Marufuku: Tabia zifuatazo kwa mwaka 2024

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,230
22,309
Kwa mamlaka niliyojipa ninapiga marufuku tabia zifuatazo kwa mwaka 2024;
1. Kufungua threads za kuwasimanga single mothers.

2. Kukopa ovyo bila mpangilio na mwisho wa siku kujikuta kwenye matatizo yasiyo ya lazima. Waalimu wengi mzingatie sana hili.

3. Wanawake kuwapa kipaumbele viongozi wenu wa kiroho kuliko waume zenu. Huu upumbavu sitaki kuuona wala kusikia kwa 2024. Kama una baba wa kiroho acha mara moja.

4. Kwenda kula vinono migahawani huku nyumbani kwako wakishindia dagaa. Wanao na mke pia wanapenda zile chapati mbili na supu ya mbuzi. Hakikisha na wao wanakula unachokula wewe. Pumbav sana.

5. Kuishi kistaa mijini huku kijijini kwenu wazazi wakiwa wanaishi kifukara kwenye mbavu za mbwa. Unajisikiaje kuishi pazuri ukisukuma ndinga kali town huku familia yako ikiishi kifukara? Huu upumbavu mwishi ilikuwa 2023.

6. Kuendekeza mambo yasiyokuongezea thamani kwa mwaka mzima kama vile kufuatilia sana mechi za mpira. Fuatilia mambo ya burudani ila jiongezee thamani. Kama mhasibu huna CPA fanya uitafute mwaka huu. Wale wa IT kuna zile professional certifications pambaneni mzipate.

7. Wale mnaouza utu na kutojali maadili kisa pesa muache mara moja. Kibaya zaidi akijitokeza mtu kukemea na kukosoa upuuzi mnadhihaki kwa kumwambia "Acha makasiriko tafuta hela"... acheni kuabudu pesa kwa mwaka 2024.

Ongeza tabia nyingine unayoona haifai kuwepo kwa mwaka huu.
 
Unataka kusema we mwaka mzima hujakopesha rafiki aliyekuomba msaada?

Mkuu , Mimi marafiki zangu wengi wapo sehemu nzuri na huwa wakikopa ni pesa nyingi za Ku-run business zao , sio hatukopani .maana hukopa bank

Tangu nianze kutengeneza hela huwa simkopi MTU Ila huwa nasapoti harakati za MTU kimawazo na kipesa inapobidi na ikatokea MTU Ana taka mkopo huwa namshauri akakope bank au Kama ni ugonjwa huwa tunachangishana .
 
wanaotukopesha vyombo unataka waache
 
Hii inaumiza sana aisee,, mtu unamdai hakulipi halafu anajisahaulisha
Unajua ukitaka kumpa MTU hela ya mkopo hela ambayo unaweza kuisamehe Fanya hivyo ili kuondoa mgongano wa kimaslahi.

Wanawake hasa huwa hawalipi madeni so ikiwa MTU anataka mkope mshauri akatafte taasisi
 
Mkuu , Mimi marafiki zangu wengi wapo sehemu nzuri na huwa wakikopa ni pesa nyingi za Ku-run business zao , sio hatukopani .maana hukopa bank

Tangu nianze kutengeneza hela huwa simkopi MTU Ila huwa nasapoti harakati za MTU kimawazo na kipesa inapobidi na ikatokea MTU Ana taka mkopo huwa namshauri akakope bank au Kama ni ugonjwa huwa tunachangishana .
That’s good of You 🤍
Hongera
 
Tena awe ni yule ambae huonani daily.. ndio mbaya sana, unamcheck anajibu tu kirahisi nakupambania best.

Simu ikikatwa kakusahau..
Kuna mtu namdai hela nyingi sana aisee,, nilijisemea moyoni nimemsamehe maana hadi leo ni mwaka wa pili umeingia na hana mpango wa kunipa..Lakini kila nikionana nae naumia na sina chakumfanya kwasababu ni mtu wangu wa karibu sana
 
Back
Top Bottom