Maria Sarungi: Independent Candidate?

Maria Sarungi: Independent Candidate?

Maria Sarungi ni binti wa Mzee Profesa Philemon Sarungi aliyewahi kuwa mkurugenzi wa kitivo cha afya cha Muhimbili na baadaye kushika nyadhifa kadhaa serikalini kabla ya kusitaafu.

Mwanamama huyu ameolewa na mwanamme mwenye asili ya Ethiopia akiwa na maskani yake Dar es Salaama ambako ana biashara zake binafsi kadhaa, mojawapo ikiwa ya kutafuta warembo wa kushiriki mshindano ya Miss World ya Donald Trump. Mmoja wa warembo waliopitia katika mikono ya Maria Sarungi ni mrembo Flaviana Matata ambaye sasa hivi anang'aa sana kwenye anga za urembo huko New York Marekani.

Ingawa sijui undani wake binafsi, najua kuwa Maria Sarungi siyo mwanasiasa, bali aliteuliwa na Rais kuingia kwenye bunge la katiba ambalo limemaliza muda wake. Mchango wake kwenye bunge hilo la katiba uko wazi.

Kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja sasa, nimekuwa nafuatlia tweets zake, na kugundua kuwa ni mwanamama mwenye msimamo thabiti ambaye hajawa corrupted na party politics za vyama. Anachukua mazuri kutoka vyama vyote na kupinga mabovu ya vyama vyote.

Ingawa hatujaruhusu kuwa na independent candidates kwenye nchi hii, mtu wa aina hiyo ndiye nilikuwa ninataka ashike uskani wa kuingoza nchi hii.

Party politics zimechangia sana kuharibu nchi yetu na tunatakiwa kuachana nazo kuanzia sasa.

Hivi kabla ya kuingia kwenye bunge la katiba aliwahi kuongelea kugombea Urais? Kama hapana ni kipi kimemvutia kwa sasa? Kama kweli ni mzalendo kwa nini hakujiuzuru kwenye bunge la katiba. Huyu anafaa kuendelea na shughuli zake za kutafuta warembo na nyinginezo lakini sio kuongoza nchi hii hata kama imekuwa na mazuzu kiasi gani.

Wanawake wengi mwaka 2005 walimchagua JK kwa sababu kubwa kuwa ni handsome, sasa na nyie mmeshindwa kusema kuwa kawavutia kwa mambo mengine na kusema kuwa anafaa sana.
 
Nadhani atakuwa amezaliwa Finland/Hungary,mume mhabeshi.anafaa kweli kuwa mzalendo
 
Kuongoza nchi kwa sababu umemfuatilia tweeter!!!!????

Seriously ndio urais umekuwa hivi sasa???!!!
Asee. .,. . . . . . !!!!!
Maria Sarungi si mwanasiasa bali ni mwanaharakati, ni bora abaki huko huko ndiko ataweza. Uanasisa uwe mnafiki kidogo, na huyu dada hayuko hivyo.
 
Kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi hii, hairuhusu mbombea asiye na chama. LAZIMA awe mwananchama wa chama cha siasa.

Kama sijakosea kuna kipengele cha mgombea binafsi katika draft ya katiba mpya inayosubiri kupigiwa kura na wananchi...
 
Tangu niandike hapa siku chache zilizopita, JF ilikuwa imefungwa ila nimekuta likes kama 18 na quotes kama 13. Na kukawa na michango mingi inayofikia page kumi. Michango imegwanyika katika mafungu manne:

(1) Kuna wanao-question allegiance yake kutokana na kuwa na mama wa Hungary, na mme wa Ethiopia. Watu hawa ni wale wenye mtazamo mfupi sana wanaoamini mtu kuwa "guilty by association." Wanasahau kuwa hata rais Barack Obama wa Marekani ana baba wa Kenya; na vile vile huenda hawajui kuwa mme wa malkia Elizabeth wa England ni Mgiriki. Tujaribu kumwangalia mtu kama mtanzania na uwezo wake. Nina imani kuwa Sarungi ana uwezo akipewa.

