Baraza la Madiwani Manispaa ya Morogoro livunjwe, limeshindwa kusimamia Manispaa

jojipoji koromije

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
991
1,412
Manispaa ya Morogoro inaongoza kwa kuwa na huduma mbovu za Barabara nje ya mji na Maji. Nje ya Mji ndiko wanakoishi wakazi wengi sio hapo mjini kati lakini mmeshindwa kuwatendea haki. sijui Mkurugenzi na Madiwani wake wanafanya kazi gani?

Ni viongozi walioshindwa kabisa kutengeneza barabara za nje ya Mji. Manispaa hii barabara za rami zipo mjini tu ila ukitoka nje ya mji huko mitaani ni shida tupu.

Nenda Lukobe, Mkundi, Tungi, Kihonda, Nanenane, huko Kasanga. Manispaa haina mipango ya kuweka rami au kukarabati barabara zake za pembezoni. Manispaa inazidiwa na Manispaa zenye mapato kidogo kama Kigoma, Tabora, Songea, Iringa etc.

Viongozi wa Manispaa hii wamekaa kama wapita njia, yaani hapa wanapita tu, wapigaji.I wish Mheshimiwa Rais avunje baraza la madiwani Manispaa ya Morogoro na iundwe tume ya kuendesha Manispaa hii.

Ukiachilia ubovu wa barabara Manispaa haina huduma ya Maji ya safi na salama. Manispaa imezungukwa na vyanzo vya maji vingi tu, lakini ina huduma hovyo sana ya maji. Hakuna Maji. Shida sana hii manispaa. Halafu eti Viongozi waliomba iwe Jiji!!!?

Hivi wanajielewa kweli hawa wapigaji? Naombeni TAKUKURU, CAG wachunguze fedha za mapato ya ndani zinatumika kufanya nini hapo Manispaa.
 
Back
Top Bottom