Marufuku ya mitumba wenzangu na mimi tutatoboa kweli?

Black Opal

Senior Member
Jan 22, 2023
199
253
Asilimia tisini kama si zaidi ya Watanzania tunapiga mitumba, ndio tunayoweza kumudu. Hatuna viwanda vinavyojitosheleza kwenye sekta hii kiasi cha kuzalisha nguo zenye ubora na gharama nafuu kwa wengi kumudu.

Mitumba imekuwa chaguo la wengi kutokana na kwamba unapata bidhaa nzuri kwa bei nafuu. Yaani ukichukua nguo mpya uliyonunua elfu 50, mtumba wa elf 10 - 20 unakuwa bora zaidi ya mpya. Walau marufuku ingekuja tukiwa tunataka kuinua viwanda vya ndani, lakini viwanda 0, hii karata Tanzania tuko tayari kuicheza kweli?

Wakuu, Tanzania ikienda na katazo hili wenzangu na mimi tutatoboa kweli? Au tutakuwa tunanunua nguo moja kwa mwaka?😂😅😅

mitumba.jpg

 
Siku hizi nguo sijui za China sio Bora Kama zamani aisee zamani nilikuwa nanunua mashati ya dukani natoboa mwaka mzima lakini siku hizi midosho fake nyingi Sana

Mitumba fake na dukani fake.
Ni kweli, wameshusha ubora ili kuendana na bei za mitumba
 
Huku vijijini haswa kanda maalumu Kuna watt huo mtumba mpk ushachanika watazi hawajaweza wanunulia Sasa special ndo itakuwa balaa Bora waruhusu gredi 1na 2 ila kuupiga ban ya mojakwamoja watatuacha uchi
Balaa, hali za watu wengi kumudu nguo special bado sana
 
Siku hizi nguo sijui za China sio Bora Kama zamani aisee zamani nilikuwa nanunua mashati ya dukani natoboa mwaka mzima lakini siku hizi midosho fake nyingi Sana

Mitumba fake na dukani fake.
Mimi napenda mtumba ase naendanga shekitangonnachua mashart makali tu suruali karume natoboa nayo
 
Back
Top Bottom