Marekani: Trump atishia kufunga mitandao ya kijamii nchini Marekani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Donald Trump anatarajia leo Alhamisi kutia saini kwenye agizo linalolenga mitandao ya kijamii, maafisa wa Ikulu ya White House wamesema, saa chahe baada ya rais huyo kutishia kudhibiti au kufunga makampuni ya mitandao yote ya kijamii, akiyatuhumu kujaribu kuzuia uhuru wa kujieleza.


Wawakilishi hao hawakutoa maelezo zaidi kuhusu yaliyomo kwenye agizo hilo la rais Trump. Haijulikani kwa wakati huu jinsi Donald Trump kupitisha tishio lake la kufunga kampuni binafsi, ikiwa ni pamoja na Mtandao wa Twitter.

Mzozo huo uliibuka Jumanne wakati Mtandao wa Twitter ulihakiki ukweli wa baadhi ya ujumbe wa Rais wa Marekani Donald Trump alioundika katika ukurasa wake. Ni mara ya kwanza mtandao huo ambao Trump anapendelea zaidi kuutumia unafanya hivyo.

Rais wa Marekani alighadhibishwa na jambo hilo na kushumu mtandao huo kwa kile alichokiita ‘kuingilia kati' uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba pamoja na uhuru wa kujieleza.
Twitter ilichukua hatua hiyo ambayo haraka ilichochea mvutano kati yake na Trump, baada ya rais huyo wa Marekani kuandika Tweet mbili akidai kwamba mtindo wa kupiga kura kwa njia ya posta huwa una udanganyifu mwingi.

Ilichofanya Twitter ni kuweka kiungo kingine chini ya ujumbe wa Trump kinachosema "Pata taarifa za ukweli juu ya kura ya njia ya posta,” na baadae kiungo hicho kinampeleka mtumiaji kwenye makala ya habari inayompa taarifa za ukweli kuhusu suala hilo, na orodha ya maelezo yanayopinga madai ya Trump.

Trump mwenye wafuasi wapatao milioni 80 katika ukurasa wake wa Twitter, anasema anautumia mtandao huo wa kijamii kupinga kile anachodai kuwa ni taarifa za upendeleo zinazotolewa na vyombo vya habari.

Trump amekuwa akidai kwamba mtindo wa kupiga kura kwa njia ya posta, una viwango vya juu vya udanganyifu katika wakati ambapo majimbo mengi yanazingatia kuitumia njia hiyo ili kulinda afya ya raia dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 wakati taifa hilo likiwa linaelekea katika uchaguzi wa rais wa mwezi Novemba
 
Udictator mpya wa Fact check unaolimit free speech ndio habari ya duniani leo.

Ni kwanini katika post zote wameweka label ya fact check kwenye tweet ya trump kukosoa vikali upigaji kura wa mail in,

Ni kwanini fact check inalupeleka kwenye lame mainstream media zinazomchukia trump

Kwanini Joe Biden asinge kosoa hio tweet kwenye twitter, Au hana influence

Kwanini Democrats wenyewe wasingekosoa

Kwanini news media kama cnn au MSNBC zisingetumika kukosoa

Binafsi naona Democrtas, Lame stream Media na hata moinzani wa trump kwenye uraisi "Joe Biden" wameishiwa ushawishi wa umma, Critics zao zisizo na mbele wala nyuma watu wamezichoka nahisi wamebakiza karata yao hii ambayo si muda itakufa kwa kutumia twitter fact check.

Pia ceo wa facebook kapinga vikali huu upuuzi walioanza twitter.
 
Trump ametunga sheria ya kuyabana zaidi makampuni ya mitandao ya kijamii baada ya kuyatuhumu kuingilia uhuru wa kujieleza.

Trump anayatuhumu hayo makampuni hasa twitter kuingilia uhuru wa kujieleza baada ya kuanza kuhariri mawazo na mada za watu wanazoweka kwenye hiyo mitandao

Kwa sheria ya sasa ya Marekani mitandao ya kijamii inalindwa na sheria kwamba haiwezi kushitakiwa kwa kuondoa mada za watu kwenye mitandao yao bila hata ruhusa ya alieweka hiyo mada na wala haitashitakiwa kwa mtu kuandika chochote kwenye hiyo mitandao

Trump anasema mitandao hiyo sasa imegeuka na kua wahariri wa mawazo ya watu na maoni ya watu kwenye mitandao yao hivyo kuondoa uhuru wa watu kutoa maoni wakati ilipaswa kua katikati(neutral ground).

Sheria mpya inasemekana itawapa watu uhuru wa kushitaki mtandao ambao utaondoa maoni yake bila ridhaa ya mwandishi. Na mwanasheria mkuu wa Marekani anasema sheria ya kuyalinda hayo makampuni ilidhamiria makampuni madogo yanayo chipukia ila sio haya ya sasa.
Trump to sign executive order about social media
 
Kwa sababu ya 'Uhuru wa Kujieleza' hatafanikiwa
Itaenda mahakamani itafutwa na kutupwa jalalani
Anasumbuka bure
 
mng'ato

Wewe unayeongozwa na intelligent king from Chamwino amefanya nini?
.
Nikikuonyesha miradi miwili tu ambayo imefanywa na federal government hiyo Tanzania itaichukua millenia kuiota tu sio kuikamilisha!
 
Back
Top Bottom