Marekani kutoa Dola Mil 800 kuchangia miradi ya maendeleo

Marekani kutoa Dola Mil 800 kuchangia miradi ya maendeleo

Hehehe tulisema
Ukiwanacho hupaswi kuwa na papala watakuja tu
Sasa wale VILAZA walio ona MCC kama hoja kuu
Naona Aibu inawaandama
Nilichojifunza ni kwamba watanzania ni masikini jeuri tunajifanya hatutaki misaada huku uwezo wa kuendesha serikali hatuna,

Ukweli mchungu ni kwamba makusanyo ya tra hayawezi kuendesha serikali mbali na nchi.
 
Hatuhitaji misaada yao....kauli hizi zilisemwa na baadhi ya Waheshimiwa ......na wakaongeza kusema makusanyo ya kila mwezi yanatosha.
Hatuwezi kuwabembeleza wakileta tunachukua.
 
Mmarekani sio kabisa. Wabongo walisema kuwa wanaweza jitegemea leo wanasherekea kupokea misahada. Hao hao ndio walisema misaada ni mizigo kwa Tz. Billion 600 za mcc walisema ni mzigo sasa 800 sio mzigo?

Acha tu tuendelee kutawaliwa.
 
hii ni habari mbaya kwa ukawa,walishangalia sana tulivyokosa pesa za MCC,lakini watakuja na kejeli kuwa misaada ni mibaya
Dah! watu wengine bhana, kwa hiyo unafurahia kupewa msaada?
 
Habari mbaya sana kwa ukawa na mafisadi wakina Lowasa na Sumaye....hawana pakujificha.
 
Du! ni aibu nchi yetu kuwa ombaomba, leo unaomba kwa kutoa habari kabisa ya kupokea msaada, Maskini Dr. shein kaachwa mwenyewe waliompandikiza wamemtelekeza.. Pole ile kauli ya maalim shein uta ielewa tu na kutekeleza.
 
Habari wanaJF,

Taarifa ya Ikulu inasema kuwa balozi wa Marekani amefanya mazungumzo na rais John Pombe Magufuli na kuahidi kuwa serikali ya Washngtone itataoa Dola Mil 800 kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo, pia huu ni uthibitisho wa kuwa baada ya kusitishwa kwa fedha za MCC awamu ya pili hakujaathili mahusiano baina ya mataifa haya mawili.
==========

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​

Marekani itatoa dola milioni 800 kwa Tanzania kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress aliyekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kutolewa kwa fedha hizo ni uthibitisho kuwa kutotolewa kwa fedha za awamu ya pili ya mradi wa changamoto za milenia (MCC-2) hakujaondoa uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Marekani ikiwemo utoaji wa misaada ya maendeleo. "Tumezungumza mambo kadhaa, na wiki hii Tanzania na Marekani kupitia shirika letu Ia misaada la USAID tunatarajia kutiliana saini mkataba wa zaidi ya dola milioni 400 kwa ajili ya mwaka ujao, pia tumezungumza kuwa kutakuwa na dola milioni 800 zitakazotolewa na Marekani kwa ajili ya miradi mbalimbali na hii haihusiani llll MCC.

"Ukweli ni kwamba tunayo mengi ya kufanya pamoja katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu na kilimo na tutafanya kila juhudi kuhakikisha haya yanafinikiwa" Amesema Balozi Mark Childress muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo na Rais Magufuli. Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali yake ya awamu ya tano itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na Marekani na kwamba fedha za msaada kutoka Marekani ni muhimu kwa maendeleo ya Tanzania .

"Amekuja kutuhakikishia kwamba watatoa hela kwa ajili ya Tanzania na anasema sasa hivi watatoa zaidi ya dola milioni 800, na mkataba mwingine tunaweza tukasaini hata kesho wa dola milioni 410, anasema kutotoa hela za MCC hakuna maana kupotea kwa urafiki wa Tanzania na Marekani, urafiki wa Tanzania na Marekani upo pale pale na sasa wanaongeza hela nyingi zaidi katika kuonesha kwamba juhudi za HAPA KAZI TU zinaendelea" amesema Rais Magufuli.

Wakati huo huo Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji Mhe. Didier Reynders Ikulu Jijini Dar es salaam, ambapo viongozi hao wamezungumzia kuendeleza na kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili hususani katika maendeleo.

Pamoja na kuzungumzia miradi ya ushirikiano inayotekelezwa kati Tanzania na Ubelgiji katika mkoa wa Kigoma, viongozi hao pia wamekubaliana kuongeza ushirikiano katika biashara na uwekezaji ambapo Mhe. Didier Reynders ameahidi kushawishi kampuni nyingi za Ubelgiji kuja kuwekeza hapa nchini.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli ameagana na Balozi wa ltalia hapa nchini Mheshimiwa Luigi Scotto ambaye amemaliza muda wake wa miaka mitatu.
Balozi Luigi Scotto amesema katika kipindi chake amewezesha kuongezeka kwa biashara kati ya Italy na Tanzania kwa asilimia 35 na ameielezea Tanzania kuwa ni nchi nzuri aliyoipenda na kwamba ataendelea kutangaza fursa zilizopo Tanzania huko Italia na kwingineko.

Mapema leo asubuhi, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametia saini kitabu cha maombelezo katika Ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Nchi za Kiarabu ya Saharawi iliyopo Mikocheni Jijini Dar es salaam, kufuatia kifo cha Rais wa nchi hiyo Mohamed Abdelaziz aliyefariki dunia Jumanne iliyopita tarehe 31 Mei, 2016.