(2) Kuna wanaopinga kutokana na kuwa nilimjudge kutoka na tweets tu. Watu hawa pia ni wafinyu na kwa bahati nzuri wengine walishajibiwa kuwa leo hii Twitter ni mojawapo ya tools kubwa sana za mawasiliano; huko Misri ni Tittwer iliyomuondoa madarakani Hosni Mubarak. Halafu pia watu hawa wameangalia neno Twitter tu badala ya kuangalia message nzima ambayo ilikuwa ni uwezo wake wa kukubali hoja nzuri kutoka pande zote za political spectrum ya nchi. Amekuwa anakubaliana na hoja nzuri zote za Ukawa na za CCM na vile vile amekuwa anapinga hoja mbaya zote za Ukawa na za CCM. Kiongozi mzuri ni yule atakayeihudumia Tanzania na watu wake bila kujali itikadi zao, na hili la kuchukua hoja nzuri bila kujali itikadi ni kipimo kizuri nilichokiona kwa huyu mama. Wengine wote wamekuwa wanavutua upande wa itikadi zao tu.

(3) Kuna watu wanaodai kluwa hata experience ya kisiasa, ni mwanamke, na kuwa kutokana na kujihusisha na kutafuta warembo hafai kuwa kiongozi mkuu wa nchi. Watu hawa pia wana upungufu mkubwa sana wa kujua aina ya kiongozi anayehitajika nchi hii. Baada ya miaka 50 ya uhuru iwapo bado tunatafuta mtu mwenye experience ya kisiasa, ni lazima atatokana na system mbovu iliyokuwapo ambayo ndiyo imedumaza nchi hii. Ili kuvunja hiyo visciuos circle ya mediocrity, ni lazima tumpate kiongozi asiyekuwa na experience mbaya hiyo. Kuhusu kuwa mwanamke ni mtizamu hasi sana kwa vile uongozi hautazwami kwa jinsia ya mtu. Ujerumani inaongozwa na Mwanamke, na historia inaonyesha kuwa mama Golda Meir wa Israel na Margaret Thatcher wa Uingereza wanakumbukuwa sana nchini mwao kama viongozi thabiti. Shughuli zake za kutafuta vipaji vya urembo haina tofauti kabisa na shughuli aliyokuwa akifanya Baraka Obama ya kutafuta na kusaidia vijana undersevred na kuwanyanyua; sijui kwa nini mtu aone kuwa hilo ni tatizo.

(4) Kuna wanaodai wanamjua vizuri huyu mama ambao wamegawanyika sehemu mbili; wale wa wanaomsupport na wale wanaompinga. Kwa bahati mbaya wanaompiga hawajatoa sababu za msingi.

Kwa mtizamo wangu, Tanzania inahitaji kiongozi ambaye hatakuwa na ellegience kwa chama kimoja bali kiongozi atakayechukulia watanzania wote kama wamoja ingawa ni wanachama wa vyama tofauti. Rais ambaye hatasita kumpa Uwaziri mtu wa CCM au wa UKAWA mradi ajuwa wana uwezo wa kuongoza nchi. Najua wapo wengi wenye sifa hizo lakini wote wanoongelewa mpaka sasa hivi ni wale ambao wana allegiance kwa vyama vyao tu, jambo ambalo siyo zuri.
 
Mama tibaijuka usingeelewa uchovu wake kama sio escrow.nilikuwa nabisha lakini mwanamke bado kidogo.Hawa viumbe utawajua wakiwa kwenye pressure ndio udhaifu wao utauona.Katiba mpya mnayoitaja inazungumza habari ya sifa za mgombea uraisi .Awe na uzoefu wa uongozi katika ngazi ya taifa.Sasa hapa mtasema alikuwa mtafuta warembo ngazi ya taifa au.Mnamkumbuka bibi Q Aquino?alisikia wanajeshi wame mutiny akajificha uvunguni.Haa unaongoza majeshi,unakabiliana na kina kenyata ,kagame,museveni.wakristo.waislamu,wauza madawa,wabunge,wana jf wana fb.hebu muulizeni Banda.Hawa wakipatiwa niniiiii ubongo unavurugwa.
 
