Mary Mramba aficha shilingi 700,000,000 chumbani kwake!

m .Mramba ! mbona hili jina la mwisho kama la yule aliye wahi kuwa waziri .wana uhusiano wowote na yule alie pandishwa kizimbani kwa matumizi mabovu ya ofisi ?
 
Kiingereza sahihi ungeuliza hivi "Did this happen in Tanzania?" Ama sivyo ungeuliza kwa kiswahili tu. Wenyewe husema titi la mama ni tamu hata kama ni la mbwa!

Hata hivyo ni sawa kwa kiasi fulani sema angesema is this happening in tanzania?
 
Uzushi mtupu hakuna wala point hapa. Hoja hasa ni nini? Who is Mary Mramba manake kuna Miramba mingi hapa bongo na haina uhusiano na Basil wala Felician. Bazili na Felician ndoo Mirambo inayotuhusu kwani inadhamana zetu. Hawa wadada kama walificha hela zao labdha za madawa ya kulevya ni issue hii? Tatizo tunasahau haraka sana. Hivi watu wamesahau yule binti ya kigogo aliyekamatwa kwenye boti huko Lindi akiwa na kijana na mama mmoja na shehena ya madawa yenye thamani ya bilion na Ushee? hiyo ilikuwa ni trip moja tu? Don't ask me kesi iliishia wapi? Nitakujibu zinakuishia zingine za madawa ya kulevya. Tupe uhusiano wa huu Mramba na sisi watanzania wengine then jenga hoja.
 
Sio trilion jaman ni million 700 hebu someni vizuri.

Common sense.jpg
Tujiaminishe kuwa jamaa alimaanisha milioni 700, kwa kuwa kimantiki hiyo hesabu nyingine si uhalisia.
 
UTATA umegubika kuhusiana na kiasi kikubwa cha fedha ambazo ni shilingi milioni 700,000,000 zilizofichwa na Mary Mramba katika kabati nyumbani kwake Stakishari eneo la Sabasaba, Ilala jijini Dar es Salaam. Fumuafumua ambayo imekuwa ikifuatilia kwa karibu sakata la fedha hizo ambazo zilifichwa kati ya Novemba mwaka jana na Januari mwaka huu, imegundua kwamba ziliibwa na watu kadhaa wakiwemo ndugu zake.

Imegundulika pia kuwa Mary alitoa taarifa Kituo cha Polisi Stakishari Septemba mwaka huu na kufunguliwa jalada la kesi STK/RB/16109/2012 na jalada la upelelezi STK/IR/12865/2012 akimtuhumu mtoto wa kaka yake aitwaye Digna Mark na wenzake kuhusiana na kesi ya kughushi hati ya nyumba na wizi huo.

Uchunguzi wa Fumuafumua umebaini kwamba mara baada ya Mary kugundua mwezi Januari kuwa fedha hizo zilikuwa zimeibwa, hakutaka kupeleka suala hilo polisi kwa sababu anazozijua yeye bali alifanya kikao na wanandugu akiwemo Digna na kubaini tayari magari matano na nyumba mbili zilizokuwa zinamilikiwa na mtu huyo ni vitu vilivyokuwa vimenunuliwa kwa fedha hizo.

Alichokifanya Mary ni kumpigia magoti Digna arejeshee hayo magari na nyumba hizo kwani hakutaka suala hilo alifikishe polisi. Pia inasemekana hata ndugu zake wengine walitoroka na zaidi ya shilingi milioni 400 kati ya fedha zilizoibwa. Imegundulika kuwa Digna aliiba shilingi milioni 300 na zingine ziliibwa na ndugu zake na kutoweka nazo. Mlalamikaji hakuwashitaki watu hao bali alikaa kimya ikidaiwa kwamba angeshitaki angeulizwa alikozitoa fedha hizo nyingi.

Imebainika kwamba wanandugu hao waliamua kuiba fedha hizo wakiamini Mary asingeweza kuwashitaki kutokana na kwamba wanajua jinsi fedha hizo zilivyopatikana hivyo alihofia kuwa siri ingevuja. Taarifa zaidi zinaeleza kwamba Mary aliamua mambo hayo yaishe kwa siri ndani ya familia badala ya kupelekwa polisi ambapo yaliisha kwa upande wa Digna kwani aliamua kurejesha mali alizonunua na fedha hizo alizochukua ambazo ni shilingi milioni 300.

