Marekani: Waliobadili jinsia waondolewa marufuku ya kujiunga na Jeshi iliyowekwa na Donald Trump

Ni ujinga sana kuingiza jeshini mashoga.. huwezi kuwa na jeshi lenye mafanikio ukiwa na mashoga wa kutosha katika jeshi
Jeshi lenu la Tanganyika lina mashoga wengi tu. I know them in person, as a matter of fact.

Ni vile tu hawa wazungu wamekuzwa katika kusimamia ukweli na kuepuka unafiki unafiki.

Na hata tukisema tuamini kuwa jeshi la Tanganyika halina mashoga, bado haliwezi japo kushika nafasi ya kumi kutoka mwisho katika majeshi bora duniani, achilia mbali Afrika.
 
Jeshi lenu la Tanganyika lina mashoga wengi tu. I know them in person, as a matter of fact.

Ni vile tu hawa wazungu wamekuzwa katika kusimamia ukweli na kuepuka unafiki unafiki.

Na hata tukisema tuamini kuwa jeshi la Tanganyika halina mashoga, bado haliwezi japo kushika nafasi ya kumi kutoka mwisho katika majeshi bora duniani, achilia mbali Afrika.
Huu sasa ni uzushi
Mtaani mnasemaga mashoga wapo na hata kwenye familia pia.

Sasa hizi umekimbilia jeshini
Hebu wataje hao mashoga jeshini ..ili kuondoa unafki ambao unasema tunao
 
Rais Joe Biden ameondoa marufuku iliyowekwa na Donald Trump ya kuwapiga marufuku watu waliobadili jinsia kujiunga na jeshi.
Marufuku hiyo ilitangazwa na Bw. Trump mwaka wake wa kwanza akiwa rais wa Marekani.

''Watumishi waliobadili jinsia hawatakabiliwa na uwezekano wa kuondolewa au kutengwa kwa misingi ya utambulisho wao kijinsia,'' Ilisema ikulu ya White House.

Kulikuwa na askari 8,980 mwaka 2019, kwa mujibu wa takwimu za Idara ya Ulinzi zilizochambuliwa na taasisi ya Palm Center.

''Rais Biden anaamini kuwa jinsia haipaswi kuwa kikwazo kwenye utumishi jeshini, na kuwa nguvu ya Marekani iko kwenye utofauti wa wake,'' Taarifa ya Ikulu iliongeza.

Waziri mpya wa Ulinzi Lloyd Austin, generali wa jeshi mstaafu, alisema kwenye taarifa: ''Idara itatumia sera hii kuhakikisha kuwa watu wanaojipambanua kuwa wamebadili jinsia wanapata uhalali wa kuingia na kutumikia jeshi.''

''Vikosi vya kijeshi vya Marekani vina kazi ya kutetea raia wenzetu dhidi ya maadui, wa nje na ndani. Natumaini tutafanikisha hili vyema ikiwa tutawawakilisha raia wenzetu wote,'' aliongeza.

Bwana Trump alitangaza kupitia ukurasa wa twitter mwaka 2017 kuwa nchi hiyo ''haitakubali au kuruhusu'' kundi hilo la watu kuhudumu kwenye jeshi, akieleza ''gharama kubwa za matibabu na usumbufu''.

Mafufuku hiyo ilianza kufanya kazi mwezi Aprili mwaka 2019. Kundi la watu waliobadili jinsia ambao tayari walikuwa wakilitumikia jeshi waliruhusiwa kuendelea lakini wale waliokuwa wakitaka kujiunga walizuiwa.

Rais Biden mara kwa mara alisema kuwa alipanga kuondoa marufuku hiyo

Kabla ya kuapishwa, ujumbe kutoka kwa Ron Klain, kwa sasa ni Katibu Mkuu Kiongozi ndani ya White House, alisema Bw. Biden alipanga kutumia wiki yake yote ya kwanza ''kuboresha masuala ya usawa na kuunga mkono jumuia mbali mbali za rangi na jumuia nyingine zilizoonekana kutotendewa haki''.

Huu ni mfano wa hivi karibuni wa Bwana Biden kutumia maagizo kubatilisha sera za enzi za Trump.

Tayari amesaini maagizo ya kusimamisha ujenzi wa ukuta wa mpaka wa Mexico, kubatilisha marufuku kwa wasafiri kutoka nchi kadhaa zenye Waislamu, na kuzindua mpango wa kuboresha usawa wa rangi.
 
Kuna watu mpo obsessed na haya mambo.

Mnayapenda na kila siku mnatuandikia ujinga huu huu.

Hivi kwa nini msituandikie jinsi wachina wanavyofanikiwa kubuni teckolojia mbali mbali badala yake mtuletee hizi habari zenu mnazozipenda?

Hivi hao wazungu hawana cha maana mtuandikie ili tufaidike kuliko habari hizi chafu ambazo zikiimbwa kwenye nyimbo zenu na akina Diamond mnawapa hadi wanenu wazikariri?

Kama haya hamyapendi toka moyoni kwa nini hamuanzi na kupinga hawa vijana maarufu wa hapa kwetu wanaohamasisha ujinga huu kwenye muziki wao?
 
Iko hivi US kuna vyama viwili Democratic na Republican na kila chama kina itikadi zake,kama wewe ni rais LAZIMA ufwate itikadi za chama chako. Ndio maana unaona upande wowote utakaoingia madarakani utafwata itikadi za chama chake.

Kufahamu zaidi soma itikadi za left wing/liberal na right wing/conservative utaelewa zaidi. Usimshangae Biden anafwata sera na itikadi za chama chake na Trump alikuwa anafwata sera na itikadi za chama chake.
 
OGOPA SAANAA.
Hilo neno "JUMUIA MBALIMBALI ZA RANGI".
Akina delicious wamepata mtetezi wao
 
Jamani kuna wakati inabidi muache ujuaji. Mjifunze kuwa watazamaji tu ili muendelee kujifunza zaidi.

Kwanza, transgender sio shoga. Ni mtu aliyebadili jinsia.

Pili, Trump hakuzuia mashoga jeshini. Aliwazuia transgenders.

Tatu, transgenders waliozuiwa ni wale ambao walikuwa bado wapo kwenye matumizi ya madawa. Gharama zao zilikuwa kubwa.

Nne, usilazimishe ujuvi usio kuwa nao. Kuokoteza okoteza habari huko na wewe unajifanya mwerevu na mchambuzi!




Mkuu ni wazi hata wewe haya mambo hauyajui vizuri ingawa unawaambia wenzako waache ujuaji,

Kifupi ni hivi,hao Transgenders (trannies,shemales) ni MASHOGA tu ingawa wao wamekwenda mbali zaidi kwa kujipandikiza maziwa,makalio makubwa (some of them) na make up kwa sana kiasi kwa nje wanaonekana kama wanawake !!
 
Back
Top Bottom