Lakini je unawajua wanawake kama vile akina Golda Meir, Margaret Thatcher, Angela Merkel, Dilma Rousseff na wengineo walioongoza nchi zao kwa msfainikio makubwa? Tofautisha kuongoza nchi na kuendesha siasa.
 
huyu mdada namfahamu sana hana dharau wala kiburi nachati naye sana twita yupo tofauti na wanawake wengine ana msimamo sana kwenye hii ishu ya escrow amenihahidi wahusika wote wataghulikiwa hakuna funika kombe mwanaharamu apite document wanazo za kutosha.

Huyu kill3 namfahamu sana hakatai . yupo tofauti sana na jinsia yake.

Huyo mwanamke hana chochote ni kama amina chifupa. Anafanya siasa ya mtandaoni . ambayo Nayo ni ya muda .

.Malaya hachungwi.
 
Nakubaliana nawe Mkuu, mie pia namfahamu sana ni mtu poa sana ana ufahamu wa hali ya juu na anaipenda sana nchi yake Tanzania pamoja na kuwa mama yake ni wa kutoka Hungary na mumewe ni wa kutoka Ethiopia. Hao wenye Baba na Mama, Bibi na Babu wote Watanzania mbona hawaionei huruma hii nchi na Wananchi wake!? Kutwa kucha wanakwapua bila huruma tena siku hizi wanakwapua trilions.

huyu mdada namfahamu sana hana dharau wala kiburi nachati naye sana twita yupo tofauti na wanawake wengine ana msimamo sana kwenye hii ishu ya escrow amenihahidi wahusika wote wataghulikiwa hakuna funika kombe mwanaharamu apite document wanazo za kutosha.
 
Hivi kabla ya kuingia kwenye bunge la katiba aliwahi kuongelea kugombea Urais? Kama hapana ni kipi kimemvutia kwa sasa? Kama kweli ni mzalendo kwa nini hakujiuzuru kwenye bunge la katiba. Huyu anafaa kuendelea na shughuli zake za kutafuta )warembo na nyinginezo lakini sio kuongoza nchi hii hata kama imekuwa na mazuzu kiasi gani.

Wanawake wengi mwaka 2005 walimchagua JK kwa sababu kubwa kuwa ni handsome, sasa na nyie mmeshindwa kusema kuwa kawavutia kwa mambo mengine na kusema kuwa anafaa sana.

Nijuavyo alitoka na UKAWA
 
Yuko vizuri na ameonyesha uzalendo ambao viongozi wetu was sasa unawashinda!!!!
 
Lakini je unawajua wanawake kama vile akina Golda Meir, Margaret Thatcher, Angela Merkel, Dilma Rousseff na wengineo walioongoza nchi zao kwa msfainikio makubwa? Tofautisha kuongoza nchi na kuendesha siasa.

Angalia hali ilivyo mbaya Liberia.Angalia age ya hao kina mama ,angalia historia zao,jilize huyo merkel marekani ilichokua inamfanyia. ndugu yangu nchi sio NGO ama SACCOS umpe mdada,Ni ajabu vijana wa kisasa mnaraisisha sana mambo mnauona uraisi juujuu.Hapo unadili na Maalim Seif na wasioutaka muungano kuna issue nyingi.Mtu hupata power kutokana na alichonacho hasa knoledge na experience.Sasa kama walio wengi watakuzidi katika haya age,knowledge and experience unajikuta una authority ila huna power. Hakuna uongozi wa nchi ambao sio siasa hiyo ndio siasa hasa .it means who gets what?when and why?Hawa wadada bado damu moto nchi inaweza pata kashfa ukasikia au ukamuona ananiniliwa si mchezo.Hebu jiulize Migiro kimya.hebu jiulize watanzania wako tayari au mnafikiri ni kitchen party mnaandaa
 
