Masha kufunguliwa mashtaka kwa kumshawishi Wenje kujitoa kugombea? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masha kufunguliwa mashtaka kwa kumshawishi Wenje kujitoa kugombea?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 3, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Habari ambazo nimezipata punde ni kuwa kuna uwezekano aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Lau Masha akafikishwa mahakamani hasa baada ya kukiri mwenyewe kuwa alimpigia simu mgombea wa Chadema jimbo la Nyamagana ili ajitoe kugombea. Bw. Masha alinukuliwa na gazeti la Raia Mwema la August 25 kukiri kufanya hivyo:

  Lakini jamaa wa Chadema waliopitia sehemu fulani ya sheria wamegundua kuwa kwa kitendo chake hicho Bw. Masha huweza kuwa amevunja sheria na anatakiwa kujibu katika mahakama ya sheria kwanini asifungwe kifungo kisichozidi miaka mitano jela. Hii ni kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi ya 1985 kama ilivyofanyiwa mabadiliko 1995. Sehemu ya Sheria hiyo (S91B) inasema hivi:


  Je, atanusurika? Je Chadema iendelee kweli na mpango huo au wamuache tu aendelee kwani "yamepita tugange yajayo"?
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Sheria lazima zifuatwe. Siyo haya ya Tendwa ya kubadilisha kanuni za kampeni baada ya mgombea wa CCM kukampeni hata baada ya saa za kampeni kumalizika.
   
 3. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Sio mzuri katika sheria ila KWA UELWA WANGU naona kama itakua ngumu kumfunga Masha kwani sheria inasema kama angemlipa au angetoa ahadi kumlipa ila amabacho sijaelewa ni paymenta ya aina gani ila kama wamereflect malipo ya Pesa then hapo hakuna kesi ila kama malipo ni katika kumsaidia Wenje asifukuzwe kazi then hiyo ni RUSHWA koz nahisi Masha anataka kutumia cheo chake cha Uwaziri wa Mambo ya Ndani katika kufanikisha swala lake.................

  Success comes with Trials and there is no Success without trial...So kama inawezekana CHADEMA wakae chini na wanasheria wao na waangalie uwezekano wa Kumikisha mahakamani ili Sheria ichukue Mkondo wake. Wawe careful on Doing so koz CCM wanalindana sana. Kama Rais anaweza kudiriki kuwasafisha hata ambao wana Kesi Mahakamani kuwa ni safi hata yule wa BAriadi ambaye anakesi ya JINAI na muungwana alisema ni Safi sidhani kama watashindwa kupangua hili na Kudai Masha ni Safi...
   
 4. M

  Mutu JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  sheria ifuate mkondo wake
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Bongo bana kumbe sheria ipo, unajua wagombea wengi in the flagship of the so called "kupita bila kupingwa" hii sheria inaweza kuwabana kama kweli vyombo kama TAKUKURU vingekuwa huru na serikali kuwa na nia ya kweli ya kudhibiti upuuzi huu.
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Jimbo la Ludewa CHADEMA walichezewa hivihivi it is high time idara ya sheria ya CHADEMA inaongezewa nguvu, ( wanataaluma wa sheria ) maana naona kesi ni nyingi sana watakuwa overwhelmed. Na hapo matokeo ya uchaguzi bado baada ya ccm kuchakua high time itakuwa balaa kwenye hiyo idara.

  Nasema hivyo kwa sababu wahusika tume ya uchaguzi na ofisi ya msajili wako kwenye usingizi mzito sana au kuna kitu ambacho wanataka kiwe achieved hivyo hawatataka kushughulikia matatizo ya kweli ya wagombea amabayo mwishoni mwa siku yatafanya ccm ishindwe.
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  MM, CHADEMA iende mahakamani ingawa watashindwa sioni ni jinsi gani kiravu ataamua kuwa kuna sababu ya kulipeleka suala hilo mahakakani, atachomoa kama anavyofanya siku zote. CHADEMA kama institution iko busy sana na kampeni countrywide na ofisi haikujiandaa vilivyo kwa ajili ya kukabiliana na hila za upinzani na chama kupokelewa vizuri na wananchi, hivyo wanajikuta wako overwhelmed kiorganizesheni.

