Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
Habari ambazo nimezipata punde ni kuwa kuna uwezekano aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Lau Masha akafikishwa mahakamani hasa baada ya kukiri mwenyewe kuwa alimpigia simu mgombea wa Chadema jimbo la Nyamagana ili ajitoe kugombea. Bw. Masha alinukuliwa na gazeti la Raia Mwema la August 25 kukiri kufanya hivyo:
Lakini jamaa wa Chadema waliopitia sehemu fulani ya sheria wamegundua kuwa kwa kitendo chake hicho Bw. Masha huweza kuwa amevunja sheria na anatakiwa kujibu katika mahakama ya sheria kwanini asifungwe kifungo kisichozidi miaka mitano jela. Hii ni kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi ya 1985 kama ilivyofanyiwa mabadiliko 1995. Sehemu ya Sheria hiyo (S91B) inasema hivi:
Je, atanusurika? Je Chadema iendelee kweli na mpango huo au wamuache tu aendelee kwani "yamepita tugange yajayo"?
Ni kweli nilizungumza naye kwa simu lakini si kwa ugomvi wala kumtishia. Nilimweleza kuhusu sera za kampuni yao kutoruhusu watumishi wake kujihusisha na siasa na kama anazifahamu. Pia nilimwambia kuhusu udanganyifu katika fomu zake na kwamba nilikuwa natarajia kumwekea pingamizi na nitamshinda hivyo bora angeachia ngazi.
Nilimshauri pia kama ndugu yangu maana siasa si ugomvi, kuwa ukiacha kuchukua fomu nitakuombea usifukuzwe kazi kulingana na sera za chombo chako kwani kitendo cha kujiingiza katika siasa atafukuzwa kazi. Na kweli niliweka pingamizi sasa huko ni kumtishia maisha?
Sijamtuma ofisa yoyote kwenda kwake na hili la uraia nimelipata kutoka kwa wapambe wake. Mimi ni mwanasheria siwezi kufanya hivyo,
Lakini jamaa wa Chadema waliopitia sehemu fulani ya sheria wamegundua kuwa kwa kitendo chake hicho Bw. Masha huweza kuwa amevunja sheria na anatakiwa kujibu katika mahakama ya sheria kwanini asifungwe kifungo kisichozidi miaka mitano jela. Hii ni kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi ya 1985 kama ilivyofanyiwa mabadiliko 1995. Sehemu ya Sheria hiyo (S91B) inasema hivi:
91B Any person who corruptly induces or procures another
person to withdraw from being a candidate -to an election in
consideration of payment or promise of payment and any
person who withdraws in pursuance of such inducement or
procurement is guilty of corrupt practice and shall be liable
on conviction to imprisonment for a term not exceeding five
years''.
Je, atanusurika? Je Chadema iendelee kweli na mpango huo au wamuache tu aendelee kwani "yamepita tugange yajayo"?