Ninaelewa uwoga wako, lakini nadhani ni kwa sababu ya kuwa na mtazamo mfupi wa future yetu kwa vile unaingalia kwa kutumia kurunzi tunayotaka kuzima, yaani ya vyama vya siasa. Nimemtaja mama huyu kutokana na kukukubalika katika anga zote za kisiasa kwetu, yaani hajaonyesha kusapoti chama kimoja tu.
 
..katiba mpya si inapendekeza kila jimbo liwe na mbunge mwanaume na mwanamke??
Ndugu yangu Jokakuu,
Hujamsoma vizuri mleta mada... hata mimi awali nilikuwa sijasoma thread mzima nikaishia kuwa na mtazamo kama wako! Mleta mada anachomaanisha mleta mada sio ubunge bali urais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania kwavile tweets za dada etu Maria ni kiboko kweli kweli hadi zimemshawishi mleta ada kwamba Maria anafaa kabisa kuwa rais!

Mkuu Pasco, kile kipindi chetu cha TV ambacho ulitutangazia kwamba kingeanza early 2014 kimeishia wapi? Au Mzee Machache amekuzibia tena? Ninakisubiri hicho kipinndi kwa hamu kubwa; and please, kikiwa tayari naomba nami niarike niwe mzungumzaji mkuu... please bro, wite sisi ni kutoka TA kwahiyo I hope hutaniangusha... najua ukinipa coverage mara mbili au tatu tu... na vile Mwenyezi Mungu wengine alivyotajaalia kuongea, trust me, baada ya hapo I hope nitapata recommendation ya kuwa one of the best presidential candidate for 2015 race!

I am reserving Salva's post exclusively for you!
 
Last edited by a moderator:
mleta mada angalie usijishushie heshma ukaonekana namna gani.Unasema humjui ni udhaifu mkubwa sana kwaiyoo unaongelea picha zake au tweets.Unasema si mwanasiasa wakati uraisi ni siasa za hali ya juu.siasa ni pamoja na kukubali ya wajinga wengi kwa mda flani kwakuwa wengi wape hiyo wanaweza fanya wanasiasa au kujifanya huna taarifa kumbe unayo au kumweka mtu kiporo kumbe ndo imetoka.Ili umpe huyo dada uraisi unatakiwa kumfahamu yeye ,familia yake(baba na mama),umjue mume wake na histori yake ,tabia zake za utoto kiundani shuleni,vyuoni na kazin.mfano kisa cha kuacha ukrugenzi na kuwa msaka warembo
 
Ninaelewa uwoga wako, lakini nadhani ni kwa sababu ya kuwa na mtazamo mfupi wa future yetu kwa vile unaingalia kwa kutumia kurunzi tunayotaka kuzima, yaani ya vyama vya siasa. Nimemtaja mama huyu kutokana na kukukubalika katika anga zote za kisiasa kwetu, yaani hajaonyesha kusapoti chama kimoja tu.

ukiwa mwanaharakati una kuwa neutral ila ukiwa raisi utakuwa supporter wa chama flani,Ndio maana hata mgombea uraisi atapaswa kujiunga na chama mara baada ya kushinda uchaguzi
 
Kichuguu acha kudhalilisha ubongo wako kama unahitaji Rais wa sifa fulani weka hizo sifa wazi ili watu wampime bosi wako kama viatu vitamtosha!!

Hilo tu, sio ukamchongee viatu halafu ndio uanze kusifia vilivyomtosha vizuri wakati vimetenegenezwa kwa kipimo chake!!!!

Who the cap fit. . . . . . . . .
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom