Marekani kutoa Dola Mil 800 kuchangia miradi ya maendeleo

Marekani kutoa Dola Mil 800 kuchangia miradi ya maendeleo

sisi huku tunataka bunge live, pili hatumtaki Tulia, tatu dr. nadalichako ni jipu na nne div o na 4 waruhusiwe kuchukua degree msiwanyanyase serikali. hayo ndo mambo ya msingi sisi ukawa tutayasimamia kufa na kupona mpaka kieleweke. kwikwikwi....
Kweli wewe ni great sinker. Kuna vitu huwa mnajitoa akili na kuonekana ovyo.
 
Kwa hesabu zangu za form two ivi hii si zaidi ya 1.6trillion kwa exchange rate ya 2119?
Sikumbuki figures ya MCC ambayo walichomoa ila hii nadhani inaizidi ile.
Karibuni tena wazee wa kwa msaada wa watu wa Marekani
 
Duh kumbe nchi ikijisimamia mambo yanaenda hawa si walitangaza kusitisha misaada yako sasa imekuwaje wakabadilisha gear angani kama UKAWA,Duh hizi ni habari mbaya sana kwa upande wa ule mtaa wa UFIPA.
 
Duh kumbe nchi ikijisimamia mambo yanaenda hawa si walitangaza kusitisha misaada yako sasa imekuwaje wakabadilisha gear angani kama UKAWA,Duh hizi ni habari mbaya sana kwa upande wa ule mtaa wa UFIPA.
Subiri wazee wa ufipa waje. Wao wapo radhi serikali ishindwe, ndicho wanachopigania, tena kwa nguvu zote.
 
Nadhani UKAWA itabidi wasitishe ziara yao ya nchi nzima ya kwenda kuishitaki serikali ya Hapakazitu kwa wananchi. USA na nchi nyingine kubwa duniani ikiwemo China wanaipa big up serikali hii isiyopenda mizaha na usanii wa hovyo hovyo.
 
Style za utawala wa magufuli zitawachanganya ukawa jaman!
 
Ukereketwa na ushabiki wa vyama kwa mwendo kasi huu watu watakufa kwa pressure!
 
Niliposoma soma taarifa rasmi kutoka Ikulu nikajiuliza yafuatayo yanayo andikwa kuhusu JPM:
  • "Kiingereza cha Rais JPM"
  • "Serikali ya Udikteta"
  • "Rais hajasafiri kwenda Ulaya"
  • "Uvunjaji wa haki za binadamu"
  • "Serikali ya kukurupuka"
  • "Tanzania kutengwa na jumuhia za kimataifa"
  • etc.
Labda somehow hiyo taarifa ni cracking joke. Vingenevyo, nitashangaa kama kuna mdau atakuja tena hapa JF na hoja on any of the above.
Mm nakuja na hiii: Dr. JMP "Hatutaki misaada, Tanzania ni nchi Tajiri sana. Kwanza inapaswa yenyewe ndio iwe inatoa misaada kwa nchi zingine"
 
na hii ni baada ya kukubali zile ndoa kisirisiri! hii sirikali inatupeleka wapi?!
 
Duh kumbe nchi ikijisimamia mambo yanaenda hawa si walitangaza kusitisha misaada yako sasa imekuwaje wakabadilisha gear angani kama UKAWA,Duh hizi ni habari mbaya sana kwa upande wa ule mtaa wa UFIPA.
Nmesoma comments za uzi huu na nilikuwa nimeamua kuto-comment kwa sababu inaelekea 'ukilaza' aliosema baba j umetamalaki. Wamarekani walipositisha MCC, hawakusema kuwa huo ulikuwa mwisho wa kutoa misaada. Na tulijaribu kuwaelewesha kuwa Marekani imekuwa ikitoa misaada kwa Tanzania kwa njia mbalimbali. MCC ilikuwa ni aina mojawapo ya misaada mingi ila tu aina hii ilikuwa na lengo maalumu na hivyo kufanyika kwa masharti yaliyohusisha mkataba kati ya serikali ya Tanzania na Bodi ya MCC. Kwa vile serikali ya Tanzania ilivunja masharti ya mkataba, hapakuwepo na namna nyingine bali kusitisha MCC. Hakuna Mtanzania aliyefurahi kupoteza msaada huo, bali wapinzani walitumia nafasi hiyo kuonesha na kusisitiza umuhimu wa watawala kuzingatia masharti ya mkataba ambayo yalikuwa na nia nzuri kabisa kwa taifa zima- utawala bora, uwazi, demokrasia, nk.
 
Habari wanaJF,

Taarifa ya Ikulu inasema kuwa balozi wa Marekani amefanya mazungumzo na rais John Pombe Magufuli na kuahidi kuwa serikali ya Washngtone itataoa Dola Mil 800 kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo, pia huu ni uthibitisho wa kuwa baada ya kusitishwa kwa fedha za MCC awamu ya pili hakujaathili mahusiano baina ya mataifa haya mawili.
==========

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​

Marekani itatoa dola milioni 800 kwa Tanzania kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress aliyekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kutolewa kwa fedha hizo ni uthibitisho kuwa kutotolewa kwa fedha za awamu ya pili ya mradi wa changamoto za milenia (MCC-2) hakujaondoa uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Marekani ikiwemo utoaji wa misaada ya maendeleo. "Tumezungumza mambo kadhaa, na wiki hii Tanzania na Marekani kupitia shirika letu Ia misaada la USAID tunatarajia kutiliana saini mkataba wa zaidi ya dola milioni 400 kwa ajili ya mwaka ujao, pia tumezungumza kuwa kutakuwa na dola milioni 800 zitakazotolewa na Marekani kwa ajili ya miradi mbalimbali na hii haihusiani llll MCC.

