Manispaa ya Morogoro huu ni wizi

Tsyamatsy

Senior Member
Sep 9, 2023
112
156
Moja Kwa moja kwenye Mada bila kuchoshana Wala kupotezeana muda, in short Manispaa ya Morogoro mnatuibia Kwa nguvu abiria tunaotumia stand kuu ya mabasi Msamvu.

Kitengo Cha ukusanyaji Ushuru stand ya mabasi Msamvu mnatumia mabavu kulazimisha Kila abiria anaetoka NDANI ya stand Ambae kwenye basi alilosafiria amepewa ticket lakini isiyo ya ki electronics mnamlipisha Ushuru wa kutoka nje.

Huyu mtu anayo ticket na anatoka kwenda nje ya stand na Wala sio kuingia ndani ya stand na katika basi alilosafiria amepewa hiyo ticket Kwanini mumzuie asitoke hadi alipie Ushuru wa kutoka nje Tena Kwa nguvu!
Kwanza Mkurugenzi hii imekaaje, kuzuia mtu asitoke ndani ya stand Hadi aoneshe ticket?

Utaratibu wenu na ni wa nchi nzima kwa vituo vyote vinavyolipisha Ushuru Kwa wanaotumia stand ni kuhakikisha anaeingia analipa Ushuru kabla ya kuingia na sio kumzuia mtu anaetoka ndani huo ni usumbufu.

Mfano mzuri ni stand ya Magufuli Mbezi, hakuna usumbufu huo wakati wa kutoka.

Na hii Mkurugenzi bila kuficha Wala kupepesa macho mmeweka MAKUSUDI kuwaibia na Kuwakomba waTanzania wasio na Uwezo na Uelewa Kwa kile kidogo walichonacho Kwa maana Wahanga wa hili nimeshuhudia wengi wao ni akina mama na wazee wasiojua electronics tickets na tickets za vitabu ambazo zimekuwa zikitumiwa miaka mingi na Sasa Latra hawazitaki.

Ingekuwa busara kama shida yenu hayo mabasi yasitoe hizo tickets ni kumchukua huyo abiria na hiyo unwanted ticket mpaka kwenye Hilo bus na kumkamata miliki wa bus Kwa kutoa hiyo ticket. Lakini ukiwaambia hao wakusanya Ushuru mwende kwenye bus husika wanasema sio kazi Yao bali ticket za bus mhusika ni Latra.

Sasa kama wao hawahusiki wanamzuiaje mtu? Basi watoe taarifa Latra na itawasaidia Latra kukamata watu wao.
 
Back
Top Bottom