taffu69
JF-Expert Member
- Feb 26, 2007
- 2,094
- 538
Naamini lile sakata la kuvunjwa kwa majengo ya Empire Properties Ltd (Masaki) litakuwa na impact mbaya kwa Serikali siku za usoni.
Niwakumbushe habari hizi:
Niwakumbushe habari hizi:
Samani zavunjwa vunjwa ghorofa za Kinondoni
Sakata la maghorofa mawili ya Kinondoni bado linaendelea, ambapo sasa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imesisitiza kuwa itamburuza kortini na kumfungulia mashtaka ya jinai mmiliki wa majengo hayo ya ghorofa nane kila moja.
Pia, Manispaa imesema itamdai fidia ya kubomoa maghorofa hayo mmiliki huyo, ambaye ni kampuni ya Empire Properties Ltd.
Halmashauri hiyo imesisitiza kuwa kampuni hiyo ilipewa kibali cha kujenga jengo moja la ghorofa mbili chenye namba 00000500 na si vinginevyo.
Imesema kibali namba 00000600 ambacho mmiliki huyo anadai kupewa na Manispaa hiyo kwa ajili ya kujenga majengo mawili yenye ghorofa nane kila moja cha Agosti mwaka 2004 ni cha kughushi na kwamba hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi ya wote waliohusika.
Katika taarifa yake jana, Meya wa Manispaa,Bw. Salum Londa, alisema kampuni hiyo iliomba kujenga jengo moja la ghorofa mbili na ilipewa kibali cha aina hiyo.
'Baada ya kupitia michoro iliyowasilishwa na kuzingatia matumizi ya mipango miji, tuliidhinisha michoro hiyo na kutoa kibali cha kujenga ghorofa mbili kama alivyoomba, ' ilisema taarifa hiyo.
Ilisema iliomba kibali cha ujenzi katika kiwanja namba 383 kilichopo katika mitaa ya Toure na Mwaya huko Masaki, ikikusudia kujenga jengo moja lenye ghorofa mbili.
Licha ya kupewa kibali cha kujenga jengo moja la ghorofa mbili, kampuni hiyo ilijenga majengo mawili yenye ghorofa nane kila moja bila kibali chochote.
Hata ukuta unaozunguka majengo hayo ulijengwa bila kibali.
Taarifa hiyo ilisema mwezi Machi mwaka huu, Manispaa ilimpa ilani abomoe majengo hayo, ambayo aliyajenga bila kibali.
Baada ya pingamizi la mmiliki wa majengo hayo kutupwa na mahakama, Manispaa imeamua kuchukua hatua ya kubomoa majengo hayo.
Kanuni za ujenzi mijini zilizotungwa chini ya Sheria ya Miji, inazipa mamlaka za miji uwezo wa kusimamia na kudhibiti ujenzi katika eneo lake, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ujenzi wa jengo lolote unazingatia sheria na taratibu zilizowekwa.
'Napenda niwahakikishie wananchi kwamba hatua za ubomoaji zilizochukuliwa, zimefanywa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi.
Vile vile napenda kuwaasa wananchi kuwa wanapaswa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kuhusu ujenzi mijini ili wasije wakapata hasara pale sheria itakapochukua mkondo wake, ' alisema Meya Londa katika taarifa hiyo.
Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni hivi karibuni iliamuru majengo hayo yaliyopo makutano ya Barabara ya Toure Drive na Mwaya, yabomolewe. Shughuli za ubomoaji majengo hayo zinaendelea.
Majengo hayo yanaweza kubomolewa wakati wowote kuanzia sasa na maandalizi yanazidi kupamba moto.
Nipashe ilishuhudia maofisa kutoka wizara mbalimbali wakiyakagua majengo hayo jana mchana.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), askari wa kawaida na mgambo wa Jiji, wameweka kambi eneo hilo.
Wachina ndio wamepewa kandarasi ya kubomoa majengo hayo na wamekiri kuwa kzi hiyo ni ngumu kuliko walivyotarajia.
Mmoja wao, ambaye hata hivyo jina lake halikupatikana mara moja, alisikika akisema kuwa watalazimika kuajiri vijana wa mtaani kwa ajili ya kurahisisha zoezi hilo.
'Hapa lazima tuwachukua vijana wa mitaani waje kutusaidia. Kazi hii ni nzito tofauti na tulivyotarajia, ' alisema
Tayari samani mbalimbali zilizokwishawekwa katika majengo hayo zimevunjwavunja na kutupwa chini ya maghorofa hayo.
SOURCE: Nipashe 05/21/2006