Rais Magufuli ambaye amepokelewa na Balozi wa Saharawi hapa nchini Mhe. Brahim Salem Buseif amesema Marehemu Mohamed Abdelaziz ambaye pia alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Polisalio Front, atakumbwa kwa juhudi zake za kupigania ukombozi na uhuru wa Saharawi.

"Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Tanzania napenda kutoa salamu zangu za pole kwa Serikali na wananchi wa Saharawi kwa kumpoteza kiongozi umbaye ulijitoa kwa ajili ya kupigania ukombozi na uhuru wa Jamhuri ya Saharawi.
"Namuombea kwa mwenyezi Mungu, aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina" Amesema Dkt. Magufuli katika salamu hizo.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU Dar es salaam
06 Juni, 2016



View attachment 354091 View attachment 354092


Mimi sisemi chochote humu, nangojea nisome tu na hasa zile za UKAWA
 
Habari mbaya sana kwa ukawa na mafisadi wakina Lowasa na Sumaye....hawana pakujificha.
Habari mbaya kwa Magufuli aliesema ni aibu kwa serikali hii kuwa ombaomba huku anaendelea kuomba na kupokea, sijui atatueleza huu ni msaada au kalipwa deni? Mtu mzima kuropoka ni hatari sana.
 
Habari mbaya kwa Magufuli aliesema ni aibu kwa serikali hii kuwa ombaomba huku anaendelea kuomba na kupokea, sijui atatueleza huu ni msaada au kalipwa deni? Mtu mzima kuropoka ni hatari sana.
Rais hajaomba huo msaada wameleta wenyewe wameufyata baada ya kuona msimamo wa Magufuli ni thabiti!
 
Nimeamini kweli watanzania ni wanafiki
Jk juzijuzi tu mlitoka kumtukana kisa kasema umuhimu wa misaada kwa nchi za afrika

Magu omba tena zaidi Tanzania inaitaji zaidi misaada
Ukimsikia mtanzania anabeza misaada wakati huu ujue ni mnafiki
 
Magufuli hapandi ndege lakini huko huko Ulaya na Marekani shughuli yake wanaifahamu vyema kabisa. Matendo yanaongea zaidi ya maneno ya kisiasa. Sasa wapinzani watakuja na hoja za kipuuzi kama ile ya Jesca, yaani mtu mzima na akili zake anaongea pointi za kipumbavu kabisa.
 
Niliposoma soma taarifa rasmi kutoka Ikulu nikajiuliza yafuatayo yanayo andikwa kuhusu JPM:
  • "Kiingereza cha Rais JPM"
  • "Serikali ya Udikteta"
  • "Rais hajasafiri kwenda Ulaya"
  • "Uvunjaji wa haki za binadamu"
  • "Serikali ya kukurupuka"
  • "Tanzania kutengwa na jumuhia za kimataifa"
  • etc.
Labda somehow hiyo taarifa ni cracking joke. Vingenevyo, nitashangaa kama kuna mdau atakuja tena hapa JF na hoja on any of the above.

Mimi mwenzio ndio nimeshangaa zaidi ni Magufuli huyuhuyu aliyetamba Tanzania hatuhitaji msaada!?

Makubwa haya ngoja niwape kitimoto chakula kwanza nitarudi.......
 
Rais hajaomba huo msaada wameleta wenyewe wameufyata baada ya kuona msimamo wa Magufuli ni thabiti!
Na wewe usicomment kama huna shule kichwani, hapo yanasainiwa makubaliano, hata mia hatujapewa na ukikiuka makubaliano wembe ni uleule wa mcc.

Hakuna pesa kutoka kwa wajomba isiyo na conditions labda kama na wewe upo kwenye payroll ya buku 7 umeamuwa kumfurahisha muajili wako uonekane unafanyakazi nzuri ya kula kinyesi.
 
Rais hajaomba huo msaada wameleta wenyewe wameufyata baada ya kuona msimamo wa Magufuli ni thabiti!
Thubutu! eti wameleta wenyewe, kama ana msimamo si ange ukataa?Amesikiliza ushauri wa JK nchi haiwezi kuendeshwa bila msaada kutoka nje, alijitia ujuaji kumbe hana lolote amekalishwa kitako akaambiwa aache ubabe na mdomo, chezea marekani wewe hata hiyo gass isingeuzika dunia hii.
 
sisi huku tunataka bunge live, pili hatumtaki Tulia, tatu dr. nadalichako ni jipu na nne div o na 4 waruhusiwe kuchukua degree msiwanyanyase serikali. hayo ndo mambo ya msingi sisi ukawa tutayasimamia kufa na kupona mpaka kieleweke. kwikwikwi....

Tanzania haiwezi kuwa nchi ombaomba, tunaweza kujitegemea. Hatuhitaji misaada ya wahisani.

Tangazo hili limewajia....
"Kwa msaada wa watu wa marekani"
 
Nampongeza Raisi na serekali yake ila hawa watu ni wajanja sana mimi nafanya kazi huko hizo hela nusu zitarudi kwao in terms of salaries &benefits,kununua equipment nk ukijumlisha hivyo vitu ni karibu asilimia 38,Asilimia 15 mpaka 17 ni indirect cost zao zinarudi marekani so mwisho wa siku ni asilimia ndogo tu inakuja kwa jamii
 
Tanzania haiwezi kuwa nchi ombaomba, tunaweza kujitegemea. Hatuhitaji misaada ya wahisani.

Tangazo hili limewajia....
"Kwa msaada wa watu wa marekani"
Ndio maana hajaomba kapelekewa ikulu. Rais atakiwi kulamba watu miguu.
 
Ni jambo la kheri sasa wamekuja kivingine
 
Back
Top Bottom