Dkt. Slaa: Polisi wamezingira nyumba ya Mwabukusi na Mdude

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,159
22,661
Salaam , Shalom!

Dr. Slaa amesema kuwa amefanikiwa kupata picha ya Police kuizingira Nyumba ya Nabii Mwabukusi.

Ikumbukwe pia, usiku wa kuamkia leo, Police walivamia Nyumba ya Askofu Mwamakula wakimtafuta bila mafanikio.

Nia ya kuizingira Nyumba ya Nabii Mwabukusi haijajulikana hadi sasa ikiwa ni kuunga mkono na kushiriki pia maandamano au ni kuyazuia.


Hatimaye harakati za kweli za upinzani zimeanza kuonekana.

Mungu awabariki, sababu HAKI haijawahi kuletwa Bure kwenye sahani, Bali HAKI hupatikana kwa Mapambano ya kuidai.

Source: Za Ndani media Tv, Bongo 24 tv.

Nawasilisha.
 
Polisi ni mijitu sitaki hata kuisikia.

Juzi kati natoka maeneo fulani, na pikipiki napigwa mkono na mshikaji, nikasimama, akaniuliza unaelekea wapi nikamjibu akasema nae anaenda maeneo hayo nimsogeze, nilivyomcheki nikaona fresh wacha nimsaidie dizaini ni kama mwanachuo aliyemaliza miaka kadhaa mtaani life limempiga.

Nikamruhusu akalie chombo, njiani sikutaka maswali mengi, nikafika sehemu ninapoishia mimi, ye anaendelea na safari, kushuka anaanza kuleta stori, mwisho nikajua ni askari akanionesha na pingu kuna mwizi gani sijui anaenda kumkamata, nikajisikia vibaya sana kwanini nilimpa lifti kenge yule., nikatamani hata nimdai nauli, nikaona sio fresh.
Akaomba tubadilishane namba za simu nikamchomolea.

We kenge uliyepandia maeneo ya mikwambe pale, ukaja shukia mjimwema una bahati hukujitaja mapema nisingekupa lifti.
 
Back
Top Bottom