Mary Mramba aficha shilingi 700,000,000 chumbani kwake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mary Mramba aficha shilingi 700,000,000 chumbani kwake!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Elijah, Oct 23, 2012.

 1. Elijah

  Elijah JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 1,671
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  UTATA umegubika kuhusiana na kiasi kikubwa cha fedha ambazo ni shilingi milioni 700,000,000 zilizofichwa na Mary Mramba katika kabati nyumbani kwake Stakishari eneo la Sabasaba, Ilala jijini Dar es Salaam. Fumuafumua ambayo imekuwa ikifuatilia kwa karibu sakata la fedha hizo ambazo zilifichwa kati ya Novemba mwaka jana na Januari mwaka huu, imegundua kwamba ziliibwa na watu kadhaa wakiwemo ndugu zake.

  Imegundulika pia kuwa Mary alitoa taarifa Kituo cha Polisi Stakishari Septemba mwaka huu na kufunguliwa jalada la kesi STK/RB/16109/2012 na jalada la upelelezi STK/IR/12865/2012 akimtuhumu mtoto wa kaka yake aitwaye Digna Mark na wenzake kuhusiana na kesi ya kughushi hati ya nyumba na wizi huo.

  Uchunguzi wa Fumuafumua umebaini kwamba mara baada ya Mary kugundua mwezi Januari kuwa fedha hizo zilikuwa zimeibwa, hakutaka kupeleka suala hilo polisi kwa sababu anazozijua yeye bali alifanya kikao na wanandugu akiwemo Digna na kubaini tayari magari matano na nyumba mbili zilizokuwa zinamilikiwa na mtu huyo ni vitu vilivyokuwa vimenunuliwa kwa fedha hizo.

  Alichokifanya Mary ni kumpigia magoti Digna arejeshee hayo magari na nyumba hizo kwani hakutaka suala hilo alifikishe polisi. Pia inasemekana hata ndugu zake wengine walitoroka na zaidi ya shilingi milioni 400 kati ya fedha zilizoibwa. Imegundulika kuwa Digna aliiba shilingi milioni 300 na zingine ziliibwa na ndugu zake na kutoweka nazo. Mlalamikaji hakuwashitaki watu hao bali alikaa kimya ikidaiwa kwamba angeshitaki angeulizwa alikozitoa fedha hizo nyingi.

  Imebainika kwamba wanandugu hao waliamua kuiba fedha hizo wakiamini Mary asingeweza kuwashitaki kutokana na kwamba wanajua jinsi fedha hizo zilivyopatikana hivyo alihofia kuwa siri ingevuja. Taarifa zaidi zinaeleza kwamba Mary aliamua mambo hayo yaishe kwa siri ndani ya familia badala ya kupelekwa polisi ambapo yaliisha kwa upande wa Digna kwani aliamua kurejesha mali alizonunua na fedha hizo alizochukua ambazo ni shilingi milioni 300.

  Hata hivyo, Mary alilazimika Septemba mwaka huu kwenda polisi baada ya kusikia kwamba Digna ameenda huko kutoa taarifa kwamba hati ya nyumba yake ilikuwa imepotea. Fumuafumua imegundua kuwa maelezo yaliyotolewa na Mary huko polisi juu ya fedha hizo ni kuwa alitumiwa na ndugu yake aitwaye Philipo Sindana aishiye nchini Italia kwa ajili ya kununua nyumba, kitendo kinachopingwa na Digna ingawa hajawa tayari kuelezea ukweli kwa sasa.

  Hata hivyo, jalada la kesi hiyo liko kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili iandaliwe hati ya mashtaka. Wakati jalada hilo halijarudi, polisi imeelezwa kwamba askari wa kituo hicho cha Stakishari walikuwa wakilaumiana kwamba maelezo yalioandikwa hayakutosheleza na kuna kitu kinafichwa. Fumuafumua imebaini kwamba jalada hilo limesharudishwa toka kwa mwanasheria na kumweleza mkuu wa upelelezi Wilaya ya Ukonga, Idd Kiogomo kwamba hamna kesi ya kumshtaki Digna juu ya wizi ama kughushi bali ni kutoa taarifa za uongo za kupotelewa kwa hati ya nyumba.

