Nmesoma comments za uzi huu na nilikuwa nimeamua kuto-comment kwa sababu inaelekea 'ukilaza' aliosema baba j umetamalaki. Wamarekani walipositisha MCC, hawakusema kuwa huo ulikuwa mwisho wa kutoa misaada. Na tulijaribu kuwaelewesha kuwa Marekani imekuwa ikitoa misaada kwa Tanzania kwa njia mbalimbali. MCC ilikuwa ni aina mojawapo ya misaada mingi ila tu aina hii ilikuwa na lengo maalumu na hivyo kufanyika kwa masharti yaliyohusisha mkataba kati ya serikali ya Tanzania na Bodi ya MCC. Kwa vile serikali ya Tanzania ilivunja masharti ya mkataba, hapakuwepo na namna nyingine bali kusitisha MCC. Hakuna Mtanzania aliyefurahi kupoteza msaada huo, bali wapinzani walitumia nafasi hiyo kuonesha na kusisitiza umuhimu wa watawala kuzingatia masharti ya mkataba ambayo yalikuwa na nia nzuri kabisa kwa taifa zima- utawala bora, uwazi, demokrasia, nk.