwa mitaji yetu.Lingine T. R. A wanasema ili urudishiwe gharama kutokana na kodi unayo wakusanyia wanataka risiti zako za gharama ziwe za mashine ya EFD'S tu.Swali, je wabeba mizigo/mama ntilie/wasukuma mikokoteni au maguta/wauza maji/mikaa/vyombo vya usafiri vyote na wao watapewa mashine hizi? Kwa sababu wafanyabiashara huwa wanashirikiana na hawa watu katika shughuli zao.

Kwa kifupi kabisa nimeonesha mfano mmoja tu, lakini yapo mengi sana yanayo tukera kama wafanyabiashara hasa mashine hizi za EFD'S ambazo ni kama zinalazimishiwa kwa wafanyabiashara ilihali Serikali haikuwa imejiandaa.
 
dddaahh:

ninachoamini ni kwamba wafanyabiashara wasingeweza sema kile ambacho kinafanya wazikatae efd..wakaishia kusema ni ghali sana..lakini kiukwelu tatizo si bei kwao..

sasa kwa hali hii kilio chenu kimesikika..machozi yamefutwa..sasa mjiandae kwa ile 'amsha amsha' ya mtaa kwa mtaa ya kutotumia mashine..na nilivyosikia awali hadi mwaka wa fedha mpya kila aina ya mfanyabiashara atatakiwa kuwa na efd tena ikibidi mbili mbili kama back up ili kusiwe na exuse ya kutotumia efd...

kingine kinachonishangaza ni kwamba walalamikaji wakubwa si walipaji wa hiyo VAT kwa maana mfanyabiashara halipi hiyo kodi isipokuwa mlaji wa mwisho ndie hulipa....

ishu ya kwamba inakata kwenye mtaji,mauzo badala ya faida...kwa muelewa wa masuala ya ulipaji kodi hawezi zungumza haya...

twende sawa...wafanyakazi wanakatwa kimyakimya...walaji wanalipa VAT kimya kimya...mfanyabiashara(wakala wa kukusanya VAT) inakubidi utupelekee kodi yetu inapohusika kimyakimya
 
Swala la mashine siyo small issue. Hili lilkuwa kero kubwa kwa wafanyabiashara wadogo! Just imagine; mfanyabiashara mdogo unatoa kati ya laki 8 hadi zaidi ya Milioni moja> mtaji wote unateketea!!!
 
wafanyabiashara wengi wamekua wakikwepa kulipa kodi kutokana na kutokua na mashine za EFD ambazo zinauzwa bei ghali. Mfano wafabiashara wanaofanya biashara za jumla kama mawakala wa vinywaji vikali kama bia wamekua wakitumia magari na Toyo kusambaza vinywaji vyao. Ukichunguza utakuta magari mawili tu kati ya matano ndo yana mashine za EFD ukiachilia mbali Toyo. Ukija mbeya utakuta Toyo nyingi zinasambaza vinywaji km bia lakini EFD hazina. TRA fanyeni maamuli kwan ukwepaji wa kodi bado mkubwa.
USHAURI. Jaribuni kulinganisha kiwango cha mzigo anachochukua wakala kiwandani na kiasi cha kodi anacholipa mtapata majibu.
 
Hata mwanzo ilikuwa unanunua kisha unarudishiwa kwa kukata katika kupeleka kodi
Sema wabongo wachacha sana wanaopeleka hesabu zao TRA

Kwa kuwa walikuwa hawalipi kodi inayostahili kwa hiyo wamejirudishia kwenye kodi waliyoiba.
 
Back
Top Bottom