  Mkuu huyo wa upelelezi ameagizwa kutoa taarifa ya kina juu ya shitaka la wizi kwani maelezo ya Mary yanaonyesha kwamba wizi ulifanyika Januari hivyo iweje atoe taarifa hizo Septemba. Kiogomo ametakiwa kuchunguza na kutoa maelezo juu ya upatikanaji wa fedha hizo nyingi na kwa nini zilihifadhiwa ndani. Vilevile Mary aeleze ni mahakama gani ilimpa kibali cha kutaifisha nyumba na magari ya Digna.

  Itaendelea wiki ijayo ikiwa na maelezo ya Mary, mumewe na jeshi la polisi.
   
 2. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kazi kweli kweli.
  Ningetarajia polisi wasingekubali kirahisi tu kwamba pesa hizo zimetumwa kutoka Italy.
  Uchunguzi wa kina ulipaswa/unapaswa kufanyika.
   
 3. S

  SWEET GIRL JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  khaaa!!kweli ukistaajabu ya musa basi hujaona ya firauni
   
 4. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  money laundering
   
 5. Anthony Lawrence

  Anthony Lawrence JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,544
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Tunaisubiri kwa hamu sehemu ya pili ya sakata hili
   
 6. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,796
  Likes Received: 36,821
  Trophy Points: 280
  Fumua fumua ndo nini?

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 7. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  is this happened in tanzania?
   
 8. grndossy

  grndossy JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tell me ua kidding men. 700m in a room!!!!!!!!!!!!!!!!! What type of joke is this?
   
 9. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  700,000,000,000,000
   
 10. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ukiwaeleza Watanzania kwamba elimu yetu ni ndogo, watakataa. Lakini ukweli ni kwamba huu hapa ndiyo ushahidi wenyewe. Ukiandika Shilingi 700,000,000 ni tofauti kabisa na kuandika Shilingi milioni 700,000,000. Kama alivyosema huyu ndugu niliyemkoti, kuandika hivyo ni sawa na kusema 700,000,000 zidisha mara 1,000,000. Matokeo yake ni 700,000,000,000,000 (Kwa hiyo hii ni trilioni 700). Hakuna anayeweza kuiba kiasi hicho cha fedha. Hata Mobutu hakufikia rekodi hiyo!
   
 11. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Yeah mkuu, true kabisa. Hii ni bajeti ya Tanzania kwa miaka kama mitano hivi
   
 12. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Kiingereza sahihi ungeuliza hivi "Did this happen in Tanzania?" Ama sivyo ungeuliza kwa kiswahili tu. Wenyewe husema titi la mama ni tamu hata kama ni la mbwa!
   
 13. Bosco Ntaganda

  Bosco Ntaganda JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 551
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Thread yako nzuri ila umakini katika somo la hisabati ndiyo umekupiga chenga
   
 14. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Huyu Mary Mramba ana uhusiano na Basil Mramba? Kama upo basi msihangaike zilikotoka pesa. Jitu lenyewe nalo ****. Kwanini kuweka pesa kama hiyo kabatini wakati Tanzania mtu yoyote anaweza kununua chochote bila kuulizwa/ Heri hao walioziiba wameona zinapotea bure. Ningekuwa Kikwete ningejinyonga kutokana na uchafu huu kufanyika chini ya utawala wangu. Hata hivyo nani amkamate nani iwapo wote ni panya?
   
 15. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kuna watu wanakufa njaa huku mwingine kahifadh 700 mil kabatin,kwel tunatofautiana maisha.je mhusika ni binti wa mramba?
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Oct 24, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Fumuafumua ni gazeti, jarida, ama?
   
 17. gmosha48

  gmosha48 JF-Expert Member

  #17
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280

  Hii kitu ni tatizo la kitaifa mkuu. Hata naibu waziri wa elimu analijua hilo!
   
 18. gmosha48

  gmosha48 JF-Expert Member

  #18
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Mkuu, bajeti ya Tz kwa mwaka huu ni trilioni 15. Kwa mwendo huu, hizi trilioni 700 ni bajeti ya mika zaidi ya 40
  !
   
 19. Jungumawe

  Jungumawe JF-Expert Member

  #19
  Oct 24, 2012
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 246
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  saSa kama waziRi wa eRiMu ni Mr. muluGO hajui chochote unategemea SiSi wengine TUTakuwaje!!!!!!!!
   
 20. Ngalangala

  Ngalangala JF-Expert Member

  #20
  Oct 24, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Sipati picha hela nyingi sana hizi kukaa nazo chmbani wakati hapo banana tu kuna bank
   
Loading...