Maria Sarungi ni binti wa Mzee Profesa Philemon Sarungi aliyewahi kuwa mkurugenzi wa kitivo cha afya cha Muhimbili na baadaye kushika nyadhifa kadhaa serikalini kabla ya kusitaafu.
Mwanamama huyu ameolewa na mwanamme mwenye asili ya Ethiopia akiwa na maskani yake Dar es Salaama ambako ana biashara zake binafsi kadhaa, mojawapo ikiwa ya kutafuta warembo wa kushiriki mshindano ya Miss World ya Donald Trump. Mmoja wa warembo waliopitia katika mikono ya Maria Sarungi ni mrembo Flaviana Matata ambaye sasa hivi anang'aa sana kwenye anga za urembo huko New York Marekani.
Ingawa sijui undani wake binafsi, najua kuwa Maria Sarungi siyo mwanasiasa, bali aliteuliwa na Rais kuingia kwenye bunge la katiba ambalo limemaliza muda wake. Mchango wake kwenye bunge hilo la katiba uko wazi.
Kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja sasa, nimekuwa nafuatlia tweets zake, na kugundua kuwa ni mwanamama mwenye msimamo thabiti ambaye hajawa corrupted na party politics za vyama. Anachukua mazuri kutoka vyama vyote na kupinga mabovu ya vyama vyote.
Ingawa hatujaruhusu kuwa na independent candidates kwenye nchi hii, mtu wa aina hiyo ndiye nilikuwa ninataka ashike uskani wa kuingoza nchi hii.
Party politics zimechangia sana kuharibu nchi yetu na tunatakiwa kuachana nazo kuanzia sasa.
Mwalimu nimeisoma Post yako na majibu mengi ya hii Post.Ni kweli Maria amejitokeza kuwa Mtanzania anayetetea maslahi ya wengi bila Uoga wala kuegemea upande mmoja (Itikadi za vyama).Maria ni Mwanaharakati wa kutetea haki sawa kwa wote.Mimi binafsi nina Imani kubwa na huyu Dada kama ataingia kwenye ulingo wa Siasa.Uwana harakati wake haumzuii kuingia kwenye Siasa.Ana upeo mkubwa wa uelewa wa mambo na ni rahisi kutolea maelezo wakati wowote.Maria hana Chama cha Siasa, na wala hatetei Status Qou,anaamini katika Utanzania na si Itikadi za vyama.Wapo hapa wanaomuhusisha siasa zake na Urafiki na Mh.Kabwe.Maria ni Mtu huru,huwezi kumchagulia rafiki eti kwa sababu tu rafiki huyo yupo upande wa pili wa Itikadi yako? Mbona hamuujadili Urafiki wa Maria na Dr.Kingwangwalla, Januari Makamba,John Mnyika, Halima Mdee au Ismail Jusa? Imekuwa Zito Kabwe tu? Kabwe kama Maria ni Watanzania zaidi kuliko Itikadi za Vyama,Urafiki wao unaweza kuwa umejikita kwenye hilo zaidi.
Kwa Mtazamo wangu Sikubaliani nawe Maria kuwania nafasi ya Urais,Nafasi hiyo ni kubwa sana kwake.Itakuwa vyema Maria aanzie (aingie) kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge kwanza.Ana nafasi nzuri kama atakwenda kwenye Ubunge katika Jimbo analotoka Baba yake au Majimbo yanayozunguka DAR kwa sababu tu ni sehemu anayoishi,na aliyokulia ana ufahamu zaidi na eneo hilo.Nawashangaa sana wanao-question uwezo wa Maria.Watu hawa watakuwa hawamfahamu huyu Dada au wanaleta ubishi kwa sababu zao binafsi.Maria toka Utoto wake ni mtu mpenda Nchi na mwenye Juhudi kwenye masuala ya Akademia (shule).Kwa maelezo yake mwenyewe "Anakinzana na Baba yake Dr.Sarungi kwa masuala mengi yanayohusu Utumishi wa Umma." Ni mtu mwenye mawazo huru na anayesimamia maamuzi yake!
Ni Mtanzania mwenzetu,Ametoka kwenye familia yenye uzoefu na public service,Tumpe ushirikiano atafute Jimbo ili awatumikie Watanzania wenzake.Siasa haina mwenyewe,huko Bungeni wapo wanasheria,walimu,wapiga disco,wanafunzi,wanaharakati,mabongoflava mpaka waganga wa kienyezi,wanaweza kuwawakilisha watu wao vizuri,Itakuja kuwa Maria ambaye kipindi kifupi cha Bunge la Katiba ameonyesha Umahiri na Ukomavu wake kisiasa? Tusimwage matusi na kujadili maisha yake Binafsi,Tumjadili Maria kutokana na mawazo yake kisiasa ktk Bunge la Katiba,Makongamano,Tweets,Instagram au Facebook.Tusijenge Hulka ya kuwakatisha Tamaa wenzetu ambao wameonyesha utashi wa kutaka kuwatumikia Watanzania wenzao..