  Watu wanaoipenda CHADEMA wanatakiwa kujitolea ili kuongeza nguvu kwa chama, tutumie taaluma zetu kwa kujitolea wakati huu wa kampeni kwa ajili ya chama chetu. Wanasiasa, wanasheria, wanasaikolojia, wachumi, waalimu etc tujitolee kwa ajili ya taifa letu tusitake mshiko kama ccm.

  MM, naomba tukiandika CHADEMA kila siku iwe in capitals, kwa nini tukifanya kwa ccm kunaweka capitals ikiwa CHADEMA kunaweka herufi ndogo.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Oct 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hivi hakuna lawyers ambao wangefanya pro bono kwa Chadema kama huko Mwanza n.k?
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,560
  Likes Received: 18,285
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />

  Mzee Mwanakijiji, kuwa lawyer bongo siku hizi ni deal kubwa, Zamani ma lawyers walikuwa ordinary people miongoni mwetu, siku hizi ni kwenye ma vogue meusi na vioo vyeusi kisa ni high fees zao ni pesa mbele, hao wakufanya pro bono watoke wapi?. Bongo sasa ni pesa mbele. Sucessiful advocates wa sasa sio tena wale mabingwa wa ku argue kwa vifungu vya sheria wa enzi za kina Murtaza Lakha, sasa ni wale ambao they use money o work for them, kina Nimrod Mkono type, no points of law but good connections.

  Chadema ina wanasheria kibao tuu ila kufanya pro borno ni issue nyingine, wao wakale wapi?.
   
 10. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Sheria ipo lakini haiwahusu vigogo, siku hizi hata wakuu wa wilaya wako "above the law", sheria inawabana maskini tu!
   
 11. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  CHADEMA should go to the court because it is their Right but also it will be a good lesson to others. Na unajua sheria hiyo wengi hawaijui!! Itawaamsha katika usingizi na pia kule ambako wanashawishiwa wajitoe au wasichukue fomu ili kuwa na "waliopita bila kupingwa".

  Mimi naona Masha ana kesi ya kujibu sababu ameahidi kumsaidia asifukuzwe kazi kuwa ukiacha kuchukua fomu nitakuombea usifukuzwe kazi kulingana na sera za chombo chako kwani kitendo cha kujiingiza katika siasa atafukuzwa kazi. Inaonekana Macha aliisha fanya underground work kutaka afukuzwa kazi mpinzani wake so hiyo ahadi ndipo kosa linapolala.
   
 12. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  MM huko ndio kuvolunteer kwenyewe lakini watu, hata wanansheria wanaogopa kweli kusikika kuwa eti wanansaidia CHADEMA, CUF, NCCR etc kisa wataonekana wabaya mbele ya watawala. Akili zetu ni mgando sana niambie unapishana na watu wangapi wenye kofia za Chadema na wanatemebea kifua mbele bila woga? Tutumie siku chache zilozobaki kuamka toka usingizini.
   
 13. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #13
  Oct 3, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Pasco, Kumbuka wanasheria wote walio CHADEMA ni wagombea kwenye nafasi zao inakuwa ngumu sana watoke majimboni waje na mahakamani na au wakae ofisini kushughulikia sheria, sio rahisi kabisa. Watu wanafanya pro bono, lakini kesi za siasa hakuna anayediriki kushika ni wachache mno. Nani anayetaka kugombana na mfalme nani asiyetaka kukaribishwa whisky Ikulu ?
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Oct 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ila kweli mwanasheria anayejiamini anaweza kufanya hivi na akajikuta anajipatia jina katika historia yetu..
   
 15. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Just right, Ona the likes of Julius Ndyanabo wanasomwa afrika nzima kwa ujasiri wa kupinga kifungu cha kuweka deposit wakati wa kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani.
   
 16. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #16
  Nov 6, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  kesi ilikufa?
   
 17. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #17
  Nov 6, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180

  Punda akikufia njiani kabla ya kufika safari hachapwi viboko, unamwacha wewe unaendelea na safari yako
   
 18. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #18
  Nov 6, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  hii sio habari ya punda kufa njiani! Ishu inabaki pale pale...masha alivunja sheria za nchi na hivyo inampasa ashtakiwe!!
   
 19. O

  Ogah JF-Expert Member

  #19
  Nov 6, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuu ulikuwa wapi siku zote za uchaguzi.............tuli-miss sana busara zako
   
Loading...