"Ukweli ni kwamba tunayo mengi ya kufanya pamoja katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu na kilimo na tutafanya kila juhudi kuhakikisha haya yanafinikiwa" Amesema Balozi Mark Childress muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo na Rais Magufuli. Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali yake ya awamu ya tano itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na Marekani na kwamba fedha za msaada kutoka Marekani ni muhimu kwa maendeleo ya Tanzania .

"Amekuja kutuhakikishia kwamba watatoa hela kwa ajili ya Tanzania na anasema sasa hivi watatoa zaidi ya dola milioni 800, na mkataba mwingine tunaweza tukasaini hata kesho wa dola milioni 410, anasema kutotoa hela za MCC hakuna maana kupotea kwa urafiki wa Tanzania na Marekani, urafiki wa Tanzania na Marekani upo pale pale na sasa wanaongeza hela nyingi zaidi katika kuonesha kwamba juhudi za HAPA KAZI TU zinaendelea" amesema Rais Magufuli.

Wakati huo huo Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji Mhe. Didier Reynders Ikulu Jijini Dar es salaam, ambapo viongozi hao wamezungumzia kuendeleza na kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili hususani katika maendeleo.

Pamoja na kuzungumzia miradi ya ushirikiano inayotekelezwa kati Tanzania na Ubelgiji katika mkoa wa Kigoma, viongozi hao pia wamekubaliana kuongeza ushirikiano katika biashara na uwekezaji ambapo Mhe. Didier Reynders ameahidi kushawishi kampuni nyingi za Ubelgiji kuja kuwekeza hapa nchini.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli ameagana na Balozi wa ltalia hapa nchini Mheshimiwa Luigi Scotto ambaye amemaliza muda wake wa miaka mitatu.
Balozi Luigi Scotto amesema katika kipindi chake amewezesha kuongezeka kwa biashara kati ya Italy na Tanzania kwa asilimia 35 na ameielezea Tanzania kuwa ni nchi nzuri aliyoipenda na kwamba ataendelea kutangaza fursa zilizopo Tanzania huko Italia na kwingineko.

Mapema leo asubuhi, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametia saini kitabu cha maombelezo katika Ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Nchi za Kiarabu ya Saharawi iliyopo Mikocheni Jijini Dar es salaam, kufuatia kifo cha Rais wa nchi hiyo Mohamed Abdelaziz aliyefariki dunia Jumanne iliyopita tarehe 31 Mei, 2016.

Rais Magufuli ambaye amepokelewa na Balozi wa Saharawi hapa nchini Mhe. Brahim Salem Buseif amesema Marehemu Mohamed Abdelaziz ambaye pia alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Polisalio Front, atakumbwa kwa juhudi zake za kupigania ukombozi na uhuru wa Saharawi.

"Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Tanzania napenda kutoa salamu zangu za pole kwa Serikali na wananchi wa Saharawi kwa kumpoteza kiongozi umbaye ulijitoa kwa ajili ya kupigania ukombozi na uhuru wa Jamhuri ya Saharawi.
"Namuombea kwa mwenyezi Mungu, aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina" Amesema Dkt. Magufuli katika salamu hizo.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU Dar es salaam
06 Juni, 2016



View attachment 354091 View attachment 354092
UKAWA HOI TENA! Wanyamwezi baada ya kuona Umoja KAmili wa WApiga dili wameanza kampeni za kuleta vurugu... wameweka HADHARANI na kwa VITENDO kuwa wanamsapoti kwa NGUVU zote JPM! poleni sana mliokwenda MBAGALA poleni sana wale wa upande wa pili.... leo hamtalala wala kula kwa VIHORO....week imeanza vizuri sana...count down end of CHADOMO!
 
Niliposoma soma taarifa rasmi kutoka Ikulu nikajiuliza yafuatayo yanayo andikwa kuhusu JPM:
  • "Kiingereza cha Rais JPM"
  • "Serikali ya Udikteta"
  • "Rais hajasafiri kwenda Ulaya"
  • "Uvunjaji wa haki za binadamu"
  • "Serikali ya kukurupuka"
  • "Tanzania kutengwa na jumuhia za kimataifa"
  • etc.
Labda somehow hiyo taarifa ni cracking joke. Vingenevyo, nitashangaa kama kuna mdau atakuja tena hapa JF na hoja on any of the above.

You sound like kind of a fool.
 
Haya ukawa endeleeni kumkebehi Rais wetu

Na muendelee kuzungusha mikono
 
Wakati taarifa ya habari ya saa mbili nimeona mh mkulu akifurahi na kupongeza baada ya Marekani kutoa msaada wa dollar 800m, ikumbukwe baada ya MCC kusitisha msaada wengi wao CCM walionekana kuwaponda wafadhiri na kusema tunaweza kujitegemea wenyewe na kusema hii sio serikali ya omba omba akiwemo mkulu.

Hii naifananisha na ile stori ya sungura
 
Back
Top Bottom