Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 2,308
- 4,687
Hii inamaana kwamba makanisa 2000 nchi nzima na wachungaji na maaskofu wote wa kanisa la ufufuo na uzima kuanzia dar mpaka huko ujiji na maeneo ya katonto huko sumbawanga wote wanaadhibiwa Kwa kosa la mtu mmoja !! Kanisa linafutwa !! Amekosea tundu lissu amekamatwa lissu na taasisi inaendelea na oparesheni zake,miaka michache iliyopita kakobe aliingia kwenye mzozo mkubwa na serikali ,walakini serikali haikulifuta kanisa la full gospel Bali wali Dili na Zachary kakobe walivyoweza wao ! Miaka ya nyuma zaidi alizuka askofu mtikila wa kanisa la full salvation church yeye alikuwa na mapambano ya wazi na serikali na mara nyingine aliwekwa ndani na kufungwa hatukuwahi kusikia kanisa la full salvation limefutiwa usajili, askofu severin niwemugizi wa huko ngara aliingia kwenye mgogoro na serikali ya jpm ,hatua kadhaa zilichukuliwa dhidi yake lakini kanisa lake halikufutiwa usajili ,mapadri wa kanisa katoliki walitoa waraka kwa serikali wakiwa kanisani ,hatukusikia kanisa katoliki limefutiwa usajili Tanzania ,mchungaji na askofu ndugu mbarikiwa mwakipesile wa huko mbeya aliwekwa gereza lakini kanisa lake halikufungwa Wala kufutwa !! Ninani amemshauri msajili kufanya maamuzi ya aina hii ? Kama ni shinikizo limetoka Kwa nani na ninani au ni taasisi Gani itafuata? Maaskofu wa makanisa mengine najua mtasema hili haliwahusu lakini tambueni kwamba hatujui ni taasisi ipi itafuata baada ya hapa ! Mungu ibariki Tanzania