Da Mwitongo unajina zuri kweli nilifikilia utalitendea haki jina mwitongo,na wasiwasi kuwa uenda hata maana yake uijui?Hakika usiwafanye watanzania ni wavivu wa kufukilia mleta thread kasema MILLIONI 700,000,000 alikuwa sahihi na yuko sahihi katika tarakimu kuwa zilizoibwa ni millioni na sio trilioni.Inaonekana tukikwambia uandike pesa hiyo kwa maandishi utaiandikaje?MILLIONI MIA SABA AU TRILIONI MIA SABA.Ludi shule inaonekana mwalimu wako wa hesabu dalasa la tano alikuwa na mapungufu!!!
Du afadhali!maana mi muda wote nasoma uzi sielewi kitu roho inanidunda tu kila nikiyatafakali hayo masifuri .yaani bao kidogo wanigeuze jambazi nianze kuvamia nyumba za mafisadi,yaani hata mkuu wa kaya akiweka pesa kama hiyo kwake nakula kichwa!Yeah mkuu, true kabisa. Hii ni bajeti ya Tanzania kwa miaka kama mitano hivi
Tuna kazi sana. Hebu tujaribu kwenda pamoja:
7 = Saba
70 =Sabini
700 = Mia saba
7,000 = Elfu Saba
70,000 = Elfu Sabini
700,000 =Laki saba
Milioni 7 = Milioni saba
Milioni 70 = Milioni sabini
Milioni 700 = Milioni Mia saba
Milioni 7,000 = Milioni Elfu saba. Lakini Kiswahili sahihi ni Bilioni saba
Milioni 70,000 = Bilioni sabini
Milioni 700,000 = Bilioni mia saba
Milioni 7,000,000 = Bilioni Elfu saba. Kiswahili fasaha ni Trilioni saba
Milioni 70,000,000 = Trilioni sabini
Milioni 700,000,000 = Trilioni Mia Saba
Milioni 7,000,000,000= Trilioni Elfu saba. Kiswahili Fasaha ni Kwadrilioni saba (Seven Quadrillion)
Ili msichanganyikiwe, nadhani inatosha kuwa kama reference. sasa rejeeni kwenye Thread then msome kujiridhisha hizo pesa ni kiasi gani
Ukiwaeleza Watanzania kwamba elimu yetu ni ndogo, watakataa. Lakini ukweli ni kwamba huu hapa ndiyo ushahidi wenyewe. Ukiandika Shilingi 700,000,000 ni tofauti kabisa na kuandika Shilingi milioni 700,000,000. Kama alivyosema huyu ndugu niliyemkoti, kuandika hivyo ni sawa na kusema 700,000,000 zidisha mara 1,000,000. Matokeo yake ni 700,000,000,000,000 (Kwa hiyo hii ni trilioni 700). Hakuna anayeweza kuiba kiasi hicho cha fedha. Hata Mobutu hakufikia rekodi hiyo!