Hata hivyo, Mary alilazimika Septemba mwaka huu kwenda polisi baada ya kusikia kwamba Digna ameenda huko kutoa taarifa kwamba hati ya nyumba yake ilikuwa imepotea. Fumuafumua imegundua kuwa maelezo yaliyotolewa na Mary huko polisi juu ya fedha hizo ni kuwa alitumiwa na ndugu yake aitwaye Philipo Sindana aishiye nchini Italia kwa ajili ya kununua nyumba, kitendo kinachopingwa na Digna ingawa hajawa tayari kuelezea ukweli kwa sasa.

Hata hivyo, jalada la kesi hiyo liko kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili iandaliwe hati ya mashtaka. Wakati jalada hilo halijarudi, polisi imeelezwa kwamba askari wa kituo hicho cha Stakishari walikuwa wakilaumiana kwamba maelezo yalioandikwa hayakutosheleza na kuna kitu kinafichwa. Fumuafumua imebaini kwamba jalada hilo limesharudishwa toka kwa mwanasheria na kumweleza mkuu wa upelelezi Wilaya ya Ukonga, Idd Kiogomo kwamba hamna kesi ya kumshtaki Digna juu ya wizi ama kughushi bali ni kutoa taarifa za uongo za kupotelewa kwa hati ya nyumba.

Mkuu huyo wa upelelezi ameagizwa kutoa taarifa ya kina juu ya shitaka la wizi kwani maelezo ya Mary yanaonyesha kwamba wizi ulifanyika Januari hivyo iweje atoe taarifa hizo Septemba. Kiogomo ametakiwa kuchunguza na kutoa maelezo juu ya upatikanaji wa fedha hizo nyingi na kwa nini zilihifadhiwa ndani. Vilevile Mary aeleze ni mahakama gani ilimpa kibali cha kutaifisha nyumba na magari ya Digna.

Itaendelea wiki ijayo ikiwa na maelezo ya Mary, mumewe na jeshi la polisi.

hapo kwenye red hiyo haipo, naona ni mpya kabisa
 
Millioni 700,000,000!!! Tobhaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa...... yaawi twafa. Hakika mwalimu alishasema kuwa ufisadi hauwezi kupita salama hata siku moja kama watu wanalalama usiku na mchana. tuendelee kusubiri tutaona na kusikia mengi zaidi.
 
Anaundugu na yule mramba aliyekuwa waziri, ambaye anashitakiwa na Jamhuri ya muungano?
 
hacha mawazo finyu, kwenye hiyo thread yake umeona hiyo sehemu tu? we huwezi kujiongeza na kujua kuwa mwandishi hapa alilenga nini? huwezi kuandika makala kama hii isiwe na mapungufu ndo mana huwa kuna wahariri. nahisi mwandishi alidhamilia kuandika millioni 700 (sh. 700,000,000) kwa sababu ukisoma kwenye maelezo yake anandika millioni 300 na sio million 300,000,000. hapo mbona hupazungumzii???????????


Ukiwaeleza Watanzania kwamba elimu yetu ni ndogo, watakataa. Lakini ukweli ni kwamba huu hapa ndiyo ushahidi wenyewe. Ukiandika Shilingi 700,000,000 ni tofauti kabisa na kuandika Shilingi milioni 700,000,000. Kama alivyosema huyu ndugu niliyemkoti, kuandika hivyo ni sawa na kusema 700,000,000 zidisha mara 1,000,000. Matokeo yake ni 700,000,000,000,000 (Kwa hiyo hii ni trilioni 700). Hakuna anayeweza kuiba kiasi hicho cha fedha. Hata Mobutu hakufikia rekodi hiyo!
 
Kuna watu wanakufa njaa huku mwingine kahifadh 700 mil kabatin,kwel tunatofautiana maisha.je mhusika ni binti wa mramba?

Siyo 700 mil,... ni million 700,000,000/= yaani 700,000,000x1,000,000 ambayo ni sawa na 700,000,000,000,000/= , kiasi ambacho ni sawa na Trillion laki 7, ambayo ni pesa nyingi mara 47,000 kuzidi bajeti yetu ya Tanzania kwa mwaka 20012/2013. Huu ni uongo!
 
Yeah mkuu, true kabisa. Hii ni bajeti ya Tanzania kwa miaka kama mitano hivi

Weee Tshs 700 trillion is Tz budget for 5 yrs.... RUDI SHULE UPESI....

U don't know where we are heading.....

TZ budget 2012/13 = 15 trillion

700 divide by 15 = 46.67 yrs

Almost 47 yrs kwa current budget...
 
Back
Top Bottom