Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,039
- 3,486
Wanabodi,
Hili bandiko la ulizo kuhusu usalama wa maisha ya wakazi wa manispaa ya Morogoro kwa kuwepo mashamba makubwa ya mkonge mali ya magereza huku idadi ya wakazi wake kuzidi kuongezeka na mahitaji ya ardhi kuwa makubwa.
Eneo kuanzia Mkambarani hadi Kingolwira kuna mashamaba makubwa kando kando ya barabara ambayo yanahatarisha usalama wa watembea kwa mguu na waendesha pikipiki kati ya Mkambarani na Kingolwira baada ya saa kumi na mbili jioni. Mashamba ya mkonge yaliyoko Kihonda mali ya magereza yaliyo kando kando ya barabara ya Moro-Dom nayo hayana manufaa sana hapo yalipo kwa kuzingatia usalama wa raia lakini pia kusababisha mahitaji ya ardhi kwa ajili ya makazi kupanda na gharama kwenda juu.
USHAURI kwa Mamlaka husika:
1. Maeneo ya mashamba haya ya mkonge yapunguzwe kwa ajili ya shughuli zingine za kiuchumi, kijamii na makazi ukizingatia treni ya mwendo kasi SGR imepitia maeneo hayo
2. Mashamba ya mkonge yahamishiwe kwingine kama Kiegea ambako jeshi la magereza watamudu vyema kuyahudumia kwa uzalishaji ulio bora kwa ajili ya viwanda;
3. Bwawa jingine kubwa lijengwe (streams water catchment) lijengwe kuhifadhi baadhi ya maji yanayotiririka kutoka katika mili Uluguru na kumwaga maji hayo ndani ya mto Ruvu au mto Ngerengere kwa matumizi ya kutosha kwa viwanda ambavyo wawekezaji wanasita kuweka miradi mikubwa kwa hofu ya kuwepo mgao wa maji maana maji ya Bwawa la Mindu huduma ya kwanza ni kwa matumizi ya binadamu
4. Kando kando ya reli ya mwendo kasi SGR wapo wawekezaji ambao wangependa kuwekeza kuchakata mazao ya chakula, biashara nk lakini ardhi ni finye sana kwa kuwa eneo kubwa ni mashamba ya mkonge mali ya jeshi la magereza kama ilivyoelezwa hapo juu
5. Pawepo na barabara ya huduma za usafiri kwa daladala kati ya Mkambarani, Kiegea hadi Mkundi mwisho hivyo kuunganisha na barabara kuu ya Moro-Dom
6. Ndani ya miaka mitano ijayo wageni wengi ikiwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa serikali kuu waliopangiwa vituo jijini Dodoma wangependelea kujenga hapo kwa makzi kutokana na hali hewa yake ilivyo ambayo inauoto wa asili halisi kwa kuliwaza;
7. Utalii haufanyio vizuri kuanzia kwenye mji wa Morogoro ijapokuwa kuna vivutio vingi tu lakini haieleweki tatizo ni nini