Mashemeji kutawala Ukweni

Mashemeji kutawala Ukweni

I completely disagree with you mkuu. Heahima lazma iwepo. Mimi ni mtoto wa kike, hata kama nitachangia shilingi kadhaa lakini kuna levels of authority hapo nyumbani. Hata kama ni kwa majadiliano tu, ni lazima nipate approval ya say kaka mkubwa na baba mdogo.

mwisho wa siku mtoa mada anatakiwa amuweke mahali pale kistaarabu. Taratibu na meseji itawafikia.
hujanisoma kwa makini, ukinisoma kwa makini utanielewa vizuri sana.
 
Aiseeee, pole sana mwanaume! Kiukweli mapigo yangu ya moyo yameenda kwa kasi sana baada ya kusoma thred hii sasa sijui kama shemeji yangu akinifanyia mimi! Pole sana cha msingi mfikishie ujumbe wa jinsi unavyojisikia kistaarabu pindi anapoonyesha tabia hizo!
WanaJF kuna jambo linanisumbua naomba ushauri,kuna Shemeji yangu kamuoa dada yangu wa Kwanza ni kikabila ni Mluguru kazi yake Mchungaji,tabia zake zimevuka mipaka anapenda Makuu na kutawala sasa hivi ndiyo kajifanya King wa familia yetu kila kitu cha familia anataka aamue yeye sijui anatumika na mkewe,ila mpaka mashemeji zetu waliooa dada zangu wengine anataka awatawale,sisi ni watu wazima kila mtu anaishi kwake ila akipiga simu masuala ya familia yetu anatufokea tu bila sababu za Msingi,nimemuheshimu mda mrefu ila nashindwa naombeni ushauri namna ya kufanya coz nafikiria kumpa 'mbovu' kutokana na kuzidiwa na Makwazo yake.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kwani nyie mkiowa/ kuolewa mnabaki hapohapo kwenu? sijaielewa vizuri, kila mtu yuko kwake na familia yake mchungaji anakuja vipi kuwaamulia mambo? Baba/Mama yenu hayupo, kama hayupo hakuna mkuu wa familia kwa sasa? huyo mchungaji anaishi hapo kwenu...? sijaelewa vizuri toa maelezo. Kwetu sisi shemeji anaishia kwenye vikao vya familia, kwenye vikao vya ukoo hayupo.

CYBER kila mtu anajitegemea hakuna anaye kaa nae,yeye anakaa na mke wake(Dada yetu) na wanae tu,Mzee Mgonjwa kapata Diabetes kumbukumbu zake haziko sawa na kwa bahati mbaya huyo mke wake ndiyo dada yetu wa kwanza,Mama naye anakereka,kila mtu anakereka ila wote hatujalelewa kwa ujasiri wa Kikurya ndiyo maana najaribu kupata Ushauri hapa Jamvini kabla ya kufanya maamuzi magumu.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Labda ki uchumi mnamtegemea yeye lazima apaze sauti na kwenu

Hakuna anayemtegemea kwa chochote kila mtu ana maisha yake,hata huo Uchumi wa kutegemewa hana ila nadhani ni Makuzi tu ya hovyohovyo na tunadhani huenda anatumwa na Mkewe sema hatuna uhakika.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Vunjeni ukimya! Samaki hukunjwa akiwa mbichi kwani mnavyomuacha hivyo ataanza kutawala familia zenu. Ni busara sana endapo mtakaa ndugu wote then mjadiliane halafu mumtume kama mjumbe akampelekee taarifa kuwa enough is enough.

HUENDA AKABADILIKA.

Ha!ha!ha!ha!Arushaone nadhani hii iko applicable.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Talk to your sister man. it may be the wisest way. Au dadako naye haeleweki?

Moto dada yangu Chenga ni ndumila kuwili vibaya mno hatumuelewi na tunadhani yeye ndiyo kashika remote anamcontrol though wer not sure.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Umesema ni pastaaaaa page is loaading kuna pasta mmoja naye yuko hivyo hivyo sijui ndo huyo kwa kabila yeye si mruguru ila kaoa waruguru
 
Labda amehisi kaharufu ka uoga na inferiority complex kwenye ukoo wenu...
 
Hakuna anayemtegemea kwa chochote kila mtu ana maisha yake,hata huo Uchumi wa kutegemewa hana ila nadhani ni Makuzi tu ya hovyohovyo na tunadhani huenda anatumwa na Mkewe sema hatuna uhakika.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
Mamlaka ya kuitawala familia yenu kayatoa wapi?
wazazi wenu wanasemaje kuhusu hilo?
Nao pia anawagombeza kama anavyowagombeza nyie?
Inawezekana familia yenu mlimchagua dada yenu (mke wake) kuwa kiongozi wa familia kwa hiyo kamwomba mumewe amsaidie, anatekeleza anachotaka mkewe........
 
Labda ki uchumi mnamtegemea yeye lazima apaze sauti na kwenu

Kwa kweli hata mimi hilo la uchumi ndio lililogonga oblangata yangu. Kama ni kweli inabidi kama familia mjipange kwanza kiuchumi. Ni ngumu kumkabili mshika dau kwa maneno matupu. Vitendo hukidhi hajq maridhawa kuliko maneno. Kama sio hii mpeni tu makavu!!!!
 
pengine sijakuelewa? lakini kwa shemeji (ama mtoto wa kike) kuwa na hela haiwezi kusababisha atunishie misuli wenye boma lao. i mean unless wako tayari kuuza haki yao ya boma
hujanisoma kwa makini, ukinisoma kwa makini utanielewa vizuri sana.
 
Back
Top Bottom