Kuna kipindi niliwahi kuwaza, kuwa nchi za africa zitenge kila nchi eneo la ukubwa wa kati ya Kata ya Idifu (Dodoma) na ile ya Majengo mkoani Kilimanjaro kwa ajiri ya kuwapa makazi ya kudumu ndugu zetu hawa wenye asili ya Africa wanonyanyaswa huko nchi za nje. Kama wanataka kurudi kufanya kazi huko wakishapata makazi ya kudumu waende kwa 'hiyari' yao lakini wajue kuwa wanasehemu ya kuishi kwa amani nyumbani kwao. Dharau wanazofanyiwa zitakoma. Ila mpago huu ili ufanikiwe ni lazima kudhibiti hujuma kama zilizofanywa kwenye uendeshaji wa KORA Africa, mpago uliokuwa unakaribia kufanikisha 're-union' hii.
=====================
Mauaji hayakubaliki.